Kainerugaba Msemakweli anatumiwa - Saed Kubenea

Watanzania ni wepesi sana kupotoshwa. Kwanza tuangalie alichosema Msemakweli, na tuangalie nyaraka alizowasilisha na anayekuja na hoja mpya, awasilishe nyaraka. Naamini mwandishi wa makala hii (Kubenea) anazo nyaraka kuonyesha CCM walitumia fedha za EPA na si yeye tu wako wengi wenye maelezo kama hayo.

Ni vyema kuyaanika lakini si kusema Msemakweli kakosea. yeye kasema ushahidi alionao ndio huo. Mwingine aje sema na mimi ushahidi ni huu, ili wahusika wawafuate kina Maranda gerezani na si kuendelea kutuchezea akili.

Pia tuangalie Msemakweli ameleta matokeo gani tangu aaanike hayo masuala hadharani. Je kuna wakati wowote Serikali iliamka na kulishukia njuga suala hili? Je kuna wakati wowote Bunge liliamua kufany kitu chochote kama taasisi kabla ya hapo? Je kuna muda wowote Yusuph Manji alitoa taarifa yoyote kuhusu hili na kushutumu KAGODA yenyewe kutoa siri kabla ya hapo?

Yusuph Manji amedai kurejesha fedha alizopewa na KAGODA lakini hamtaji kAGODA ni nani. Yusuph Manji anadai KAGODA mwenyewe ndioe anayetoa siri. Waziri Meghji alituambia KAGODA ni usalama wa Taifa Je kuna ukweli wowote kuwa KAGODA ni usalama wa Taifa? Iweje Usalama wa Taifa ummpe hela Yusuph Manji kupeleka CCM halafu tena usalama wa Taifa utoe siri na nyaraka na kumpa Msemakweli.

Je, KAGODA ni usalama wa Taifa kweli? Au KAGODA ni muasi kutoka ndani ya CCM au KAGODA ni mmoja wa mafisadi ambaye aidha anataka au ametolewa kafara kuwaacha wengine wanusurike lakini yeye hataki kufa peke yake. Nani huyo KAGODA?

Yusuph Manji anamjua, Rais anamjua na CCM inamjua na wanajua nguvu zake na pengine hata inamuhofia.

Nadharia yangu ni kuwa KAGODA alitengeneza gamba na kulitumia kuwaficha wengine ndani ya gamba hilo. Akaonekana yeye peke yake. Sasa ametakiwa ajivue gamba ili abaki uchi.

Yeye alitengeneza gamba kuwaficha wengine kwa matarajio ya kufichwa na yeye kwani na wengine pia akiwafikisha walipo watakuwa na magamba ya kumficha. Wamemgeuka na kumtaka ajivue gamba abaki uchi. Kwa kuwa staha yake inaharibika wakati aliowasitiri wakiendelea kuheshimiwa nae ameamua nao kuwavua magamba. Sasa anataka kutuambia kuwa tulichokiamini ni uongo alioutengeneza wakati ukweli wenyewe ndio huu.

Mwache Msemakweli aseme kwani waliotengeneza uongo kuwa ukweli na bado wanataka watu waendelee kuamini kwa maslahi yao watabishana na wale walioutengeneza uongo kuwa ukweli na sasa wanataka wananchi waufahamu ukweli halisi ili anagalau kuhifadhi kaheshima kao kadogo kalikobaki. Mavuno yetu watanzania tutafahamu kuwa hawa wote ni majambazi sasa wanagombana baada ya kutoafikiana namna ya kugawana kile walichopora.

Bila kugombana wenyewewe kwa wenyewe sisi hatutopata kitu, mwacheni Msemakweli aseme.
 
Shahidi zikishakinzana then tunawrite off!! NI UZUSHI!! Mafia masterminds good deal thanks Kubenea.
 
Hili gazeti kama limeingia akili mwangu, tokea huyu Msema kweli atoke na hii single yake michango yangu juu ya hoja zake imekuwa ikihoji haya maswali na anafanya kazikwa maslahi ya nani?

Nilifikia hatua katika mchango mmoja kusema kuwa anatumiwa na CCM na hasa kwasababu ya Uchaguzi wa Igunga.
 
picture-4.jpg

Na Saed Kubenea - Imechapwa 07 September 2011

Gumzo la Wiki



MTU huyu anatumika kuficha ukweli. Ni Kainerugaba Msemakweli. Anasema mabilioni ya shilingi yaliyokwapuliwa na kampuni ya Kagoda Agriculture Limited (KAL), ndani ya Benki Kuu ya taifa (BoT) hayakutumika kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

Anasema wezi wa Kagoda walichota fedha BoT, Februari 2006, na kwamba uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani ulimalizika Novemba 2005. Yote haya yanaonyesha jinsi Msemakweli, ama anavyotumika bila kujijua, au anavyotumiwa na watu wenye malengo binafsi.

Kile ambacho wengi hawajakifahamu, ni nani anayemtumia Msemakweli. Je, aweza kuwa anatumiwa na Kagoda au anatumiwa na wapinzani wa Kagoda?

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari (Alhamisi iliyopita jijini Dar es Salaam, Msemakweli amekuja na madai mawili makubwa. Kwanza, fedha za Kagoda hazikutumika kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Anasema ushahidi wake ni "nyaraka zinazoonyesha Kagoda iliiba fedha BoT, Februari 2006 na ilizisafirisha nje ya nchi Machi 2006."


Pili, Msemakweli anatetea Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa hakikutumia sehemu ya fedha hizo kuingia madarakani. Hatua hii inaleta maswali mengi kuliko majibu; yakiwa ni pamoja na iwapo Msemakweli anafahamu anachikitenda.

Kwanza, hati ya kiapo ya wakili Bhyidinka Sanze wa kampuni ya mawakili ya Malegesi – Malegesi Law Chambers – ya Dar es Salaam, kwa Kamati ya rais ya kushughulikia wizi kwenye akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), inaeleza fedha za Kagoda ziliibwa ili kufanikisha kampeni za CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.


Sanze anakiri kuwa ni yeye alishuhudia "…mikataba ya Kagoda na makampuni mengine ya nje."


Andishi lake linaeleza kuwa Rostan Aziz, Peter Noni na Bered Malegesi walimthibitishia kuwa Rostam alikuwa kwenye kikao ambako rais mstaafu Benjamin Mkapa alitoa maelekezo kwa Gavana wa BoT, Dk. Daudi Ballali kutoa fedha hizo kwa Rostam kwa ajili ya uchaguzi.


Sanze anasema, "Niliitwa na Bw. Malegesi ofisini kwa Bw. Rostam Aziz…Nilipofika…niliwakuta Bw. Rostam Aziz, Peter Noni (Mkurugenzi Mtendaji wa sasa wa benki ya raslimali) na Bw. Malegesi; wakaniambia fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya kugharamia uchaguzi wa CCM na rais wake."


Hili ni andishi ambalo mpaka sasa halijakanwa na serikali, Mkapa, Rostam, Sanze, Meregesi wala Peter Noni.


Je, Msemakweli anayedai amefanya utafiti wa suala hili kwa miaka miwili mfulululizo hajaliona andishi hili? Hakulitafuta? Kama ameliona, kwa nini anataka kuficha ukweli? Kama hakuliona, kwa nini hakuuliza walilonalo?

Kama hakuliona andishi la Sanze, hakulitafuta na hakuuliza walilonalo, anatoa wapi ujasiri wa kusema, "fedha za Kagoda hazikuibwa kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2005?" Anamtumikia nani na nani anataka kumuokoa au kumzamisha?

Kampuni ya Kagoda ilikwapua jumla ya dola za Kimarekani 30,732,658.82 (Sh. 40 bilioni) katika Akanuti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya BoT.


Fedha hizi ziliibwa kati ya Septemba 2005 na Novemba 2005. Kagoda ilifanikiwa kuchukua fedha BoT na kuzipitisha katika matawi saba ya benki ya CRDB jijini Dar es Salaam kwa mtindo wa "kuingiza na kutoa papo hapo."


Aidha, serikali imekuwa ikijikanyaga kuhusu wizi huu. Aliyekuwa waziri wa fedha, Zakia Meghji aliwaandikia maodita wa kampuni ya Deloitte & Touche ya Afrika Kusini akisema, fedha za Kagoda zilitumika kwa "kazi za usalama wa taifa."


Katika barua yake ya 15 Septemba 2006, Meghji anasema, "Kama unavyofahamu vema, mamlaka ya serikali huwa na siri, vilevile haja ya kugharamia matumizi ya busara.


"Kwa hiyo... malipo ya dola 30,732,658.82 za Marekani yaliyofanywa na BoT kwa Kagoda Agriculture Limited, yaliidhinishwa na serikali kugharamia matumizi yake nyeti na ilikuwa lazima kuchukua hatua hii ya kudumisha usiri huu."


Msemakweli anajichanganya pia katika eneo jingine ambamo anamtaja mmoja wa wafanyabiashara mashuhuri nchini, kwamba ndiye aliyesafirisha fedha hizo Machi 2006.


Lakini nyaraka ambazo amezitumia kupeleka shauri hilo kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), zinaonyesha mfanyabiashara anayemtaja, ameingia mkataba wa kukopeshana fedha na Kagoda 12 Septemba 2005, kipindi ambacho Kagoda yenyewe ilikuwa haijasajiliwa.


Kuna visingizio vingi vimetumika kuhalalisha wizi huu na kutaka kuisafisha CCM. Kwa mfano, mara kadhaa serikali kupitia Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamnbana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Waziri wa Fedha, Mustaph Mkullo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba na DPP, Eliezer Feleshi wamedai, kwa nyakati tofauti kuwa Kagoda haifahamiki na haijulikani iliko.


Lakini ni Kagoda inayodaiwa kumuondoa nchini aliyekuwa gavana wa BoT, Dk. Daud Ballali. Baadaye serikali ikaeleza, "gavana Ballali ameaga dunia."


Pili, Msemakweli anasema fedha zisingeibwa mwaka 2006 ili kutumika mwaka 2005. Hata kama tukikubaliana na Msemakweli, kwamba fedha ziliibwa benki mwaka 2006, bado huo hauwezi kuwa utetezi.


Je, haiwezekani wezi wa Kagoda wakaipa CCM fedha mwaka 2005 kwa makubaliano kuwa wajilipe mwaka 2006 kwa kutumia EPA?


Nyaraka zinaonyesha kuwa hata kabla kampuni hiyo kusajiliawa, Kagoda tayari ilishachota sehemu ya fedha ilizokwapua.


Kwa mfano, aliyeitwa Meneja Mkuu wa Kagoda, John Kyomuhendo anaonekana akimwandikia Gavana wa BoT tarehe 12 Septemba 2005. Barua nyingine ya Kagoda, ikikumbushia nia ya kuhamisha fedha kutoka BoT iliandikwa tarehe 7 Oktoba 2005.

Naye gavana anajibu mawasiliano hayo kwa barua Kumb. Na. 6054/1355 ya 13 Oktoba 2005 inayofuatwa na barua ya Kagoda ya 20 Oktoba ikielekeza uhamishaji wa fedha kwenda benki.

Maelekezo ni kwamba fedha hizo ziwekwe kwenye akaunti Na. 01J021795700 iliyoko benki ya CRDB tawi la Holland jijini Dar es Salaam.


Barua kutoka Kagoda inayoelekeza jinsi ya kuhamisha zaidi ya Sh. 25 bilioni ilipokelewa na benki siku hiyohiyo ya 20 Oktoba 2005, kuwekwa katika faili na kupewa namba (folio) 7.


Wakati mawasiliano yote yakifanyika, ikiwa ni pamoja na kuchota mabilioni ya shilingi, Kagoda ilikuwa haijasajiliwa. Biashara ilikuwa "mali kauli."


Kagoda ilisajiliwa na Msajili wa Makampuni (sasa wakala wa usajili wa makampuni – BRELA) tarehe 29 Septemba 2005 na kupewa hati Na. 54040, huku wakiwa tayari wamekwapua mabilioni ya shilingi kwa kauli tu.


Pamoja na uhalifu huu wa wazi wa Kagoda, kwa kushirikiana na BoT, ambao ulifahamika kwa wajumbe wa Timu ya Rais na bila shaka kwa rais mwenyewe, Msemakweli anataka kulinda wezi.


Hapa inaonyesha jinsi Msemakweli alivyokuwa tatizo badala ya suluhisho katika sakata la Kagoda. Kisheria, Msemakweli anageuka shahidi tata au shahidi adui, na kwamba vyombo vya – upelelezi (ofisi ya DCI, DPP na TAKUKURU), ni sharti viwe makini naye.


Shahidi anayefunua ukweli na kuufunika hapohapo huwa ana dalili za kutumiwa na wale anaodai kuwa anawashitaki bila yeye kujijua. Msemakweli anajua, kwamba Rais Jakaya Kikwete aliunda Kamati Maalum ya rais ya kufuatilia walioiba benki. Anafahamu Kamati Maalum ya rais ilivyomweleza Rais.


Kwamba baadhi ya wezi waliorudisha fedha na kusamehewa kinyume cha sheria, wanalalamika kutapeliwa kwa kuwa wamelazimika kurudisha hata fedha ambazo walizigawa kwa CCM ili kufanikisha harakati zake za uchaguzi mkuu wa 2005. Miongoni mwao, ni Kagoda Agriculture Limited.


Kama Msemakweli hayafahamu haya, basi hana sababu ya kusema amefanya utatiti. Aseme, "Nimehadithiwa na walionituma." Ikiwa wezi wenyewe wanakiri kurudisha fedha kwa niaba ya Kagoda, Msemakweli anapata wapi ujasiri wa kuisafisha CCM kuwa haikuchukua fedha hizo?

Vilevile, wanaotuhumiwa kuiba fedha kwa mgongo wa Kagoda, wanalalamikiwa na baadhi ya wana-CCM, kwamba hawakuwakilisha fedha yote waliyoiba benki ndani ya
chama. Badala yake, wanadaiwa kutumia fedha hizo kujitajirisha binafsi.


Ni utajiri huo ndio unaotumika kuwanyanyasa wale ambao hawakupata mgawo. Je, madai haya ni ya uongo? Kama ndiyo, mbona ndani ya CCM kumeibuka minyukano isiyoisha, inayotokana na tuhuma za wizi wa fedha hizo, kwamba baadhi ya wanaotuhumiwa kushiriki wanasema zimetumika kuingiza serikali hii madarakani?

Rais Kikwete mwenyewe siyo tu anaamini hivyo, bali mbele ya wananchi anatazamwa kama mtoto wa Kagoda na mjukuu wa EPA.

Hata baadhi ya wananchi wa kawaida, wakiwamo wana-CCM na viongozi wake, wanaamini Kagoda ndiyo iliingiza serikali hii madarakani. Kagoda ndiyo sababisho la minyukano isiyokwisha ndani ya chama.


Aidha, ni kiini cha kuibuka kwa tamthilia mpya ya kujivua gamba na ndiyo sababu ya serikali kuingia katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni Igunga, miezi 10 baada ya kumalizika uchaguzi mkuu.


Katika mazingira haya, wananchi wamebaki na jambo moja la kuamini. Kwamba ni kweli kuwa Msemakweli ametumwa na waliomtuma wanafahamika. Ni wale waliokuwa mstari wa mbele kujionyesha wanapambana na ufisadi, lakini papohapo wakikumbatia ufisadi wa kisingizio cha kuitetea CCM.


Ndiyo msingi wa madai yake haya. Kwamba "fedha za Kagoda hazikutumiwa kufanikisha mgombea wa CCM kuingia madarakani."


Jambo moja ni muhimu. Hatua ya Msemakweli kutetea CCM, kwamba haikutumia fedha za Kagoda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, inazidisha kiu ya wananchi kutaka kufahamu Kagoda ni nani na ana uhusiano gani na Msemakweli anayemtetea?


Jingine ambalo wananchi watataka kufahamu kwa kutumia mizani ya Msemakweli, ni serikali inashughulikia vipi "ukweli" aliousema Msemakweli na kuachana na propaganda zake za kuwasafisha wezi.




Rostam Aziz and Yusuf Manji orchestrated and financed a campaign to spread misinformation that the monies stolen by Kagoda Agriculture Company Limited and Quality Finance Corporation Limited were used to finance the 2005 CCM election campaigns. This propaganda concealed the following salient facts that:

a. CCM does not and has never directly or indirectly owned or been involved with any of the companies which are implicated in the fraud which are Kagoda Agriculture Company Limited, Quality Finance Corporation Limited and Afritainer (T) Limited;

b. Only a sum of Tshs 3,081,648,500 out of the criminal proceeds stolen from the Bank of Tanzania was withdrawn from the accounts of Kagoda Agriculture Company Limited as cash in the period between November and December 2005;

c. The sum of Tshs 31,710,000,000 representing the bulk of the criminal proceeds was transferred from Kagoda Agriculture Company Limited to the Quality Finance Corporation Limited during the first week of January 2006 vide 4 banker's cheques dated the 27th and 29th December 2005 and 2nd January 2006. By this time the national elections had already taken place.

d. The criminal proceeds transferred from Kagoda Agriculture Company Limited to the bank account of the Quality Finance Corporation Limited remained in that account for several months way past April, 2006 more than 4 months after the national elections had taken place.

e. From the account of Quality Finance Corporation Limited the criminal proceeds were not paid to any person, company or to CCM but instead smuggled out of Tanzania over a period of several months so as not to raise suspicion.
 
Shahidi zikishakinzana then tunawrite off!! NI UZUSHI!! Mafia masterminds good deal thanks Kubenea.

Kufikiri kwataka akili. Ukitegemea kuwa kuna mtu yupo kwa ajili ya kukusaidia kufikiri na wewe ungoje kukariri na kunakiri basi hautahitaji kuwa na akili na wala hutaona umuhimu wa kufikiri kwa sababu yupo mwenye akili wa kukusaidia kufikiri. Ingawa hujui urefu wa maisha kwa kuwa akili za kufikiri hazipo wala hutataka kufikiri atakapokufa nani atakusaidia kufikiri. Majibu rahisi, maswali magumu
 
Kubenea tunaomba na wewe uje na ushahidi wa "Makaratasi", vinginevyo mimi nadhani wewe ndiye unayetuchezea akili zaidi ya MsemaKweli!
 
Kubenea tunaomba na wewe uje na ushahidi wa "Makaratasi", vinginevyo mimi nadhani wewe ndiye unayetuchezea akili zaidi ya MsemaKweli!

Huyo kubenea alikuwa wapi muda wote?

Yeye kama alikuwa na ushahidi angejitokeza mapema si kusubiri wengine waje yeye apande kwa juu huo ni unafiki?

Kama una ushahidi wa kutosha zaidi ya msemakweli panda hewan ita wandishi wa hbr wenzio then ruka mpaka kwa DPP akupe muongozo?

Tumia vizuri katiba Ibara 26 kifungu (1&2)
Ibara ya 27 kifungu (.1&2)
 
Rostam Aziz and Yusuf Manji orchestrated and financed a campaign to spread misinformation that the monies stolen by Kagoda Agriculture Company Limited and Quality Finance Corporation Limited were used to finance the 2005 CCM election campaigns. This propaganda concealed the following salient facts that:

a. CCM does not and has never directly or indirectly owned or been involved with any of the companies which are implicated in the fraud which are Kagoda Agriculture Company Limited, Quality Finance Corporation Limited and Afritainer (T) Limited;

b. Only a sum of Tshs 3,081,648,500 out of the criminal proceeds stolen from the Bank of Tanzania was withdrawn from the accounts of Kagoda Agriculture Company Limited as cash in the period between November and December 2005;

c. The sum of Tshs 31,710,000,000 representing the bulk of the criminal proceeds was transferred from Kagoda Agriculture Company Limited to the Quality Finance Corporation Limited during the first week of January 2006 vide 4 banker's cheques dated the 27th and 29th December 2005 and 2nd January 2006. By this time the national elections had already taken place.

d. The criminal proceeds transferred from Kagoda Agriculture Company Limited to the bank account of the Quality Finance Corporation Limited remained in that account for several months way past April, 2006 more than 4 months after the national elections had taken place.

e. From the account of Quality Finance Corporation Limited the criminal proceeds were not paid to any person, company or to CCM but instead smuggled out of Tanzania over a period of several months so as not to raise suspicion.
Sijui kwa nini huyu Kubenea anamshambulia Msemakweli wakati kila kitu kiko wazi. Aje na ushahidi kupinga ukweli kuwa zaidi ya 90% ya pesa yote ilihamishiwa nje baada ya uchaguzi kumalizika.
 
Msemakweli anatumiwa na CCM (according to Kubenea), jee na yeye Kubenea anatumiwa na nani!!!

Nilivyomuelewa Msemakweli ni kwamba kulinguwa na mchezo mchafu zaidi katika suala zima la Kagoda, nalo ni money laundering, USD walizokwapua BOT walizihamisha baada ya kuzisafisha kwenye benki zetu wenyewe ie CRDB, benki zingine ziligoma kwa sababu zilinusa kuwepo kwa uhalifu huo. Kuna waziri alimtamkia Kimei wakati wakizindua tawi la CRDB kuhusu benki hiyo kutumika kusafisha fedha haramu.

Fedha inayonekana kuchangiwa na kina RA kwenye kampeni za CCM ni za madafu wanazokwapua kupitia miradi yao feki hapa nchini.

Kubenea katika hiyo makala ameonyesha uwezo mdogo wa kuchambua mambo, na yote hii ni kutokana na hulaka yake ya kujadili personalities badala ya issues.

Msamakweli kasema ukweli zaidi ya porojo za kina kubenea, amezama na kuibua tatizo kubwa linaloikabili nchi la money laundering, aungwe mkono na sio kumbeza.

Mbona Kubenea hatuelezi naye anavotumika na hao jamaa. Jambo moja analopaswa kukumbuka ni kwamba Watanzania sio Mabwege, tunaelewa kinachoendelea, hata mlengo wa hiyo makala unaeleweka.
 
The missing link kwenye version ya Msemakweli ni mahali pesa zilipokwenda akiamini zilitoroshewa nje ya nchi. Vielelezo vya Msemakweli ni toilet paper which is rubish after use.

Kwa lugha nyingine baada ya Kagoda kutumia fedha zile kwa matumizi yaliyokusidiwa wakafanya paper work ili kuisafisha CCM na Msemakweli akaingia maboya. Kitu ambacho Msemakweli hakukitaja ni jina la hilo duka lililotumika kizisafirisha fedha hizo kwa sababu angetaja ingekutikana there was no any transfer of funds.

BOT ndio ina-monitor foreign transfer kwenye maduka yote ya fedha hivyo kama ilifanywa transfer BOT wanayo record na kwa vile Msemakweli hakulitaja jina la hilo duka wala, hakuna details za transfer then the truth transfer ni kwa CCM kufidia madeni ya uchaguzi.
 
Jamani eeh hadanganywi mtu hapa!! Kama CCM hawakutumia kagoda kuingia madarakani kigugumizi cha kuichukulia hatua kinatoka wapi mika yote hii? Na kwanini CCM waliamua "kumuuwa" Balali kiaina? Na kwa nini Megji alitangaza kagoda inahusika na usalama wa nchi? Je PCCB, polisi na wanasheria wa serikali wameshindwa kujua ukweli kuhusu kagoda kwa kutumia tume ya rais huyu mtu mmoja ndo aje ya taarifa ya ukweli kwa kuwasafisha CCM? Huu uwongo wote wa CCM na serikali yake ni wa nini??

Hatudanganyiki na huyu boya wenu msemauwongo, CCM wote ni majizi tu.
 
We unaejii NSESI acha kuandika mambo kibwana mdogo hapa. Ebu andika maana na money laundering hapa uone ulivyoenda chaka kwa uliyo yaandika. Kimsingi wanaoficha ukwapuaji na matumizi ya pesa ya KAGODA ni CCM na Kikwete na ndo wanaofanya money laundering hapa kwa maana yake nyepesi.
 
Jamani eeh hadanganywi mtu hapa!! Kama CCM hawakutumia kagoda kuingia madarakani kigugumizi cha kuichukulia hatua kinatoka wapi mika yote hii? Na kwanini CCM waliamua "kumuuwa" Balali kiaina? Na kwa nini Megji alitangaza kagoda inahusika na usalama wa nchi? Je PCCB, polisi na wanasheria wa serikali wameshindwa kujua ukweli kuhusu kagoda kwa kutumia tume ya rais huyu mtu mmoja ndo aje ya taarifa ya ukweli kwa kuwasafisha CCM? Huu uwongo wote wa CCM na serikali yake ni wa nini??

Hatudanganyiki na huyu boya wenu msemauwongo, CCM wote ni majizi tu.

akili za watu zinashangaza sana, Eti msemakweli anawasema akina Manji na Rostam kwa kuitetea CCM? Hivi huyu anayesema hayo akiambiwa aionyeshe CCM ataweza? Je CCM ni huyu mjumbe wa nyumba kumi hapa jirani kwetu? CCM ni katibu wa chama wa Wilaya au CCM ni Mwenyekiti na Sekretariati yake au Ni wafadhili wanaokipatia hela Chama cha mapinduzi? Jamani tufikiri kwanza kabla ya kusema chochote.

Kubenea eti analaumu CCM kwa wizi lakini hataki kuambiwa kuwa Manji na mwenzake ndiye waliofanya wizi. Eti kwani ni hela za Kagoda tu ndizo zilizotumika kuiweka CCM madarakani na zile nyingine basi zilienda wapi? nani ali audit?
 
The missing link kwenye version ya Msemakweli ni mahali pesa zilipokwenda akiamini zilitoroshewa nje ya nchi. Vielelezo vya Msemakweli ni toilet paper which is rubish after use.

Kwa lugha nyingine baada ya Kagoda kutumia fedha zile kwa matumizi yaliyokusidiwa wakafanya paper work ili kuisafisha CCM na Msemakweli akaingia maboya. Kitu ambacho Msemakweli hakukitaja ni jina la hilo duka lililotumika kizisafirisha fedha hizo kwa sababu angetaja ingekutikana there was no any transfer of funds.

BOT ndio ina-monitor foreign transfer kwenye maduka yote ya fedha hivyo kama ilifanywa transfer BOT wanayo record na kwa vile Msemakweli hakulitaja jina la hilo duka wala, hakuna details za transfer then the truth transfer ni kwa CCM kufidia madeni ya uchaguzi.
Duka lenyewe ni Macsons na alichoweka MSemakweli kama unavyosema wewe si toilet paper na hao MAcsons walihojhiwa na tume ya mwanyika na ilionekana kweli na maduka mengine kama Masai Bureau de Change yakafungiwa kwa mchezo hup\o wa kupeleka fedha nje kwa mtindo wa hawala.

Ukweli ni kwamba watu walijitengenezea fedha kwa mgongo wa CCM kwa kujifanya wametumia fedha zao na hii si mara ya kwanza. Mchezao huu unafanywa na majambazi wa kawaida kwa kujibebesha ukamanda wa CCM ama ufadhili kupata kinga.
 
Back
Top Bottom