Kama facebook wataanzisha huduma ya mobile money.Je Mpesa na Tigo-pesa zitabaki salama?

MAHENDEKA

JF-Expert Member
Jul 9, 2010
306
152
Wakuu kuna kitu huwa nakiwaza sjui nyie mnaonaje?

Hiv facebook na whattsap wakilaunch project yao ile ya kutuma pesa popote duniani itakuaje? Mitandao ya simu hususan kwetu hapa watafanyaje?

Nakumbuka Mark Zuckenberg alikuja Kenya juzi juzi kujifunza namna mobile money inavofanya kazi ili aweze kuiweka kwenye website yake ya facebook na kwenye whattsap ambazo kwa kiasi kikubwa zinatumia data.

Watu si watahamia huko kabisa? Sipati picha mtu anaeza kutuma pesa kwa facebook na whattsap kwa bei sawa na bure(free), Mpesa, Tigo pesa na Airtel money zitaweza pambana na facebook na whattsap sokoni ? si zitakosa watu halafu mwishowe zitakufa?.Akina nani watabakia nazo ?

Siku hizi kupiga simu kwenda mataifa ya nje ni kwa skype tu au whattsap na viber na ni bei ndogo kuliko kutumia simu kawaida (voice) na unaweza fanya video call na video conference kabisa.

Haya mambo ya kununua dakika na sms haya mnayaonaje yana muda mrefu kweli?, mtazamo wangu biashara ya voice kwa kadri siku zinavyokwenda imeshaanza kua irrelevant

Mtu una simu ya tochi unanunua kifurushi vodacom/tigo unapewa dakika za kuongea na mb juu sasa za kazi gani?
 
Watanzania wangapi wanatumia facebook na Whatsapp mpaka ziue mobile money?

Afu ana intergrate Mobile money kwenye hizo media ili tukitumiana hela tukaitolee wapi?

Niliona facebook messenger tayari ina payment gateways kwa watu wa US,je ni kwa kiasi gani imekua tishio kushinda makampuni mengine yanayo process malipo ya Online?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom