Kafulila: Kuiondoa CCM madarakani, Uwezo tunao na Sababu tunazo

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,797
71,215
Kauli mbiu aliyoitoa Bungeni akichangia hotuba ya makadirio ya Budget ya wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi kuwa CCM itaondoka madarakani kwani uwezo tunao na sababu zipo na kuwa hata wao CCM wanaelewa hilo maana hata katika makorido wanakiri imenifurahisha.

Jee wadau tunasemaje kwa kauli hiyo thabiti na ya kutia moyo?
 
Kina Kafulila au kina Slaa? Kambi hizi zina historia ya kufurahisha.
 
Kauli imeleta burudani ya ajabu. Nimemwona Mwakyembe ambaye alitegemea atasifiwa na Kafulila kama wanavyofanya ccm, ameiponda bajeti vibaya mno, na kusema haina majibu wala jipya. Ameshangaa ni kwa vipi
tunazidiwa na mashirika ya ndege ya Rwanda na Burundia. Amesema bora tusingemfukuza mkoloni, maana tangu alipotuachia meli hiyo moja ziwa Tanganyika, bado ipo hiyohiyo baada ya miaka 50.
 
Mzee PJ ni kweli dogo kamwaga ugali na ujumbe ume sink hasa kwenye akili zao na kama hawaamini basi waingie kavu kavu bila polisi na usalama wa Taifa waone ngoma ilivyo
 
Mzee PJ ni kweli dogo kamwaga ugali na ujumbe ume sink hasa kwenye akili zao na kama hawaamini basi waingie kavu kavu bila polisi na usalama wa Taifa waone ngoma ilivyo
Mkuu ni kweli Dogo kazungumza kwa ujasiri sana. Hata taarifa iliyotolewa na Mbunge mmoja wa CCM kuhusu bandari ya Rotterdam ilipokuja kupewa counter attack na Mbatia akimtetea Kafulila imenipa raha kuwa sasa timu imetulia na inagonga 4/4/2 kwenda mbele.
 
Kauli hii japo inaweza kuwa mwiba mioyoni ni ya kweli sana! Yaani kuna vitu havijabadilika (in a +ve way) toka enzi za mkoloni bali vimebaki hivyo hivyo au kuelekea kwenye -ve. Reli, Ndege na Bandari ni matatizo makubwa sana kwa nchi yetu leo kuliko ilivyokuwa zamani.
 
Mkuu ni kweli Dogo kazungumza kwa ujasiri sana. Hata taarifa iliyotolewa na Mbunge mmoja wa CCM kuhusu bandari ya Rotterdam ilipokuja kupewa counter attack na Mbatia akimtetea Kafulila imenipa raha kuwa sasa timu imetulia na inagonga 4/4/2 kwenda mbele.

Hata mimi nimewaona Kafulila na Mbatia bega kwa bega, hapo vipi?
 
haaah! haaa! haaaa! Ndugu yangu LUNYUNGU umenifurahisha hapa
".....kama hawaamini basi waingie kavu kavu bila polisi na usalama wa Taifa waone ngoma ilivyo"

I HATE CCM, NAICHUKIA CCM
 
Kauli imeleta burudani ya ajabu. Nimemwona Mwakyembe ambaye alitegemea atasifiwa na Kafulila kama wanavyofanya ccm, ameiponda bajeti vibaya mno, na kusema haina majibu wala jipya. Ameshangaa ni kwa vipi
tunazidiwa na mashirika ya ndege ya Rwanda na Burundia. Amesema bora tusingemfukuza mkoloni, maana tangu alipotuachia meli hiyo moja ziwa Tanganyika, bado ipo hiyohiyo baada ya miaka 50.

Huyu dogo mchango wake wa leo nimeufurahia sana!
 
Hata mimi nimewaona Kafulila na Mbatia bega kwa bega, hapo vipi?

pale dogo kawaga hoja za msingi mno , mbatia ana wajibu wa kumuunga mkono , sababu ya hoja zake.namzimia sana hasa kwa kusema "tunawasikia makoridoni wakikiri kuwa mambo magumu.Kuna ukweli jaribu kuanaglia sekta zote, hakuna la maana zaidi ya ghiriba.bajeti zinapita hata mbovu kama ya afya, kilimo na nk huku hazina majibu ya kwli kutatua na kukata kiu ya maisha bora kwa kila mtanzania
 
Kina Kafulila au kina Slaa? Kambi hizi zina historia ya kufurahisha.

mbona ushahidi wa hilo upo wazi ukiangalia tu budget za wizara zote zimepunguwa au zinapunguwa kila mwaka wakati huo thamani ya pesa pia inashuka.......mfano wizara ya afya jana wanategemea wahisani kwa 97%
 
itaondoka madarakani baada ya miaka 50 ijayo. wapinzani wenyewe wabinafsi, wabaguzi, wapo kwa matumbo yao hasa CHADEMA.
 
Back
Top Bottom