Kafulila atishia: Nikishindwa kesi nitahamia chama kingine

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi), David Kafulila, amesema yuko tayari kukihama chama chake na kujiunga na chama kingine ikiwa atashindwa kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama aliyoifungua mahakamani.

Kafulila aliyasema hayo wakati akizungumza na NIPASHE jijini Mbeya na kuwa ana uhakika wa kushinda kiti cha ubunge kwenye jimbo lake hata kama atagombea kupitia chama kingine, hivyo uamuzi wa kutimuliwa NCCR Mageuzi hamuumizi kichwa.

Alisema kuwa endapo mahakama itaamua kubariki uamuzi wa yeye kufukuzwa NCCR Mageuzi, hana mpango wa kukata rufaa katika Mahakama ya juu, badala yake atahamia chama kingine na kurudi jimboni kuomba ridhaa ya wananchi aendelee kuwa mbunge wao.

Hata hivyo Kafulila hakuwa tayari kutaja chama anachokusudia kuhamia, akisema kuwa hilo atalisema baada ya mahakama kutoa uamuzi wa kesi aliyoifungua mahakamani.

“Nimesema nitahamia chama chochote, tusubiri uamuzi wa mahakama kama utaniondoa NCCR Mageuzi ndipo nitakuwa tayari kutamka chama gani najiunga nacho,” alisema Kafulila. Kafulila alijiunga na NCCR Mageuzi mwaka 2010 akitokea Chadema.

Hata hivyo mwaka jana alihitlafiana na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia hali iliyosababishwa avuliwe uanachama kabla ya kukimbilia mahakamani.

CHANZO: NIPASHE
 
Ili chama kisipoteze ruzuku ndio maana Mh. Mbatia kateuliwa, sasa ajiandae kutafuta chama tu, nadhani mahakama zetu kama kawa zitakuwa na maelekezo o juuuuuuuuuu
 
Akishindwa kesi automatically atakuwa siyo mwanachama wa NCCR, sasa anatishia nini.
Labda angesema hata akishinda kesi atahamia chama kingine hapo inge make sense.
 
We swahiba wa Zito, Hakuna binadamu asiye na kasoro. Nakushauri muombe msamaha rais we2 mtarajiwa Dr. Slaa, kisha rudi kundini CDM. Hilo jimbo lako utalipata, vinginevyo sahau ndoto ya ubunge.
 
Nakumbuka nilishaleta uzi hapa jamvini nikamshauri aombe msamaha arudi kundin hata kama ni kupoteza ubunge lkn nyota yake ya kisiasa izidi kung'ara. Akikataa ni ubishi wake,atakua kama Shitambala wa mbeya!
 
Alitakiwa kusema akishindwa kesi, atajiunga na chama kingine na sio kwamba atahamia chama kingine. Maana kama akishindwa kesi, hatakuwa mwanachama wa chama chochote mpaka hapo atakapoomba uanachama na kuruhisiwa kuingia chama husika ikiwa ni pamaoja na NCCR-Mageuzi !!!!
 
Kigoma wana mashine 2 mbili zitto kabwe na kafulila kichwa hicho hakiwezi kutoweka walamawese hawabahatishi.huoni NCCR imejikita zaidi kigoma? ni baada ya mafisadi kuteua wagombea ambao ni mafisadi then wananchi wakaamua kuweka wanafunzi. Wala mawese na Migebuka ni balaa hawadanganyiki.ila tunasikia kuna mbunge mwenzake wa kigoma hukohuko anamwandama sana na ndo wako karibu sana na mbatia siajabu na yeye ccm.
 
Back
Top Bottom