Kakobe aitunishia misuli TANESCO

Kakobe aliwataka Tanesco kwenda kujifunza kwake masuala ya umeme kwani amesoma kuliko wao na watarajie kupata upinzani mkubwa kutoka kwa waumini hao wenye uelewa mkubwa wa athari ya ememe huo.

Hivi ni Athari za Umeme kwani katisani kwake wanatumia vibatari?

"Huu ni ufisadi unaofanyika hapa,na tutakuwa hapa mpaka kieleweke hata kama ni mwaka mzima kwani huu umeme chuo kikuu waliukataa kutokana na madhara yake hivyo sisi hatuutaki pia na tutapambana" alisema Askofu Kakobe.

Nataka Madhara ya Umeme ambayo Kakobe anayazungumzia, Watoto wa Chambega hebu mwageni Lecture hapa

Pia Kokobe aliendelea kusema kuwa hayo yanayofanyika hapo Serikali haiwezi wala kuthubutu kuyafanya katika makanisa mengine hasa kwa Kardinal Pengo.
"Huu ni ujinga mtupu,na kama angekuwa Kardinal Pengo asingethubutu kuuruhusu kufanyika kwake kamwe" alisema.

Haya sasa ni Ugomvi huo
 
Hivi ni kweli chuo kikuu walikataa umeme huo kupita maeneo yao??

Nafikiri tungepata mwewnye hizi data we could come out of Darkness!!
 
eti,hao waumini wanaoshinda hapo wanafanya kazi saa ngapi????
 
Wana JF,
Napenda kuwa uliza is this what we call Democracy au?? Last yr migomo,maandamano,epa yani vitu chungu mzima, Sasa Sielewi ni tatizo la Mipango miji ndilo sasa latuletea shida? viongozi hawa wajibiki katika fani zao ipaswavyoo? au?

Ivi hii hali itaisha lini kama waumini wa kanisa hilo nao wamenza itakuwaje me pia nadhani wamepata nguvu baada ya wafanyakazi wa shirika la Reli (TRL)kupambana na wawekezaji wa kihindi na kuwashinda ktk kudai haki zao ni dalili tosha kabisa kwa sasa na popote pale ndani ya nchi hii kwa watu kuanzisha migomo au maandamano, mfano mwingine ni wama ng'ati na aridhi yao na mapolice wanapigana mikwala mbaya.

Kwakweli sijui hii 2010 tunavyoianza na mkizingatia kipindi hiki ni cha uchaguzi kutakuwa na matatizo mengi sn mtake msitake mtajionea wenyewe.
 
Why is Kakobe Protesting? Kabla ya kutoa allegations tungejadili sababu zinazomfanya mtumishi huyu wa Bwana apinge Tanesco kupitisha Power Transmission facility karibu na Kanisa lake

Ni kweli kabisa, kuna tetesi kuwa suala hili linashughulikiwa kidini zaidi na kigogo mmoja ndani ya Tanesco, je kunaukweli wowote? mwenye data atuletee.
 
Printer ni mfanyabiashara. Hata ukimpelekea 'art work' iliyoandikwa 'Yesu si Mungu' ata print. Mbona magazeti yetu, hasa NIPASHE yana print matangazo ya waganga wa jadi wanaodai wanazo dawa za mapenzi, za kurefusha uume, n.k? wala hawashtakiwi?
Kuhusu Kakobe, nina wasiwasi kwamba anapokwenda sipo!!

Ukiliangalia kwa undani swala hili inaonyesha kakobe hajatendewa haki, na kwa utamaduni uliojengwa na serikali yetu (haki haitendeki bila mgomo mzito) Kakobe nae kaamua kutumia njia hii ya mgomo kudai haki yake. Kuna baadhi ya vyanzo vinaelekeza TANESCO imewalipa fidia baadhi ya watu/wathirika wa mradi lakini kakobe hajalipwa wala TANESCO haikutaka kuzungumza nae kuhusu mradi huu na utaratibu wa fidia bali kushurutisha kung'oa mabango yake. Endapo habari hizi ni sahihi, nadhani Kakobe yupo sahihi na si vyema kumhujumu kwa sababu zozote ziwe za kidini au kisiasa.
 
