KAFULILA:"MAONI yangu juu ya marekebisho ya sheria ya KATIBA- Hakuna Jipya"

Alichosema au kiandika Kafulila ni cha muhimu sana, ila kama kawaida kwa sababu siyo chadema au la, basi hatasikilizwa

Huyu jamaa hana nguvu ya chama, hana support ya wapinzani wengine

cdm na ccm wakubaliana kukubaliana

Ila bado kuna siku hili litazua matatizo

KAFULILA HONGERA SANA
 
Viva Kafulira umeonesha kuw ulikuwa makini na nn kinaendelea, ulikuwa na hoja za msingi ingawa ndo hivo zimechinjiwa bahari, bt uckate tamaa maana angalau hata hapo mlipofikia kuliko pale walipokuw wameishia magamba, naamini kabsa mtu km Cheyo, Maria Hewa, na wbunge wengi wa magamba mpk bunge linahitimishwa wala hawakuwa wakijua nn kinaendelea.
 
Kufuatia kupitishwa kwa SHERIA ya marekebisho ya KATIBA leo Bungeni, Mh. Kafulila atoa maoni yake akitofautiana na maamuzi yaliyopitishwa leo. Mh. Kafulila ameandika waraka huu akiufafanulia UMMA juu ya mchakato huo uliopitishwa jinsi gani hauna TIJA wala hautaleta mabadiliko yoyote ambayo wanaharakati na wananchi kwa ujumla wameazimia.

MAONI YA MH. DAVID KAFULILA

Habari Watanzania,


Nina maoni tofauti kuhusu hiki kinachoendelea kuhusu marekebisho ya sheria ya kusimamia mchakato wa katiba mpya.
Nimejaribu kuomba kuchangia ili niweke maoni yangu wazi lakini imeshindikana, Spika amesema NCCR amepewa mtu mmoja tu Mh. Machali hivyo nikaona ni vema niwajulishe kupitia mtandao maoni yangu.



UTANGULIZI

Hapa ningependa kukumbusha kuwa kutoka NCCR ni mimi David Kafulila na Felix Mkosamali ambao tulikuwa wajumbe wa kamati ya sheria na Utawala. Mh.Mkosamali ni mjumbe wa kudumu kwenye kamati hii, mimi ni miongoni mwa wajumbe walio ongezwa wakati wa kupitia muswada huu. Pia ikumbukwe kuwa ni mimi na Mkosamali ambao tuliungana na CHADEMA kutoka nje katika mkutano wa tano wa Bunge kupinga namna mchakato ulivyoendeshwa. Niliomba kuchangia bungeni lakini imeshindikana kabisa kupata nafasi lakini kwa kuzingatia umuhimu wa jambo hili na nafasi niliyokuwa nayo katika jambo hili naona kuna umuhimu wa kuzungumza kitu kwani hata wale mabalozi wa nchi tano za Ulaya walipokuja bungeni kwenye mkutano wa tano ni mimi niliyekuwa mmoja wa wabunge waliokutana nao kutoa maoni.


MAONI

Nimeshangaa kuona mvutano wa kisiasa kuhusu mabadiliko yaliyoletwa na serikali kwani ninavyofahamu kuna mambo mengi ya msingi katika sheria hii ambayo yalipaswa kubadilishwa, na nilidhani ndiyo yangeletwa kwenye marekebisho ya sheria hii baada ya vikao vya Rais na wadau wengine vikiwemo vyama vya siasa. Mabadiliko yaliyoletwa sio issues za msingi ambazo zingesaidia kuiboresha tume na mchakato mzima wa katiba mpya.

Kwa mfano;




1. Hoja ya kumwondoa DC na Kuweka Mkurugenzi (DED)

Wabunge wengi wa CCM wanataka DC ndio asimamie, wakati hotuba ya kambi rasmi ya upinzani inapendekeza DED.
Ukweli ni kwamba wote DED na DC hawafai kwasababu wote ni sehemu ya serikali na badala yake ilipaswa jukumu hilo litekelezwe na Tume yenyewe ambayo inapaswa kuwa huru.


2.Hapa ndipo inakuja hoja ya mchakato huu mzima wa kura ya maoni kusimamiwa na Tume huru.
Uamuzi wa kuifanya Tume ya sasa ya Uchaguzi kusimamia mchakato huu ni kinyume cha msimamo wetu wa awali kama wapinzani kwasababu moja ya hoja ya mahitaji ya katiba mpya ni tume huru ya uchaguzi, sasa inawezekanaje tume mbovu ya uchaguzi isimamie mchakato wa kupata katiba huru?. Hili lilikuwa muhimu sana. Tungekubaliana kuhusu kupata kwanza tume huru ya uchaguzi kisha tume hiyo isimamie mchakato wa katiba mpya tungekuwa na uhakika wa kupata katiba ambayo watanzania wanaitaka.

3.Hoja ya Tume huru ya kusimamia mchakato wa katiba

Hii pia ni hoja iliyoachwa kwasababu Tume hii ya sasa inateuliwa na Rais na kwa namna ilivyo bado Rais ndio mwenye mamlaka ya kumtoa mjumbe yeyote. Marekebisho yaliyoletwa leo yanapendekeza namna ya kumtoa mjumbe wa tume hii ambaye anayetuhumiwa kukiuka kanuni za maadili, kwamba Rais atateua Kamati ya kufanya maamuzi. Hapa haikupaswa Rais kuteua kamati badala yake ilitakiwa sheria itamke rasmi kamati hiyo itakuwa akina nani ili kamati hiyo iwe huru kuliko iteuliwe na Rais, pengine kosa la mjumbe ni mvutano unaohusu nguvu za serikali kwa tume.


4. Hoja ya Sekretariet huru.

Kwa mujibu wa sheria hii Sekratariet itaundwa na waziri mwenye dhamana. Hii inaondoa uhuru wa utendaji wa sekretariet, ilipaswa Sekretariet iteuliwe na Tume na iwajibike kwa tume ili kupunguza mkono wa serikali kwenye mchakato na utendaji wa kupata katiba mpya.


5. Hoja ya ushiriki wa Jumuiya za kiraia, taasisi za dini vya vyama vya siasa

Marekebisho yaliyoletwa sehemu A, kifungu cha 7 yanatoa uhuru wa jumuiya hizi kushiriki kwa kualikwa na Rais, lakini sehemu hiyo hiyo ya marekebisho kifungu cha 8 inatamka kuwa Rais hafungwi na mapendekezo hayo kuteua watu wengine kuwa wajumbe. Hapa kwa tafsiri rahisi ni kwamba, haki imetolewa kwenye kifungu cha 7 na imepokonywa kwenye kifungu cha 8 kwa kuwaweka wananchi tayari wasishangae itakapotokea mapendekezo yaliyopelekwa na jumuiya yoyote kukataliwa yote. Ingepaswa kuweka wazi kuwa Rais atalazimika kuteua miongoni mwa walipendekezwa na sio nje ya waliopendekezwa.


Kwa ujumla pamoja na sheria hii kupitishwa leo lakini ina matundu makubwa sana kuweza kuifanya isimamie mchakato huu muhimu kwa uhakika. Bado ni sheria ambayo inategemea sana dhamira ya Rais mwenyewe kuliko mfumo tulioweka.

Napenda ifahamike kuwa, sheria hii iliyopitishwa leo haijafanya mabadiliko ya msingi ambayo sisi sote ( wananchi, wanaharakati na wanasiasa) wenye moyo wa dhati wa kuleta mabadiliko kitaifa tulitazamia.

Pamoja katika kujenga Taifa
David Kafulila



Kulingana na hoja zako mkuu Kafulila nakuvulia kofia....Umetugusa haswa pale wananchi tulipowekea mashaka yako. Madai yako yote ni ya msingi na ndiyo yaliyotangulia wananchi wote kuupinga muswada toka siku ya kwanza. Kama kweli ulivyoeleza hapa ndivyo itakavyokuwa basi sina sababu kabisa ya kukubaliana na wengine waliopokea kupitishwa kwa marekebisho ya sheria. Tutaipokea katiba inayolinda maslahi ya watu na sio mwongozo kwa wananchi wote.
 
tukiacha kuwa biased na vyama tutaendelea lakini itikadi za vyama ndo zinatuponza sasa watanzania.
aliyoyasema Kafulilla ni ya msingi sana sielewi kwa nini wananchi tunakuwa wagumu kuellewa kiasi hicho ukizingatia lugha illiyotumika ni kiswahilli, hivi angeandika kiha hapa tungelewana?

kwa hali iliyojionyesha huko bungeni kufuatia marekebisho ya sheria ya katiba, ni wazi kwamba watanzania tumeingizwa chaka.

tuombe busara ya Rais tu sasa.
 
Kafulila nusu anayosema ni ya kweli na nusu anayosema muda wake haujafika, MPAKA KIELEWEKE kaelezea vzr sana, Pia sio kila walichotaka chadema ilikuwa lazima kikubaliwe, kwa kufanya hvyo hatutapiga hatua yeyote ndo maana mbowe alisema funika kombe mwanaharamu apite, chini ya ccm hatuwezi kupata katiba perfect ila tunaweza kupunguza mabaya yatakayowezekana. Chadema sio miungu wa kuweza kila kitu ila tuwapongeze kwa hiki walichoweza. km cuf na nccr nao wangepigania yao machache ingewezekana kabisa tume ingekuwa km kafulila alivyotaka ila wao wamekaa pembeni wanasubiria chadema wakosee ndo waseme
 
Hongera mh kafulila. Alijua ungepata nafasi ungechaafua hali ya hewa na mjadala ungeanza upya. Ukweli ktk hili cdm imeingizwa chaka na *******. Mana nilimwona lissu anamsifia jk moyo ulilipuka kuwaza ni tuzo gani jk katupatia watz hata asistahili maneno mazito ya lissu? Yaani lissu alionesha jk ni rais wa pekee kutokea nchi hii. Kweli upinzani tuna safari ndefu. Sijui ile juicce ya ikulu ilikuwa rangi gani? Big up kafulila. Wewe ni jembe ambalo hata kama unajua ******* watakutoa muda wowote hapo mjengoni lakini hauhofi kuwapa ukweli. Never compromise.
 
Back
Top Bottom