Habari za Asubuhi wanaJF!
Kumekuwepo na umilikaji wa silaha za kivita, ambazo ni hatari na raia yoyote hapaswi kumiliki. Silaha hizo hutumika kwa ujambazi, katika mapori kadhaa yaliyo maeneo ya kanda ya ziwa na mikoa ya jirani. Silaha hizo zinatumika pia kwa ujangili na wizi wa mifugo katika maeneo ya hifadhi za taifa na kwa wafugagi. Aidha, silaha hizo pia zimethibitika kutumika katika vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi za Rwanda, Burundi na Congo.
Baba yangu ni mmoja ya watanzania waliopigana vita vya Kagera. Jana nilipata wasaa mzuri wa kuzungumza naye kuhusiana na vita vya Kagera. Pamoja na mambo mengine yahusuyo vita hivyo, naomba kuwasilisha hiki kipengele kidogo, "Improper Retreat of our Armies After the War"
Baada ya vita vya Kagera kuisha, kulikuwa na matukio mengi sana ya uporaji yaliyofanywa na wanajeshi wetu, matukio haya yalienda sambamba na kuuwana kwaajili ya kugombea vitu vilivyoachwa na waganda, kama redio, TV, pikipiki, magari na vitu vingine walivyoona ni vya thamani.
Pamoja na sababu nyingine, kama furaha ya ushindi, Vitendo hivi vilipelekea amirijeshi mkuu, Mwl. J.K Nyerere kuamuru majeshi yarudishwe nyumbani haraka sana.
Retreat haikufanywa kwa utaratibu unaotakiwa, kwa kawaida ingewalazimu kukaa huko Uganda hata angalau kwa kipindi cha miaka miwili.
Kutokana na kutofanywa vizuri kwa retreat, hapo ndipo wenzetu wakurya walipopata mwanya wa kujitwalia silaha kali na za kivita kwa idadi waliyoweza kuchukua. Katika kuhakikisha hili linafanikiwa, walitumia mbinu kama kuchonga majeneza na kukata vitako vya bunduki ili ziweze kuingia nyingi ndani ya jeneza na kuonekana kama wamebeba maiti, na kwasababu walikuwa wanatoka vitani, hawakuruhusu wakaguzi waangalie majeneza hayo.
Mbinu nyingine iliyotumika ni kuvaa vyeo vya ngazi ya juu, kama Kanari, meja, Captain na kupitisha mizigo bila kukaguliwa kwa kigezo cha cheo.
Pia jina la Msuguli, mkuu wa majeshi wakati huo na aliyeongoza vita hivyo, lilitumiwa vizuri kupitisha silaha hizo.
Hali ilivyo sasa. Kwa uchache tu, wilaya ya tarime eneo la Nyamongo ulipo mgodi wa ABG. Katika eneo hilo karibu kila mwanaume wa kikurya anamiliki silaha, kuna mahandaki ya kutosha tu yaliyojaa silaha kali za kivita kama sub-machine gun, machine gun na nyinginezo nyingi. Silaha hizi zimetumika sana na majambazi ambao ni matajiri sana wa kanda hii, wanaomiliki viwanda na makampuni makubwa ya usafirishaji abiria na mizigo.
Silaha hizo zinapelekea maeneo hayo yashindwe kutawalika kwa utawala wa sheria. Hivi karibuni kumeibuka vita, sijui kama watanzania wenzangu mmesikia hiyo!? Ni vita kali sana kati ya wananchi na vyombo vya dola, ulinzi na usalama, issue ni mgodi wa north mara.
Yote haya, pamoja na sababu nyingine, ni matokeo ya "POST WAR IMPROPER RETREAT"
Selikari, tafadhali ufanyike msako wa hali ya juu maeneo hayo, silaha zote zichukuliwe toka mikononi mwa hawa jamaa, hali ni tete sana! Ujambazi ni mkubwa sana na mauaji ni mengi sana ila watanzania hawapati habari hizi.
Naomba kuwasilisha.