Kaka yangu alizaa na mke wa mtu

Ozzie

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
3,217
1,259
Leo nimepigiwa simu na kaka yangu. Mazungumzo yetu yalikuwa kama hivi:
Bro: Hello… Mambo vipi?
Mimi: Poa tu
Bro: Hapo nyumbani hawajambo?
Mimi: Tunamshukuru Mungu sisi wazima
Bro: Mnaendeleaje?
Mimi: Aaah! Huku hakuna issue. Mambo 50/50. Bado tunateseka na mgao wa umeme.
Bro: Sasa Ozzie, kuna shemeji yako anakaa mitaa ya chini kule karibu na mto. Anasema alikuwa anakuona mara nyingi ukipita na gari.
Mimi: Nani huyo shemeji? Mbona mimi simjui? (Ninadakia nikiwa na hofu, isije ikawa kuna sehemu nimeharibu)
Bro: Yupo kule chini, yeye anakufahamu. Anasema huwa mnaonana mara kwa mara.
Mimi: Dah! Labda nitakuwa namfahamu, ila kuna dada huwa anakuwa kama anaonesha dalili za kunifahamu, lakini huwa nakausha. Kwani yeye ni mweupe?
Bro: Hapana! Atakuwa siye. Yeye ni maji ya kunde.
Mimi: OK! Sasa kwa nini anaogopa kunisalimia au kujitambulisha.
Bro: Aaah! Sijui, ila nadhani anashindwa namna ya kukuanza
Mimi: Basi mwambie kama tutaonana tena asisite kunisalimia na kujitambulisha (maana kwa sasa nimepunguza mizunguko ya mitaa ile). Lakini sijaelewa ni shemeji yangu kivipi?
Bro: Nilizaa naye bwana.
Mimi: Mbona mimi sijui kama ulizaa na mtu mwingine zaidi ya mama Phine (Nikadakia).
Bro: Aah basi tu! Kwa sasa mtoto ni mkubwa sana. Anasoma form one shule ya …. (Shule Fulani inasifika kwa kufaulisha wanafunzi)
Mimi: Aah, haiwezekani bwana. Kwanini unasema sasa baada ya miaka yote hiyo kupita? Mama anajua? (Baba alifariki kitambo)
Bro: Ndiyo, Mama anajua (Najua kanidanganya, Mama angejua angeniambia, na angemtafuta mtoto huyu)
Mimi: Sasa siku zote hizi nani anamhudumia mtoto? Wewe unapeleka pesa za matumizi na ada ya shule?
Bro: Hapana, sipeleki chochote. Yule dada ni mke wa mwanajeshi
Mimi: Duh, ina maana jamaa ameamua kuchukua mzigo wa kumtunza mtoto asiye wake.
Bro: Yeye hajui kama mtoto sio wake. Nilimpa mimba mkewe wakiwa kwenye ndoa.
Mimi: Duh! ebwanae? Ndiyo kipindi kile unavuta sigara na bangi nini? (kwa sasa ameokoka)
Bro: Aah! Mimi sijui. Sasa mwanamke kachanganyikiwa kichizi. Haachi kunipigia simu. Anasema siku zinapozidi kusonga mbele na ndivyo mtoto anavyozidi kufanana na mimi.
Mimi: Sasa si bora aende kwa mama kumtambulisha mtoto?
Bro: Kwanza anaogopa sana kwenda kwa Mama (naanza kujua Mama hajui), pili hata asipoogopa atamwambia nini yule mtoto. Unadhani anaweza mtambulisha kwamba ana baba mwingine?
Mimi: Yaani hapo balaa. Sasa mimi nitamwonaje huyo mtoto?
Bro: Nitamwambia akutafute mapema, akiwa na mtoto au hata asipokuwa naye
Mimi: Duh! Poa
Naombeni ushauri. Nimtafute huyu mtoto ili nimwone au nichunie tu.
 
achana na uzinzi wa kaka yako! kama anataka kuanzisha cha moto basi mwambie mwenyewe huyo mjeshi kichwa kichwa ambapo nina hakika kuwa atakachoambulia ni manundu, na ndicho anachostahili angalau kwa sasa....huyo mtoto si wake hapa duniani wala akhera.
 
Duh!! nahic kiti kinazalisha joto ....anyway kaambali na hiyo mambo aisee utalipuka jombaa ..........waachie waliyoianzisha wataimaliza .
 
Nakushauri mtafute mfahamu huyo mtoto then mkae familia kama familia mtoto afahamike na amjue baba yake halisi kwani ni damu yenu hiyo, afahamiane na ndugu zake,la sivyo mtaficha hadi lini?
 
Mjini hapa watu wengi ndio wako hivyo..mtaani kwetu jamaa ni kiongozi mkubwa serikalini na analea watoto wawili wa jamaa tulikua nae chuo..dunia!na hawa wake?lol..
 
kama mjeda amefunga nae ndoa kihalali basi bro ako hana chake, kwenye ndoa wanasema
kitanda hakizai haramu mradi tu mko kwenye ndoa,,sasa huyo bro ako kwani hana watoto
wengine !!!! mwambie ampotezeee
 
Kumbukeni tu kuwa wanajeshi wengi huwa wana access ya SMG au bastola na huwa hawachelewi kuzitumia wanapochanganywa.
 
kaka ukienda kumuona hakikisha unaenda na kikopo cha grisi, maana mjeda akikukamata tu umekatwa seal
 
....kaa chonjo,hiyo kesi haikuhusu!tena hama kabisa huko maana huyo mtoto pia atakuwa anafanana na wewe tu
 
Nashindwa kuelewa mke wa mtu unajiachia tuuuu mpaka unapata mimba, akili haifany kazi ama
 
kama unataka kumwagiwa tindikali na mwenye mali nenda! Mwambie kaka yako a-solve Kiranga chake mwenyewe
 
Back
Top Bottom