916.jpg




918.jpg

Hii ni mtihani mwingine kwa kikwete, kwa udhaifu alionao sijui kama ataweza kufanya kile watanzania wanataka, yaani kuvunja hilo kanisa la kakobe na kupitisha njia ya umeme.

Hatua inayostahili kwa kakobe ni kupiga marufuku kanisa hilo nchini na yeye kuwekwa rumande kama wachungaji wa DECI kwa kosa la uzurulaji.
 
Kama hakuna tatizo lingine ila ni sababu tu za kijinga zinazotolewa na kakobe.....basi ikibidi hata kanisa lake lipigwe marufuku kwani linapingana na mipango ya maendeleo.
 
Kakobe aitunishia msuli TANESCO

• Waamini wapiga kambi saa 24 kanisani

na Betty Kangonga

WAUMINI wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship wamepiga kambi ya saa 24 kanisani kwao Mwenge, Dar es Salaam, kulizuia Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kupitisha umeme wa msongo mkubwa wa kilovolti 132 mbele ya kanisa lao.

Waamini hao wanaume kwa wanawake, tangu jana wamepeana zamu kwa kupangiana makundi ya kuikabili TANESCO usiku na mchana.

Ujumbe mzito wa kanisa hilo kwa shirika hilo la umeme umewekwa wazi katika fulana maalumu walizovaa, zenye maandishi ya maonyo na kejeli yasomekayo: “TANESCO muogopeni Mungu” (mbele) na “Baada ya Richmond mmegeukia Kanisa” (nyuma).

Akizungumzia tukio hilo huku akiwa amezungukwa na waamini hao, Askofu Mkuu, Zakary Kakobe, alisema wamefikia uamuzi huo baada ya shirika hilo kutoa taarifa kwamba kazi ya kupitisha nyaya hizo itaanza mapema mwezi huu na kwamba wametengeza fulana zaidi ya 50,000 ili waamini wakataokuwa kwenye kambi hiyo waweze kutambulika.

“Waamini wamevaa fulana hizo ili kujitofautisha na wapitanjia na kuanzia leo watapiga kambi ya saa 24 huku wakibadilishana zamu za kuingia na iwapo TANESCO watafika mahali hapa kwa ajili ya kuanza kazi hiyo itakuwa rahisi kukabiliana nao.

“Tumeamua kufanya hivyo maana taarifa ya TANESCO ilieleza kuanza kazi mwanzoni mwa mwezi huu, hivyo waamini watakuwepo wakati wote mahali hapa,” alisisitiza.

Askofu Kakobe alisema uchunguzi waliofanya umebaini kuwa ufisadi wa mkataba tata wa kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond umerudishwa kwa mfumo mwingine ambao kwa sasa unataka kuwalaghai wananchi wanyonge.

“Huu umeme ulikuwa upitishwe upande wa pili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kule wakakutana na wasomi ambao walitoa athari za nyaya hizo na kuishauri TANESCO ijaribu kupitisha chini ya ardhi, lakini wakaogopa gharama,” alisema.

Kakobe alisema baada ya TANESCO kuona imeshindikana walihamia upande wa pili (wa kanisa) ambako walijua Walokole ni wanyonge na kwamba wataishia kuingia kanisani na kupiga magoti wakikubali madhara hayo yawafike.

“Hili suala tumelichunguza kwa mapana tumegundua kuwa ule ufisadi wa Richmond umerudi kwa njia tofauti, hivyo tumeweka kambi mahali hapa kuanzia sasa kwa kupokezana na tutakuwa tayari kukabiliana nao, lakini si kwa silaha,” alisema Askofu Kakobe.

Aidha, Kakobe alihoji iwapo umeme huo hauna madhara, inakuwaje TANESCO wang’ang’anie kuvunja mabango ya kanisa yenye urefu wa mita 13 huku nguzo zinazobeba umeme huo zikitakiwa kuwa na urefu wa mita 23.

Alisema baadhi ya wananchi wamekuwa kimya kwa kutopinga upitishaji wa umeme huo zikiwepo taarifa zisizo rasmi kuwa wamekwishalipwa fidia ya sh milioni 100 hasa kuanzia maeneo ya Ubungo.

