Kakobe apinga nyaraka za viongozi wa dini; akemea kauli ya Pengo

Kila ngoma ina mchezaji wake
Ila nawaambieni watanzania kwamba huko tuendako siko kwema kabisaaaa.

hii inaonesha kwamba siasa siyo safi kwani haiaminiki tena kama itaweza kuwakomboa watu kutoka katika ufukara wao hivyo watu wa dini wanataka kuingia na kujaribu. Tatizo hapa ni kwamba kila mmoja anajiona ana hekima mbele ya macho yake na hataki kusahihishwa......

Ukiwa fisadi wa matendo , kwa mfano wa CCM kutumia tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo kwa nguvu, Wazee na vinara wa CCM kupora ushindi na kufanya mikutano ndani ya makanisa kwa nguvu, polisi na usalama kutumika kudhulumu haki za watanzania na hasa wakati wa kura , wale wanaweza kupata neno waka ongoka na si kuokoka na kuacha ufisadi ule .Ila Kakombe ana ufisaidi wa matendo na Mawazo .Uko akilini kila mara hakika si rahisi kumuokoa hata kama ataombewa na wachungaji Dunia nzima . Nilijua haya yatamkuta maana waraka wa katoliki umetulia bwana .
 
Wakati Mh.Rais Dr Kikwete akihutubia wazee wa Dar es salaam (wa CCM) pale Diamond uwepo wa Askofu Kakobe ulikuwa wazi.Iwekeni ile picha hapa janvini.Siku ile ndipo swala la "ajali ya kisiasa" kwa Mh.Lowassa lilizungumzwa.
 
Kusema kwamba Kakobe kakosea ni kukosea.

Wait, kusema kwamba kusema Kakobe kakosea ni kukosea ni kukosea

No, my point is, katika swala hili, ukisema fulani kakosea unakuja na wrong approach - accusatory/ unnecessarilyconfrontational- tuonyeshe alternative iliyo sawa ni ipi na kwa nini.
 
Kama hujaiona alternative ipi iko sahihi hata akija Musa hutaweza kuiona
 
I tell you this guy is smarter than we think of him!
Do you still stand with your words?

kakobe is just a stupid fellow, without vision.
The quote above should tell you how he is regarded by intellectuals. Kakobe ni sawa na Kingunge tu. Wananyang'anya watu hata kidogo wlicho nacho. Watu hawajasahau alivyokusanya mikufu ya dhahabu kutoka kwa wajinga waliomwamini.
 
Kakobe hajakosea hata mahala pamoja ,kusema kweli amewagusa ndipo na sasa mnabaki kupiga mayowe ,haya mambo ya waraka kutoka kanisani au misikitini yanamatatizo katika nchi yenye wananchi wanaofuata dini mbalimbali ,sasa tusubiri masingasinga na mabaniani nao watoe waraka wao.Lazima waseme Rasi awe anatafuna pilipili kila wakati ,hapo ndipo mtakapo elewa kuwa bangi si mboga.
 
Wakuu nimekuwa nikitafakari sana press release ya Zakaria Kakobe na insticts zangu zimekuwa zikinishawishi kwa kiasi kikubwa nikiamini kwamba ama anatumiwa na CCM (divide et impera) au anajipendekeza kusafisha uhusiano wake mbaya na CCM tangu mwaka 2000 (kama sikosei) wakati akimuunga mkono ALM (mzee wa Kiraracha.
Katika kuperuzi kwangu nikakutana na bandiko moja la Faustin S. Munishi (maarufu kwenye nyimbo za injili) akielezea sura halisi ya Zakaria Kakobe (bandiko ni refu kidogo but its worth reading):

Askofu Kakobe msiyemjua

kakobendogo.jpg

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Sishangai watu wanaposema kwamba kanisa analoliongoza la Full Gospel Bible Felloship ndilo linaloongoza makanisa ya Kipentekoste kwa idadi ya watu. Lakini hiyo haimaanishi kwamba kanisa hilo ndilo kipimo cha makanisa Tanzania kwani hata wengi mara nyingi hukosea. Ila nisieleweke kama ninayesema kwamba kanisa la Kakobe siyo la kweli, lakini siwezi pia mia kwa mia kusema kinyume chake. Mungu pekee ndiye mwenye kipimo cha kuhukumu kanisa gani la kweli. ILa siyo vibaya watumishi wa Mungu wakitoa tadhimini yao kuhusu yale wanayoyaona na kuyasikia, na kwa sababu wana roho wa Mungu ndani yao, mara nyingi hawatakosea sana. Nisemayo nayasema kama mtumishi wa Mungu. Pengine niseme kwamba mimi ni mtumishi wa Mungu. Ninajiamini hivyo. ila simzuii mwingine kuniona vinginevyo kwani hata ninayemsema hapa pengine naye anajiamini ni mtumishi wa Mungu. [/FONT]

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]....Baadaye ndipo nilipokuja kuelewa kwamba Lengo la mkutano lilikuwa ni kuweka mikakati ya kujenga mahusiano mazuri kati ya kanisa na serikali. Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mwenyekiti wa umoja huo Askofu Sylvester Gamanywa alisema, wakati umefika kwa serikali kutowapuuza wapentekoste. Alidai kwamba wapentekoste hawapewi nafasi katika vyombo vya habari vya kitaifa jambo ambalo alisema limechangiwa na dhana potovu kwamba walokole ni watu waliochanganyikiwa kimaisha na hawana lolote la kuweza kuisaidia serikali kiutawala. Naye Askofu Kitonga wa kanisa la Redeemed Kenya alisema anaunga mkono kongamano hilo na akasema anafurahi kuona askofu Kakobe akiufuata ushauri wake wa kutoipinga serikali iliyoko madarakani. Aliongeza kwamba nchini Kenya serikali iliyokuwa madarakani ilitambua umuhimu wa wapentekoste na iliwatumia sana katika kuwasilisha sera za serikali kwa wananchi ambao wengi ni washirika wa makanisa hayo. Lakini wale wanaopinga wazo la kanisa kununuliwa na serikali wanasema, Kanisa ni chombo cha kukemea maovu katika jamii na serikali ikiwa mojawapo. Waliongeza kwamba Kanisa linapokubali kununuliwa na serikali, hiyo ni hatari kubwa. Walisisitiza kwamba Inasikitisha kuona kwamba kanisa la Tanzania limekubali kununuliwa na serikali ya CCM ambayo sifa yake ni kuwaua raia wasiokubaliana na sera zao mbovu za wizi , Ukandamizaji, na uonevu wa kila namna kwa raia wa Tanzania. Mungu lisaidie kanisa lako Tanzania. [/FONT]​
Yes, it was worth reading. Naona Joyceline imemkolea anataka zaidi :)

attachment.php

(Mwenye blue) Ndani ya Diamond Jubilee Dar-es-Salaam kwenye mkutano wa wazee wa CCM.
 
Attachments

  • kakobe.jpg
    kakobe.jpg
    61.7 KB · Views: 179
Kusema kwamba Kakobe kakosea ni kukosea.

Wait, kusema kwamba kusema Kakobe kakosea ni kukosea ni kukosea

No, my point is, katika swala hili, ukisema fulani kakosea unakuja na wrong approach - accusatory/ unnecessarilyconfrontational- tuonyeshe alternative iliyo sawa ni ipi na kwa nini.

One thing has that has been revealed in this whole saga is that there is a power vacuum in this country and as they say "power abohors vacuum". Kukiwa na ombwe la uongozi imara nchi ni rahisi kuyumbishwa.

