Kama haumo humu wewe si Fisadi!!

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Kama kwenye Orodha ya mambo haya au matendo haya wewe haumo basi jua wewe si fisadi bali ni mtu safi!!!

  1. Kama hujawahi kununua mtihani ili ufaulu
  2. Kama kwenye fomu ya maombi ya kupata mkopo wa elimu ya juu hujaandika kwamba wewe kwenu mna nyumba ya Udongo (wakati ya kwenu ni ya matofali tena imeezekwa bati) au wewe ni Yatima wakati wazazi wako wako hai
  3. Kama hujatoa rushwa ili upate kazi uliyo nayo sasa
  4. Kama hujachukua hela za mradi unaousimamia na kujengea nyumba au kununulia gari
  5. Kama unalipa Kodi kwa kila pato unalolipata.
  6. Kama hutumii madaraka uliyonayo kwa manufaa yako binafsi.
  7. Kama hujaomba rushwa ili utoe huduma unayoistaili kuitoa kwa mujibu wa kazi yako
  8. Kama hujaghushi jina unalotumia kupatia ajira
  9. Kama ulipojenga si eneo la kijamii ila wewe umelipora
  10. Kama hutumii vifaa vya ofisi ya umma kwa shughuli zako binafsi
  11. Kama huzidishi thamani ya gharama ya vitu unavyonunua kwa ajili ya ofisi ya umma unayofanyia kazi
  12. Kama hupati mgao kutokana na ufisadi unaofanywa kwa jamii
  13. Kama wakati wa kazi za umma wewe uko kwenye supu au shughuli zako binafsi.
 
Mhhh napita tuu hapa nitarudi baadae maana duh kuna vingine vinanigusa ila sio wizi wa mtihani wala kusema kudanganya kwenye form ya mkopo wa chuo au kutoa rushwa kupata ajira au kughushi jina ninalotumia ila no tano hiyo ni noma sana
 
Mkuu naona kama umeamua kunishambulia mimi. Itakuwaje katika vipengele vyote 13 nikidhi 10?
 
Kati ya hivyo vyote mimi nimo na zaidi ya hayo_hivyo ninaweza kuwa nimevuka viwango wa ufisadi na kwa maana hiyo mimi sio fisadi.
 
"Man is conceived in sin and born in corruption and he passeth from the stink of the didie to the stench of the shroud. There is always something." - Robert Warren Penn, All The King's Men.
 
Wewe ni gamba na fisadi mkubwa unayetaka kuonyesha jamii kwamba we are all sinners na hivyo tuachane na kupinga ufisadi. Shame on you
 
Ikiwa hayo uliyoyasema ndiyo ufisadi basi hakuna asiye fisadi. Kila mtu anaweza kuwa fisadi kwa mfano,

Ni watu wangapi mpaka leo hii wamesomeshwa na bodi ya mikopo lakini wamefight ili wasilipe?
 
Kama kwenye Orodha ya mambo haya au matendo haya wewe haumo basi jua wewe si fisadi bali ni mtu safi!!!

  1. Kama hujawahi kununua mtihani ili ufaulu
  2. Kama kwenye fomu ya maombi ya kupata mkopo wa elimu ya juu hujaandika kwamba wewe kwenu mna nyumba ya Udongo (wakati ya kwenu ni ya matofali tena imeezekwa bati) au wewe ni Yatima wakati wazazi wako wako hai
  3. Kama hujatoa rushwa ili upate kazi uliyo nayo sasa
  4. Kama hujachukua hela za mradi unaousimamia na kujengea nyumba au kununulia gari
  5. Kama unalipa Kodi kwa kila pato unalolipata.
  6. Kama hutumii madaraka uliyonayo kwa manufaa yako binafsi.
  7. Kama hujaomba rushwa ili utoe huduma unayoistaili kuitoa kwa mujibu wa kazi yako
  8. Kama hujaghushi jina unalotumia kupatia ajira
  9. Kama ulipojenga si eneo la kijamii ila wewe umelipora
  10. Kama hutumii vifaa vya ofisi ya umma kwa shughuli zako binafsi
  11. Kama huzidishi thamani ya gharama ya vitu unavyonunua kwa ajili ya ofisi ya umma unayofanyia kazi
  12. Kama hupati mgao kutokana na ufisadi unaofanywa kwa jamii
  13. Kama wakati wa kazi za umma wewe uko kwenye supu au shughuli zako binafsi.

Duu nimo nyavuni
 
"Man is conceived in sin and born in corruption and he passeth from the stink of the didie to the stench of the shroud. There is always something." - Robert Warren Penn, All The King's Men.

Wewe si huwa unasema hakuna Mungu? sasa neno sin umelitumia kwa misingi ipi?.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
Back
Top Bottom