Kama Dowans walitoa Huduma kwa kiwango cha makubaliano walipwe kwa hilo

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,551
8,642
Watanzania pamoja na kuwa na mapambano na ufisadi ni lazima tuwe wa wazi na watu wenye kufuata sheria kama tuntaka maendeleo ya nchi yetu. Mimi sielewi hili swala kwa kina sana lakini kama mambo yako kama ninavyofikiria chini basi inabidi Dowans walipwe.

1. Kama malipo ni ya huduma tu iliyotelewa. Hii ni umeme uliouzwa kwa Tanesco kwa rate ambayo walikubaliana.
2. Hakuna kulipa riba wala pesa ya kukatisha mkataba.

Hatuwezi kukutaa kuwalipa Dowans kwa huduma waliyoitoa wakati tunawalipa kampuni nyingine. lakini malipo yasihusishe riba ya deni na faini nyingine kama za Lawyer na kutatisha mkataba. Hatuwezi kuwa na serikali inayo rusha watu haki zao hata kama mkataba ulikuwa badili Tanesco isingenunua umeme. Mfano kama kuna kituo cha mafuta ambacho kinafanya kazi bila kibali serikali inatakiwa kukifunga na kupiga faini lakini sio kuchukua mafuta ya kituo hicho bila malipo hiyo siyo sheria.
 
Kawalipe hela zako mwenyewe na wala usije ukatushirikisha katika zoezi lako hilo mpaka mwisho wake. Yeyote atakayeilipa mrithi wa KAMPUNI HEWA hapa shauri yake.
 
Watalipwa na hamna kitachotokea.........kelele nyingi tu, valangati hamuwezi!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom