Kama bado waamini kuna waganga wa kienyeji wanaunga mifupa iliyovunjika...

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,240
4,466
Wazazi wa huyu mtoto hawakumtendea haki. Baada ya sangoma kushindwa kuunga mfupa, wakakimbilia kwa daktari bingwa wa mifupa.

image.jpeg

image.jpeg
 
Nadhani hiyo kisheria ni kosa na huyo mganga wa kienyeji ilibidi achukuliwe hatua za kisheria
Na utuambie huyo utalaamu wa kuwachomeka watu miti yeye amjifunzia wapi Na umethibitishwa Na Nani?

Serikali kama utakuwa inawakalia kimya watu kama hao itakuwa inapoteza watu wake wengi sana.
 
'Nimejaribu kuvaa kiatu cha huyo mtoto....
'nayahisi maumivu alio yasikia....
'kwani nahakika hakukua na ganzi'
 
Tutaaminije kwamba sangoma ndiye aliyesababisha hayo? Kama kuna chanzo cha taarifa kutoka mtandaoni tuwekee hapa link tupate maelezo ya kutosha ikikuwaje?
 
Mimi naamini kuna waganga wa kienyeji mataperi mfano ni huyo kwa huyu mtoto. Mimi nilivunjika mkono nikiwa mtoto mdogo baba alitupeleka ukweni maeneo ya Bupandwa huko Biharamulo na nikapata ajali wakati nabebea. Nilipelekwa Bugando (na ndiyo ilikuwa siku ya kwanza kupanda meli ya MV. Victoria katika bandari ya Nyamilembe Chato. (Nyumbani kwa wazazi ikiwa Geita), nilipofikishwa Bugando kutokana na maelezo ya baba ilitakiwa mkono ukatwe baba akanitoroshea Seketoure Hosp hata hapo akaambiwa nikatwe na ndipo bibi akatuma baba wadogo wanifuate Mwanza na nikachukuliwa huku uvimbe ushakuwa mkubwa. Nakumbuka bibi alikuwa ananifanyia dawa iitwayo "Bulabuka" kwa mafuta ya ng'ombe huku akichanganya dawa kwa mikono na kuipasha moto mikono yake (viganja) baadaye anaanza kuuga mifupa hewani pasipo kunigusa akisema kuwa akinigusa basi taoza huo mkono. Nilipona na hadi sasa huwezi kunitambua kama nishawahi kuvunjika mkono. Dawa za shamba zipo lkn mataperi ni wengi sana
 
Back
Top Bottom