Nini hasa kimepelekea mpaka tukafika hapa;
-Serikali kuijingiza katika mambo ya dini kwa sababu tu ya kupata kura. Kutoa ahadi ambazo imeshindwa kutekeleza na hivyo kusababisha baadhi watu kutaharuki. Kingunge analijua hilo na ndio maana alitaka kulizima lakini bahati mbaya the ginie was out of the bottle.

-Swala la ufisadi na haswa unaowausisha marafiki wa karibu wa Rais limemdhoofisha kwa kiasi kikubwa bwana mkubwa. Rais wetu amezongwa hapa na anakosa kuamua mambo magumu ya kiuongozi. Hu ni udhaifu kwa upande wake na serikali.

What Next: We seriously need a national dialogue short of that the country is at a very critical crossroads.
 
Hakuna lolote lile; Kakobe ni miongoni mwa wachungaji ambao wanasubiri wengine wawalishe kondoo na kufukuza wezi halafu yeye aje na kifimbo chake na kuwaongoza zizini mwake!

a. Ni lini Kakobe alisimama kutetea haki za wananchi?

b. Ni lini aliandamana na watu kuonesha kuchoshwa kwake na maovu?

c. Wakati wa sakata la Buzwagi Kakobe alikuwa upande gani?

d. Wakati tunapiga kelele kuhusu BoT yeye alifanya nini hata kuunga mkono?

Iweje leo baada ya wengine kufanya kazi aje yeye na kuvuna!? Kama kweli yeye si mnafiki ashike Bango na kuandamana kusema "Mkapa ahojiwe".. na asimame na Biblia yake mkononi na kusema Mramba ajiuzulu!

Point tupu mkuu..
 
Kusema kwamba Kakobe kakosea ni kukosea.

Wait, kusema kwamba kusema Kakobe kakosea ni kukosea ni kukosea

No, my point is, katika swala hili, ukisema fulani kakosea unakuja na wrong approach - accusatory/ unnecessarilyconfrontational- tuonyeshe alternative iliyo sawa ni ipi na kwa nini.

Mkuu uko sawa kuwa jamaa alitakiwa atoe alternative ambayo na wewe ungeweza kuitoa. Lakini pia aliyekosea ni Kakobe kwani hakutoa maoni yake based kwenye zile nyaraka bali anachofikiri. Kwani lazima huweke wazi kuwa kasoro zilizopo kwenye hizo nyaraka wakati wa kujenga hoja. Mimi mpaka sasa sijaona kasoro kwenye waraka wa wakatoliki, waraka wa shula (unaoitwa wa waislamu) bado sijauona siwezi kucomment. Lakini waliouona wanasema si mzuri hata kidogo.
 
Uamuzi wa Kakobe kushambulia waraka wa Katoliki na maaskofu unazua maswali mengi. Ingawa baadhi ya watu wamesema kuwa ametumia mwanya wa waraka kuendeleza chuki yake ya siku nyingi dhidi ya Kanisa Katoliki. Huku wengine wakisema anatafuta sifa kirahisirahisi kwa kujilinganisha na maaskofu wanaopatikana kwa mfumo unaoeleweka kwa kuwa amejipachika uaskofu yeye mwenyewe, kwa maoni yangu naona sababu nyingine za nyongeza pamoja na kukubaliana na hizo zilizotajwa.

Binafsi sijawahi kumsikia Kakobe akiitisha waandishi wa habari kuungana na watanzania wengine kupiga vita ufisadi na kuwapinga mafisadi. Badala yake ameibuka na kupinga kabrasha linaloelimisha watu namana ya kung’oa mizizi ya ufisadi na mafisadi. Hapa ndipo nashawishika kuanza kuamini kuwa huenda Kakobe ni fisadi pia kanisani kwake kwa kuwa inasemekana anawakamua waumini wake hadi kukosa nauli ya kupandia daladala kurudi kwao. Imeshaelezwa kuwa Mayaya na wanafunzi hawajasalimika kutokana na unyonyaji wa Kakobe. Cha kushangaza zaidi hatujasikia Kakobe kuwa amejenga Hospitali, shule, chuo wala darasa la chekechea. Mwenendo huu unafanana na ule wa mafisadi ambao hawajali chochote hata kama watanzania hawapati huduma za jamii.

Je upinzani wa Kakobe dhidi ya waraka ni dalili za kuficha ufisadi anaowafanyia waumini wake au ameanza kuwa kuadi wa mafisadi ili mkono wake uende kinywani?
 
....Binafsi sijawahi kumsikia Kakobe akiitisha waandishi wa habari kuungana na watanzania wengine kupiga vita ufisadi na kuwapinga mafisadi. Badala yake ameibuka na kupinga kabrasha linaloelimisha watu namana ya kung’oa mizizi ya ufisadi na mafisadi. Hapa ndipo nashawishika kuanza kuamini kuwa huenda Kakobe ni fisadi pia kanisani kwake kwa kuwa inasemekana anawakamua waumini wake hadi kukosa nauli ya kupandia daladala kurudi kwao. Imeshaelezwa kuwa Mayaya na wanafunzi hawajasalimika kutokana na unyonyaji wa Kakobe. Cha kushangaza zaidi hatujasikia Kakobe kuwa amejenga Hospitali, shule, chuo wala darasa la chekechea. Mwenendo huu unafanana na ule wa mafisadi ambao hawajali chochote hata kama watanzania hawapati huduma za jamii.

Je upinzani wa Kakobe dhidi ya waraka ni dalili za kuficha ufisadi anaowafanyia waumini wake au ameanza kuwa kuadi wa mafisadi ili mkono wake uende kinywani?

Very good observation mkuu.
Sina mengi ya kumdiscuss Kakobe as i think i will be wasting my time.
He is just a looser.
 
humu ndani watu huwa mnapenda mawazo ya aina moja tu,kinyume chake au tofauti na mawazo yenu hamtaki...
kakobe ana uhuru wa kutoa maoni yake....
asiitwe fisadi kwa kuwa tu hakubaliani na kanisa katoliki,
sio kila wanaopinga waraka wa katoliki ni mafisadi
acheni hizo cheap name calling,
hebu jielimisheni maana ya " to agree to disagree"
na jaribuni kukuza uwezo wa kuelewa kwanza kabla ya
kukuza uwezo wa kuzungumza.
 
Haina mjadala kwamba makanisa mengi ya Fellowship ni matawi ya elaborate crime practitioners. Wengi walio waovu miavuli yao ni ulokole. Na hasa hawa wanaojifanya wanatenda miujiza. Wanachofanya ni kuwalewesha watu maneno yenye matisho bila kuwapa uhuru wa kufikiri wala kujadili mambo. Hushangai aliyekuwa wa kwanza alikua Mwingira ? Ndo hao hao. Mwangalie naye Gertrude Rwakatale, what do you ezxpect from these people? Unganisha na ishu ya Mtikila, hapo utapata mduara mzima. Kakobe ni fisadi mazima, tena pia mshirikina na mzinifu wa hatari.....watch out, hao ni ma CIA
 
kuna mahali biblia inatuambia, kuwa wayahudi wa kale walifanya shauri kumkamata Yesu kutokana na kuenea kwa mafundisho yake, kukawa na mwalimu mmoja nadhani gamaliel huyu alikuwa mtu mwenye busara akawaambia,. kama anayofundisha Yesu yanatoka kwa Mungu kamwe hamtaweza kumnyamazisha lakini la hasha kama ni yake mwenyewe hayatadumu, akawapa mfano wa mtu aliyeitwa yuda aliyekuwa amewakusanya watu na kuwapa mafundisho yake, lakini yuda alipofariki kundi lile likatawanyika ikawa ni mwisho wa kila kitu, akina kakobe, mwingira na wengine kama wanayofundisha yanatoka kwa Mungu yatadumu milele la hasha yataondoka na wao!
 
HOja kuonesha ufisadi wa Kakobe zimetolewa, hujaonyesha kwa hoja kuwa Kakobe si fisadi
 
Haina mjadala kwamba makanisa mengi ya Fellowship ni matawi ya elaborate crime practitioners. Wengi walio waovu miavuli yao ni ulokole. Na hasa hawa wanaojifanya wanatenda miujiza. Wanachofanya ni kuwalewesha watu maneno yenye matisho bila kuwapa uhuru wa kufikiri wala kujadili mambo. Hushangai aliyekuwa wa kwanza alikua Mwingira ? Ndo hao hao. Mwangalie naye Gertrude Rwakatale, what do you ezxpect from these people? Unganisha na ishu ya Mtikila, hapo utapata mduara mzima. Kakobe ni fisadi mazima, tena pia mshirikina na mzinifu wa hatari.....watch out, hao ni ma CIA

Pole hujasema lolote la kueleweka katika post yako ee mwana wa Ibilisi.
 
Mimi ninavyoona ni kuwa hawa WAKATOLIKI wamekosa demokrasia kwani wao maamuzi yao yote lazima yatoke Vatican, hata Peng, maaskofu wote na mapadre wote wanachaguliwa toka Vatican.

Na wamefundishwa kuwa hakuna mtu mwenye uwezo wa kupingana na kanisa. Na akitokea mtu kupingana na kanisa katoliki basi wao wanamtenga. Mfano Father Nkwera au hata Rafiki yangu kutoka kule Ibwera Padre Privatus kalugendo.

Sasa ni lazima tuamini kuwa KAKOBE yupo sahihi kabisa. Na kwa taarifa hata Serikali ya mapinduzi Znz imeweka bayana Waraka mwisho Chumbe. marufuku Znz.

Serikali ya Muungano mnasubiri nini?
 
kuna mahali biblia inatuambia, kuwa wayahudi wa kale walifanya shauri kumkamata Yesu kutokana na kuenea kwa mafundisho yake, kukawa na mwalimu mmoja nadhani gamaliel huyu alikuwa mtu mwenye busara akawaambia,. kama anayofundisha Yesu yanatoka kwa Mungu kamwe hamtaweza kumnyamazisha lakini la hasha kama ni yake mwenyewe hayatadumu, akawapa mfano wa mtu aliyeitwa yuda aliyekuwa amewakusanya watu na kuwapa mafundisho yake, lakini yuda alipofariki kundi lile likatawanyika ikawa ni mwisho wa kila kitu, akina kakobe, mwingira na wengine kama wanayofundisha yanatoka kwa Mungu yatadumu milele la hasha yataondoka na wao!

Mwikimbi!

Umenena yaliyo ya kweli. Ila nakutahadharisha usimfananishe yule mwana mazinga ombwe Zakariah Kakobe na nabii hata wa uongo hakaribii. Yule ni tapeli anaganga njaa tena wako wengi akina Mwingira, Munuo wa Sloam anayejifanya nabii wakati ni mwizi tunamfahamu alikuwa anaiba sana spea za magari ya watu. Hawa walifanikiwa tuu kupanda ngazi kwa ajili ya upumbavu wa mtu mmoja kwa jna anaitwa Ruksa au Alhaji Ali Hassan Mwinyi kwa masikitiko na bahati mbaya aliwahi kuwa rais wa Tanzania.

Sera yake ya kipumbavu ya ruksa imekuwa ni janga la kitaifa na litatusumbua kwa zaidi ya karne moja ijayo ila hawa wapuuzi wanaoitwa CCM bado wanamuenzi na kumpatia ulinzi badala ya kumpeleka anakostahili jela lakini anaambiwa aongoze kamati sijui ya nini? Hii laana sijui wameachiwa na nani au kawaachia Nyerere nini?
 
Back
Top Bottom