Kafulila: CCM bado haijatawala nchi au imeshindwa kuongoza

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
*Asema serikali yake haijui rasilimali zilizopo
*Adai ina mfumo dhaifu kudhibiti fedha za umma
*Asisitiza hali ya umaskini inazidi kuongezeka nchini
*Ampongeza Dkt. Shein, azungumzia utata wa Dowans

Na Eckland Mwaffisi

MBUNGE wa Kigoma Kusini kwa tiketi cha Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. David Kafulila, amesema Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), bado haijaweza kutawala nchi ndio maana hadi sasa haijui kiasi cha rasilimali zilizopo nchini.

Bw. Kafulila aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika mahojiano maalumu na gazeti hili na kutoa maoni yake juu ya Kamati za Kudumu za Bunge kubaini ubadhirifu mkubwa wa fedha unaofanywa katika na taasisi mbalimbali za umma.

Alisema tatizo kubwa linalochangia ubadhirifu huo ni mfumo dhaifu unaotumiwa na CCM katika kudhibiti matumizi ya fedha kwa viongozi na bodi zilizopewa dhamana ya kusimamia taasisi hizo ambao wengi wao huziongoza kwa maslahi binafsi.

Alisema jambo la msingi kwa sasa ni Serikali ni kutengeneza mfumo ambao utadhibiti ubadhirifun huo na kufanya tathmini ya kujua idadi kamili ya mali zilizopo.

"Mwaka 2009, Serikali ilifanya tathmini ili kujua idadi kamili ya mashirika yaliyopo, kimsingi hadi sasa Serikali ya CCM haijui utajiri wa nchi upo kwa kiasi gani.

"Ukiwauliza tuna ardhi kiasi gani kwa ajili ya kilimo cha Pamba, Kahawa na mazao mengine ya biashara na chakula, huwezi kupata jibu la kueleweka," alisema Bw. Kafulila.

Hali ya umaskini nchini

Akizungumzia hali ya umaskini nchini, Bw. Kafulila alisema, idadi ya Watanzania maskini inazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka akitolea mfano kuwa, mwaka 2005 idadi ya Watanzania ambao hawana uhakika wa kula mlo mmoja kwa siku ilikuwa milioni 11.

Alisema pamoja Serikali mwaka 2005 kutoa ahadi ya kupunguza umaskini kwa asilimia 50, ahadi hiyo imeshindwa kutekelezwa ambapo mwaka 2009/2010, idadi ya Watanzania maskini iliongeaeka hadi kufikia milioni 12.7.

"Nilitegemea idadi ya Watanzania maskini ingepungua na kufikia milioni 5.5 mwaka 2009/2010, kama Serikali ilivyoahidi kupunguza umaskini kwa asilimia 50, hii inaonesha ni jinsi gani Serikali ilivyoshindwa kutekeleza ahadi zake," alisema.

Aliongeza kuwa, Tanzania ni nchi yenye utajiri mkubwa wa rasilimali pia ni miongoni mwa nchi saba duniani inayopata misaada mingi kutoka kwa wahisani lakini imeshindwa kupiga hatua ya maendeleo yaliyotarajiwa na Wtanzania wengi katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru.

"Tanzania ni nchi ya tatu kwa kuwa na dhahabu, pia ni nchi ya 11 kwa kuwa na mito mingi barani Afrika, nchi hii pia ndio inaongoza kwa nchi za Afrika Mashariki kuwa na ardhi ya kutosha kwa matumizi mbalimbali .

"Hivi sasa nchi yetu ni ya tatu kwa kuwa na gesi nyingi duniani lakini tatizo kubwa lipo katika uongozi, tunazidiwa na nchi ambazo hazina rasilimali lakini zimepiga hatua kubwa kiuchumi.

Alisema nchi ya Rwanda pamoja na machafuko yaliyodumu muda mrefu, Serikali yao inamiliki ndege saba kati ya hizo, mbili ni kubwa ambapo hivi sasa, wamefanikiwa kumwezesha kila raia kuwa na nyumba ya bati lakini Tanzania yenye utajiri mkubwa, raia wake wanaishi kwa mateso makubwa.

Uongozi makini wa Dkt. Shein

Bw. Kafulila anasema, katika kipindi cha mwaka mmoja cha utawala wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, ameonesha umakini mkubwa wa kuifanya Zanzibar yenye neema inawezekana.

Alisema kiongozi huyo na dhamira ya kweli kuhakikisha Zanzibar inapiga hatua kwa haraka zaidi kuliko Tanzania Bara lakini anapaswa kuwa makini na mfumo wa chama chake ambazo ambao unaweza kukwamisha malengo yake.

"Kimsingi mfumo wa chama tawala unaathiri uwajibikaji ndio maana nikasema anapaswa kuwa makini katika hili ili dhamira yake ya kuifanya Zanzibar yenye neema iweze kufanikiwa," alisema.

Sakata la ushoga

Akizungumzia sakala la ushoga ambalo liliibuka hivi karibuni, Bw. Kafulila alisema ameshtushwa na msimamo wa Serikali ya Ungereza kupitia Waziuri Mkuu wake David Cameron na chama chake.

Alisema historia inaonesha kuwa, vyama vya mlengo wa kushoto siku zote vinakuwa na msimamo wa kupinga mambo yasiyo ya msingi hasa kwa kuzingatia kuwa, familia ndio msingi wa ujenzi wa Taifa lolote duniani hivyo msimamo wa Uingereza ni changamoto kubwa kwa vyama vya aina hiyo.

"Kauli ya Bw. Cameron na Serikali yake ni changamoto kwa nchi za Afrika kuacha kushirikiana na mataifa ambayo hayana masharti magumu, binafsi nashauri Tanzania iimarishe ushirikiano wake na Taifa la China," alisema.

Aliongeza kuwa ni aibu katika dunia ya leo kuona Taifa moja linasema mataifa ambayo yatapinga suala la ushoga linavunja uhusiano.

Utata wa malipo kampuni ya Dowans

Bw. Kafulila alisema, Serikali ilipeleka kesi hiyo mahakamani ili kuwaridhisha Watanzania lakini lengo lake lilikuwa kushindwa kesi ndio maana aliandaa hoja binafsi kwa lengo la kuipeleka bungeni.

Alisema baada ya Bunge kuangiza mkataba wa kampuni hiyo uvunjwe, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), lilipata ushauri wa kisheria kutoka Kampuni ya Rexy Atorney ambayo ilishauri mkataba huo uvunjwe kwani hakuna madhara yoyote yanayoweza kutokea kisheria.

Aliongeza kuwa, Kampuni ya Rexy ilitumika kama mshauri wa Kmapuni ya Kufua Umeme ya Dowans, ili iweze kupata mkopo katika Benki ya Stanbic ambapo kampuni hiyo, iliuthibitishia uongozi wa benki hiyo kuwa Dowans ina mkataba halali ambao hauna matatizo.

Bw. Kafulila alisema, pia Kampuni ya Rexy ilichukuliwa na TANESCO kwenda kuiwakilisha katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC lakini ilishindwa kesi.

"Upo mkanganyiko mkubwa wa kampuni ya Rexy, kutumiwa na watu wawili wanaodaiana kwa maana ya Dowans na TANESCO, pili kampuni hii haina rekodi ya kushinda kesi za kimataifa sasa tunataka kufahamu kigezo gani kimetumika kuitumia Kampuni ya Rexy kusimamia kesi kubwa kama hii.

"Ukweli ni kwamba hapakuwa na mchakato wowote uliotumia kuchagua kampuni ya uwakili ambayo itasimamia kesi kubwa kama hii ndio maana tumeshindwa, hii inaonesha kuwa lengo la Serikali tangu mwanzo lilikuwa kushindwa kesi," alisema Bw. Kafulila.

Aliongeza kuwa, kutokana na sakata hilo ndio maana alidhamiria kupeleka hoja binafsi bungeni lakini alizuiwa kwa sababu ya kesi ambayo ilifunguliwa mahakamani na wanaharakati kupinga malipo hayo.

"Dhamira yangu ilikuwa Serikali itupe maelezo kwa nini imetufikisha katika deni la sh. bilioni 94 ambazo hivi sasa zimeongezeka, hapa tulipofikia sasa ni udhaifu wa Serikali ambayo ilikusudia kushindwa kesi hii.

"Wakati bunge linaazimia kuvunja mkataba na Dowans, Serikali ilikubali kwa shingo upande, kimsingi tulishakosea tangu uteuzi wa Kampuni ya Uwakili, kesi zilizofunguliwa kama zitaendelea mahakamanideni tunalodaiwa litazidi kuongezeka," alisema.

Alisema suala hilo bado linaweza kupelekwa bungeni ili liweze kujadiliwa na wabunge
 
Back
Top Bottom