BONGE BONGE
JF-Expert Member
- Oct 19, 2011
- 3,721
- 2,106
.......dogo (zito) simkubali kabisa siku hizi kwa sababu sio yeye yule tunayemfahamu, siku hizi ama anatumika au kutumikia kitu/watu
Gazeti la mwanahalisi lina habari nzito tena za kushtusha.
Mbunge wa Kasulu mjini Moses Machali amemshutumu vikali David Kafulila kwamba anatumiwa na Naibu Katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe kukivuruga chama hicho.
Mbunge huyo wa Kasulu anadai lengo kubwa la Kafulila ni kumwondoa mwenyekiti wa chama hicho James Mbatia ili yeye awe mwenyekiti.
Pili Machali amedai kwamba baada ya Kafulila kuwa mwenyekiti atamkaribisha Naibu Katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe ili awe mgombea Urais kupitia NCCR.
Moses machali ameendelea kudai kuwa baada ya mpango huo kukamilika watatumia mbinu mbalimbali kuivuruga Chadema kwa kuhama na kundi kubwa la wanachama wake.
Mbunge huyo ameendelea kudai kuwa kamwe hatakubali mbinu hiyo kwani Zitto na Kafulila wanatumika kuua upinzani.
Alipoulizwa kwanini watake kumuondoa Mbatia kwanza amesema hiyo ni kutokana na sababu kwamba kamwe Mbatia hatamkubalia Zitto kugombea urais kupitia NCCR.
Source: MwanaHalisi