Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
M. M. Mwanakijiji (Tanzania Daima Jumatano)
SIPENDI kweli watu wenye kuamini kuwa hawawezi. Na sipendi zaidi viongozi ambao wanatumia lugha ya kutokuweza. Leo hii tumeanza kutukuza kutokuweza na kuanza kuamini kama imani ya kidini.
Wapo kati yetu wagombea ambao wanatuhubiria kuwa hatuwezi na wapo wananchi ambao wanarudia kauli hii kana kwamba wamekula yamini kuwa wasiporudia basi makubwa yatawakuta.
Na kinachoniudhi ni hoja kwamba hatuwezi kuwapatia watoto wetu elimu ya bure hadi kidato cha sita na kuhakikisha kuwa kila kijana wa Kitanzania anayetaka shahada ya kwanza anaweza kuipata.
Wanasiasa, mashabiki wao na baadhi ya watu wanataka tuamini uongo kuwa haiwezekani kuwapatia watoto wetu elimu ya bure. Wanasema hivi kwa kujiamini na kama kwa kujisifia. Lakini watu hawa hawa tukiwabana kuwauliza wanakuja juu na kudai mengine yanawezekana.
Ni hawa hawa waliotuambia kuwa hatuwezi kuendelea bila wawekezaji na hivyo wameendelea kupiga magoti katika madhabahu ya wawekezaji na ni hawa hawa waliotuambia kuwa hatuwezi kuwalipa wafanyakazi wetu mishahara minono yenye kuendana na hali ya uwezo wetu wa kiuchumi. Na ni hawa hawa ambao wanarudia kutuambia kuwa hatuwezi kupigana na ufisadi!
Ati kuwapatia watoto wetu elimu ya bure haiwezekani lakini mengine ya kwao yanawezekana!
Wao wameweza kununua dege la Rais kwa karibu bilioni 50 kwa ajili ya matumizi ya mtu mmoja na kikundi cha watu wachache wenye uwezo wa kukodi.
Hata tungemuuliza msimamizi wa ndege za serikali atuambie ni kiasi gani cha gharama ya ununuzi wa ndege hizo kimeweza kurudi karibu miaka kumi baada ya kununuliwa na itachukua muda gani tutaweza kukirudisha?
Tulipowaambiwa kuwa haiwezekani wafanye hivi walikuwa juu na mmoja wao akatuambia kuwa ati hata kula nyasi tutakula lakini serikali itaweza kununua dege hilo! Kuwapa watoto wetu elimu ya bure ati haiwezekani!
Wakanunua rada ya kijeshi ambayo kwa nchi yetu tungeweza kupata rada nyingine bora zaidi. Tena wakanunua kwa bei ya kuruka wakiwa na suti zao na tai tena kwa mbwembwe! Kwa shilingi nyingine karibu bilioni 40 wakanununa rada hiyo. Tukawapigia kelele na kusema haiwezekani fedha hizo tungeingiza kwenye elimu na kusaidia watoto wetu. Wakatubeza na kudai kuwa sisi nchi huru tutafanya tunalotaka bila kuingiliwa na nchi yoyote. Kumbe wakatuambia ati tunaweza! Kuwapa watoto wetu elimu ya bure wanasema haiwezekani!
Wakajenga uwanja wa Taifa wa Mpira wa Soka kwa mbwembwe kwa shilingi nyingine bilioni 50 ambao hadi hivi sasa sikumbuki ni lini umeweza kujaza maelfu ya watu maana hata mechi ya Brazili ilishindwa kujaza watu! Uwanja huo mzuri na wenye kusifiwa ukiwa na vikolombwezo vya kila aina uko kilomita chache tu kutoka shule zenye madirisha mabovu na nyingine bado watoto wake wakisoma kwenye vumbi! Tukiwauliza tuliwezaje kufanya hilo wanatuambia kwa sababu tunaweza. Lakini kuwapa watoto wetu elimu ya bure haiwezekani.
Ni hawa hawa chini ya utawala wao ambapo wizi mkubwa wa zaidi ya bilioni 133 ulitokea na upotevu mwingine wa mabilioni ya shilingi kutoka Benki Kuu. Katika ujanja wao wanaoujua wao wakaweza kurudisha kama bilioni 60 (msiniulize zilitoka wapi, kwa nani, zilirudishwa vipi na wapi). Na hapo hapo wakazisamehe bilioni nyingine nyingi huku kesi za wahusika zikiendelea kuzunguka taratibu katika baraza la haki. Ndipo tukajua kuwa kuna fedha nyingi tu zimechezewa na wajanja benk kuu. Yote hayo yaliwezekana. Lakini kuwapa watoto wetu elimu ya bure ati haiwezekani!
Na ni watawala hao hao walioshindwa ambao walisimamia chini yao makampuni hewa yaliyochotewa mabilioni ya fedha na hadi hivi sasa hawataki hata kuyazungumzia kwenye kampeni zao. Makampuni ya Meremeta, Tangold, Deep Green, n.k yote yalishirikiana kuchota mabilioni ya fedha kama vile kisimani na yakatokomea huku wahusika wake wakipigiwa kampeni kurudi tena Bungeni na wengine wakipewa pongezi mbalimbali za kutulizwa. Karibu bilioni 200 zimetoweka hivi hivi kupitia mikono ya wajanja hawa. Hilo linawezekana. Lakini kuwapa watoto wetu elimu ya bure ati haiwezekani.
Ni hawa hawa ambao wameweza kutenga mabilioni ya shilingi kila mwaka kwa ajili ya samani na chai katika maofisi yao katika kile wanachokiita kukirimia wageni. Mwaka mmoja tu uliopita walitenga bilioni 30 hivi za chai! Ati hilo linawezekana! Watawala wetu wanatuamini kuwa ipo haja ya lazima sana kutenga kiasi hicho cha fedha lakini upande wa pili wanawaambia watoto wetu kuwa haiwezekani kuwapatia elimu ya bure kwa sababu Taifa halina fedha!
Niseme nini tena? Nirudie mifano gani mingine ya upotevu wa karibu shilingi trilioni 3 katika miaka hii michache tu iliyopita. Niseme nini kuhusu matumizi ya Halmashauri, Taasisi na Wakala mbalimbali? Niseme juu ya kiasi kinachotengwa kwa ajili ya posho za vikao si mtazimia? Mnataka nikumbushe posho wanayolipwa mawaziri, wabunge na watendaji wa serikali wanaposafiri ndani na nje ya nchi? Niseme kuhusu ununuzi dege la Airbus? Nikumbushie suala la mikataba ya umeme (Richmond, IPTL, Dowans n.k)? Nirudie kwenye suala la mikataba ya madini kuanzia ya Buzwagi? Mnataka nigusie mauzo ya mbuga zetu na nyara zetu? Au mnataka nizungumzie upotevu wa utajiri wa Tanzanite na Dhahabu yetu?
Yaani yote hayo yanawezekana chini ya watawala wetu walioshindwa isipokuwa suala la kuwapa watoto wetu elimu ya bure?
Lakini kipo kingine kinachoniudhi mimi zaidi. Wapo watu kati yetu ambao kweli wanaamini haiwezekani. Nimemuona mwandishi mmoja juzi kwenye kipindi kimoja cha TV akishangaa inawezekana vipi? Nimewasikia watangazaji kwenye radio moja nao wakihoji hilo linawezekana vipi? Yaani, wapo watu kati yetu kabisa ambao wanaamini haiwezekani kuwapa watoto wetu elimu ya bure na kuwaandaa kwa elimu ya juu! Naam wapo wagombea urais, ubunge na udiwani ambao wanaamini haiwezekani!
Sasa ninajiuliza kama hawa watu wanaona haiwezekani kutumia kila aina ya uwezo na raslimali zetu kuwapatia watoto wetu tunu na zawadi na haki ya elimu tutumie fedha zetu kwa vitu gani? Naam! Tunajua baadhi ya vitu tunavyotaka kutumia fedha hizo. Lakini inakuwaje mamilioni ya watu wetu wanaamini uongo huu na kuukumbatia?
Ndugu zangu, wapiga kura wa Tanzania wamepewa uchaguzi mwepesi kweli na wa moja kwa moja. Vijana wa Tanzania wamepewa uchaguzi huo na wazazi wa Tanzania wamepewa uchaguzi huo huo. Kwamba waendelee kuchagua watu wenye fikra za kutokuweza kutoa elimu ya bure kwa watoto wetu au kujaribu wale wanaoamini kuwa wanaweza kufanya hili.
Kwa wale ambao wanajua haiwezekani ni lazima wachague CCM na wagombea wake wote kwani watakuwa wamepigia kura kukata kwao tamaa!
Watakuwa wamepigia kura kutokujaribu na kutokuweza. Kwa kadiri ya kwamba CCM haitaki kuamini kuwa elimu ya bure inaweza kutolewa (aidha kwa kuwaogopa IMF au Benki ya Dunia miye sijui) basi wamechagua kuwa chama cha kutokuweza.
Wanachama na mashabiki wake lazima washangilie na kuchekelea kutokuweza huku. Wale wote wanaoamini kuwa hatuna uwezo wa kutoa elimu bure kwa watoto wetu ni LAZIMA wachague CCM kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wamefuata dhamira zao.
Kwa wale ambao wanaamini inawezekana kufanya hivyo na kuwa tunao uwezo wa raslimali wa kuweza kutoa elimu ya bure kwa watoto wetu uchaguzi wao nao uko wazi na watatakiwa kufuata mioyo yao. Kuna vyama viwili ambavyo vinaahidi elimu ya bure.
Wapo CUF na wapo CHADEMA. Linapokuja suala muhimu kama elimu ambalo kwangu naamini ni muhimu sana basi mpiga kura ni lazima ajiulize je nataka mtoto wangu asome bure hadi kidato cha sita au chuo kikuu?
Akijibu ndiyo basi ni lazima achague mojawapo ya vyama hivyo kuendana na ajenda zao nyingine. Na akisema hapana kwa sababu haiwezekani ni lazima achague CCM. Ni chaguo la kimantiki.
Wanasema kwa mapozi, hili haliwezekani,
Kama wao hawawezi, kura waomba za nini?
Kama hili kwao kazi, tuwachague kwa nini?
Nawauliza jamani, si bora waje wengine?