Kaimu Mkurugenzi Mkuu Wa TAKUKURU Atangaza Kiama Kwa Wala Rushwa Hasa Watumishi Wa Umma

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
739
484
Asema:

  • TAKUKURU yatoa Onyo kwa wasimamizi wote wa fedha za serikali
  • Maofisa wa serikali wanatumia maduhuli ya serikali wazingatie kanuni na taratibu
  • Wasimamizi wa manunuzi ya serikali wawe makini
  • Ununuzi wa hati fungani za serikali uchunguzi unaendelea na hakuna atakaeachwa
  • Maofisa wa umma waliozoea kula rushwa wanashauriwa kama hawawezi kufuata utaratibu wa umma basi waaachie ngazi
  • TAKUKURU haita mwacha ofisa yoyote atakaekiuka kanuni za serikali katika matumizi ya fedha au kutumia cheo vibaya.

1.jpg


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (Takukuru), imetoa onyo kwa taasisi nyeti nne hapa nchini ikiwemo wanaohusika na matumizi ya fedha za Umma kufuata sheria, taratibu na kanuni.

Pia,Takukuru inashughulikia kukamilisha kesi kubwa 36, zinazowahusu watumishi wenye ushawishi na hadhi kubwa hapa nchini ambapo kati ya hizo zipo zilizokamilika na kupelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo , Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Valentino Mlowola alisema kumekuwepo na malalamiko mengi kwa wananchi kuwajulisha matendo ya rushwa na ufisadi yanayoendelea hapa nchini.

Alisema kutokana na hali ya wananchi kuona nia ya serikali ya awamu ya tano katika kushughulikia matatizo ya rushwa na ufisadi hapa nchini ametoa onyo kwa maofisa wa umma wanaofanya rushwa na ufisadi kuwa sehemu yao ya kazi na miradi ya kuwaingizia kipato.

“Natoa onyo kwa maofisa wa umma ambao wamefanya rushwa na ufisadi kuwa ni sehemu ya kazi zao na miradi ya kuwaingizia kipato, wajitafakari kabla hawajaamua kujihusisha na vitendo vya rushwa,”alisema.

Alisema hawatasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa watumishi watakaojiingiza katika kulihujumu taifa na wananchi kwani wananchi wanakiu ya kupata maendeleo na maisha bora na kuwataka watambue wananchi wa jana si wa leo kwani wamedhamiria kuunga mkono juhudi za serikali yao.

Mlowola alitoa onyo kwa maofisa maduhuli na watekelezaji wa jukumu la kukusanya kodi za wananchi kwa kutomuonea mtu haya kwa atakayejihusisha na ubadhirifu wa fedha na mali ya umma.

“Wakusanye kodi halali ya serikali kwa kufuata sheria, taratibu na Kanuni zinazowaongoza kukusanya kodi, tutachukua hatua stahiki pale kutakapokuwa na ukiukwaji wa sheria, taratibu na kanuni zilizopo,”alisema.

Pia, Mlowola alitoa onyo kwa watakaohusika kwenye matumizi ya fedha za umma kwamba wafuate sheria, taratibu na kanuni zinazowaongoza kwani taasisi hiyo haitawavumilia watakaokiuka fedha za serikali isiyo halali.

Mbali na hilo, pia Kaimu huo alitoa onyo kwa watumishi wa umma wenye jukumu la kuhudumia mahitaji ya umma kwa kutojihusisha na rushwa kwa kutekeleza majukumu yao katika muda uliotakiwa, weledi na uaminifu.

Alisema taasisi hiyo haipo kwa lengo la maslahi ya watu wabadhilifu wa mali ya umma kwani uchunguzi wa kesi ya kuisababishia hasara serikali shilingi bilioni 8.5 kutokana na ukwepaji wa kodi wa kampuni ya Mafuta ya Lake Oil kwa kufanya udanganyifu wa kuuza mafuta ndani ya nchi Petrol lita 17,461,111.58 kwa kudanganya zilisafirishwa umefikia hatua nzuri.

“Takukuru imekamilisha shauri hili na mtuhumiwa wamepewa miezi miwili kurejesha mikononi fedha zote .Tutawarudisha mahakamani endapo watashindwa kurejesha kiasi hicho,”alisema.

Alisema mbali na shauri hilo, wapo kwenye hatua nzuri ya kukamilisha ya uchunguzi wa kesi ya hati fungani ya malipo yaliyolipwa na kampuni ya Enterprise Growth Markert Advisor(EGMA), kiasi cha dola 6,000,000 kwa lengo la kuisaidai Tanzania kupata mkopo wa dola 600,000,000.

“Takukuru imebaini fedha hizo dola 6,000,000 zilitakatishwa na watumishi wa umma wasio waaminifu wakishirikiana na baadhi kutoka sekta binafsi huku wakijua fedha hizo wamezipata kwa njia haramu,”alisema.

Akizungumzia hatua aliyochukua rais, Dk. John Magufuli kwa kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO, Mhandisi Benhadard Tito kwa tuhuma zinazomkabili tayari wanachunguza shirika hilo la reli.

Alisema kulikuwepo na ukiukwaji wa kuwapata wazabuni kwenye ujenzi wa reli ya kisasa ya kimataifa(Standard Gauge) unaosimamiwa na Shirika la Hodhi la Reli Nchini(RAHCO), watuhumiwa wamekamatwa akiwemo raia wa Kenya aliyekuwa kwenye mchakato huo, Kanji Muhando.

Kaimu huyo alisema shauri la kesi ya mabehewa ya kokoto 25 ya shirika la reili nchini (TRL), ya kukiuka sheria ya manunuzi ya umma Na.21/2004 pamoja na kanuni zake kutoka kampuni ya Hindustha Engineering and Industries Limited limekamilika.

“Uchunguzi umekamilika na tumeshapeleka kwa mkurugenzi wa Mashtaka kuomba kibali cha kuwafikisha watuhumiwa waliobainika kujihusisha na matendo ya rushwa na ukiukwaji wa sheria, taratibu na kanuni za ununuzi wa umma mahakamani,”alisema.

Alisema rais alijipa kazi ya kutumbua majipu hivyo aliwasihi watumishi wa taasisi hiyo kutumikia wananchi kwa weledi huku akibainisha tayari wanatekeleza azma na dhamira ya rais ya kupambana na rushwa.

Akitolea ufafanuzi swala la kumsubiri rais kutumbua majipu ndio taasisi hiyo ifanye ufafanuzi, Mlowola alisema taasisi hiyo imejipanga vilivyo tangu Novemba 20 mwaka jana wakati rais alipohutubia bungeni alipoonesha dhamira na nia ya dhati ya kupambana na rushwa na ufisadi bila kumuonea mtu haya.

“Nitoe rai kwa wananchi kutoa taarifa ili tuweze kujua kabla hatujapigwa, tukiweza kuisaidia serikali kuokoa fedha kabla hatujapigwa zitasaidia wananchi kutoa elimu bure, upatikanaji wa dawa na mishahara mizuri,”alisema.

Alisema tayari wameshaanza kuchunguza madai ya aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kwani tayari wapo hata viongozi wakubwa.

Akizungumzia maofisa takukuru waliofukuzwa kazi a rais baada ya kukiuka maagizo ya rais ya kupata kibali cha kusafiri nje, alisema maofisa hao walikwenda kwenye mkutano wa taasisi za kupambana na rushwa uliofanyika Congo-Kinshasa.


Kaimu Mkurugenzi Mkuu Wa TAKUKURU Atangaza Kiama Kwa Wala Rushwa Hasa Watumishi Wa Umma | PPM Media
 
unafki tu. siku zote hawakujua kazi yao. fanyeni kazi kimya kimya kazi yenu ikiwa njema watu watawasifia wenyewe.
 
kama kweli kadhamiria aanze kwanza na mafisadi wa escrow maana wengine ni wenyeviti wa bunge. inauma sana mhimili mmoja wa nchi unaongozwa na fisadi. hii ni hatari sana.....
 
unafki tu. siku zote hawakujua kazi yao. fanyeni kazi kimya kimya kazi yenu ikiwa njema watu watawasifia wenyewe.
Lazima watangaze nia ili vibaka kama wewe ufahamu hii serikali si ile iliyopita....na yakikukuta usiseme haujaambiwa
 
Bila adhabu ya kunyongwa hadharani rushwa haiwezi kwisha katika nchi nyingi za Africa TANZANIA in particular
 
Angalau hiyo taarifa ya TAKUKURU itakuwa ya faraja kubwa kwa wale wafanyakazi waliokuwa wakifanya kazi kwa uaminifu mkubwa bila kutaka kupokea rushwa kwenye maeneo yao ya kazi.

Kwa kuwa siku zilizopita kulikuwa na dhana miongoni ya waTZ kuwaita 'mabwege' wale wafanyakazi waaminifu wanaoonekana hawataki kuzichangamkia fursa za kupokea rushwa kwenye ofisi zao na hivyo kuwafanya waendelee kuishi maisha ya kilofa.

Badala yake wale wafanyakazi waliokuwa wanaibuka na kupata utajiri wa haraka haraka, huko mitaani walikuwa wakisifiwa sana na kuonekana wajanja na kuyapatia maisha.

Lakini kwa mwenendo wa serikali hii ya awamu ya 5 inavyoendelea, upo uwezekano baadhi ya mafisadi, wameshaanza kimya kimya kuwakabidhi ndugu na jamaa zao mali zao hususani yale majumba yao ya kifahari, wakiamini wanapoteza ushahidi.

Hata hivyo kwa wale watakaoona wamepata Bingo na kuamini kuwa neema imewashukia kwa kupata nyumba hizo za 'chee' watambue kuwa mbele ya safari nyumba hizo zitakuwa za moto kwao na zitakuja kuwatokea puani.
 
Wapo baadhi ya watumishi wa Umma walikuwa wakionekana kufanya miujiza humu mitaani kwetu tunamoishi.

Utakuta kijana mdogo tu ambaye ametoka chuoni, anafanya kazi kwa kipindi kifupi sana cha chini ya miaka 2 lakini ameshakuwa bilionea kwa mali anazozimiliki, hususani 'mahekalu' mengi anayomiliki na anavyobadilisha magari ya kutembelea kama mwingine anavyobadilisha mashati yake anayovaa!

Na mbaya zaidi hao waTZ waliokuwa wakijipatia utajiri wa haraka haraka kwa kutuibia watanzania walifikia hatua ya kumkufuru Mungu wetu kwa kuwakebehi wale wote ambao ni walala hoi kuwa ni wavivu na wazembe na hawatumii akili zao vyema kuweza kuzichangamkia fursa zinazowajia!
 
unafki tu. siku zote hawakujua kazi yao. fanyeni kazi kimya kimya kazi yenu ikiwa njema watu watawasifia wenyewe.
Acha kuponda juhudi za serekali ni muhimu kutangaza ili watumishi wote waovu wasikie waache maramoja
 
kama kweli kadhamiria aanze kwanza na mafisadi wa escrow maana wengine ni wenyeviti wa bunge. inauma sana mhimili mmoja wa nchi unaongozwa na fisadi. hii ni hatari sana.....

Na sio hao mafisadi tu. Tumezoe kusema mafisadi wakati sisi wananchi tunatoa rushwa kila siku. Ukikamatwa tu na trafic hapo tunakimbilia kutoa rushwa. Je kuna mtanzania ambaye hajawahi kutoa rushwa?
 
Kesi 36 za watumishi wenye hadhi kubwa nchini ?? Je hiyo ni pamoja na Mwigulu na Nape au ??? Kwenye kampeni si mlijifanya kuwatuhumu ni watoa rushwa ??
 
hii issue ya mabehewa feki, nitashangaa mwakiembe asipoonekana mbele ya hakimu.
 
Na sio hao mafisadi tu. Tumezoe kusema mafisadi wakati sisi wananchi tunatoa rushwa kila siku. Ukikamatwa tu na trafic hapo tunakimbilia kutoa rushwa. Je kuna mtanzania ambaye hajawahi kutoa rushwa?

Swali hili inabidi kila mtu ashike msahafu wa kitabu anachokiamini, na nikuhakikishie kwa muumini wa kweli, hawezi kusema hajawahi kutoa au kupokea rushwa, kupata favor asiyostahili nk. Kumbuka kupata favor usiyostahili au stahiki ambayo siyo halali yako nalo ni kosa la kimaadili. Kwenye foleni tu unakuta mtu anajifanya anaharaka!
Rushwa, upendeleo, favor isiyostahiki, kujilimbikizia mali nk ni adui mkubwa wa Ustawi wa Nchi!
 
Kesi 36 za watumishi wenye hadhi kubwa nchini ?? Je hiyo ni pamoja na Mwigulu na Nape au ??? Kwenye kampeni si mlijifanya kuwatuhumu ni watoa rushwa ??

Je,na Mwenyekiti wa Bunge Mzee wa Vijisenti yumo?UDA je?Escrow wameiweka??Kama hizi hazipo basi bora wanayamaze maana tumeshazoea usanii
 
Je,na Mwenyekiti wa Bunge Mzee wa Vijisenti yumo?UDA je?Escrow wameiweka??Kama hizi hazipo basi bora wanayamaze maana tumeshazoea usanii
Yaani mimi sijui hata niamini nini Tanzania hii ?? Imefikia hatua sina imani na mtu au chombo chochote Tanzania hii ,tusubiri tuone
 
Yaani mimi sijui hata niamini nini Tanzania hii ?? Imefikia hatua sina imani na mtu au chombo chochote Tanzania hii ,tusubiri tuone

Unamwambia LAKE OIL ati usilipa ndani ya miezi miwili nakupeleka mahakamani shit....Amevunja sheria ,kesi ni ya uhujumu uchumi,ni criminal case kukwepa kulipa kodi,wizi wa mchana kweupe,leo unakuja na Bongo movie star search.........Halafu tunasema tuna TAKUKURU,hakika TAKUKURU ianhitaji TAKUKURU iii-TAKUKURU
 
Back
Top Bottom