Kafulila atishia: Nikishindwa kesi nitahamia chama kingine

"Nimesema nitahamia chama chochote, tusubiri uamuzi wa mahakama kama utaniondoa NCCR Mageuzi ndipo nitakuwa tayari kutamka chama gani najiunga nacho," alisema Kafulila.

Anaongea kama alikuwa amekunywa KONYAGI!! Anafanya nini huko Mbeya au alienda kuwasha Mwenge??
 
Kafulila akishdwa kesi anafulia. Anatapatapa mno huyu kijana. na asipoangalia ataporomoka kisiasa moja kwa one
 
Mtoto akinyea mkono, huukati, huyo Kafulila arudi tu CDM na tutampokea kamwa mwana mpotevu...
 
Nionavyo mimi hapa Kafulila anatishia nyau CCM ili kama mahakama itamwondoa aiadhibu CCM.
 
Mtaniwia radhi but toka zamani wabunge wa upinzani toka Kigoma wamekuwa vimatatizo mara wanapoaminiwa na wananchi.. Kuanzia Amani Kaborou (samahani kama nimelikosea jina)..
 
Binafsi huwa naangalia quality ya mwanasiasa mwenyewe, sawa kafulila naye ana matatizo yake mda mwingine lakini inabidi arudi kundini (CDM) kujiunga na jeshi la ukombozi kwani kijana anaweza sana but kitakachompasa ni nidhamu 2 na kuheshimu viongozi wake pia anachotakiwa asiwe na chembechembe za unafiki kwani huu ndio huwa mgonjwa mbaya kwenye siasa au kama atarudi CDM basi asubirie katiba mpya itampa acces ya kugombea ubunge.
 
kafulila:Dr.Slaa alikwambia uwe na nidhamu,JK alikwambia uwe na Breki,. Sasa utaishi maisha ya kutanga tanga
 
huyu naye ingekuwa kwenye ngono tungesema malaya hana msimamo hata kidogo sijui IQ yake ikoje namuona yuko makini ila maamzi ndio zero kabisa
 
Mtaniwia radhi but toka zamani wabunge wa upinzani toka Kigoma wamekuwa vimatatizo mara wanapoaminiwa na wananchi.. Kuanzia Amani Kaborou (samahani kama nimelikosea jina)..

upo sahihi,.zitto na kafulila..cjui kwa nini hawana msimamo.
 
wahenga walisema usitukana wakunga uzazi ungalipo....huyu jamaa alikuwa akiwakandia sana chadema pamoja na kupigania kuwepo kwa kambi mbili za upinzani bungeni yeye na hamadi shashidi wake.....i hope atahamia Alliance for Democratic Change(ADC) akaungane na hamad rashid.
 
Back
Top Bottom