Kafulila: Watanzania Wanachagua Mtu, Siyo Sera!

Yaani majimbo 23 tu ambayo ukweli zaidiya nusu yake yamepatikana kutokana na magomvi ya ndani ya CCM na sio kukubalika kwenu kwa dhati tayari arrogance ya power imewazidi kiasi hiki?


Acha Taarabu.

Subiri 2015.
 
David Kafulila mbele ya microphone.

Mbele ya macho ya Watanzania.

Anasema (nanukuu):

"Kama Watanzania wangezingatia sera za vyama wakati wa kuchagua viongozi, basi chadema kisingeshinda". Hajasema kivipi.

Sababu?

"Chadema ni chama cha kibepari" (akapigwa swali na mtangazaji, 'kwani ulipokuwa chadema ulikuwa hujui kama chadema ni cha kibepari?' hajajibu mpaka dakika hii). Akaendelea.....

"Sera za kubepari haziuzi Tanzania".

Maoni yangu.

Watanzania wa leo si wakupigia matarumbeta. Unapokosoa vyama vingine, ukumbuke na kutoa alternative. Chama gani ni bora zaidi ya Chadema?

Nilichokiona kwa bwana Kafulia ni uso wa mtu 'aliyetumwa'. wivu na chuki dhidi ya chadema. Chadema kitasimama.

Kama bwana kafulia amechaguliwa kama 'mtu' na si kwa 'sera', basi hilo ni tatizo la wananchi wake. ana kazi ya kutoa elimu ya uraia kwa wananchi wa jimbo lake. na nina uhakika kama wananchi wa jimbo lake wataipata vema hiyo elimu ya uraia 2015 atarajie kupungukiwa wabunge kwenye chama chake au kukosa wabunge kabisa.

kwa ujasiri nasema:

Chadema msikubali kuungana na CUF na hawa waganga njaa kina kafulia.

Jamani mwacheni dogo bado ndio anapevuka kisiasa. bado akili yake ni nzito ku-edit mambo kabla ya kuongea ndio maana mara nyingi hujikuta akiropoka na akibananishwa anakosa majibu...
Anyway, Kigoma wamechagua wapinzania kwa sababu wamechoshwa na ahadi hewa za Chama cha CCm, hivyo wanajaribu kuwa opportunistic labda huenda mambo yao baadaye yakanyooka. Ndio maana wakamchagua dada mmoja kule Kasulu vijijini anaitwa Buyogela ambaye aliishia darasa la 5. Wameongozwa na watu mpaka maprofesa kama Prof.Mbwiliza lakini maisha yakaendelea kuwa magumu, hivyo wameamua kujaribu NCCR kuona kama kitaeleweka...Toka Uhuru wanaambiwa kuwa barabara za kigoma ziko kwenye upembuzi yakinifu na wameshasaini mkataba na mkandarasi...lakini ni vumbi na tope tu!! vilevile tokea uhuru kuna wananchi hawafahamu kama hapa duniani kuna kitu kinaitwa umeme...maana hawajawahi kuuona..
 
Kwa demokrasia hii mnayohubiri ni wazi hakuna nafasi itakayopatikana kwa kuwa na kiongozi ama viongozi bora kwani kwenu ninyi kiongozi bora ni yule anayewakilisha chuki, maslahi na ndoto zenu pekee na kuwa tayari kufokea uvundo wa wengine na kufunika uozo wenu.....
Ukweli wenyewe omarilysis unatoa majibu ya kijumla mno mimi nadhani wewe unaishi kwenye hisia zaidi ya ukweli kwa sababu ungetoa basi mfano halisi wa nani anawakilisha chuki na kukumbatia uvundo zaidi ya CCM mi nadhani kama wote ni wazalendo lazima tukubaliane kuwa na mfumo wa watu kutofautiana kiitikadi maono na imani badala ya kutaka watu waingie msituni kitu ambacho hakuna kitakaye msaidia zaidi ya kuangamiza taifa, vilevile unavyoona sisi tunaegemea upande mmoja ndio hoja stahiki ambayo inaonyesha kuwa pia wewe tayari katika kichwa chako umejenga imani ya kumchukia fulani ,au chama fulani hata bila kuwa na sababu za msingi kwa sababu tuu ya kuamini kitu fulani tafadhali tusijumlishe vitu kwa manufaa yakufurahisha nyoyo zetu, nchi hii ni yetu sote tuangalie mustakabali wa taifa tukubalieane kupingana kwenye hoja lakini sio tuashie kupigia kwata na saluti watu wanaotaka kuturudisha nyuma kama wewe ukiwa katika umri mdogo kiasi hicho kwa kudhani wao ndio waelewa na wenye misimmamo stahiki na kwamba hata wanapokosea hawastaki kukosolewa kwani akina Omari watakuja juu
na kutoa hoja zisizo kuwa na kichwa wala miguu
 
Ujamaa ni Itikadi iliyokufa na ni Itikadi iliyobaki kwenye Vitabu tu hata CCM wenyewe siyo wajamaa tena
 
Ukweli wenyewe omarilysis unatoa majibu ya kijumla mno mimi nadhani wewe unaishi kwenye hisia zaidi ya ukweli kwa sababu ungetoa basi mfano halisi wa nani anawakilisha chuki na kukumbatia uvundo zaidi ya CCM mi nadhani kama wote ni wazalendo lazima tukubaliane kuwa na mfumo wa watu kutofautiana kiitikadi maono na imani badala ya kutaka watu waingie msituni kitu ambacho hakuna kitakaye msaidia zaidi ya kuangamiza taifa, vilevile unavyoona sisi tunaegemea upande mmoja ndio hoja stahiki ambayo inaonyesha kuwa pia wewe tayari katika kichwa chako umejenga imani ya kumchukia fulani ,au chama fulani hata bila kuwa na sababu za msingi kwa sababu tuu ya kuamini kitu fulani tafadhali tusijumlishe vitu kwa manufaa yakufurahisha nyoyo zetu, nchi hii ni yetu sote tuangalie mustakabali wa taifa tukubalieane kupingana kwenye hoja lakini sio tuashie kupigia kwata na saluti watu wanaotaka kuturudisha nyuma kama wewe ukiwa katika umri mdogo kiasi hicho kwa kudhani wao ndio waelewa na wenye misimmamo stahiki na kwamba hata wanapokosea hawastaki kukosolewa kwani akina Omari watakuja juu na kutoa hoja zisizo kuwa na kichwa wala miguu

Haya endelea na hoja zako zenye kichwa, miguu na pengine akili na moyo.....
 
Je hivi sasa tupo kwenye Siasa Za Ujamaa na Kujitegemea.......... au Tupo kwenye siasa za Ubepari....
 
Omarlyas pole,muda wa kupamba ufisadi umepita,isingekuwa nguvu ya dola tungekuwa tunaongelea sio majimbo 23 ni nchi nzima kasoro pemba
 
Yes my friend you have actually confirmed that Kafulila was right! isnt it?
Waberoya hajaelewa kinachojadiliwa/bishaniwa hapa ni nini. Labda ni kutokana na heading aliyotumia mwanzisha thread! Huyo Kafulila point yake kuu ni kuwa CHADEMA inafuata itikadi ya kibepari hivyo ni vigumu kukubalika Tz.... ina maana hata hizo kura walizopata ni kwa kuwa wapiga kura walipigia watu na si chama! Kutu ambacho si kweli!
 
"inaelekea siku hizi hana akili tena. kwa sababu mtu mwenye akili hawezi kuongea utumbo aliokuwa anazungumza leo star tv.

amejaa majivuno tu. kama rafiki yake."

Mkuu ni kuwa umaarufu unapunguza uwezo wa akili.
 
Hajawahi kusoma na Zitto, wakati yuko Form 2 (au F3 hapa) alikuwa Naibu Katibu mwenezi NCCR Mageuzi wa either wilaya au kata (hapa uhakika sio mkubwa).
Baada ya kumaliza form 6 alijiunga na Chadema na alikuwa kwenye kampeni za Zitto (Zitto saw that the guy is potential and he was using him for his things)

Kafulila alipata nafasi ya kusoma chuo cha Tumaini University-Iringa, Chadema wakamwomba aache ili asome masomo ya jioni huku akiwa anafanya kazi za chama.

NOTE: Zitto na Kafulila wanatoka majimbo tofauti.

Huyu Ndg ni Kafulila au ni Kafulia? Anadhani hii nchi inaendeshwa na sera gani, za ujamaa au ubepari? Kafulia huyo hana sera, nadhani huyu Kafulia arudi shule aelewe mambo ya kina Putini na Bush. Afunguke macho aelewe Tanzania ya sasa na ya jana. Elimu bure ni ubepari?????????
 
umeongeza neno BAADHI.

kama CCM wenyewe wanatekeleza sera za Chadema (wengine wanasusia hata mashangingi), itakuwa halmashauri?

Acha upotoshaji.

Inaelekea hujui unachokisema.

nyamaza.

Ngwananga usiwaachie unao hao, wako tu mpaka kieleweke wachovu tuu.
Sorry I am some how late, but better late than never.
 
Ngwananga usiwaachie unao hao, wako tu mpaka kieleweke wachovu tuu.
Sorry I am some how late, but better late than never.

mimi ni muathirika wa utawala mbovu wa CCM. From my roots. Hali ni mbaya na hakuna tumaini.

mtu anayekuja kubeza chama chenye dira ya kunikomboa (chadema) namuona ni msaliti na mnafiki mkubwa.

nita-deal naye bila uvumillivu wala haya.
 
Bwana mdogo Kafulila ana Kibri ndio maana anasema kuwa watu walimchagua yeye kama yeye na sio sera za NCCR. Hiki ni kibri ambacho mwenyezi mungu hakipendi mja wake kuwa nacho. Nijuavyo mimi pamoja na mapenzi kwa mgombea bado SERA za Chama alichosimamia mgombea zilichangia watu kumchagua . Namshauri KAFULILA Aachane na CDM ajiunge na CUF/TLP/UDP na CCM waipinge CDM.Hukumu tutaitoa sisi wananchi 2012 na kuhitimisha 2015.
 
akajifie huko anatuletea mbwembwe kwa sababu kashinda

siyo mbwembwe.

aliishiwa hoja.

alikuwa anataka kuonesha uma-chachari. anasahau kuwa vijana machachari wako chadema

zitto mjanja sana. kampeleka chambo msela kwenda nccr. sema kafulia hajui tu.

jana kaidhihirishia dunia kuwa si kwamba sera za kibepari haziuzi, bali nccr ndiyo haiuzi.
 
Wanasiasa wote duniani wako hivyo, you can imagine sera za wanafunzi wote shule ya msingi watakuwa na computer ili waweze kufundishwa kwa online katika nchi kama yetu hii si upumbavu?
Mi naona kuwe na Technologia mtu akikuudhi na yuko kwenye TV unamshuti apo apo kwenye screen na anakufa huko aliko.

Hiyo teknolojia ingekuwepo hao mafisadi wakuu wasingekuwepo kwani watu wangewagombania kwenye TV screens.

By the way huyo Kafulila kweli amefulia, kwani kinachoamua mrengo wa chama chochote (kushoto au kulia) ni sera zake.
Vyama vinavyotaka sera za kusaidia wananchi moja kwa moja huwa ni vya mwelekeo wa kijamaa (kushoto), na vyama vilivyo na sera za kujali zaidi wafanyabiashara huwa vinaitwa vya mwelekeo wa kibepari (kulia).

Vyama vya Ulaya na Marekani vilianzishwa kukidhi mahitaji ya makundi mawili; wananchi/wafanyakazi (vyama vya kushoto), na wafanyabiashara/wenye viwanda (vyama vya kulia):
Vyama vya kushoto ni kama Democratic (Marekani), Labour (Uingereza), na Social Democratic (Ujerumani).
Vyama vya kulia ni kama Republican (Marekani), Conservative (Uingereza), na Christian Democratic (Ujerumani).

Kwa hiyo SERA ndiyo zinatambulisha mrengo/muelekeo wa chama chochote, na kamwe si matamshi tu.

CCM ilikuwa chama cha mrengo wa kushoto, ila kwa sera zake na mwenendo wake baada ya Nyerere, kimekuwa Chama cha mrengo wa kulia kinachojali zaidi wafanyabiashara na wawekezaji.

Vyama vyenye sera za kujali wananchi wengi ndivyo vya mrengo wa kushoto. Vyama hivi husisitiza zaidi unafuu wa huduma za jamii kwa wananchi (maji, umeme, elimu, huduma za afya nk.) zipatikane kwa unafuu kadri inavyowezekana, au bure (kwa maana zigharamiwe kutokana na kodi ya jumla ya wananchi kutoka hazina). Hii ni sera ya CHADEMA, na pia CUF.
 
...Ukifuatilia mazungumzo na kauli za wanasiasa wengi tulionao, bila kujali ni ccm, cdm, cuf, nccr, n.k utaona kwamba wengi wao si makini na mara kadhaa hawajui wanachosema kina-maanisha nini.

...Nitatoa mifano michache. Kwanza, Ndugu Kafulila anaposema cdm ni cha ki-bepari, chama kipi ni cha kijamaa? halafu, mabepari huwa na sera za kutoa elimu na afya bure?....anayo mifano? Pili, Ndugu Chiligati aliposema watapeleka hoja ya kuwaondoa wabunge wa cdm kwenye vikao vya bunge, alikuwa anafahamu kanuni za bunge, je, alikuwa anafahamu au amebashiri matokeo yake yatakuwa nini kama wangefanikiwa? je, angekuwa ametia maji kwenye moto au petroli? Tatu, Ndugu Hamad Rashid alipogusia suala la posho ya kiongozi wa upinzani bungeni na marekebisho ya kanuni walizozitengeneza wao wenyewe, alikuwa anajua anatafsirika vipi? je, hakufahamu kuwa ataonekana analichukulia suala zima kuwa too personal, na pengine anasononeka kukosa posho ile na kuukosa uongozi wa upinzani.

...waTanganyika bado hatujapata viongozi makini wa kutosha na ndio maana kuna madudu mengi kila siku yanaibuka kwenye vyombo vya habari juu ya viongozi. Hutana nafasi ya kutosha kujadili issues za maendeleo, tumebaki kuongelea pumba za viongozi kila kukicha! Nchi inaenda pabaya hii.

Mh. Zitto Kabwe, hakuna Rais bora nchi hii kama JK kwani mambo aliyowafanyia watu wa Kigoma hakuna Rais yoyote aliye pita amewafanyia hivyo.
 
Back
Top Bottom