Kadi yako ya mwaliko ni ya kichina

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,895
31,106
Jumamosi kama ilivyo kawaida ni siku ambayo kunakuwa na harusi nyingi,bahati nzuri mimi ni mmojawapo kati ya wageni waalikuwa kwenye harusi moja kubwa ambayo niliichangia fedha nyingi kiasi, kwasababu Bwana harusi ni mtu wangu wa karibu.

Nafika getini [Arusha City Park] nakumbana na walinzi wanaodai kadi ya mwaliko nawakabidhi kadi bila kusita,walinzi wanakagua kadi kwa makini dk mbili tatu zinapita wananirejeshea kadi yangu na kuniambia huwezi kuingia ndani kwasababu kadi yako ni feki walinzi wengine wananiambia kadi yangu ni ya kichina !!!!!!!!!!.Bahati nzuri mwanakamati moja anapita getini na kuwaelekeza walinzi waikubali kadi yangu bila kuelezwa sababu za kudhalilishwa kiasi kile.Wachina kweli wakali yaani mpaka kadi za mwaliko tunawasingizia
 
Wewe ngongo wewe kwani mchina hujui kila kitu chake feki?
so walinzi walimaanisha kadi yako ilikuwa ya kugushi ..ulizamia haruis ya watu eeeh:)
 
Hahahaha mie mchina Namzimia kinoma anamfanya Obama na watu wake wasipate usingizi, sisi huku Africa anatuua taratiiiiiiiibu kwa Vitu Vyake feki
 
Wewe ngongo wewe kwani mchina hujui kila kitu chake feki?
so walinzi walimaanisha kadi yako ilikuwa ya kugushi ..ulizamia haruis ya watu eeeh:)

Heshima kwako FirstLady,

Siwezi kuzamia nilialikwa kwa kufuata taratibu zote.Kilichoniacha hoi ni kuambiwa kadi yako ni ya kichina [feki] nilibaki nacheka nikajiuliza maswali mengi sana bila kuapata majibu.Iko siku wewe FirstLady utatuletea mjukuu utaambiwa ni wakichina sijui utasemaje ?.Hoja yangu hapa ni kwanini kla kitu amabacho si genuine tunawapakazia waCHINA.Nadhani hatuwatendei haki wachina kuna vitu vizuri sana wametufanyia watanzania labda nitaje vichache.
[1] TAZARA
[2] UWANJA WA TAIFA
[3] MIKOPO YA MASHARTI NAFUU KWA NCHI ZA AFRIKA TANZANIA IKIWEMO.
[4] WALIUNGA MKONO NCHI ZA AFRIKA DHIDI YA UKOLONI WA NCHI ZA MAGHARIBI.

Naomba kukuuliza reli ya TAZARA na Uwanja wa michezo wa taifa ni feki ? kama si feki ni kwanini tunawalaumu wachina kwa kila jambo baya.

Hahahaha mie mchina Namzimia kinoma anamfanya Obama na watu wake wasipate usingizi, sisi huku Africa anatuua taratiiiiiiiibu kwa Vitu Vyake feki

Hapana tunakubali kirahisi propaganda za wamarekani
 
Ebana ndugu ulitokea pati silo lako nini? Au ulitoa photoopy ya card?
 
Jumamosi kama ilivyo kawaida ni siku ambayo kunakuwa na harusi nyingi,bahati nzuri mimi ni mmojawapo kati ya wageni waalikuwa kwenye harusi moja kubwa ambayo niliichangia fedha nyingi kiasi,

Ngongo,

Ni nadra sana kwa wanaochangia fedha nyingi shuguli kudaiwa kadi getini! Huwa wanaeleweka kabla na Kamati ya Ulinzi - For sure yawezekana ulito-copy!
 
Ngongo,

Ni nadra sana kwa wanaochangia fedha nyingi shuguli kudaiwa kadi getini! Huwa wanaeleweka kabla na Kamati ya Ulinzi - For sure yawezekana ulito-copy!

Haalfu mambo ya kutuambia alitoa fedha nyingi ndo yale yale ya mtu aliyemwachia secretary hela yeye akaenda Estonia na kutma gari lisaidie harusini ni kujipaisha? Hiyo kadi ilikuwa ni KANYANGA
 
Ngongo,

Ni nadra sana kwa wanaochangia fedha nyingi shuguli kudaiwa kadi getini! Huwa wanaeleweka kabla na Kamati ya Ulinzi - For sure yawezekana ulito-copy!

Heshima kwako Baba_Enock,

Ni kweli wachangiaji wakubwa mara nyingi wanakuwemo kwenye kamati lakini si lazima kamati ya ulinzi.Nikuwemo kwenye kamati ya usafiri ingawa mahudhurio yangu hayakuwa mazuri.
Mkuu wangu Baba Enock getini walikuwepo KK guards si wanakamati.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom