howard
Senior Member
- Feb 21, 2011
- 188
- 28
NAHISI KAMA KUCHANGANYIKIWA KUNA THREAD NYINGINE HUMU INAONYESHA KAFULILA KAIPONDA CHADEMA NA HII JE?
MBUNGE wa Kigoma Kusini David Kafulila (NCCR-Mageuzi) amemshangaa Rais Jakaya Kikwete kuogopa kazi nzuri inayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya kuzungumza na wananchi.
Licha ya kumshangaa rais Kikwete kwa hofu aliyonayo amekipongeza CHADEMA na kusema chama chake kinajipanga kwenda kwa wananchi kwa kuwa ni utekelezaji wa kazi za siasa.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya NCCR-Mageuzi Dar es Salaam jana, Kafulila aliyewahi kuwa kada wa CHADEMA, alisema hofu ya kupinduliwa aliyonayo rais inatokana na watawala kushindwa kutimiza wajibu wao na kusababisha wananchi wengi kukata tamaa.
Mbunge huyo aliweka wazi msimamo wake kwamba licha ya kutofautiana kwenye baadhi ya mambo na chama alichokuwepo mwanzo alisema kazi nzuri inayofanywa na CHADEMA mikoani inastahili kuigwa na vyama vingine.
Alisema sababu ya kutoweka kwa hali ya amani nchini sio wanasiasa bali ni watawala kushindwa kutimiza wajibu wao hivyo ni rahisi kwa waliokata tamaa kufanya lolote watakaloona inafaa.
Rais Kiwkete ni rais wetu namheshimu lakini katika hili natofautiana nae CHADEMA wapo mikoani wanazungumza na wananchi, hiyo ni kazi ya chama chochote cha siasa binafsi nawapongeza, mimi na chama changu tunawaunga mkono. Wapo sahihi kabisa.
Hata sisi tutakwenda kwa wananchi tutafanya mikutano, unajua kuvunjika kwa amani ni matokeo ya watawala kushindwa kutimiza wajibu wao sasa wananchi wanakata tamaa wanaamua kufanya yao, alisema Kafulila.
SOURCE: TANZANIA DAIMA