Kafara!!

DKNY

Member
Nov 4, 2010
30
10
Hbr za kuaminika,ni kwamba bodi ya mikopo imetolewa kafara,na inavunjwa!plus,DOWANS,haitalipwa!
 
very good.....kusiwe na kuzungukana lakini,we are watching them,manake tumechoka kupigwa changa la macho kila siku....ole wao!!!
 
Once Upon a time nilikuwa Waziri Mkuu katika chuo Kikuu hapa Bongo, nilichojifunza wakati ni kitendo cha Hazina kutopeleka fedha Bodi kwa Wakati so kama hilo tatizo bado lipo hata wakivunja Bodi wakaunda taasisi bado Wasomi wa vyuo vikuu wataendelea kusota tu
Hbr za kuaminika,ni kwamba bodi ya mikopo imetolewa kafara,na inavunjwa!plus,DOWANS,haitalipwa!
 
Bodi haina kosa lolote, sidhani kama wanajisaidia fedha chooni; kama wanapewa Bajeti hewa watawapa nini wanafunzi CCM siku zote ni kichwa cha mwenda wazimu, wanajaribu kila policy na strategy bila tafiti kama zinafaa au ni uozo, kuvunja hiyo bodi ni strategy hovyo ambayo itazidi kuonyesha kwamba bado wamelala.
Tutajua mengi zaidi mara baada ya kuivunja
 
Once Upon a time nilikuwa Waziri Mkuu katika chuo Kikuu hapa Bongo, nilichojifunza wakati ni kitendo cha Hazina kutopeleka fedha Bodi kwa Wakati so kama hilo tatizo bado lipo hata wakivunja Bodi wakaunda taasisi bado Wasomi wa vyuo vikuu wataendelea kusota tu

Kuna matatizo mawili; la kwanza ni kutegemea fedha toka "hazina" kuendesha bodi ya mikopo - kwa hiyo moja kwa moja itakuwa inakutana na ukiritimba. Tatizo la pili ni utaratibu - utaratibu unatungwa na kusimamiwa na bodi ya mikopo. Utaratibu wao ni mbovu kuliko wowote ambao umewahi kubuniwa na watu wenye akili timamu.
 
Bado naendelea kuhusisha neno KAFARA na matukio hayo mawili yaani Bodi ya mikopo na Dowans. Kama ni kafara kwa maana ya kuiokoa serikali mbele ya macho ya watanzania basi 'it is too late to act'. Sisemi wasichukue hatua hizo, lakini wazichukue wakijua kuwa watanzania tumechoka tena tumechoka sana. Kwa kifupi ni kwamba ccm tumeichoka, tumeichoka jamaani. Kwa hali ilivyo, hata serikali iboreshe utendaji wake kiasi gani, bado haiwezi kufuta mawazo yetu wananchi kuiondoa madarakani. Eeehh Mungu tupitishe salama hadi 2015 tutakapopata kiongozi makini mwenye kuitakia mema nchi yetu.
 
Bodi ya Mikopo inadai zaidi ya Billion 50 za kitanzania.hizi ni zile za wanafunzi waliomaliza na kustaili kulipa kidogokidogo.Laiki Viogozi wa Bodi wanaspendi zaidi ya bilioni 3 kwamwaka kukusanya madeni yasiozidi 700 millions,Na walipataka kusaidiwa ili wacollect pesa kwa wingi japo altleast asilimia 25 kwa mwaka awataki.Ni walaji wakubwa.Iwapo wangeendesha bodi kwa makini wasingekuwa na aja ya kutegemea hazina ambayo ilishaawaambia kuwa kusanyeni old madeni ili muendelee kukopesha wanafunzi wengi zaidi lakini Uongozi wa bodi ni wapumbavu.eleweni ya kuwa hazina kuipa bodi ya mikopo pesa ambazo azirudi ni sawa na kutupa tu hizo pesa za walipa kodi.
Kama itavyonjwa ni SAWA kabisa kwani Uongozi wa BOdi ya Mikopo ni walafi,wezi na mafisadi wakubwa tena sana.
Nnawajua vizuri.siropoki
 
La kuvunda halina ubani!!! Hata wafanye nini kwa sasa hawa CCM hatuwataki!!! We can't take the sheet no more!!!
 
Hii bodi ya Nyatega imekaa kibabaishaji, ukifika pale mlangoni unakutana na mgambo sekretari ambae anataka umwambie yeye shida zako, ukifika ndani mpangilio mbovu, hawana data za wanafunzi na uzembe kibao.Ila yote ni serikali yakichovu ya Kikwete
 
nyatega baba charles ambae alipata dv 0 form six dakawa, bodi ishamshinda miaka mingi ther very disorganized. Pia siamin kama bodi imevunjwa source ya habari si ya kuaminika.
 
BODI YA MIKOPO INAWEZA KUVUNJWA LAKINI DOWANS LAZIMA WALIPWE
mpende msipende
 
Bodi ikivunjwa nisione mtu anakata mshahara wangu kulipa mkopo niliokopa wakati nasoma, kwani mdai wangu atakuwa kafa...
 
Kulingana na hali halisi iliyopo ni dhahiri thread hii 'it's a mere speculation"; kwanza imeteuliwa kamati ya kuchunguza matatizo ya vyuo vikuu. Hivyo hatuakama hiyo haina budi itokane na mambo yatakayoibuliwa na kamati hiyo. Kuhusu Dowans sasa hivi suala hilo liko mahakamani, hivyo kulipa au kutolipa kutategemea mahakama imeamua nini.
 
Back
Top Bottom