Kadi feki za CHADEMA zachapishwa na CCM kuwapa raia wazirudishe ktk mikutano yao

Habari za kuaminika kutoka katika chanzo kimoja ambacho kwa sasa nisingependa kukitaja.
CCM wameanza mchezo mchafu wa kuchapisha kadi feki za CDM na kuwapa baazi ya wanachama wa CCM kwa masharti yakuzirudisha wafanyapo mikutano yao kwa nia na mazumuni ya kupotosha Umma wa watanzania kwamba CDM haikubaliki kitu ambacho si sahihi.

CHAKushindwa (CHADEMA) mtasema mengi sana ( huu ni umbea pure) , Nape amewashika pabaya sana CHAKushindwa , sasa mmeanza kumpaka matope ili mvunje nguvu yake, ila muelewe hiki ni Chama Tawala kina mbinu nyingi na wazoefu wa kila nyanja
 
Jamani hawa chama cha magamba wameishiwa kabisa,wanachotaka nikujionesha mbele za watu kuwa wanapendwa wakati sio kweli
 
Habari za kuaminika kutoka katika chanzo kimoja ambacho kwa sasa nisingependa kukitaja.
CCM wameanza mchezo mchafu wa kuchapisha kadi feki za CDM na kuwapa baazi ya wanachama wa CCM kwa masharti yakuzirudisha wafanyapo mikutano yao kwa nia na mazumuni ya kupotosha Umma wa watanzania kwamba CDM haikubaliki kitu ambacho si sahihi.

Naamini ujumbe umefika lakini huu uharibifu wa lugha ufanyiwe kazi. Unatakiwa kusoma post yako kabla hujaibandika/ tuma.
 
Jana Kule Sumbawanga walishindwa kuitumia hii,maana mkutano ulihudhuliwa na watoto tu!Inaonyesha hata viongozi wa Chama walisusa...
 
Jambo Kama hilo kufanywa na binaadamu hawa walioshindwa(ccm)sishangai kwa kweli.Atakaeshangaa kutengenezwa kwa kadi feki nami pia nntamshangaa pesa feki zenyewe zinatengenezwa iweje kwa kadi!!!!!?Ccm bado wanaweweseka ikifikia kuanguka wataamini wale wote waliokuwa hawaamini.VIVA CHADEMAAAAA
 
Ishakuwa kasumba kadi feki zimetengenezwa na CCM ata rushwa katika mikutano imetoka CCM huu sasa ni uvivu wa kufikiri na upofu wa mawazo ivi ni kweli kila jambo baya ya CDM linatoka CCM ila zuri ndio la CDM acheni zile za kipendacho roho naona sasa mnadiliki kura nyama mbichi na mnaona imeiva kwa sababu imepikwa na CCM
 
Ishakuwa kasumba kadi feki zimetengenezwa na CCM ata rushwa katika mikutano imetoka CCM huu sasa ni uvivu wa kufikiri na upofu wa mawazo ivi ni kweli kila jambo baya ya CDM linatoka CCM ila zuri ndio la CDM acheni zile za kipendacho roho naona sasa mnadiliki kura nyama mbichi na mnaona imeiva kwa sababu imepikwa na CCM

Hapana mkuu. Labda tuangalie kwa mtizamo mwingine tofauti kidogo. CCM tumekaa nao nyumba moja for over 30 years now hatujaona jipya; actually tabia zime-advance to the worst. Mwizi akiniibia kwa muda mrefu alafu siku akaja kwa jema, siwezi kumuamini unless naona amebadilika kabisa e.g amevunjika mguu hataweza kukimbia tena, hana macho etc.CDM sijawahi kukaa nao nyumba moja and personally sija-commit kwa CDM either. Naona CDM wanafanya kazi nzuri ku-challenge CCM. However I still have unanswered questions about them. Lakini am not worried for now because; their not the rulling party wachapishe kadi wasichapishe they will not gain or lose anything. CCM wako used na ubabaishaji. Tumeuona wazi kwenye kura za maoni so hiyo haiitaji mifano zaidi. Chama kina watu wale wale waliotuletea matatizo alafu wanakuja na lugha tofauti kweli kwa mtu mwenye akili zake atawaamini vipi? Chochote CCM kinachofanya sasa hivi lazima kitaonekana ni kibaya kutokana na reputation waliojiwekea, na wala wasilaumu. Huwezi kutumia watu wale wale walioleta tatizo na strategy zile zile kuondoa tatizo.
 
Du;nape noma hawatia hasara cdm,warudisha kadi zaidi ya 500

Mkuu tujitahidi basi kuongea kiswahili fasaha. Samahani km nimekukwaza lkn.
 
Kadi 500 unazishikaje kiganjani? Mbona naona ipo ya Chadema moja, NCCR Mageuzi na nyongine vyama vingine? Kuna taarifa kuwa kadi alizokuwa nazo Singida ndo hizi hizi, anawezje kuprove tofauti?
 
Kwanini ni kadi za chadema tu? hakuna vyama vingine? i think there is wrong somewhere!
 
We Tumaini letu umetokea wapi? Wenzako walishaeleza humu jamvini kuwa kadi hizo zinazoitwa cha CDM zinatengenezwa na CCM baadaye wanazigawa kwa WanaCCM halafu unafanyika usanii wa kurudisha katika mikutano yao.
 
Uanachama ni itikadi ya akilini, sio mavazi au kadi. Kwa udanganyifu uliofanyika siku za nyuma kwa kuwapa watu kanga, vitenge, t-shirt na kofia, kununua shahada za kupigia kura nk, sioni ajabu kupata kadi 500 kutoka Tanzania nzima kwa ajili ya kujionesha kila mahali. Hata kama ni kweli, switching allegiance is not a crime. Ndio maana ya kuchagua!!
 
Back
Top Bottom