KAFULILA:"MAONI yangu juu ya marekebisho ya sheria ya KATIBA- Hakuna Jipya"

April

Member
Nov 14, 2011
35
21

Kufuatia kupitishwa kwa SHERIA ya marekebisho ya KATIBA leo Bungeni, Mh. Kafulila atoa maoni yake akitofautiana na maamuzi yaliyopitishwa leo. Mh. Kafulila ameandika waraka huu akiufafanulia UMMA juu ya mchakato huo uliopitishwa jinsi gani hauna TIJA wala hautaleta mabadiliko yoyote ambayo wanaharakati na wananchi kwa ujumla wameazimia.

MAONI YA MH. DAVID KAFULILA

Habari Watanzania,

Nina maoni tofauti kuhusu hiki kinachoendelea kuhusu marekebisho ya sheria ya kusimamia mchakato wa katiba mpya.
Nimejaribu kuomba kuchangia ili niweke maoni yangu wazi lakini imeshindikana, Spika amesema NCCR amepewa mtu mmoja tu Mh. Machali hivyo nikaona ni vema niwajulishe kupitia mtandao maoni yangu.

UTANGULIZI

Hapa ningependa kukumbusha kuwa kutoka NCCR ni mimi David Kafulila na Felix Mkosamali ambao tulikuwa wajumbe wa kamati ya sheria na Utawala. Mh.Mkosamali ni mjumbe wa kudumu kwenye kamati hii, mimi ni miongoni mwa wajumbe walio ongezwa wakati wa kupitia muswada huu. Pia ikumbukwe kuwa ni mimi na Mkosamali ambao tuliungana na CHADEMA kutoka nje katika mkutano wa tano wa Bunge kupinga namna mchakato ulivyoendeshwa. Niliomba kuchangia bungeni lakini imeshindikana kabisa kupata nafasi lakini kwa kuzingatia umuhimu wa jambo hili na nafasi niliyokuwa nayo katika jambo hili naona kuna umuhimu wa kuzungumza kitu kwani hata wale mabalozi wa nchi tano za Ulaya walipokuja bungeni kwenye mkutano wa tano ni mimi niliyekuwa mmoja wa wabunge waliokutana nao kutoa maoni.

MAONI

Nimeshangaa kuona mvutano wa kisiasa kuhusu mabadiliko yaliyoletwa na serikali kwani ninavyofahamu kuna mambo mengi ya msingi katika sheria hii ambayo yalipaswa kubadilishwa, na nilidhani ndiyo yangeletwa kwenye marekebisho ya sheria hii baada ya vikao vya Rais na wadau wengine vikiwemo vyama vya siasa. Mabadiliko yaliyoletwa sio issues za msingi ambazo zingesaidia kuiboresha tume na mchakato mzima wa katiba mpya.

Kwa mfano;

1. Hoja ya kumwondoa DC na Kuweka Mkurugenzi (DED)

Wabunge wengi wa CCM wanataka DC ndio asimamie, wakati hotuba ya kambi rasmi ya upinzani inapendekeza DED.
Ukweli ni kwamba wote DED na DC hawafai kwasababu wote ni sehemu ya serikali na badala yake ilipaswa jukumu hilo litekelezwe na Tume yenyewe ambayo inapaswa kuwa huru.

2.Hapa ndipo inakuja hoja ya mchakato huu mzima wa kura ya maoni kusimamiwa na Tume huru.
Uamuzi wa kuifanya Tume ya sasa ya Uchaguzi kusimamia mchakato huu ni kinyume cha msimamo wetu wa awali kama wapinzani kwasababu moja ya hoja ya mahitaji ya katiba mpya ni tume huru ya uchaguzi, sasa inawezekanaje tume mbovu ya uchaguzi isimamie mchakato wa kupata katiba huru?. Hili lilikuwa muhimu sana. Tungekubaliana kuhusu kupata kwanza tume huru ya uchaguzi kisha tume hiyo isimamie mchakato wa katiba mpya tungekuwa na uhakika wa kupata katiba ambayo watanzania wanaitaka.

3.Hoja ya Tume huru ya kusimamia mchakato wa katiba

Hii pia ni hoja iliyoachwa kwasababu Tume hii ya sasa inateuliwa na Rais na kwa namna ilivyo bado Rais ndio mwenye mamlaka ya kumtoa mjumbe yeyote. Marekebisho yaliyoletwa leo yanapendekeza namna ya kumtoa mjumbe wa tume hii ambaye anayetuhumiwa kukiuka kanuni za maadili, kwamba Rais atateua Kamati ya kufanya maamuzi. Hapa haikupaswa Rais kuteua kamati badala yake ilitakiwa sheria itamke rasmi kamati hiyo itakuwa akina nani ili kamati hiyo iwe huru kuliko iteuliwe na Rais, pengine kosa la mjumbe ni mvutano unaohusu nguvu za serikali kwa tume.

4. Hoja ya Sekretariet huru.

Kwa mujibu wa sheria hii Sekratariet itaundwa na waziri mwenye dhamana. Hii inaondoa uhuru wa utendaji wa sekretariet, ilipaswa Sekretariet iteuliwe na Tume na iwajibike kwa tume ili kupunguza mkono wa serikali kwenye mchakato na utendaji wa kupata katiba mpya.

5. Hoja ya ushiriki wa Jumuiya za kiraia, taasisi za dini vya vyama vya siasa

Marekebisho yaliyoletwa sehemu A, kifungu cha 7 yanatoa uhuru wa jumuiya hizi kushiriki kwa kualikwa na Rais, lakini sehemu hiyo hiyo ya marekebisho kifungu cha 8 inatamka kuwa Rais hafungwi na mapendekezo hayo kuteua watu wengine kuwa wajumbe. Hapa kwa tafsiri rahisi ni kwamba, haki imetolewa kwenye kifungu cha 7 na imepokonywa kwenye kifungu cha 8 kwa kuwaweka wananchi tayari wasishangae itakapotokea mapendekezo yaliyopelekwa na jumuiya yoyote kukataliwa yote. Ingepaswa kuweka wazi kuwa Rais atalazimika kuteua miongoni mwa walipendekezwa na sio nje ya waliopendekezwa.

Kwa ujumla pamoja na sheria hii kupitishwa leo lakini ina matundu makubwa sana kuweza kuifanya isimamie mchakato huu muhimu kwa uhakika. Bado ni sheria ambayo inategemea sana dhamira ya Rais mwenyewe kuliko mfumo tulioweka.

Napenda ifahamike kuwa, sheria hii iliyopitishwa leo haijafanya mabadiliko ya msingi ambayo sisi sote ( wananchi, wanaharakati na wanasiasa) wenye moyo wa dhati wa kuleta mabadiliko kitaifa tulitazamia.

Pamoja katika kujenga Taifa
David Kafulila

Sasa kama NCCR wamepewa nafasi mmoja kwa nini huyo bwana asiwasilishe mawazo ya chama au kwa nini hukupeleka mawazo yako huko ili wayafanyie kazi na kuyawakilisha?? Au kwa vile NCCR wamekutimua then hakuna chama kinachoweza kukusikiliza tena??
 
wacha umbumbumbu, kwanini usiwasilishe maoni yako kwa maandishi kwa spika au unataka show off, uonekane kwenye runinga halafu wananchi waone ulionewa na wakuonee huruma
 
  • Thanks
Reactions: FJM

Si ndo hapo! Halafu pia hao N.C.C.R. si walienda kumwona rais pale ikulu? Kwanini hakupeleka maoni haya pamoja wakati wa ujumbe ule?
 
wacha umbumbumbu, kwanini usiwasilishe maoni yako kwa maandishi kwa spika au unataka show off, uonekane kwenye runinga halafu wananchi waone ulionewa na wakuonee huruma

Labda hafahamu kama kuna utaratibu huo?!?!
 
Kufuatia kupitishwa kwa SHERIA ya marekebisho ya KATIBA leo Bungeni, Mh. Kafulila atoa maoni yake akitofautiana na maamuzi yaliyopitishwa leo. Mh. Kafulila ameandika waraka huu akiufafanulia UMMA juu ya mchakato huo uliopitishwa jinsi gani hauna TIJA wala hautaleta mabadiliko yoyote ambayo wanaharakati na wananchi kwa ujumla wameazimia.

Hakuna hoja hapo kwani kitendo cha kuifanya tume iwe inachaguliwa kutokana na majina yaliyopendekezwa na vyombo vyao hii italeta tija kubwa kwani tume itakuwa na uhuru kiasi.

MAONI YA MH. DAVID KAFULILA

Habari Watanzania,

Nina maoni tofauti kuhusu hiki kinachoendelea kuhusu marekebisho ya sheria ya kusimamia mchakato wa katiba mpya.
Nimejaribu kuomba kuchangia ili niweke maoni yangu wazi lakini imeshindikana, Spika amesema NCCR amepewa mtu mmoja tu Mh. Machali hivyo nikaona ni vema niwajulishe kupitia mtandao maoni yangu.

UTANGULIZI

Hapa ningependa kukumbusha kuwa kutoka NCCR ni mimi David Kafulila na Felix Mkosamali ambao tulikuwa wajumbe wa kamati ya sheria na Utawala. Mh.Mkosamali ni mjumbe wa kudumu kwenye kamati hii, mimi ni miongoni mwa wajumbe walio ongezwa wakati wa kupitia muswada huu. Pia ikumbukwe kuwa ni mimi na Mkosamali ambao tuliungana na CHADEMA kutoka nje katika mkutano wa tano wa Bunge kupinga namna mchakato ulivyoendeshwa. Niliomba kuchangia bungeni lakini imeshindikana kabisa kupata nafasi lakini kwa kuzingatia umuhimu wa jambo hili na nafasi niliyokuwa nayo katika jambo hili naona kuna umuhimu wa kuzungumza kitu kwani hata wale mabalozi wa nchi tano za Ulaya walipokuja bungeni kwenye mkutano wa tano ni mimi niliyekuwa mmoja wa wabunge waliokutana nao kutoa maoni.

Maoni yako yalikuwa nini? kwa hao mabalozi ?Mbona hujawahi kuyaweka bayana hayo maoni yako ili yaweze kupimwa na watu wengine?

MAONI

Nimeshangaa kuona mvutano wa kisiasa kuhusu mabadiliko yaliyoletwa na serikali kwani ninavyofahamu kuna mambo mengi ya msingi katika sheria hii ambayo yalipaswa kubadilishwa, na nilidhani ndiyo yangeletwa kwenye marekebisho ya sheria hii baada ya vikao vya Rais na wadau wengine vikiwemo vyama vya siasa. Mabadiliko yaliyoletwa sio issues za msingi ambazo zingesaidia kuiboresha tume na mchakato mzima wa katiba mpya.

Kwa mfano;

1. Hoja ya kumwondoa DC na Kuweka Mkurugenzi (DED)

Wabunge wengi wa CCM wanataka DC ndio asimamie, wakati hotuba ya kambi rasmi ya upinzani inapendekeza DED.
Ukweli ni kwamba wote DED na DC hawafai kwasababu wote ni sehemu ya serikali na badala yake ilipaswa jukumu hilo litekelezwe na Tume yenyewe ambayo inapaswa kuwa huru.

Ukisoma utaona kuwa hawa wamepewa jukumu la kuitisha mikutano kama tume itaona kuwa kuna haja ya kufanya suala hilo, kifungu kinachobadilishwa ni cha 17 (5) (a) ambacho kinasomeka kuwa "kwa Tanzania Bara ,kumtaka mkuu wa wilaya ,Afisa mtendaji wa kata au mtaa au afisa mtendaji wa kijiji kuitisha mkutano wa wakazi wa mji ,kata ,mtaa au kijiji kwa vyovyote itakavyokuwa" hivyo jukumu hilo kuondolewa huko na kupewa DED ni sahihi kwani huyu ndio mwenye uwezo wa kuwa na timu ya kazi kama hao watendaji wa kata na vijiji,

2.Hapa ndipo inakuja hoja ya mchakato huu mzima wa kura ya maoni kusimamiwa na Tume huru.
Uamuzi wa kuifanya Tume ya sasa ya Uchaguzi kusimamia mchakato huu ni kinyume cha msimamo wetu wa awali kama wapinzani kwasababu moja ya hoja ya mahitaji ya katiba mpya ni tume huru ya uchaguzi, sasa inawezekanaje tume mbovu ya uchaguzi isimamie mchakato wa kupata katiba huru?. Hili lilikuwa muhimu sana. Tungekubaliana kuhusu kupata kwanza tume huru ya uchaguzi kisha tume hiyo isimamie mchakato wa katiba mpya tungekuwa na uhakika wa kupata katiba ambayo watanzania wanaitaka.

Hakuna kipengele hata kimoja ambacho kinasema kuwa tume ya uchaguzi ya sasa ndio itasimamia zoezi la kura ya maoni , na kwa sasa mabadiliko yote yanahusika na tume ya katiba na sio vinginevyo.

3.Hoja ya Tume huru ya kusimamia mchakato wa katiba

Hii pia ni hoja iliyoachwa kwasababu Tume hii ya sasa inateuliwa na Rais na kwa namna ilivyo bado Rais ndio mwenye mamlaka ya kumtoa mjumbe yeyote. Marekebisho yaliyoletwa leo yanapendekeza namna ya kumtoa mjumbe wa tume hii ambaye anayetuhumiwa kukiuka kanuni za maadili, kwamba Rais atateua Kamati ya kufanya maamuzi. Hapa haikupaswa Rais kuteua kamati badala yake ilitakiwa sheria itamke rasmi kamati hiyo itakuwa akina nani ili kamati hiyo iwe huru kuliko iteuliwe na Rais, pengine kosa la mjumbe ni mvutano unaohusu nguvu za serikali kwa tume.

Hapa napo Kafulila amepotoka kwani mabadiliko yanasema kuwa tume ya nidhamu itakuwa na wajumbe wafuatao;

1. Jaji wa mahakamani ya rufani- mwenyekiti

2. kamishina wa tume ya haki za binadamu na utawala bora

3.kamishina wa secretariat ya maadili ya viongozi wa umma

4.wakili wa mahakama kuu kutoka znz atakayependekezwa na chama cha mawakili znz

5.wakili wa mahakama kuu atakayependekezwa na TLS

Hii ni sawa na kusema kuwa wajumbe hawa hawateuliwi na Rais bali wapo kwenye sheria na hivyo lazima lazima pawe na chombo cha kutaja majina husika ndio maana Rais atateua. Kafulila hana hoja kwenye hilo.

4. Hoja ya Sekretariet huru.

Kwa mujibu wa sheria hii Sekratariet itaundwa na waziri mwenye dhamana. Hii inaondoa uhuru wa utendaji wa sekretariet, ilipaswa Sekretariet iteuliwe na Tume na iwajibike kwa tume ili kupunguza mkono wa serikali kwenye mchakato na utendaji wa kupata katiba mpya.

Hapa nako hakuna hoja , kwani mamlaka ya nidhamu ya secretariat hii yapo mikononi mwa tume yenyewe kwa mujibu wa maraekebisho haya ambayo yanasomeka katika kifungu cha 13 (7) "tume itakuwa mamlaka ya nidhamu kwa wajumbe wa Secretariat"

5. Hoja ya ushiriki wa Jumuiya za kiraia, taasisi za dini vya vyama vya siasa

Marekebisho yaliyoletwa sehemu A, kifungu cha 7 yanatoa uhuru wa jumuiya hizi kushiriki kwa kualikwa na Rais, lakini sehemu hiyo hiyo ya marekebisho kifungu cha 8 inatamka kuwa Rais hafungwi na mapendekezo hayo kuteua watu wengine kuwa wajumbe. Hapa kwa tafsiri rahisi ni kwamba, haki imetolewa kwenye kifungu cha 7 na imepokonywa kwenye kifungu cha 8 kwa kuwaweka wananchi tayari wasishangae itakapotokea mapendekezo yaliyopelekwa na jumuiya yoyote kukataliwa yote. Ingepaswa kuweka wazi kuwa Rais atalazimika kuteua miongoni mwa walipendekezwa na sio nje ya waliopendekezwa.

Kwa ujumla pamoja na sheria hii kupitishwa leo lakini ina matundu makubwa sana kuweza kuifanya isimamie mchakato huu muhimu kwa uhakika. Bado ni sheria ambayo inategemea sana dhamira ya Rais mwenyewe kuliko mfumo tulioweka.

Napenda ifahamike kuwa, sheria hii iliyopitishwa leo haijafanya mabadiliko ya msingi ambayo sisi sote ( wananchi, wanaharakati na wanasiasa) wenye moyo wa dhati wa kuleta mabadiliko kitaifa tulitazamia.

Mabadiliko haya kimsingi yanazungumzia juu ya tume ya katiba na haijabeba vifungu vyote.

Pamoja katika kujenga Taifa
David Kafulila

Baada ya kujadili hayo nafikiri ingefaa Kafulila akakaa chini na kusoma mabadiliko haya hatua kwa hatua na kujua nini kimepelekwa bungeni na kuweza kujua kuwa nini kimepelekwa Bungeni na tafsiri yake kwa ujumla wake na sio kama alivyokurupuka hapa na kutoa maoni na utashangaa kuna magazeti yataandika kesho hivyo hivyo.

Haya ndio maoni yangu na ufafanuzi japo kwa kifupi najua atasoma na kufanya rejea ya mabadiliko husika kama yalivyowasilishwa.
 
Ni kweli mh kafulira ila wanachojaribu kukufanyia Ccm ni kukuweka kama pambo la mbunge endelea kupambana hii tutaihoj
 
Kufuatia kupitishwa kwa SHERIA ya marekebisho ya KATIBA leo Bungeni, Mh. Kafulila atoa maoni yake akitofautiana na maamuzi yaliyopitishwa leo. Mh. Kafulila ameandika waraka huu akiufafanulia UMMA juu ya mchakato huo uliopitishwa jinsi gani hauna TIJA wala hautaleta mabadiliko yoyote ambayo wanaharakati na wananchi kwa ujumla wameazimia.

MAONI YA MH. DAVID KAFULILA

Habari Watanzania,

Nina maoni tofauti kuhusu hiki kinachoendelea kuhusu marekebisho ya sheria ya kusimamia mchakato wa katiba mpya.
Nimejaribu kuomba kuchangia ili niweke maoni yangu wazi lakini imeshindikana, Spika amesema NCCR amepewa mtu mmoja tu Mh. Machali hivyo nikaona ni vema niwajulishe kupitia mtandao maoni yangu.

UTANGULIZI

Hapa ningependa kukumbusha kuwa kutoka NCCR ni mimi David Kafulila na Felix Mkosamali ambao tulikuwa wajumbe wa kamati ya sheria na Utawala. Mh.Mkosamali ni mjumbe wa kudumu kwenye kamati hii, mimi ni miongoni mwa wajumbe walio ongezwa wakati wa kupitia muswada huu. Pia ikumbukwe kuwa ni mimi na Mkosamali ambao tuliungana na CHADEMA kutoka nje katika mkutano wa tano wa Bunge kupinga namna mchakato ulivyoendeshwa. Niliomba kuchangia bungeni lakini imeshindikana kabisa kupata nafasi lakini kwa kuzingatia umuhimu wa jambo hili na nafasi niliyokuwa nayo katika jambo hili naona kuna umuhimu wa kuzungumza kitu kwani hata wale mabalozi wa nchi tano za Ulaya walipokuja bungeni kwenye mkutano wa tano ni mimi niliyekuwa mmoja wa wabunge waliokutana nao kutoa maoni.

MAONI

Nimeshangaa kuona mvutano wa kisiasa kuhusu mabadiliko yaliyoletwa na serikali kwani ninavyofahamu kuna mambo mengi ya msingi katika sheria hii ambayo yalipaswa kubadilishwa, na nilidhani ndiyo yangeletwa kwenye marekebisho ya sheria hii baada ya vikao vya Rais na wadau wengine vikiwemo vyama vya siasa. Mabadiliko yaliyoletwa sio issues za msingi ambazo zingesaidia kuiboresha tume na mchakato mzima wa katiba mpya.

Kwa mfano;

1. Hoja ya kumwondoa DC na Kuweka Mkurugenzi (DED)

Wabunge wengi wa CCM wanataka DC ndio asimamie, wakati hotuba ya kambi rasmi ya upinzani inapendekeza DED.
Ukweli ni kwamba wote DED na DC hawafai kwasababu wote ni sehemu ya serikali na badala yake ilipaswa jukumu hilo litekelezwe na Tume yenyewe ambayo inapaswa kuwa huru.

2.Hapa ndipo inakuja hoja ya mchakato huu mzima wa kura ya maoni kusimamiwa na Tume huru.
Uamuzi wa kuifanya Tume ya sasa ya Uchaguzi kusimamia mchakato huu ni kinyume cha msimamo wetu wa awali kama wapinzani kwasababu moja ya hoja ya mahitaji ya katiba mpya ni tume huru ya uchaguzi, sasa inawezekanaje tume mbovu ya uchaguzi isimamie mchakato wa kupata katiba huru?. Hili lilikuwa muhimu sana. Tungekubaliana kuhusu kupata kwanza tume huru ya uchaguzi kisha tume hiyo isimamie mchakato wa katiba mpya tungekuwa na uhakika wa kupata katiba ambayo watanzania wanaitaka.

3.Hoja ya Tume huru ya kusimamia mchakato wa katiba

Hii pia ni hoja iliyoachwa kwasababu Tume hii ya sasa inateuliwa na Rais na kwa namna ilivyo bado Rais ndio mwenye mamlaka ya kumtoa mjumbe yeyote. Marekebisho yaliyoletwa leo yanapendekeza namna ya kumtoa mjumbe wa tume hii ambaye anayetuhumiwa kukiuka kanuni za maadili, kwamba Rais atateua Kamati ya kufanya maamuzi. Hapa haikupaswa Rais kuteua kamati badala yake ilitakiwa sheria itamke rasmi kamati hiyo itakuwa akina nani ili kamati hiyo iwe huru kuliko iteuliwe na Rais, pengine kosa la mjumbe ni mvutano unaohusu nguvu za serikali kwa tume.

4. Hoja ya Sekretariet huru.

Kwa mujibu wa sheria hii Sekratariet itaundwa na waziri mwenye dhamana. Hii inaondoa uhuru wa utendaji wa sekretariet, ilipaswa Sekretariet iteuliwe na Tume na iwajibike kwa tume ili kupunguza mkono wa serikali kwenye mchakato na utendaji wa kupata katiba mpya.

5. Hoja ya ushiriki wa Jumuiya za kiraia, taasisi za dini vya vyama vya siasa

Marekebisho yaliyoletwa sehemu A, kifungu cha 7 yanatoa uhuru wa jumuiya hizi kushiriki kwa kualikwa na Rais, lakini sehemu hiyo hiyo ya marekebisho kifungu cha 8 inatamka kuwa Rais hafungwi na mapendekezo hayo kuteua watu wengine kuwa wajumbe. Hapa kwa tafsiri rahisi ni kwamba, haki imetolewa kwenye kifungu cha 7 na imepokonywa kwenye kifungu cha 8 kwa kuwaweka wananchi tayari wasishangae itakapotokea mapendekezo yaliyopelekwa na jumuiya yoyote kukataliwa yote. Ingepaswa kuweka wazi kuwa Rais atalazimika kuteua miongoni mwa walipendekezwa na sio nje ya waliopendekezwa.

Kwa ujumla pamoja na sheria hii kupitishwa leo lakini ina matundu makubwa sana kuweza kuifanya isimamie mchakato huu muhimu kwa uhakika. Bado ni sheria ambayo inategemea sana dhamira ya Rais mwenyewe kuliko mfumo tulioweka.

Napenda ifahamike kuwa, sheria hii iliyopitishwa leo haijafanya mabadiliko ya msingi ambayo sisi sote ( wananchi, wanaharakati na wanasiasa) wenye moyo wa dhati wa kuleta mabadiliko kitaifa tulitazamia.

Pamoja katika kujenga Taifa
David Kafulila

Ha ha ha aaaa PRO CDM ambao wanajigamba humu kuwa mawazo yao yamesikilizwa kumbe wameliwa na kuingizwa mjini. CDM mmeyaona hayooooooo ya kafulila?

Bwana Kafulila mjadala wa huo mswada uko Bungeni, na wewe ni Mbunge kwa nini usipeleke "schedule of amendment" na ukaitetee huko Bungeni?

Ni sawa kueleza maoni yako binafsi, lakini nadhani kwa kuwa wewe ni mwakilishi na una haki ya kupeleka schedule of amendment, unapaswa ufanye hivyo, badala ya kulalamika. Ni heri ufanye sehemu yako hata kama amendment haita pita.
 
Nimeshangaa ametuletea sisi waandishi, wakati kwa kanuni za bunge. Mbunge hata akikosa nafasi ya kuzungumza anaweza kuchangia kwa maandishi, Kafulila angetumia hii njia kuibana serikali bungeni. Naona pia anaelekea kusahau kwa kuwa CHADEMA ilishasema kwenye vyombo vya habari baada ya mazungumzo na Rais kwamba muswada huu ungefanyiwa marekebisho kwa awamu. Awamu ya kwanza kuhusu tume ya kukusanya maoni ya katiba, awamu ya pili kuhusu bunge la kutunga katiba na awamu ya tatu kuhusu kura ya maoni kusimamiwa na tume ya uchaguzi.

Kafulila alipaswa kusema kwenye awamu hii ya kwanza kuna jambo gani lilipaswa kuwepo kwenye marekebisho ambalo halipo? Ndio angeweza kutusaidia vizuri zaidi waandishi. Hizo awamu zingine CHADEMA na wadau wengine wameshasema kwamba wanazisubiria kwenye hatua zinazofuata kwa kuwa huu ni mchakato wa mpaka mwaka 2014 kwa kadiri ya hotuba za Pinda na Kikwete.

PM
 
Mh Kafulila muambie huyo aliyekutuma ajipange upya alafu akutume tena,maana hoja hii haina mashiko!
 
Ndugu,

Kama bunge limepitisha marekebisho ya sheria ya katiba na hakuna aliyepinga kwa maana aidha ya kutoa shilingi au kutoka nje sisi wananchi tunasema BUNGE limepitisha kwa kauli moja na hiyo ndiyo itakayokuwa sheria. Kama kanuni za bunge hazikukiukwa Kafulila akubaliane na matokeo maana uwezi kumridhisha kila mmoja.
 
Kafulila na Hamad Rashid ndio waliokuwa mstari wa mbele wakimtaka Speaker kubadilisha kanuni za bunge ili tafsiri ya 'kambi ya upinzani' ibadilike. Na wawili hawa wamefukuzwa kwenye vyama vyao speaker wa CCM ameamua kwenye hii issue atajificha kwenye hoja ya separation of power ili wabunge hawa waendelee!

Hadi leo sijaelewa ni kwanini Speaker au hata msajili wa vyama vya siasa wameamua kuwatetea hawa watu ili wabakie bungeni? Kafulila anafanya kazi za NCCR Mageuzi wa za CCM? Na hizi hoja alizoandika hapa ni za chama kipi? alikaa na mwenyekiti wa chama kipi?
 
Sina hakika kuwa kikao kijacho utakuwepo, kwahiyo toa dukuduku lako la mwisho mapema ndugu!!!

Back
Top Bottom