Hata hivyo alieleza wamejipanga vilivyo kukabiliana na upitishwaji wa umeme huo kwani kuna uwezekano hapo baadae kuja kubomoa eneo la mbele la kanisa hilo ukiachana na mabango.

“Sisi tunafahamu kinachotaka kufanyika hapa, ndiyo maana tumeamua kujipanga. Lazima wajiulize mbona kipindi cha ujenzi wa barabara hatukupingana na wakala wa barabara Tanroads? Wakati wa upanuzi tulitoa ushirikiano mkubwa. Tulifanya hivyo kwa kuwa walitushirikisha kabla hawajaanza,” alisema.

Pamoja na mambo mengine, askofu huyo alisema uchunguzi waliofanya umebaini kuwa serikali imepanga kunyanyasa baadhi ya makanisa.

“Wamezoea kusema kuwa Kardinali Pengo ni mlima, eti Kakobe ni kichuguu ndiyo maana kama lingekuwa kanisa lake wasingeligusa, sasa napenda kuwaeleza kuwa Kakobe si mlima Kilimanjaro tu bali ni Everest,” alisisitiza.

Alisema anashangazwa na maelezo yanayotolewa na TANESCO kuwa upitishaji wa umeme huo ni kwa ajili ya jamii, huku kwa upande mwingine wanaharibu maendeleo yaliyofanywa na jamii hiyo hiyo.

Hata hivyo, alisema katika kipindi hiki Watanzania wanatakiwa kuwa makini na propaganda zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa serikali, kwani nyingi zina madhara.

Alitoa mfano kuwa wakati wa uingizwaji wa dawa za uzazi wa mpango, kinamama walielezwa hazina madhara, lakini baada ya kutumia wakaelezwa kwamba zina madhara.

Mfano huo aliufananisha na upitishaji wa umeme huo ambao kwa sasa TANESCO wanasisitiza hauna madhara, lakini itafika kipindi watatangaza madhara ya umeme huo kwa watu wanaoishi jirani.

Alisema hawako tayari kukubali upitishwaji wa umeme huo, akaongeza kwamba hata Wajapan waliofadhili mradi huo hupitisha miundombinu kabla ya wananchi kuingia katika eneo husika. “Nimetembea nchi nyingi ikiwemo Japan, tena kule kwao miundombinu hupitishwa kabla ya wananchi kuanzisha makazi. Sasa iweje hapa nchini wapitishe wakati tayari kuna watu wanaishi katika maeneo hayo?” alihoji Kakobe. Hivi karibuni TANESCO lilitoa taarifa ikiwaondoa hofu waamini wa kanisa hilo kwamba hawataathiriwa na upitishaji wa umeme huo mradi ambao umefadhiliwa na Serikali ya Japan.
 
hapa watu wengi tunaongelea ushibiki tu, kanisa lipigwe marufuku, kakobe awekwe lupango, kova atume vijana wake, nchi ya utawala wa sheria haiendeshwi namna hiyo ndugu zangu. Mngesema serikali ikae na Kakobe imsikilize na kama madai yake si ya msingi iyatupilie mbali, au Kakobe aende mahakamani kusimamisha hilo zoezi la uwekaji nguzo kisheria. Watu hamtaki hata kumsikiliza Kakobe, mtu kawaambia kuna athari jiulizeni kwanza je amesema kweli au laa.
 
Nashangaa mtanzania wa kawaida anayepinga swala la Kakobe, tuna matatizo ya mipango miji.Mtanzania hata siku moja hawezi kujiamini alipojenga au anapoishi simply kwa sababu mipango miji ni dynamic!

Failures hizi ndio zinaleta matatizo kama haya, serikali imekuwa ikitumia ubavu , haitaki kusikiliza na wakitokea watu wa aiina ya kakobe tunawaona watovu wa nidhamu, very same people tunapiga kelele ufisadi humu!

ukondoo huu mbaya jamani, watu wanapaswa kuwajibika na kuwa waona mbali hasa kwenye mipango miji, kwa style hii hakuna nyumba salama! unless kuna watu hawajui uchungu wa kujenga nyumba na kuhamishwa!

Iddi simba was right?? bado naangalia hii mechi!!!
 
