Kama Bagenda, huyu naye anataka kumtapeli Kikwete?

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
6,376
6,708
IMG_1953.JPG

Tapeli aitwaye Novatus Mutoka na kitabu chake cha "HARAKATI ZA DKT JAKAYA KIKWETE KATIKA KUMUENZI MWL JK NYERERE" mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo ofisini kwake mkoani Dodoma

Kwa wanaokumbuka kitabu cha hovyo cha "Tumaini Lililorejea" kilichoandikwa na Prince Bagenda akijikomba kwa Kikwete ili amkumbuke kama alivyofanya kwa Salva Rweyemamu, wanajua kilichofuatia. Bagenda akiwa msomi lakini mjinga, aliandika kitabu cha sifa za uongo sawa na Julius Nyang'oro ambaye hivi karibuni alikutikana na kashfa ya kughushi.

Naona sasa amejitokeza tapeli mwingine pichani aitwaye Novatus Mutoka ambaye eti ametunga kitabu cha kueleza Kikwete alivyomuenzi Nyerere! Ama kweli akutukanaye hakuchagulii tusi. Kikwete anaweza kumuenzi Nyerere kwa madudu anayofanya?
 
Angalia kijiofisi chake kinadhihirisha bila Shaka yeyote kuwa Bwana Huyu njaa inamuuma, njaa Haina umri ndugu zangu.
 
Kumbe Mzee Yusuf Makamba aliona mbali sana, maana nadhani yeye ndio muhasisi wa sanaa hii ya kuandika vitabu vya kumpamba huyu Given PHD.

Ni aibu sana kama JK Nyerere alikuwa anaandika vitabu yeye mwenyewe na kwenda pale Nkrumah Hall UDSM kupata challenge za wasomi leo aje kufananishwa na huyu Kikwete, nadhani sasa Mwalimu Nyerere foundation lazima walinde maadili na jina la Nyerere lisitumike tena na waganga njaa kutimiza agenda zao za utapeli.
 
Pengine kapewa tenda ya kuandika ili angalau kuwepo na kumbukumbu zake kwenye dunia ya vitabu. Si unajua mpenda masifa alivo. Asiposifiwa hutafuta wa kumsifia.
 
Hivyo vitabu huwa vinananunuliwa na nani?
Duh! mkuu Matola, nchi iliyojaa rushwa na ufisadi kama hii usishangae kusikia viongozi njaa pale wizara ya Elimu waka lazimisha kitumike kufundishia somo la Uraia (Civics) kwenye shule za Kata (St.Kayumba).
 
Upande mmoja kuna mwakyembe, mwandosya, ulimboka, mwangosi mwingine ni hao akina bagenda, mutoka, rweymamu! Mmmh!
 
I think one side of the coin is the one which calls a spoon a spoon and the other side they call a spoon whatever!
 
Nimewasahau prof.mukandara, dr.bana and kuna wengine walio okoka kama dr.lweitama! Huyu ni dr wa ukweli si mnafiki!
 
IMG_1953.JPG

Tapeli aitwaye Novatus Mutoka na kitabu chake cha "HARAKATI ZA DKT JAKAYA KIKWETE KATIKA KUMUENZI MWL JK NYERERE" mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo ofisini kwake mkoani Dodoma

Kwa wanaokumbuka kitabu cha hovyo cha "Tumaini Lililorejea" kilichoandikwa na Prince Bagenda akijikomba kwa Kikwete ili amkumbuke kama alivyofanya kwa Salva Rweyemamu, wanajua kilichofuatia. Bagenda akiwa msomi lakini mjinga, aliandika kitabu cha sifa za uongo sawa na Julius Nyang'oro ambaye hivi karibuni alikutikana na kashfa ya kughushi.

Naona sasa amejitokeza tapeli mwingine pichani aitwaye Novatus Mutoka ambaye eti ametunga kitabu cha kueleza Kikwete alivyomuenzi Nyerere! Ama kweli akutukanaye hakuchagulii tusi. Kikwete anaweza kumuenzi Nyerere kwa madudu anayofanya?

Watanzania wa leo hawahitaji kuandikiwa maana wanayaona wenyewe hao wanaoandika wanapoteza muda tu
 
SATURDAY, OCTOBER 06, 2012

KITABU CHA HARAKATI ZA DKT JAKAYA KIKWETE KATIKA KUMUENZI MWL JK NYERERE CHAZINDULIWA RASMI LEO MKOANI DODOMA

Mwanaharakati Novatus Mutoka kutoka Mkoani Dodoma akiongea na waandishi wa habari (hawapo picha) leo mkoani Dodoma wakati akitambulisha kitabu chake kinachoitwa"HARAKATI ZA DKT JAKAYA KIKWETE KATIKA KUMUENZI MWL JK NYERERE" ambapo pia alielezea lengo la yeye kuandika kitabu hiko mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani)

Mwanaharakati Novatus Mutoka akionyesha kitabu alichoandika yeye kinachoitwa "HARAKATI ZA DKT JAKAYA KIKWETE KATIKA KUMUENZI MWL JK NYERERE" mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo ofisini kwake mkoani Dodoma.

SATURDAY, OCTOBER 06, 2012 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom