Kakobe aitunishia misuli TANESCO

Tanesco hawana ugomvi wowote na kakobe, ni swala la kukubaliana tu. Lakini kuna mahali pengine waya hizo zinaweza ku-diverge zifike huko au ni hapo hapo tu?
 
Hivi huku kuonyeshana ubabe kati ya TANESCO na Mchungaji Kakobe na waumini wa kanisa lake sijui nani mwenye haki na nisingependa kutaka ku argue ili hali sina facts zote

Je sheria inasemaje?

Na kama TANESCO wana makosa kwa nini wanawasumbua hawa waumini? Kama ni kweli kwa nini wanatumia tactics za kibabe kufanya kazi yao nje ya sheria kama wanavyotuhumiwa?

Na kama KAKOBE na kanisa lake wana makosa kwenye hili kwa nini wasi kae pembeni na kuacha TANESCO wafuate sheria ili watu na zahanati zipate umeme ambao utaokoa maisha ya wengi na kuleta unafuu wa hali zao?

Jamani nimeuliza Sheria inasemaje na kama hakuna mwenye kujua basi tuache speculations na si vibaya kama Badra akafikishiwa ujumbe kuwa this doesnt look good on TANESCO na aje aweke wazi msimamo wao kwa public
 
Pamoja na kutojua sheria, waumini kwanini wanakesha wakilinda pale? Inamaana kuna siku kitu kikitokea ambacho mchungaji hakimpendezi, basi anaweza kuwaamuru kufanya lolote lile na likafanyika. Siamini dawa ya tatizo ni kulinda eneo lile.
 
Naamini kuna mambo bado hayana sheria, na sheria ingekuwepo sidhani kama serikali ingeshindwa kufanya wanachotaka, na kama zipo basi ni za zamani, hazijaendana na ishu za sasa zinazotaka miradi kama hiyo lazima ifanyiwe EIA. Hapa ilikuwa ni twende twende umeme upite, sina hakika kama EIA ilifanyika, watu wameamka siku hizi!

, very same Idea ndio wanayoitumia serikali kusema Kahama kumejengwa vizuri, lakini madini wanayochukua ni na athari za mazingira hazilipiki

Kama tunataka maendeleo , ni fursa pia tusiharibu maendeleao yalikwisha fikiwa.

Ishua ya umeme mkubwa yes zio mzuri, lakini sio kuwa haiwekeni kuzuia athari zake, ni vitu vinawezekanika, Tanesco wana vipanga kibao wa umeme, hoja ya kakobe wanaweza kuitatua technically badala ya watu kulala nje na wao Tanesco kutokwenda na schedule yao! I do belive in engineering

Tanzania tutaendela tu, ikiwa vitu vitafanyika kwa usahihi, bila kujali nani anafanya na kwa nani na kwa umuhimu gani, nadhani very same reason ndio ilimwondoa EL madarakani, hata kama dhumuni ni zuri ukishakosea tu taratibu basi umekwisha!
 
TANESCO wanajenga kwenye hifadhi ya barabara (ROW) au Right of Way. ukiangalia pale kwa Kakobe eneo lake ni kuanzia kwenye fence na kuingia ndani, huku nje si kwake. hivyo hata magari yalipaswa yawe na parking ndani ya fence yake.
hawa akina kakobe ni wale wananchi wapinga maendeleo. anapinga umeme usijengwe pale kwa sababu anataka kutumia eneo la hifadhi ya barabara kwa parking na mambo mengine na hii ni makosa.
 
Pamoja na kutojua sheria, waumini kwanini wanakesha wakilinda pale? Inamaana kuna siku kitu kikitokea ambacho mchungaji hakimpendezi, basi anaweza kuwaamuru kufanya lolote lile na likafanyika. Siamini dawa ya tatizo ni kulinda eneo lile.
Tafadhari sana usije ukalinganisha na yale yaliyotokea kule Uganda kwa Kibwetere ambapo alikuwa akiwaamuru wafuasi wake wafanye kile anachotaka yeye na matokeo yake wengi tumeyasikia,lakini hapa Bongo watu wana akili bwana!
 
Brainwashing ya Kakobe, Mwingira, Mzee wa Upako hasa kwa akina mama na dada zetu inaelekea kubaya na serikali yetu inatazama tu. Rais wetu aifute hati ilipojengwa kanisa lile la Kakobe ili shughuli za TANESCO ziendelee.
 
But nasikia wako kwenye Round table na Tanesco kwa upande mmoja na Wizara ya Nishati kwa Upande mwingine

Lakini swali la kujiuliza Umeme mkubwa unapaswa kupita wapi?
 
Brainwashing ya Kakobe, Mwingira, Mzee wa Upako hasa kwa akina mama na dada zetu inaelekea kubaya na serikali yetu inatazama tu. Rais wetu aifute hati ilipojengwa kanisa lile la Kakobe ili shughuli za TANESCO ziendelee.

Mkuu huo utakuwa ni Udictator, Sheria Ifuate Mkondo wake itazamwe haki kama Kakobe ana haki basi na iwe hivyo kama Tanesco wana haki basi na iwe hivyo.
 
Mkuu huo utakuwa ni Udictator, Sheria Ifuate Mkondo wake itazamwe haki kama Kakobe ana haki basi na iwe hivyo kama Tanesco wana haki basi na iwe hivyo.
Ndege,
Nasema hivyo kwa sababu zifuatazo:
1. Sio kanisa la Kakobe tu lililoko upande huo zinakotakiwa kupita hizo nyaya.
2.Bila shaka TANESCO na Wizara wamefanya upembuzi yakinifu wakishirikiana na Taasisi nyingine kama NEMC na wakaridhika kwamba hakuna madhara yoyote yatakayotokana na nyaya hizi kupita pale. Hazianzii wala kuishia pale.
 
Unao ushahidi usio shaka ya kuwa competent bodies zilipitisha hii project ya TANESCO??
 
Mkuu huo utakuwa ni Udictator, Sheria Ifuate Mkondo wake itazamwe haki kama Kakobe ana haki basi na iwe hivyo kama Tanesco wana haki basi na iwe hivyo.

Unajua humu ndani kuna watu wana fikra za ajabu sana. Halafu ndio tunajiita Great Thinkers ??
 
Unao ushahidi usio shaka ya kuwa competent bodies zilipitisha hii project ya TANESCO??
Ndio maana nimeanza na maneno "Bila shaka". Project ya billions kama hii haiwezi kupita bila masharti na vigezo vyake kuzingatiwa labda kwa Tanzania tu!
 
Ndio maana nimeanza na maneno "Bila shaka". Project ya billions kama hii haiwezi kupita bila masharti na vigezo vyake kuzingatiwa labda kwa Tanzania tu!

Kwa hiyo 'bila shaka' ndio jibu lako?? Great Thinker?
 
Hatuwezi kufanana woote humu ndani kwa fikra. Maana na uwepo wa forum hii utaathirika sana!

Soma context ya hoja sio maneno kwenye sentensi. Ukifanya hivyo hutoelewa ninachokikusudia. Huwezi ukafuta hati ya ardhi kwa sababu tu kikundi fulani cha watu kinaprotest jambo fulani. Unless kama kuna jingine ambalo hutuambii hapa.
 
Kama kuna uvunjifu wa sheria, kwa nini Kakobe asiende mahakamani kuzuia hizo nyanya zisipite karibu na kanisa lake na badala yake ameamua kutumia nguvu? Ni kweli Kakobe na waumini wake wana nguvu lakini nguvu hizi ni bora wazitumie vema la sivyo wanaweza kupoteza haki yao(kama ipo!) ikiwa wataendelea kulinda tu pale nje bila kwenda kwenye vyombo vya sheria.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom