Kafulila na Zitto wanaivuruga NCCR - Moses Machali

Status
Not open for further replies.

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Gazeti la mwanahalisi lina habari nzito tena za kushtusha.

Mbunge wa Kasulu mjini Moses Machali amemshutumu vikali David Kafulila kwamba anatumiwa na Naibu Katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe kukivuruga chama hicho.

Mbunge huyo wa Kasulu anadai lengo kubwa la Kafulila ni kumwondoa mwenyekiti wa chama hicho James Mbatia ili yeye awe mwenyekiti.

Pili Machali amedai kwamba baada ya Kafulila kuwa mwenyekiti atamkaribisha Naibu Katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe ili awe mgombea Urais kupitia NCCR.

Moses machali ameendelea kudai kuwa baada ya mpango huo kukamilika watatumia mbinu mbalimbali kuivuruga Chadema kwa kuhama na kundi kubwa la wanachama wake.

Mbunge huyo ameendelea kudai kuwa kamwe hatakubali mbinu hiyo kwani Zitto na Kafulila wanatumika kuua upinzani.

Alipoulizwa kwanini watake kumuondoa Mbatia kwanza amesema hiyo ni kutokana na sababu kwamba kamwe Mbatia hatamkubalia Zitto kugombea urais kupitia NCCR.

Source: MwanaHalisi
Moja, sina mpango wowote wa kuhama CHADEMA. Kila siku nasema nimekuwa mwanachama wa chama kimoja tu cha siasa maisha yangu yote, nimekuwa mwanachama wa CHADEMA toka nikiwa na umri wa miaka 16 na namwomba Mungu kila siku nife nikiwa ndani ya chama hiki.

Najua kuna watu wanapenda sana nitoke CHADEMA kwa maslahi yao ya kisiasa wakiniona mimi ni tishio kwao. Napenda kuwaambia nimetumia nguvu nyingi sana kujenga chama hiki na sitahama. Waache kabisa kunizushia na kunijengea chuki mbele ya umma.

Pili, sihusikikwa lolote lile na yanayoendelea ndani ya NCCR na wala sina interest ya kuyajua. Mbunge wa Kasulu mjini ambaye alikuwa mwanachadema na kushinda Ubunge kwa sababu ya kutumia jina langu huko kwao Kasulu anaropoka (kama kweli kasema maneno hayo) na nitakapotoka Hospitali nitamtaka anithbitishie anayoyasema. Vijana wanapojiingiza kwenye siasa za uwongo kama wazee wao ni hatari sana kwa nchi. Sihitaji kwenda NCCR ili kugombea Urais kwani chama changu ni kikubwa zaidi na kitanipa Urais kwa urahisi kuliko NCCR ambacho ni chama kisicho na rekodi yeyote ya kupigania maslahi ya nchi hata wakati kilipokuwa chama kikuu cha upinzani nchini.

Katiba hainiruhusu kugombea Urais mwaka 2015 na hata kama ikibadilishwa na kuniruhusu kugombea kwangu kutategemea sana mwafaka ndani ya chama changu. Anayedhani kwamba nia yangu ya kuwa Rais wa Tanzania ni ya kufa na kupona hamjui Zitto. Sifanyi siasa za kufa na kupona. Ninao uwezo wa kuwa Rais bora maana nina ajenda na ninatoka chama bora. Lakini pia nipo tayari kufanya kazi yeyote ile ambayo chama changu kitanipa.

Zittophobics wanaishi kwa siasa za kumwaza Zitto na wamo kwenye vyama vyote vya siasa hapa nchini. Ninafanya kazi zangu za Ubunge kwa ufanisi na mafanikio makubwa sana, ninafanya kazi zangu za Uenyekiti wa Kamati ya Mashirika ya Umma kwa umakini mkubwa na ninafanya kazi zangu za Uwaziri Kivuli wa fedha katika hali ya kuridhisha sana.

Maadui zangu wa kisiasa wanatamani nianguke. Kwa uwezo wa Mungu sitaanguka.

Tatu, Gazeti la Mwanahalisi limekuwa ni gazeti linalonisakama sana kila kukicha lina ajenda yake. Gazeti ambalo limepoteza mvuto wake kwa jamii halinishughulishi. Hata juzi Mzee Samweli Sitta amelishutumu kwa kununuliwa na mafisadi na kutumiwa. Niseme nini zaidi kuhusu gazeti hili linaloongozwa na mtu ambaye hata hajamaliza darasa la saba.

MwanaHalisi wanajua kwamba wakiandika habari yenye jina langu mauzo yao yanakua makubwa. Hili ni gazeti mufilisi ambalo kazi yake ni kutumiwa tu.

Toka MwanaHalisi:
SIRI kubwa kuhusu mwenendo wa Zitto Kabwe (Mb) ndani ya chama chake zimeanikwa mitaani na zinaweza kumzamisha kisiasa, MwanaHALISI sasa linaweza kuripoti.

Siku nne baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Willibrod Slaa kusema wamenasa taarifa za mawasiliano ya Zitto, baadhi ya taarifa zimepatikana jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Zitto ananukuliwa akiapa kusaidia wagombea uongozi katika vyama vingine; na katika moja ya taarifa ananukuliwa akisema atasaidia David Kafulila kupata ubunge "hata kabla ya akina John Mnyika…"

Mnyika ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA na Kafulila alikuwa Afisa Habari ambaye baada ya kuondolewa wadhifa huo amekimbilia NCCR-Mageuzi. Mnyika anatarajia kugombea ubunge jimbo la Ubungo.

Naye Zitto amenukuliwa na gazeti la Mwananchi la Jumatatu akilalamika kuwa ameingiliwa katika mawasiliano yake ya baruapepe (e-mail); jambo ambalo Mkurugenzi wa Upelelezi, Robert Manumba, amedakia haraka na kusema Zitto akiwapelekea malalamiko watashughulikia.

Kwa mujibu wa mpangilio wa taarifa husika, lazima aliyezitoa amepata ufunguo wa baruapepe (password) wa ama Zitto au mwandishi wa habari wa Mwananchi, Denis Msacky.

Karibu mawasiliano yote ni kati ya Zitto na Msacky juu ya "ushujaa" wa Zitto na jinsi anavyopendwa nje ya chama huku "akichukiwa" na viongozi wake wakuu.

Katika moja ya mawasiliano, inaonyeshwa kuwa Msacky alimwandikia Zitto akieleza, "Leo hii Mrema (Augustine Lyatonga) anasema anakuheshimu wewe, lakini si Mbowe; hivyo hivyo, Lipumba (Profesa Ibrahim) na James Mbatia wanasema wewe una visheni."

Katika mawasiliano hayo ya Jumanne, 1 Desemba 2009, saa 6.45 adhuhuri, Msacky anaonyeshwa kumwambia Zitto pia kuwa, "CCM nao…wanakusifu kwamba pamoja na kwamba unawaliza sana, lakini ni kiongozi shupavu."

"Leo hii siasa za CHADEMA zingekuwa zinatisha kama ungekuwa mwenyekiti wa CHADEMA, vijana nchi nzima wangejiunga na chama, uko nao karibu, unaongea nao, una elimu nzuri, unajua mambo, unasoma sana," imeeleza sehemu ya mawasiliano kutoka kwa Msacky kwenda kwa Zitto.

Kinacholeta wasiwasi ndani ya CHADEMA kinaweza kuwa lugha inayotumiwa katika mawasiliano hayo. Kwa mfano, katika waraka huohuo, Msacky ananukuliwa akiandika:

"Wanataka kukumaliza, nami sitakubali mtu ammalize rafiki yangu nikiangalia…wanasema Mbowe hata Mbatia akikaa vema anaweza kumpita kama siasa za kufukuza zitaendelea. Muhimu, usisikilize watu, tulia, urudi tupange tufanye nini? Lakini ukweli ni kwamba sasa wanakuogopa…Mwenyekiti Mtarajiwa…"

Mawasiliano yanaonyesha kuwa Zitto hakufurahishwa sana na taarifa za Mwananchi kuwa amemsaidia Kafulila magari matatu kwenda Kigoma kufanya kampeni chini ya NCCR-Mageuzi, lakini Msacky anaonyesha kumfariji.

"Kaka, mimi nimeiona story, haina matatizo zaidi ya kuwafanya akina Mbowe kusitisha mpango mbaya dhidi yako maana wanaanza kuogopa. Hata Mrema Lyatonga amesema kwamba Zitto huwa unamsaidia akiwa na shida. This shows that ur a leader katika opposition, wewe ni mtu wa maridhiano, unakuza upinzani Kigoma," anaeleza.

Anasema, "Leo nasikia akina Mnyika wanahaha sana, waambie familia yako wasiingie katika mtego wa kuanza kuhojiwa na akina Kubenea (Saed wa MwanaHALISI), watawachanganya. Wewe usiongee kitu chochote, wabaki wanahaha, lakini for sure you are safe, na hizo kampeni za Mnyika kukuchafua huku akitaja majina ya Kafulila, ataziacha."

Akionyesha juhudi za kushawishi, kuliwaza au kufarakanisha, Msacky anaandika, "Katika hili Zitto, mimi niko na wewe, huna kosa ambalo umefanya, na wala usihofu maana wewe utakuwa nguzo ya upinzani Tanzania…Wanakupa majina ya ajabu, wanakuita Mr Dowans, wanatumia akina Halima Mdee kukuchafua katika magazeti…"

Awali Zitto alikuwa amemwandikia Msacky akisema, "Stori niliyoiona kwenye mwananchi itaniletea matatizo sana." Hiyo ilikuwa Jumatatu 30 Novemba 2009, saa 5.21 asubuhi. Baruapepe hiyo ilikuwa na kichwa kisemacho: "Muhimu na haraka."

Aidha, katika mawasiliano mengine, Zitto anaendelea kuonyesha kutofurahishwa na taarifa juu ya magari matatu kwa safari ya Kafulila.

Naye anaandika kwa Msacky, "tatizo la stori ni wingi wa magari, itaonekana mimi nina magari mengi na ni fisadi unajua? Hilo ndio tatizo."

Saini ya Zitto inatofautiana katika baadhi ya baruapepe. Pengine anaandika "zitto" na kwingine anaandika "Zi."

Moja ya mawasiliano ambayo yanazua mashaka yanaonyesha Zitto akikiri kuwa na mawasiliano na waasi nchini Kongo akiandika, "take it from me (niamini), nina contacts nyingi sana Congo na hao rebels (waasi) huwa wananiomba sana ushauri na kutaka kuwaunganisha."

Katika moja ya mawasiliano, Msacky anamwonya Zitto kutotumia baruapepe ya "CHADEMA kwa mawasiliano ya siri" na kutaka amwambie mama yake Shida Salum akatae kuongea na waandishi wa habari. "…nasikia Mbowe anataka mama awe akiongea na waandishi, usikubali," alieleza.

Zitto alipoulizwa kuhusu taarifa ya Mwananchi kuwa anatembea na barua mfukoni ya kujiuzulu uanachama CHADEMA, alisema "Sina la kusema."

Alipong'ang'anizwa kwamba imekuwaje hawezi kuzungumzia suala hilo ambalo ni muhimu kwa mustakabali wake wa kisiasa kwa chama chake, Zitto alisema, "Ni kwa sababu sitaki kuingia katika malumbano na katibu mkuu wangu (Dk. Willibrod Slaa) kwani malumbano hayo hayataijenga CHADEMA."

Alipotakiwa kueleza juu ya baruapepe ambazo zinadaiwa kuwa mawasiliano kati yake na Msacky, haraka alijibu, "Sina la kusema."

Alipoelezwa umuhimu wa yeye kueleza msimamo wake juu ya baruapepe hizo, Zitto alijibu, "Chochote nitakachosema sasa hivi, kitawachanganya Watanzania.

"Sitaki malumbano. Hakuna sababu ya kuwachanganya Watanzania. Hiyo haina maana yoyote," alisema Zitto kwa sauti ya ukali. Zitto alikuwa akiongea kutoka Ujerumani kwa simu Na. +4915222493231.

MwanaHALISI ilimtafuta Msacky. Baada ya kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa, hatimaye aliandika ujumbe "Kaka, niko katika kikao. Tuma ujumbe."

Msacky aliulizwa, "Kaka, tumesikia kwamba umetajwa katika sakata la Zitto na chama chake na kwamba wewe ndiye mtibuaji. Je, ni kweli?" Hakujibu ujumbe na alipopigiwa simu ilikuwa inaita hadi kukatika.

Gazeti lilipowasiliana na Mnyika na kumueleza kwamba amekuwa akitajwa katika ujumbe wa Zitto na Msacky, alikiri kupokea ujumbe huo wa baruapepe uliotoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni "Mtanzania mwema."

Alisema alipoona ujumbe mmoja unahusu Zitto kushauri Msacky kutochapisha habari za mkutano wake na waandishi wa habari, ndipo aliamua kupeleka ujumbe huo kwa Zitto.

"Nilimuuliza kuna hiki kitu nimetumiwa. Je, haya ni maandishi yako au kuna mtu ameingilia emaili yako na kujiandikia haya? Hadi leo hii, bado sijapata jibu," alisema Mnyika kwa sauti ya masikitiko. Alisema yeye hana cha kusema na kuongeza, "labda umuulize Zitto."

Alipoulizwa anachukuliaje suala hilo, Mnyika alisema, "Ukiniuliza mimi kwa upande wangu, nilitegemea mambo hayo yangemalizwa katika vikao vya chama na si kwa vyombo vya habari. Lakini kwa hatua ya hivi sasa, nadhani Zitto bado anayo fursa ya kulieleza hili.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe alipoulizwa juu ya madai ya kuwapo njama za kuhujumu chama chake zinazofanywa na Msacky kwa kumtumia Zitto, haraka alijibu, "tuna utaratibu wetu wa kushungulikia mambo ndani ya CHADEMA."

Alisema, "Sina la kusema. CHADEMA ina utaratibu wake wa kushughulikia mambo yake."

Kwa kadri mawasiliano ya Zitto na Msacky yanavyoonyesha na iwapo yatathibitishwa kuwa kweli, jambo ambalo linaanza kuthibitishwa na Zitto kwa kulalamika kuingiliwa kwenye faragha, basi uhusiano wake katika chama utakuwa umepata nyufa.

Wachunguzi wa siasa za upinzani nchini wanasema kwa hali hii, uwezekano wa Zitto kubaki ndani ya chama chake ni mdogo. "Ama atajiondoa mwenyewe au hatimaye atafukuzwa," ameeleza mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Hata hivyo, Zitto amenukuliwa na Mwananchi akisema, "Sitaki kugombana na mtu mimi. Wala msiniweke kwenye kifungo cha siasa. Ni bora niishi huru kuliko katika mateso ya siasa za kipumbavu kabisa. Nitafanya maamuzi ambayo hayajawahi kufikiriwa."

Wiki iliyopita Kafulila aliwaambia waandishi wa habari kwamba Zitto atafanya maamuzi makubwa ambayo hawakutegemea.
 
Good news..Kwa mtindo huu kuiondoa serikali ya CCM madarakani itakuwa ni ndoto!
 
Kafulila na Zitto iko kazi mbele yao.

Lakini huyo Mbatia tumesikia muda mrefu akitakiwa na wajumbe wa chama chake aachie ngazi, akitajwa Hashim Rungwe kuongoza huo mkakati, sikuwahi kumsikia Kafulila akihusishwa na huo msukumo.

Au kafulila anacheza mpira nje ya uwanja.
 
Niliwahi kucoment kuhusu suala hili katika moja ya posts kwa facebook wall ya Zitto kipindi cha October - January wakati sakata lake likifukuta ndani ya CDM..alifuta comments zangu zote ambazo zilikuwa liked na watu kadhaa na kuni-block from friendship..!

I can bet..90% of this news is TRUE.

Unafikiri kwa nini alisema kwenye kampeni zake za ubunge mwaka jana huko Kigoma Kaskazini kwamba 2015 atarudi kama mgombea urais wakati huo huo chama chake kina mgombea wa urais na yeye bado hajajihakikishia kugombea kupitia CDM 2015!!!???

Wait and see.
 
Chanzo cha habari kwa machali ni kipi? Inawezekana ikawa na ukweli au isiwe na ukweli lakini tusubiri time will tell. Machali ni mtu makini namkubali sana.
 
Mbomoa nchi ni Mwananchi mwenyewe na ndiye mjenga nchi, ZITTO hawezi kuibomoa NCCR katu hizi ni chuki binafsi dhidi ya ZITTO maana hapo awali walisema anampango wa kuhamia NCCR kisa, kumfuata rafiki yake Kafulila.

Hiki chama hakieleweki mara tatizo ni M/kiti leo ZITTO mara Kafulila asingekuwa Kafulila wangepata hata huo ushindi wanao uona leo wa 4mps. Tatizo ni nini ? kama hawalioni wafanye uchaguzi mpya chama kisukwe upya kuanzia juu hadi chini
 
Mbomoa nchi ni Mwananchi mwenyewe na ndiye mjenga nchi, ZITTO hawezi kuibomoa NCCR katu hizi ni chuki binafsi dhidi ya ZITTO maana hapo awali walisema anampango wa kuhamia NCCR kisa, kumfuata rafiki yake Kafulila.

Hiki chama hakieleweki mara tatizo ni M/kiti leo ZITTO mara Kafulila asingekuwa Kafulila wangepata hata huo ushindi wanao uona leo wa 4mps. Tatizo ni nini ? kama hawalioni wafanye uchaguzi mpya chama kisukwe upya kuanzia juu hadi chini

Mbona kila kitu kiko wazi mkuu? Usibishane na ukweli
 
Chanzo cha habari kwa machali ni kipi? Inawezekana ikawa na ukweli au isiwe na ukweli lakini tusubiri time will tell. Machali ni mtu makini namkubali sana.

Inawezekana magamba yametengeneza habari hii kupunguza nguvu ya zitto na kafulila
 
Chanzo cha habari kwa machali ni kipi? Inawezekana ikawa na ukweli au isiwe na ukweli lakini tusubiri time will tell. Machali ni mtu makini namkubali sana.

Anadai awali Kafulila alimshirikisha mpango huo akakataa
 
Na sisi watanzania tusipende kusema bila kufanya uchunguzi,tujiulize ni kwa nini asemee mwanahalisi.Na yeye anatumiwa na nani.ni mbatia au ni nani hasa.

Tangu lini Mbatia akawa mpinzani hadi ionekane anayetaka kumpindua ni mhaini asiye na nia nzuri. Ni nani ndani ya hicho chama chao alishawahi kuhoji dhamira ya mbatia hasa pale anaposimamia mstari tata wenye mwelekeo wa mahaba na CCM.

Tatizo wenyeviti wa vyama vya siasa Tanzanzania hawataki challenge wanandhani uenyekiti ni haki ya kuzaliwa.hizi hulka za do or die political mentality zinadumaza demokrasia. Baadhi ya Wenyeviti wa vyama vya siasa na hasa upinzani wana mawazo ya kijima katika kufanya siasa na imefikia hatua wanaogopa watu wanaowapa changamoto za kweli na hasa vijana.Hili ni pigo kwa demokrasia.

Sitaki kuingilia mambo ya ndani ya NCCR lakini tujiulize ina maana huko NCCR hakuna mwenye haki ya kupinga mwenyekiti au kugombea nafasi ya juu ya uongozi ndani ya chama hicho...na je ina maana Mbatia ndiye mwenye kauli ya mwisho katika kupitisha nani awe mgombea urais kupitia NCCR....

WanaJF, ukiona Mbunge anajadili watu bila kuwa na uhakika wa anachosema ujue ni dalili za watu kuwa na ombwe la fikra. Sisi tunaingia mkenge kisa kasema mtu ambaye unamkubali SANA ! ! ! Tunaacha kufikiri kwa sababu mtu unayemkubali sana kasema, tuwe makini yasije yakatukuta yale ya Kibwetere kule Uganda
 
Mbomoa nchi ni Mwananchi mwenyewe na ndiye mjenga nchi, ZITTO hawezi kuibomoa NCCR katu hizi ni chuki binafsi dhidi ya ZITTO maana hapo awali walisema anampango wa kuhamia NCCR kisa, kumfuata rafiki yake Kafulila.

Hiki chama hakieleweki mara tatizo ni M/kiti leo ZITTO mara Kafulila asingekuwa Kafulila wangepata hata huo ushindi wanao uona leo wa 4mps. Tatizo ni nini ? kama hawalioni wafanye uchaguzi mpya chama kisukwe upya kuanzia juu hadi chini

Umeongelea hisia zako, lakini ukweli Zitto ni mtata. Kama CHADEMA ingekuwa kama CCM ya leo ingesambarataratika kwani Zitto amewahi kukituhumu chama kwa udini na ukabila. Kama hiyo haitoshi mara baada ya uchaguzi mkuu 2010 Zitto alitangaza kugombea urais 2015 kinyume na taratibu za chama, kama si hekima za uongozi wa CDM na mama mzazi wa zito tusingefika hapa tulipo. Hii yote ni kwa sababu anaamini ana wapenzi wengi.

Watanzania tubadilike tuache mapenzi ya mtu kwenye siasa tuangalie sera za chama. Tujifunze KWA JK WENGI WALIMPENDA KWA STAILI KAMA HII YA ZITTO LAKINI NAAMINI LEO JK HATA UKIMPA UKUU WA SHULE YA SEKONDARI HATA FANYA VIZURI
 
Na sisi watanzania tusipende kusema bila kufanya uchunguzi,tujiulize ni kwa nini asemee mwanahalisi.Na yeye anatumiwa na nani.ni mbatia au ni nani hasa.

Ben,sidhani kama ni tatizo kusemea mwanahalisi.Kifupi tu ni kwamba NCCR ina mgogoro na sasa kila kundi linaanika kundi lingine.Ifahamike Machali na Kafulila walikuwa marafiki wakubwa.Hatuwezi kupuuzia kila habari.Tufanye utafiti wa kweli.Na lazima muda si mrefu kila kitu kitakuwa hadharani.
 
absolutely true Mhe Machali. Endeleeni kutafuta ushahidi. Lakini habari ndo hio hio. Mungu yupo bwana.
 
Ben,sidhani kama ni tatizo kusemea mwanahalisi.Kifupi tu ni kwamba NCCR ina mgogoro na sasa kila kundi linaanika kundi lingine.Ifahamike Machali na Kafulila walikuwa marafiki wakubwa.Hatuwezi kupuuzia kila habari.Tufanye utafiti wa kweli.Na lazima muda si mrefu kila kitu kitakuwa hadharani.

Ben nae yumo kweli hilo group, either kwa kujua au kutokujua. Mungu hatawaacha waja wake.
 
Mbomoa nchi ni Mwananchi mwenyewe na ndiye mjenga nchi, ZITTO hawezi kuibomoa NCCR katu hizi ni chuki binafsi dhidi ya ZITTO maana hapo awali walisema anampango wa kuhamia NCCR kisa, kumfuata rafiki yake Kafulila.

Hiki chama hakieleweki mara tatizo ni M/kiti leo ZITTO mara Kafulila asingekuwa
Kafulila wangepata hata huo ushindi wanao uona leo wa 4mps. Tatizo ni nini ? kama hawalioni wafanye uchaguzi mpya chama kisukwe upya kuanzia juu hadi chini

Kaka unachemka!
 
hizo mbinu haziwezi kufua dafu hata kidogo. HATA KAMA ZITTO akiondoka, chadema hakitatetereka wataingia maelfu wenye uwezo hata zaidi ya huyo ZITTO. Ila tusubiri tuone
 
Mbona kila kitu kiko wazi mkuu? Usibishane na ukweli
sipo kubisha kitu, wao NCCR wamelalamika sana kuwa tatizo lao ni M/kiti wao na wamempa siku 21 ajieleze tuhuma anazotuhumiwa undani wake otherwise aachie ngazi Naweza nikawa sielewi eleza undani wake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom