Kakobe mtumishi wa mungu au tapeli;waumini kuandikisha malizao ,mishahara,

SIO NA SISEMI AMINA.....!

kuorodhesha mali ni utapeli...? Mbona serikali inahitaji watumishi wake waorodheshe mali zao? je na huo ni utapeli au UTAWALA BORA...?
QUOTE]

Aaah baba mahesabu, usijaribu kufananisha hata kidogo serikali na mambo ya kanisa. Kwanza ni vitu ambavyo haviendani kabisa. Kanisa ni masuala ya kiimani zaidi na serikali ni mambo ya siasa. Hata Yesu walimtega namna hiyo lakini aliwastukia mapema akawaauliza picha iliyopo kwenye sarafu ni ya nani? wakamwambia ni ya Kaisari..." Akawaambia ya kaisari mpeni kaisari na ya Mungu mpeni Mungu"
Sasa kakobe yeye mali za watu zinamuhusu nini? Kwani nini Lengo la kanisa lake? kuhubiri injili ili watu wamjue Mungu au kujua mali walizonazo watu.
Lakini pia hata kama waumini wake watajaza hizo fomu wanaweza pia kumdanganya.

MI nadhani anawapima waumini wake ni jinsi gani wanavyomuamini yeye na sio kumwamini yesu Kristo.
 
Last edited:
Na je akishajua kuwa nina kipatao kikubwa na sehemu ninayokaa akishirikiana na majambazi kuja kunivamia inakuwaje hapo!!!

zaka ama fungu la kumi ni wewe na mungu wako sio kwa askofu mimi ni mkristo ninajua nn maana ya zaka. Kakobe hapaswi kuwapa waumini fomu ya kuzaza kuonyesha detail zote hizo maybe alitaka kuweka formu za zaka kama makanisa mengine wafanyavyo but hizo fomu huwa niaonyesha jina kamamili, shughuli ufanyayo na zaka utakayo mtolea mungu wako kwa mwaka ni kiasi gani basi hakuna masuala mengine,

kama ne anataka kuanzisha deci yake aseme anatafta ufadhiliwa lazima...
kakobe hapo amechemka
 
Jamani, Kakobe ni tapeli, yani haoni hata aibu kuwataka waumini waorodheshe mali zao. Huyu Mchungaji sijui anatumia dawa gani kuwatoa akili waumini wake.
 
Kakobe yupo right.
epuka mafisadi kwa kujihakikishia kama wanachotoa ni ada au si muamala.
 
Sidhani kama kakobe anakosea nafkiri yuko sahihi hasa ikizingatiwa watu wake wamekata shauri na wako tayari kwa lolote; usijali sana juu ya mali,magari au mishahara bali wao wanataka uzima wa kiupako' wangetaka vitu hivyo wangehama au wakafata kule ambako hawataulizwa juu ya kuandikisha mali au mishahara' jiulize ewe mtanzania mbona unaandikisha gari,kiwanja au masuala ya mirathi kwa watu au serikali ambayo huna imani nayo' mwache kakobe' dunia!?

Ndugu...unajua maana ya kuwa "brainwashed"??
 
Suala la DECI alikuwa na haki ya kulinena kwakuwa ilikuwa ni ukweli na ndiyo maana ikawa kama kama ilvyotoikea na imewalinda waliomsikia na kutii!!ungependa akae kimya na watu aliokabidhiwa na Mungu waingie kwenye upuuzi huo????kwanini

MKUU SIKUKUU

NA LILE LA MREMA KUWA RAIS NALO LILITIMIA...?????TUOMBE TOBA
 
Huyu bwana ni tapeli, na anahitaji kuchunguzwa.
Wafuasi wake wameshapumbazwa na miujiza feki inayotendeka, siyo miujiza yote itokayo kwa mungu. Inawezekana kuna njia mbadala inayo tumika. Hawa ndo wale ambao wametabiriwa hata katika maandiko kwamba watakuwapo manabii wa uongo. Kazi kwenu, mwenye masikio na asikie.!



BADO NAENDELEA KUSEMA KUWA FOMU HIZO NA NYUMBA NYINGINE ZA IBADA INABIDI IPATE NAKALA ZAKE KWANI ZINAWAEPUSHA PIA WATU HAWA KUWA NA VYANZO VISIVYO HALALI VYA MAPATO YAO , UKWEPAJI KODI N.K
Pia huenda ni mkakati wa kuleta ELIMU ya FEDHA NA UCHUMI ili watu waboreshe vipato vyao.....!
PIA ITASAIDIA WATU AMBAO HUWA HATUWEKI KUMBUKUMBU NZURI ZA VIPATO VYETU NA AKIBA KUFANYA HIVYO ILI KUJUA TUNAFANYA KAZI YA HASARA AU YA FAIDA....!
MUNGU APEWE SIFA...!
 
kama anaandikisha waumini na mali zao basi pia aandikishe wamezipataje maana isije ikawa watu wakishajifisadi wanawahi kutubu. lazima walipe saba mara sabini ebo!
 
Pdidy na wenzako..........!
askofu kakobe nimeona ametoa majibu ya hoja zenu........ to be fair ni vyema majibu hayo pia mkayaweka wapitiaji humu nao tuyaone....!
 
Kakobe ametoa waraka leo ktk Mwananchi kujibu na kufafanua hii hoja.
kama kuna mwenye nafasi (Invisible) pls aiscan aiweke hapa ili kutoa nafasi kwa wadau kuijadili pia.
 
Mimi naona Kakobe yuko sahihi kwani tukiangalia kanisa la mwanzo ambalo Yesu Kristo ambayo viongozi wake walikuwa mitume yaani wale wanafunzi wa Yesu, tunasoma; "Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alichonacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika. Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote. Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliuza, wakaleta thamani ya vitu vile vilivyouzwa, wakaiweka migiini pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya alivyohitaji." Matendo ya mitume 4:32-35.

Kwa hiyo kutakana na maandiko haya kutoka katika biblia ambao ndiyo muongozo kwa wale wanaomwamini Bwana Yesu, inawezekana Kakobe akawa na mtazamo huu wa kanisa la mwanzo.

Kwani kinachopelekea leo hii kuibuka kwa mafisadi na kundi la watu wachache kumiliki njia kuu za uchumi ninaona ni kutokana na ubinafsi uliojengeka katikati ya jamii.

Lakini kama tutafanikiwa kurudi katika mtazmo huu wa kanisa la mwanzo basi itakuwa ni mwisho wa ufisadi.

Kwa hiyo inawezekana Kakobe ameona njia pekee ya kumaliza ufisadi ni kurudi katika mstari, kwa kuanza na washirika wake.

Lakini ninaona mtazamo mwingine kwamba "Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji". Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa Kakobe anataka kuitumia hii katika kubalance maisha ya washirika wake.

Kwa hiyo tuingeangalia na upande mwingine kuliko kuangalia zaidi selfish ya Kakobe, kwani ninaamini Kakobe anaongoza waumini wengi na mambo haya hufanyika kwa njia ya kuelimishwa sawa na neno la Mungu na hatimaye watu kufikia kukubalia kutekeleza katika lile walilofundishwa.
 
narudia tena P DIDY na wenzako ambao mmekua wa mstari wa mbele kumuita mtumishi wa Mungu 'words' jitokezeni tena kwani amewajibu katika muda muafaka......!
 
Ila pia niulize kwamba pamoja na kuwa Kakobe hamiliki chochote hata akaunti. Je nani ni signatory wa akaunti za kanisa lake? na fedha zinazotolewa sadaka zinazofikia bilioni ushee zinasaidia vipi waumini wasio na uwezo? maana hata kanisa la mwanzo walichangishana kwa imani kwamba washirikia na kugawana ukwasi wao kwa ujumla na si kama kanisa la sasa.

ops! nimeanza kumgeuka
 
Jamani, Kakobe ni tapeli, yani haoni hata aibu kuwataka waumini waorodheshe mali zao. Huyu Mchungaji sijui anatumia dawa gani kuwatoa akili waumini wake.


Ndiyo maana nchi za wenzetu kuna body inayoshughulikia charitable giving zote kuanzia kwenye dini mpaka NGOs na wanatakiwa kufile returns kila mwaka. Hii inawapa imani zaidi wachangiaji na kuona umuhimu wa kuchangia. Ila bongo hii ni miradi na ukiona mtu kachangia basi ujue katishwa akifa hatafika mbinguni au anataka kugombea nafasi ya kisiasa (e.g udiwani, ubunge n.k). Shame on you unayetumia michango vibaya.
kpleo.jpg
 
SIO NA SISEMI AMINA.....!
BISHOP KAKOBE anabaki mtumishi wa MUNGU aliye juu.....! anaweza kuwa na mtazamo tofauti juu ya jambo fulani lakini bado anabaki GOD'S SERVANT.....!
kuorodhesha mali ni utapeli...? Mbona serikali inahitaji watumishi wake waorodheshe mali zao? je na huo ni utapeli au UTAWALA BORA...?
Anachofanya mtumishi wa MUNGU aliye hai ni KUWAEPUSHA WAUMINI NA DHAMBI YA ANANIA NA SAFIRA....! au mimi ndo nasoma BIBLIA TOFAUTI NA YA WENGINE....?
WATU HAWA KATIKA BIBLIA WALIFICHA TAARIFA MUHIMU NA WOTE MAUTI ILIWAKUTA.....!
HALAFU BIBLIA KATIKA WARAKA WA YAKOBO INATUELEZA TUSIWE WEPESI WA KUNENA BALI TUWE WEPESI WA KUSIKIA.....!
TUANGALIE TUSIJEINGIA UPOTEVUNI KWA KUWA WASEMAJI.....!

SASA NASEMA BWANA YESU APEWE SIFAAAA.!


Mtaumizwa sana.KAKOBE et. al, wamegeuza dini kuwa NGO na vifungu vya biblia vimegeuka silaha za kuangamiza akili za kufikiri kwa baadhi ya Watanzania (wawaaminio) na hivyo kuwakamua pesa zao na kuwageuza maskini. Kisa eti wanapewa matumaini eti wanakuwa matajiri wa roho......

Wizi mtupu.....watawalamua maziwa yaishe mpaka wawatoe damu....
 
African people are forever slaves through these bronze age mythologies.. Why should you need Kakobe to mediate your relationship with a God who is supposed to hear everyone's thoughts etc... It makes no sense.. People just need to think a lil bit..
 
Mtaumizwa sana.KAKOBE et. al, wamegeuza dini kuwa NGO na vifungu vya biblia vimegeuka silaha za kuangamiza akili za kufikiri kwa baadhi ya Watanzania (wawaaminio) na hivyo kuwakamua pesa zao na kuwageuza maskini. Kisa eti wanapewa matumaini eti wanakuwa matajiri wa roho......

Wizi mtupu.....watawalamua maziwa yaishe mpaka wawatoe damu....

Hapo nilipopa-bold ndio penyewe, ktk pitapita zangu zoote ukiangalia hawa 'wachungaji wa kondoo' standard ya maisha wanayoishi ni tofauti kabisa na mazingira ya jamii inayomzunguka. Utakuta anaishi nyumba nzuri watoto wanasoma na wana afya tele, gari au magari, n.k. Lakini angalia waumini wake walivyochoka mbaya..

Hawa ndo wachungaji wa mshahara, hawana hata uchungu na hali za kondoo wao. Wao wanajali tu maendeleo ya 'NGO' yao kimapato..lol
 
Ndiyo maana nchi za wenzetu kuna body inayoshughulikia charitable giving zote kuanzia kwenye dini mpaka NGOs na wanatakiwa kufile returns kila mwaka. Hii inawapa imani zaidi wachangiaji na kuona umuhimu wa kuchangia. Ila bongo hii ni miradi na ukiona mtu kachangia basi ujue katishwa akifa hatafika mbinguni au anataka kugombea nafasi ya kisiasa (e.g udiwani, ubunge n.k). Shame on you unayetumia michango vibaya.

Taib,

Taasisi za dini mara nyingi hakuna accountability kwenye mambo ya fedha na mipango na ndio maana sisi 'watoaji' wengine tulishaacha kutumbukiza talanta zetu kwenye kapu lisiloratibiwa, yaani kila kitu shaghalabaghala.

Ni bora serikali iingilie kati na ikatunga sheria na kufanya iwe lazima ukaguzi wa mapato kufanywa kwa hizi taasisi za kidini, kuwalinda waumini ambao wengi wao ni watu wa 'kawaida' na their gullibility inaweza kutumiwa vibaya na hawa self-appointed nabiiz.
 
WAPENDWA KATIKA SAKATA HILI ........tumeona pia na katuni ikimuonyesha KAKOBE akitoa jibu........ila mbona MAJIBU YAKE MWENYEWE HAYAWEKWI.....?
NA mwanzisha mada ndo haonekani kabisaaaa....!
"SHAME UPON DEVIL & HIS ADVOCATES.........!"
 
PDIDY,

KUBALI YAISHE, acha wanaoorodhesha mali zao waendelee, maana

wameelimishwa, ni watu wenye visomo mbalimbali (kama alivyosema

WABEROYA)na ni waelewa. Kumbuka ile ni habari ya IMANI, na imani huweza

kuhamisha milima!
 
Back
Top Bottom