Kaka na Dada wapeana mimba

Edwin Chapa

Member
Jun 3, 2011
54
12
Katika hali isiyo ya kawaida,kaka na dada ambao mama zao ni mkubwa na mdogo wamepeana mimba,stori yenyewe ilikuwa hivi,huyu msichana aliyepewa mimba alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na kaka yake yaani mtoto wa mama yake mkubwa ambaye ni tumbo moja na mama yake mzazi, kipindi wapo katika mahusiano ndugu walikaa kikao cha kuwakanya na cha ajabu mama mzazi wa msichana mwenye mimba amekataa kabisa ya kuwa mwanaye hawezi kutembea na kaka yake kwani bado mdogo na tena ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza.

Ndugu wakahairisha kikao bila maamuzi, ikapita kama muda hv ndugu wakaona mabadiliko ya yule msichana ndipo jana wakenda kumpima na kukutwa ya kuwa ana mimba ya miezi saba na akamtaja ya kuwa mwenye mimba ni kaka yake ambaye ni mtoto wa mama yake mkubwa.

Naombeni ushauri wa kumpatia huyu dada kwani hajawahi kwenda kliniki hata siku moja na pia mwaka huu ndo anaingia kidato cha pili...Hii ni kweli kwani mimi ni mmoja wapo wa ndugu
 
Ushauri unaoomba ni upi sasa? Kama mnajadili jambo la kwenda kliniki hata nyie mnahitaji kujadiliwa!!!!!!....kliniki siyo jambo la kujadili, MPELEKENI kwa ajili ya usalama wake na usalama wa mtoto aliyeko tumboni.

Na kama wao wako tayari kuoana fungisheni ndoa, kwishnei! Huyo mama yake alikuwa haamini kama katoto chake wanakachakachua, na akachukua nafasi ya mwanae kukataa kwamba anatembea na kaka yake!!

..akili yake inahitaji kujadiliwa! Haya mambo ya kukaa wanandugu KUJADILI KUJADILI KUJADILI KUJADILI hata mambo yasiyo na msingi ni upotevu wa muda na rasilimali! Mimba tayari anayo, kuzaa si suala la kujadili!
 
hapo hakuna tatizo kibaiolojia, kidini, kijamii. wapeni baraka na ushirikiano
 
Ndg yangu hata kuomba hujui yaani unatuelekeza tukupe ushauri ambao tayari umetuelekeza. Kama hajawahi kwenda kliniki jibu lake unalo yatakiwa aende. Je kama hajawahi kwenda kliniki unadhani ingemsaidia asipate mimba??? Kwa kifupi tabia ya Kaka na Dada kufanya mapenzi ni tabia ya kizazi kipya na sasa hata inatokea hata wazazi nao wanajaza mimba watoto wao. Hii ni laana ya kizazi hiki cha nyoka.

Unaangalia picha za ngono mbele ya watoto wako unadhani mwisho wake nini??? Ninajisikia uchungu sana kwa stori hii. Ushauri wangu turudi kwenye mila zetu za zamani ambapo hata kumuangalia angalia dada yako tu ilikuwa ni kosa na endapo jamii inayokuzunguka iliweza kubaini tabia yoyote chafu waliweza kushirikiana na kumkanya kijana.

Lakini leo hii usijaribu kumkanya kijana wa jirani yako kwani unaweza kuishia Segerea. Mwambie huyo binti aende kliniki kwani muda si mrefu atakuwa mama-shangazi na kijana atakua baba-mjomba.

Hongereni "KIZAZI KIPYA"
 
Waoane ila kwa dini ya kikristo sijui utaratibu ukoje maana hao ni ndugu. Mwenye kujua zaidi atujuze na je kama ndoa itashindikana mtoto atakuwa wa nani yaani babake
 
Ngoja nitafute maandiko kwenye baibo ndo naweza kulaani kubariki.

Tunaongozwa na biblia sio hisia za watu flani au jamii.
 
Maoni yangu mimi,kwanza wamrudie Mungu,ili hilo pepo la ngono liwaachie,Pili huyo binti aende klinic,tatu wa mwombe Mungu wao msamaha kwa dhambi hiyo ya aibu.
 
Alaaniwe yule alalae na "umbu lake yaani binti wa mama yake" Maandiko haya yapo ndani ya Biblia sipakumbuki. Hivyo ni makatazo tosha wala hatuhitaji kupindisha Katiba Hii ya Mwenyezi Mungu.
 
hivu kuna maandiko yanakataza hilo?...huyo aliyempa mimba mwanafunzi sheria ichukue mkondo wake...
 
Kwa jirani zetu wa Rwanda na Burundi mambo ya kawaida sana hayo.
 
Ndg yangu hata kuomba hujui yaani unatuelekeza tukupe ushauri ambao tayari umetuelekeza. Kama hajawahi kwenda kliniki jibu lake unalo yatakiwa aende. Je kama hajawahi kwenda kliniki unadhani ingemsaidia asipate mimba??? Kwa kifupi tabia ya Kaka na Dada kufanya mapenzi ni tabia ya kizazi kipya na sasa hata inatokea hata wazazi nao wanajaza mimba watoto wao. Hii ni laana ya kizazi hiki cha nyoka. Unaangalia picha za ngono mbele ya watoto wako unadhani mwisho wake nini??? Ninajisikia uchungu sana kwa stori hii. Ushauri wangu turudi kwenye mila zetu za zamani ambapo hata kumuangalia angalia dada yako tu ilikuwa ni kosa na endapo jamii inayokuzunguka iliweza kubaini tabia yoyote chafu waliweza kushirikiana na kumkanya kijana. Lakini leo hii usijaribu kumkanya kijana wa jirani yako kwani unaweza kuishia Segerea. Mwambie huyo binti aende kliniki kwani muda si mrefu atakuwa mama-shangazi na kijana atakua baba-mjomba. Hongereni "KIZAZI KIPYA"

Super view!
 
Alaaniwe yule alalae na "umbu lake yaani binti wa mama yake" Maandiko haya yapo ndani ya Biblia sipakumbuki. Hivyo ni makatazo tosha wala hatuhitaji kupindisha Katiba Hii ya Mwenyezi Mungu.

Binti wa mama yake hiyo ni sawa inaeleweka kwani ni ndugu yake halisa (yaani tumbo moja kwa kiswahili). Jee binti wa mama mkubwa/ mdogo (binamu)? Hapa ndipo penye issue.
 
Hao sio kaka na dada, hao ni binaam. Anaeweza kufanya ngono nje ya ndoa, huyo hana tofauti na mnyama na anaweza akafanya ngono na yeyote yule hata kaka yake wakuzaliwa tumbo moja au baba yake mzazi. Kitamshinda nini ikiwa kaweza kumvulia mtu wa nje nguo?
 
Back
Top Bottom