Kama hawakuridhiswa na Zanzibar Chadema basi Wavunje Muungano.

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=1]Baraza la Wawakilishi(BLW) na Smz Roho ya Zanzibar na moyo wa Znz inawaangalia nyiyi ktk hatma ya Zanzibar na kizazi cha badae.[/h]Written by amini // 16/11/2011 // Habari // No comments


ROHO YA ZANZIBAR NA KIZAZI CHA ZANZIBAR KINAWAANGALIA NYIYI.

[caption id="attachment_33886" align="alignnone" width="300" caption="Zima ya Z,bar iko juu yenu power iko kwenu."] [/caption]
Sio wakati tena hivi sasa wa wajumbe wetu kutafautiana au kutupiana lawama kwa mitazamo ya chama , Zanzibar hivi sasa iko hali mbaya na inahitaji umoja na mshikamano na uzalendo wenu smz ikiwa wazee yani Baraza letu la uwakilishi na Smz litayumba basi tujuwe Zanzibar itakuwa tumeshaipoteza na historia ya kizazi cha Wzanzibar kitakuja kuwahukumu.
Nilazima wawakilishi wetu wajuwe majukumu yao na kazi zao walizo chaguliwa na wananchi ,uongozi ni zima mbele ya Allah na kila mchunga ataulizwa kwa alicho kichunga, hivi sasa wananchi wa Zanzibar hawana nguvu yoyote wamebanwa na sauti zao hazina nguvu , nguvu zote ziko kwa voingozi wa Baraza la uwakilishi na wao ndio wenye kubebe zima ya Zanzibar na kizazi cha wzanzibar kusambaratishwa.
Jee viongozi wetu muko tayari kuiona Zanzibar iko powerless kama wanavyo ota Chadema? Hivi sasa Chadema wanajitahidi kuwa Zanzibar ingizwe ktk mchakato wa katiba kama chama cha upinzani na sio kama nchi ilioungana ukapatikana Muungano .
Utata huu wa Chadema umekuja kutokana na mfumo mbovu wa Muungano tulio nao maradhi yake kukuwa na kupatikana kero kubwa za Muungano , vigezo vya Chadema nikuwa Zanzibar sio nchi kama vile Tanganyika sio nchi.
Hii wazanzibar wawakilishi wetu Serekali yetu ya Smz hii wanayo ihubiri Chadema nihatari kwa mazara ya uhai wa Zanzibar, Zanzibar ni nchi yenye watu kidogo na ardhi ndogo pindipo tukiruhusu kuwa Tanzania ni nchi moja na Zanzibar ikawa haina hadhi yoyote basi Wallah kizazi cha Zanzibar kitakuwa na wakati mgumu na huenda kikapotea.
Sikweli kuwa Chadema hawajuwi kuwa Tanganyika haijafa ipo na nguvu ya Tanganyika ipo pale pale, hakuna ilicho lose au kupoteza Tanganyika ipokuwa jina tu, nikama Zaire kuita Kongo.
Lakini nguvu ya Zanzibar haipo Zanzibar ya zamani sio hii ya leo , Zanzibar imekuwa powerless haiwezi hata kujiamulia mambo yake ya ndani kama haijapata izini kutoka Bara na ikionekana jambo hilo halina maslahi kwa Bara hata kama lina maslahi na Zanzibar linapingwa.
Zanzibar ni nchi jina tu nguvu kubwa yote iko Bara na Bara na Tanganyika katika mwevuli wa Muungano wa Tanzania imekuwa ikifaidika zaidi ktk ulimwengu wa kimataifa kuliko Zanzibar ambayo ilikuwa dolo kamili nchi na mambo yake.
Sasa sikweli Chadema na Wtanganyika kuwa Tanganyika imekufa, iliokufa ni Zanzibar kuwa haina uezo wowote ispokuwa jina tu, na kama nikusulubiwa Zanzibar na kuhukumiwa kutokana na kifo cha Tanganyia ? Jee Tanganyika iliuliwa na wzanzibar au nikifo chakujitakia wenyewe? Bunge la Tanganyika lilipokaa na kuamua kuiuwa Tanganyika hakuna Mzanzibar yoyote alio shirikiswa au kushauriwa kuhusu kufa kwa Tanganyika.
Sasa vipi leo Chadema mutugeukie sisi Wzanzibar na kusema kwa vile Tanganyika imekufa na nilazima na Zanzibar ife? Kufa kwa Zanzibar nikuvunja Muungano, sizani kuwa Wzanzibar wote wako tayari kuona Zanzibar imeyayukoa na wote kuwa Watanzania.
Kuna hatari ya kuletewa mambo huko mbeleni tusio yapenda kwanza jamii yetu ya kizanzibar na nchi yetu ni ndogo na yenye watu kidogo ukilinganicha na mkoa moja tu wa Bara, tafauti yetu sisi na mkoa nikuwa sisi ni watu tulokuwa na taifa letu na watu wake.
Isichukuliwe watu wa mkoa wa Murogoro million 2 wakalinganishwa na Zanzibar na tukasulubiwa kuitowa nchi yetu no. Samani ya nchi yetu na udogo wake nitafauti na mkoa wa Murogoro wenye watu wengi kuliko Zanzibar.
Kama mawazo ya Chadema nikama mawazo ya Wtanganyika wote basi nibora kuvunja Muungano na tukawa nchi mbili zenye ujirani mwema hatuko tayari kutaka tuisalimishe Zanzibar yetu ,hayotulokwisha salimicha yanatocha Rais wetu kuvuliwa umakamo wa Rais na kushiriki ktk vikao vya mawaziri na kuwa mjumbe na Waziri asio na wizara malumu.
Hii nizarau yamwisho kwa yeye mwenyewe na Zanzibar nzima hichi nikitendo cha aibu na hakuna nchi hata moja ikubalio hivyo kupiga magoti Raisi wao , kama Chadema wanasema Zanzibar imepewa sehemu kubwa ktk mchakato wa katiba ya Muungano? Basi sisi Wzanzibar tunaona Zanzibar bado haijadendewa haki ktk maswala ya katiba ya Muunganio.
Kifupi sisi ilikuwa tuingizwe ktk mchakato kama nchi kujadili mambo yalio tunganicha na kukubali kusema hili tuna litaka au hili laa tujatiliane, sio kuingizwa kutokana na nguvu ya wabunge ktk Bunge la Muungano kama fikra Zao ya uchoyo na uchu Chadema.
Swala hili la katiba sisi Zanzibar hatujiwakilishi kichama tunajiwakilicha kinchi kwa maslahi ya Zanzibar na Wzanzibar wote, kwa vile ni suala la mambo ya Muungano basi nilazima tujadili hatma ya pande zote mbili zilizo ungano ktk mambo yao ya Muungano.
Kama Chadema wanahisi sio haki kwa vile Wabunge kutoka Zanzibar siwo wengi ktk Bunge kuliko wao sisi tuko tayari kuuondosha utata huu na mizozo hii ya kila mtu kujihisi hatendewi haki na njia yake ni fupi tu nikuvunja Muungano na ikawa mataifa mawili kama hapo mwanzo.
Na wasahau wana siasa wa Bara kuzani kuwa sisi Wzanzibar hatuwezi kuvunja Muungano au kufika siku kuisarenda Zanzibar kutokana na wafanya biashara au Wzanzibar waloko Bara, hili nijambo dogo .
Wzanzibar wako kila nchi na hizo nchi sio kama ziko ktk Muungano wa Tanzania laa, kwa hio sizani kuwa hicho kitakuwa kigezo cha kututicha au kutufanya tusalimu ambri no, wao hawajakatazwa kuja kukuza biashara Zao Zanzibar na hata wakiwepo huko basi watafuata sherea zote za nchi kama nikuomba uraia au kuishi kama wageni na kufuata taratibu za kisheria kama vile wachina na wasouth Africa waloko huko.
Na wabara watakao kuweko Zanzibar basi itakuwa ni hivyo hivyo na tutaishi kwa ujirani mwema sizani kuwa hii itakuwa nitatizo la kuwazibu Wzanzanzibar kutokana na kuvunjika kwa Muungano? Muungano ilikuwa ni hiari tu ya Mwalimu Juliasi na Mh Abedi A Karume kwa hio kama wataona wananchi waupande moja hawakuridhishwa na mambo ya Muungano nawakataka kujitenga basi Chadema muko right kuvunja Muungano pindipo upande moja wa Muungano unajihisi unazulumiwa.
Laa ikiwa Chadema Muungano wana utaka lakini wanataka inakamize nchi ya Zanzibar kutokana na udogo wan chi yenyewe na watu wake Basi sisi Wzanzibar tuko tayari kwa hilo kuvunja Muungano na hilo nazani nihaki yetu lakini tumebanwa na Jeshi lenu na hio katiba fake.
Kwanza Chadema walitaka wajuwe uhalali wenyewe wa Muungano ulivyo jee Wananchi wa pande zote mbili walishirikishwa ktk kuunganicha?a. b. Jee kabla yah ii katiba lipi lakujadiliwa mwanzo katiba au Muungano? Kwa sababu Muungano ndio wenye kero nyingi na kama hazijashuhulikiwa hizo basi misuguana na mivutano ipo pale pale mpaka itatuliwe au kuvunjwa kwa Muungano wenyewe.
Kutatua matatizo ya Muungano nikuwauliza wadau wote wa pande mbili za Muungano ni Muungano gani wanautaka au ikiwa upande moja utasema hautaki Muungano basi sio Zambi kujitenga.
Lakini hili limekuwa hofu kubwa kutokuwauliza wananchi na inabakia huu Muungano kuwa utata na wananchi kuhisi niwakulazimiswa bila ya ridhaa yao, ndio ukaona kuna vipengele vingi tu vyakubana kuwa Muungano usijadiliwe lakini chakuchangaza chama kimoja tu cha ccm ndio chenye kujadili Muungano hii sio haki.
 
Ndugu yangu Kakke, upi sasa msimamo wako? Je yupi kwenu (Zanzibar) ni hatari zaidi kwenu, yule anayewafunulia ukweli ambaye ni chadema/Lisu au yule anayewaonyesha / tenda kwa maslahi yake (ccm) akiwaonyesha kuwa anawajali kumbe anaweka mitego ya kuwaingizeni mkenge? Hivi tatizo liko wapi la chadema/Lisu, ni lugha aliyotumia kwenye hotuba haieleweki kwenu/au hata kwa ccm/na wengine pia? au maudhui? au mitizamo? au hamjasoma bali mmehadithiwa tu kuwa lisu kawadharau?

Ebu muwe na mtizamo dhabiti unaojitegemea, mijadala ya wabunge dodoma ya ccm, cuf, au hao wengine isiwatoe kwenye ajenda yenu ya msingi ilokuwepo hata kabla ya mchakato huu wa katiba mpya nayo ni kero za muungano. CCM ni wajanja msipoangalia watafanikiwa kuwatoa kwenye hoja yenu ya msingi kwa kuwafanya mjisikie mmepewa heshima kubwa sana kwenye huu mchakato wa katiba mpya na siku ya mwisho bado kero zenu zitakuwa palepale.

Nionavyo mie, Lisu kawasaidia kuwaambia kuwa ccm inawadanganya tu, haina dhamira ya kweli ya kuwaondolea kero za muungano. Mimi nimesoma hotuba ya Lisu mwanzo mwisho tena nikiwa nimetulia na sina upande, wabunge wengi hata wale wanaosema lisu arudishwe shule tena nionavyo mimi au wanasumbuliwa na itikadi au uwezo wao wa kuelewa mambo uko chini sana au wanajipendekeza kwa mamlaka, au basi wanashida binafsi mioyoni mwao.

Halafu pia haiingii akilini kabla ya siku ya kusomwa huo mswada wa katiba wabunge wa ccm wakae kwenye kikao kama kamati ya wabunge wa ccm hadi saa 6 usiku na kesho yake eti wabunge wa ccm wanaujali, wanajadili nini basi hapo wakati tayari msimamo wao walikwisha uweka na ndo huo tunauona. Watanzania wenzangu bara na visiwani tusicheze na maisha na maendeleo ya nchi yetu. Wakati sisi tunacheza na kupiga maktaimu wapo wenzetu wako very serious na maendeleo ya nchi zao.

Katika kusoma kwangu hotuba ya Lisu, katika kila kipengele amechambua kifungu cha huo mswada kisha akasema "....sisi tunapendekeza yafuatayo...." kwa mtu mwelewa na makini anawezakuona kumbe hajasema ni lazima yafanyike yafuatayo.... inamaana kunamajadiliano hapo yanaendelea. Sisemi kuwa kila pendekezo la hotuba ya Lisu basi ndo ni sawa... ila kwanini wana ccm na pengine cuf waje kwa jazba namna ile. No hiyo si sawa hasa kwa chama tawala na pengine hata wazanzbari ebu jaribuni kuisoma tena hiyo hotuba na muone katika positive attitude/mind

Ningekuwa mimi ni spika wa bunge kwanza nisingechukua upande ningekuwa kama referee maana hili ni jambo muhimu sana kwa historia ya nchi yetu kisha basi ningemwita kiongozi wa upinzani bungeni ofisini kwangu ningemskiliza mwanzo hadi mwisho, ningemwita Lisu naye pekee yake ningefanya hivo hivo, halafu ningetumia nafasi yangu kuchukua hoja muhimu na ningeitisha kamati tendaji/uongozi ya bunge ambayo ina viongozi wote wa kamati za bunge na kisha ningewaagiza tuweke ushabiki na itikadi pembeni na let us discuss for our nation, kisha tufikie maamuzi ya pamoja

Mwisho nimalizie kuhusu Zanzibar, ebu jaribuni kuelewa hotuba kwa mtizamo chanya, is not about kudharauliwa but about the future of the two nations (Zanzibar and Tanganyika) then toeni maoni ya kujenga pande zote mbili na tuitake ccm wote kwa pamoja kuwa wawazi na wakweli kuhusu muungano na zanzibar and Tanganyika, na pande zote mbili tuache kunung'unika let us face the reality and work out our differences according to the current material time.
 
Mchakato wa kuvunja muungano ndio umesha anza hivyo, kwani wewe huoni au unataka mpaka uambiwe kua muungano utavunjika. Labda nikurahisishie kwa kusema hivi, jinsi ccm na cuf wanavyoendesha mambo yao ndio wanaupeleka muungano kaburini na mpaka sasa wamesha ufikisha icu.
 
[h=1].Utata huu wa Chadema umekuja kutokana na mfumo mbovu wa Muungano tulio nao maradhi yake kukuwa na kupatikana kero kubwa za Muungano , vigezo vya Chadema nikuwa Zanzibar sio nchi kama vile Tanganyika sio nchi. Zanzibar ni nchi yenye watu kidogo na ardhi ndogo pindipo tukiruhusu kuwa Tanzania ni nchi moja na Zanzibar ikawa haina hadhi yoyote basi Wallah kizazi cha Zanzibar kitakuwa na wakati mgumu na huenda kikapotea.
Contradiction tupu. Kwamba mambo wanayozungumza chadema yanatokana na mfumo mbovu wa muungano tulio nao; kwa hiyo mwandishi anatueleza kuwa mfumo tulio nao ni mbovu; Katika hatua nyingine anatujuza kuwa mfumo uliopo ukibadilishwa zanzibar itapata shida kutokana na ardhi ndogo na watu kidogo; kwa mantiki hayo mfumo uliopo unaifaa zanzibar!Hapo ndipo contradiction inapokuja; huku mfumo ni mbovu, huku unawafaa! Mwandishi unapaswa kujua kuwa kama unautaka muungano then uwe tayari kupoteza baadh ya vitu kwa manufaa ya muungano; siyo zanzibar unavyotaka iwe -ina ardhi ndogo, watu kidogo lakini unataka bado iwe nchi yenye maslahi sawa na tanganyika yenye watu wengi na ardhi kubwa! Ndiyo maana utasikia watu wanasema muungano uvunjike kwanza then uundwe upya kama ni lazima kwa mfumo ambao tutakubaliana pamoja, siyo huu wa sasa wa Nyerere kuogopa eti kutokana na udogo wa zanzibar serikali moja ingeonekana tanganyika imeimeza zanzibar! Nawashukuru wazanzibari waliopeleka barua UN kutaka muungano uvunjike!
 
Usipoziba ufa hutajenga ukuta... Ni heri akuambiae ukwel kuliko akuachae kinafki fikra akijua unaingia shimon... 2ache ushabik let us avoid mapema whats so called KERO ZA MUUNGAANO, achen ushabik wabunge wa CCM na CUF Kesho yake mnarud oooh.. MUUNGANO UU UNAPENDELEA WAP SIJUI.... Acheni UNAFKI MTARAANIWA.
 
Back
Top Bottom