Kalimanzila a.k.a Buraza "K"

Hofstede

JF-Expert Member
Jul 15, 2007
3,577
1,107
Kalimanzila ni mkazi wa Kasulu. Baada ya kupigika sana na njaa aliamua kuingia kwenye shamba la mihogo la jirani na kuchimba kiroba kimoja. Kabla hajaondoka mwenye shamba akatokea akiwa na upinde na kumwamuru asikimbie na kushikwa na kupelekwa polisi akiwa na ushahidi mkono. Kesi ilikuwa rahisi sana mahakamani kutokana na kuwepo kwa ushahidi, lakini kabla ya kuhukumu kesi hakimu alimpatia Kalimanzila nafasi ya kujitetea na mazungumzo yakawa kama ifuatavyo:

Hakimu: Mshtakiwa kalimanzila ushahidi upo wazi je una la kujitetea?

Kalimzanzila: Ngo, ndiyo hakimu ninataka kujitetea

Hakimu: endelea

Kalimanzila: ndugu hakimu ngo ninaomba kumuuliza maswali mwenye shamba

Hakimu: endelea

Kalimanzila: Ngo, je nilipokuwa nachimba mihogo shambani kwani ilikuwa lini?

Mwenye shamba: Ilikuwa jumatatu muheshimiwa hakimu

Kalimanzila: Ngo, hola, umekosa!! ilikuwa jumatano!

Kalimanzila: Ngo, je nilipokuwa nachimba mihogo nilikuwa nimevaa shati gani

Mwenye shamba: Jekundu mheshimiwa hakimu

Kalimanzila: Ngo, hola, umekosa!! lilikuwa jeusi

Kalimanzila: Ngo, muheshimiwa hakimu ni hayo tu, ngo nilitaka kuonesha kuwa mwenyeshamba, ngoananisingizia, ngo wote mneona ngo alivyokosa maswali yote, ngo kama alinikamata angejua siku na nguo niliyokuwa nimevaa!

Hakimu: kesi inaahirishwa mpaka itakapotajwa tena kwa ajili ya kusoma hukumu
 
Back
Top Bottom