Kama hii habari haikuengezwa chumvi, Basi wa Tanzania Tutateketea wengi.

Babylon

JF-Expert Member
Feb 5, 2009
1,332
82
4000 waambukizwa Ukimwi Kinondoni ndani ya miezi mitatu
Monday, December 28, 2009 1:11 PM
IMEDAIWA kuwa ndani ya miezi mitatu kati ya Julai hadi Septemba mwaka huu watu wapatao 4072 wameambukizwa virusi vya ukimwi katika Manispaa ya Kionodnoni jijini Dar es Salaam Hayo yalijulikana baada ya kamati ya Kudhibiti Ukimwi katika Manispaa hiyo kutoa takwimu hiyo.

Kati ya watu hao, 1,165 ni wanaume na 2,911 ni wanawake ambapo wote walipewa rufaa kwenda katika vituo vya kupatiwa dawa za kupunguza makali ya VVU nchini.

Katika taarifa iliyotolea na kamati hiyo imesema watu hao wataanza tiba ya huduma ya kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU na katika Manispaa hiyo kuna jumla ya vituo 17 vya kupata vidonge hivyo.

Imesema kwa sasa katika vituo hivyo wameshafikia wagonjwa 12,829 ambao wamejiandikisha.

Pia taarifa hiyo ilidai kuwa kwa sasa wagonjwa wanaotumia dawa hizo ARVs ni 7,033 huku wengine wakiendelea na huduma za uchunguzi na ufuatiliaji na endapo CD4 zitashuka chini ya 200 wataanzishiwa dawa.

Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa manispaa imetenga kiasi cha Shilingi. milioni 109.9 ili kuimarisha vita dhidi ya kuenea ugonjwa huo katika kipindi cha mwaka wa fedha unaoishia Julai mwakani.
 
Sidhani kama ni maambukizi yaliyotokea ndani ya miezi hiyo mitatu, bali ni watu waliokuwa nao tangu huko nyuma lakini wamegundulika katika kipindi cha miezi mitatu. Anyway! sijui ni nini kifanyike, manake hata udhibiti wa mambo haya ni mgumu sana. Labda guest house zote zifungwe, manake wengi tunagawana ukimwi huko.
 
Jamani, kwanza nawasalimuni wote, mimi mgeni (new comer).

Kwa hili tatizo la UKIMWI, nashauri tu tuache njia zetu mbaya (matendo maovu) na kumrudia Mungu. Kama upo kwenye ndoa tulia na mwenzi wako huyo huyo, tuache tamaa za kutaka huku na kule, tutakwisha!!!
 
wakuu hiyo idadi ni ndogo ukilinganisha na idadi ya watu waliopo katka chuo kimoja mjini mosh, na maambukiz yanayorekodiwa kila mwez kupitia hospital kadhaa! Taarifa zinatisha,hasa baada ya wale watoto wa mama kik kuletwa pale kwa wing mwaka juz na jana!. Yaan inasemeka kila watu 5 walipo 3 wamepata kitu! Mazee tujal afya zetu! Tujal wanaotuzunguka.
 
Ama kweli tumwombe Mungu kwa sana kwa sababu ukimwi utatumaliza ee Mungu tuongoze kukabiliana na hili janga
 
Jamani, kwanza nawasalimuni wote, mimi mgeni (new comer).<br />
<br />
Kwa hili tatizo la UKIMWI, nashauri tu tuache njia zetu mbaya (matendo maovu) na kumrudia Mungu. Kama upo kwenye ndoa tulia na mwenzi wako huyo huyo, tuache tamaa za kutaka huku na kule, tutakwisha!!!
<br />
<br />
we unaweza kukaa ndoani?
 
guest mitaani kwetu ni zaidi ya nyumba za kawaida za watu,hii inshu ni ngumu sana,madanguro kila sehemu na sio siri tena kwa mambo yanafanyika waziwazi
 
Tuepuke Mipango ya kando! Tule "chakula" mezani tena nyumbani tu!
Biashara ya kando imekuwa noma Mazee
 
Aliyeambukizwa last month anaanza dawa next month? Sema wamepimwa na kukutwa na maambukizi!

Nani alisema humu ndani kuwa HIV haileti Ukimwi?
 
Kwani kuna mtu hafi? Ngoma ni kisingizio tu! Sema isikie kwa jirani tu! Walaji Tujipe moyo hivyo
 
Back
Top Bottom