Kama hakuna tatizo lingine ila ni sababu tu za kijinga zinazotolewa na kakobe.....basi ikibidi hata kanisa lake lipigwe marufuku kwani linapingana na mipango ya maendeleo.

magezi sababu gani za kijinga alizotoa Kakobe?
 
.......Hivi huyu Kakobe ni mwanasiasa au kiongozi wa dini? Maana hata simuelewei elewi, sasa kanisa na richmond/tanesco wapi na wapi.
 
Let us discuss the matter with independent mind tusiingie katika mitego ya ushabiki wa dini kwani itaharibu kabisa the way we discuss the issue

Kama 1:

Suala ni Fidia na Kakobe anastahili Fidia ( kwa mujibu wa Sheria) then Tanesco inabidi wamlipe fidia Vinginevyo itakuwa ni Ubabe usio na Msingi na Kakobe atasimama katika haki

Ila Kama Suala ni Athari za Nyaya za Umeme ( Field Strength), Kakobe anachemka kwa sababu hizo athari hawezi kuzithibitisha, na Kama anaamini zipo basi akae afikirie kwamba hata huo umeme unaotumika kwake umefika hapo ukipita juu ya paa za nyumba za watu all the way from power plant mpaka kanisani kwake, kama hajafikiria hivyo basi atakuwa ni mbinafsi tu
 
Sababu ya kufanya hivyo ni kugomea kung'olewa kwa mabango ya kanisa lao ili kupisha usimikaji wa nguzo za tanesco zinazotoka ubungo kwenda sub station ya makumbusho.

Nilifikiri ni kanisa linolobomolewa kumbe mabango tu????!!!!!
 
Pale alipojenga nafikiri ni residential plot na si for public use. amewanunua watu waliokuwa wakiishi pale na kujenga kanisa. sijui kama amebadilisha USE ya eneo lake hilo kama hajafanya hivyo ni makosa kujenga kanisa kwenye eneo lililotengwa kwa ajili ya makazi (residential)
Makanisa mengi (mf. RC) yanajengwa kwenye maeneo yaliyotengwa (public) na yenye nafasi, na wanapewa na mamlaka husika.
 
Pale kwenye kanisa la full gospel kuna vijana kama sabini na nne wamevaa ma tshirt yameandikwa tanesco muogopeni mungu kwa mbele na nyuma yameandikwa richmond imewashinda mnakimbilia makanisa.
Wamesema watakaa hapo hadi waje kutolewa kwa bunduki.
Sababu ya kufanya hivyo ni kugomea kung'plewa kwa mabango ya kanisa lao ili kupisha usimikaji wa nguzo za tanesco zinazotoka ubungo kwenda sub station ya makumbusho.

Sioni kama kuna mantiki yoyote ka kakobe kugomea na kutaka vita.

Haya tuone kama hilo jeshi lake litaweza kupambana na Dola chini ya Kova
 
Pale alipojenga nafikiri ni residential plot na si for public use. amewanunua watu waliokuwa wakiishi pale na kujenga kanisa. sijui kama amebadilisha USE ya eneo lake hilo kama hajafanya hivyo ni makosa kujenga kanisa kwenye eneo lililotengwa kwa ajili ya makazi (residential)
Makanisa mengi (mf. RC) yanajengwa kwenye maeneo yaliyotengwa (public) na yenye nafasi, na wanapewa na mamlaka husika.

Katika master plan ya Dar es Salaam lile eneo alilojenga kanisa kakobe lilikuwa ni Open space. Serikali imefumba macho siku zote sasa kama ataendeleza choko choko zake wanaweza kumtoa kabisa
 
Katika master plan ya Dar es Salaam lile eneo alilojenga kanisa kakobe lilikuwa ni Open space. Serikali imefumba macho siku zote sasa kama ataendeleza choko choko zake wanaweza kumtoa kabisa

Open Space....?????? dar kuna open space kweli? mbona zote zimekwisha uzwa. unaleta mambo ya azimio la arusha wakati wa azimio la mafisadi la zanzibar? Kakobe na Tanesco wacompromise tu!!! it is the only solution. Na Kakobe azingatie kuwa tanesco kupitisha pale si kwa nia ya kumkomoa. I think jazba badala ya busara imemtawala zaidi juu ya suala hili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom