Kagera: Tunahitaji bendera Mpya za CHADEMA na pia ziwe nyingi

Ta Muganyizi

R I P
Oct 19, 2010
5,361
2,734
Bendera za CDM kwa sasa ni dalili ya Ujasiri na Kuonesha kuwa uko tayari kwa lolote kuitetea nchi yako bila kificho kwa wana Kagera walio wengi. Zamani ili gari lako lisisimamishwe au ufanye shughuli zako bila bugdha ilibidi uwe na bendera ya CCM. Hali kwa sasa ni tofauti..........aliyetundika bendera ya CCM watu wanamshangaa wakiwemo hata watoto wa Primary..........wa msekondari ndo usiseme. Lakini kwa aliyetundika bendera ya CDM anapata heshima kwa sasa na kuonekana kuwa ni mtu aliyeko serious na anayeutngazia umma kuwa haungi mkono hali ya mambo ilivyo kwa sasa. Bendera za CDM zilizoko maeneo mengi hapa Kagera zimechakaaaa na kuonesha kuzeeka wakati chama kwanza ndo kinashika hatamu.

Tunaomba CDM watangaze wazi kuwa bendera hizo zinapatikana wapi, na ikiwezekana zigawiwe hasa kule vijijini ambako wanatamani kujitambulisha kwa jamii kuwa ni wanamapinduzi lakini wanakosa jinsi. Naomba ufafanuzi na response juu ya hili kutoka kwa wahusika.
 
Huo ndio ukweli wenyewe,tunapopita na magari sehemu za vijijini na kuona bendera za CDM huwa tunaambizana kuwa watu wengi wanataka mabadiliko ona bendera za CDM nilivyo nyingi, na tukiona za CCM ni nyingi tunaambizana hapa bado pana mambo ya kizamani. Hivyo kumbe bendera ni ishara fulani naomba viongozi wa CDM watoe bendera kwa wingi na wanaozihitaji muwe tayari kuzilinda
 
Mkuu yaani mwenye bendera wanamtamani na imefikia vijana hapa Bukoba mjini waendesha pikipiki wanaibiana bendera na kugombana sababu ya bendera............CDM fanyeni mpango mtuweke wazi.
 
Huo ndio ukweli wenyewe,tunapopita na magari sehemu za vijijini na kuona bendera za CDM huwa tunaambizana kuwa watu wengi wanataka mabadiliko ona bendera za CDM nilivyo nyingi, na tukiona za CCM ni nyingi tunaambizana hapa bado pana mambo ya kizamani. Hivyo kumbe bendera ni ishara fulani naomba viongozi wa CDM watoe bendera kwa wingi na wanaozihitaji muwe tayari kuzilinda

Uko sahihi bendera ya CDM ndo kitambulisho cha mtu aliyejikomboa kifikra. Juzi nilipita kijiji fulani Kibaha nikaona bendera ya CDM nikamuonyesha mwenzagu akasema huyu mwenye bendera ni shujaa kuliko Profesa wa UD maana haogopi kuji express katika ya CCM
 
Bado kidogo, na magwanda yatapanda bei, Ngoja nitafute la kwangu, nilifungie kabatini kungojea sherehe za ukombozi.
Siku yenyewe tutafungua bigscreen kila makao makuu ya wilaya ili wananchi wasioweza kufika taifa waweze kufuatilia kwa karibu. M4C Forever.
 
NikwTathimini yako ni ya kweli kabisa Ta Muganyizi. Nilikuwa kijiwe flani, watu walikuwa tayari hata kununua bendera za CDM kuliko kupewa bure za hiki chama kingine. Huu mvumo ni mkubwa kuliko ilivyotarajiwa. Sijui hadi 2015 itakuwaje, maana hekaheka zimeanza mapema.
 
Sasa jamani kama hili linaonekana tunalitatua vipi? Aingie basi kiongozi wa CDM aeleze kwenye Strategic Plan ya CDM mwaka huu sulala la bendera ambalo psychologically lina influence kubwa wanalisemea vipi?
 
Halafu kagera mnahitaji ukombozi wa fikra maana magamba yamewafunika majimbo yote. Huo usomi wenu uko wapi?

si ndo juhudi zenyewe hizo............hata hivyo tuna mmoja wa jimbo la Biharamulo..............na wananchi huku wanajuta ila wanasema ubunge wwaliwapa ccm ila Urais walimpa Slaa japokuwa hakushinda.
 
Nikweli Ta Muganyizi!! Mimi nilishapiga kelele sana hapa JF!! Nilishauri hata Dr. Slaa, badala ya kwenda Mwanza aende Kagera, Mwanza watu wameshajitambua pia kuna wabunge ambao wanaweza kueneza sera!
Hakika Bukoba tumekuwa kama yatima kwenye ukombozi!! Hata bendera ni tatizo!!? Nashindwa kuelewa kwanini tumetengwa kiasi hiki wakati wananchi wana mwamko wa kutosha!! Kinachotakiwa ni viongozi kupiga kambi kidogo tu hakika hutoamini macho yako!! Viongozi wetu wanaweka petrol kuliko na moto tiyari.eg:Mwanza, Arusha, Mbeya na Iringa!! Wakati kuna maeneo yanafuka moshi hata hawaji kupulizia angalau moto uwake!!

"EBU NIPE NAMBA YA RWAKATARE KAMA UNAYO MKUU." Tweyememu!!
 
Nilishangaa hata vijiji vya mkoa wa Lindi ndani kabisa kule nyumba zile za udongo bendera za CDM zinzpepea vizuri,
Viongozi wa CDM wangesambaza jeshi la ukombozi hasa vijana kuhamasiha vijijini,dalili ni njema
 
Huku Iramba mashariki Chadema inapendwa sana ila tatizo lililopo ni kukosekana kwa uongozi thabiti wilayani.
 
si ndo juhudi zenyewe hizo............hata hivyo tuna mmoja wa jimbo la Biharamulo..............na wananchi huku wanajuta ila wanasema ubunge wwaliwapa ccm ila Urais walimpa Slaa japokuwa hakushinda.
2015 mnatakiwa mlinde kura zenu ili ya Karagwe yasijirudie.
 
Mwana Kagera mwenzangu wazo lako la kuwa na Bendera nyingi za chama cha Demockarasia na Maendeleo ni zuri tu lakini nakuomba Uguswe na jambo moja tu kuhamasisha vijana wengi wajiandikishe wakati ukifika, waziuze shahada zao ukifika wakati wa kupiga kura, walinde kura zao kipindi muafaka kikifika, vijana wasibadilike kama vinyonga wakati wa kupiga kura,hapo bendera zileta maana sana katika mkoa wa Kagera.
Nasema hivyo kwa mifano mingi tu Ndugu W.Lwakatare alikuwa anaongoza katika mikutano yake kipindi cha Uchaguzi lakini ikifika wakati wa kupiga kura vijana wengi shahada wameuza zilikuwa zikiokotwa katika mabox kwenye njia Panda zote za mji wa Bukoba. vijana kwa wazee tuanze mshakamano kama mikoa mingine Ukombozi unahitaji umoja na sio maneno. Mujwahuzia.
 
Mwami, waba otakanyoile kakawa? Kuuza shahada na kulinda kura wapi na wapi?
 
Back
Top Bottom