Kakobe na tanesco tena

steering

Member
Nov 28, 2011
71
12
Kakobe aishukuru TANESCO

na Betty Kangonga

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBC), Zachary Kakobe, amemshukuru aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja pamoja na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kwa kutumiwa na Mungu kupitisha umeme juu ya kanisa hilo hatua iliyochangia kuwa na maono makubwa.

Akizungumza wakati wa kuzindua tovuti mbili za kanisa hilo juzi, Askofu Kakobe, alisema kuwa hatua ya serikali kupitisha umeme katika eneo hilo imempa changamoto zaidi katika kuhubiri Injili ulimwenguni, kupitia tovuti hizo za intaneti ambayo itaangaliwa na watu wengi zaidi kuliko ilivyokuwa kwa televisheni ya Holiness ambayo ingetazamwa na watu wachache.

Hata hivyo, alidai pamoja na kupitisha umeme juu ya kanisa lake lililoko Mwenge, jijini Dar es Salaam, hadi sasa hakuna nguvu ya umeme inayopita katika nguzo hizo namba 19 na 20, na kuwa kama umeme ulishindwa kupita katika makaburi ya machifu mkoani Iringa hata katika nguzo hizo hautapita kwa kuwa Mungu anayemhubiri ni zaidi ya hao machifu.

Askofu Kakobe aliingia katika mgogoro na TANESCO baada ya serikali kuruhusu upitishwaji wa umeme wenye msongo wa kilovoti 132 mbele ya kanisa hilo.
 
Tunaomba wataalamu w aTANESCO waje watudhibitishie kama umeme haupiti pale kwa kakobe!!
 
Mzee katoka mbali,
Enzi zake alikuwa na bendi ya muziki wa dansi kisha,
Recording Center kule Kariakoo,
Ikiitwa MULANGA Recording Center,
ambayo ilifungwa ghafla,
na tangu siku hiyo ni mhubiri.
 
Wewe ndio mwenye porojo, wala hujui unalolizungumza. Waulize TANESCO mara ngapi wamehangaika na nyaya hizo mpaka sasa wameacha tu. Kwa sababu ya kushindana na mtumishi wa Mungu. Kama umesoma vizuri hiyo habari aliyoandika Betty kuwa umeme pale haupo hata leo. Hivi huangalii yaliyowapata waziri wa Nishati na Madini pamoja na Katibu wake na sasa meneja wa Tanesco angalia sana maneno unyozungumza yatakudhuru.
 
Hyponotized!
 
ina maana TANESCO wanaumia rohoni na wanakufa kisabuni, kumbe umeme haupiti? kumbe nguzo ni geresha tu? inawezekana Kakobe amesahau kuwa Maombi yamesaidia Ngeleja na Mhando wametemwa kazi
 
Back
Top Bottom