Kadhia ya kiwanja cha Mbweni Karume ajibu mapigo

hapo umenena, tatizo na kanisa kukaa karibu na mzee mzima.

Si amedai kwamba analiheshimu na amekuwa analihudumia hilo kanisa au ni unafiki tu? Na ilikuwaje akawa anahudumia kanisa huku akidai halina uhalali kuwepo pale?
 
Mawazo ya kimasikini. Badala ya kusema tuungane pamoja na waanglikana kudai haki yetu tuliyodhulumiwa nyinyi mnasema tukose wote! Matatizo yenu ni kuweka mbele udini kwamba kwa nini wamisheni wapewe haki yao wakati nyie wadini wenzao mnanyimwa. Mnasahau kuwa dhuluma haina dini. Kanisa halikudhulumiwa na serikali bali mtu binafsi. Rais mstahafu mwenyewe amekiri kuwa eneo hilo miaka nenda rudi alikuwapo yeye na waangalikana peke yao. Kama tangu enzi za utawala wa marehemu baba yake eneo hilo lilikubalika kuwa ni la waangalikani itakuwaje leo amkubalie mwanae amege? Au mnataka kutuambia kuwa alijua kuwa kwa sababu ni wamisheni wanaodhulumiwa hakuna atakaye-sympathise nao. Hata wale ambao nao wamedhulumiwa! Kwa mtaji huo, haki itapatikana kweli?

Amandla.......


Kulikuwa na Azimiao la Arusha Tanganyika na Zanzibar kulikuwa na utaifishaji na hilo kanisa lilikuwa mali ya wazungu sasa hawa wanao sema mali yao wameitolea wapi ?
 
Kulikuwa na Azimiao la Arusha Tanganyika na Zanzibar kulikuwa na utaifishaji na hilo kanisa lilikuwa mali ya wazungu sasa hawa wanao sema mali yao wameitolea wapi ?

Unajua kweli unachoongea? Kanisa lilikuwa mali ya wazungu! Sasa ikiwa rais mstaafu mwenyewe amekiri kuwa hao waanglikana walikuwepo hapo miaka nenda rudi, wewe nani kuuliza mali yao walitolea wapi?

Amandla.......
 
Mawazo ya kimasikini. Badala ya kusema tuungane pamoja na waanglikana kudai haki yetu tuliyodhulumiwa nyinyi mnasema tukose wote! Matatizo yenu ni kuweka mbele udini kwamba kwa nini wamisheni wapewe haki yao wakati nyie wadini wenzao mnanyimwa.. Rais mstahafu mwenyewe amekiri kuwa eneo hilo miaka nenda rudi alikuwapo yeye na waangalikana peke yao. Kama tangu enzi za utawala wa marehemu baba yake eneo hilo lilikubalika kuwa ni la waangalikani itakuwaje leo?

Amandla.......

Fundi Mchundo naona wewe ndiye unaeleta udini na fikra za umaskini bila hata kujua hilo eneo husika ni la nani na nani hapo. Mbona siku zote walinyamaza mpaka yalipowafika wao na hiyo ardhi inaeleweka wenyewe ni akina nani? Ingekuwa wamesimama kwa misingi ya dini yao mbona hawakusema kitu kabla?

Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu eh!
 
Hili kanisa si ndio lile lilikuwa na matatizo ya mkuu wake mmoja (mwanamme) kuolewa na mwanamme mwenzie kule Merekani na sokomoko likafika mpaka huku?

Naomba na hawa viongozi wa hili kanisa huko Unguja watazamwe, wasiwe na kale kamchezo kabaya, kwani wanashangaza. Jee, kama wao wamiliki halali kabla ya Fatma kwa nini wasitowe na wao hati zao, si zingeonesha tu kama ni chao au cha Fatma?

Pili, haya makanisa Tanzania nzima, yatazamwe upya kwani yana ardhi kubwa sana kupita kiasi, jee hiyo ardhi yote ni ya nini lwa kanisa?

Baada ya Serikali, kanisa ndio lenye ardhi kubwa Tanzania. Kwa nini?
Soma tena jina la kanisa. Ni Anglican, as in Anglia, England.
 
..hapa kuna maoni ya wanachama wa forum ya wazenj: mzalendo.net.

..kusema ukweli kwa hawa wenzetu udini umeshika kasi kwelikweli.


mzalendo.net said:
mie nashangaa hawa makafiri wanasema kanisa lao na ardhi yao
hili kanisa ni mali ya zanzibar sio ya watanganyika wala hilo kanisa hawakujenga makafiri wa tanganyika
ni makanisa yakiyojengwa na wakoloni sasa vipi iwe mli yao?
shein na makamo wa pili wote ni tanganyika. tutalinga mapinduzi na tutadumisha muungano
kuwepo wakiristo zanzibar ni muungano na mapinduzi.
karume kafanya makosa lakini kuiba ardhi lakini na hawa makafiri sio kanisa lao wala sio ardhi yao
shein na balozi idi hawa makafiri warudi makwao.
amani karume kazi bado, unafikiria ccm walipenda ulivuounganisha serikali ya cuf na ccm.
basi kama shein na balozi idi munaipenda zanzibar na wazanzibar basi mutoe kauli ya kula ya maoni je wazanzibar munataka muungano?
hapo ndio nitawajua kuwa nyie kweli ni wazanzibar


mzalendo.net said:
tukae tukijua wanaanza kuja mwilini hao makafiri maana washaanza kutaka kufanya maandamano,jeshi la polisi wakiandamana makafiri risasi tu kwenda mbele kama kawaida yenu utavunja miguu kisha tuone kama wataweza kwenda kanisani hao.
Pia nimechangia sijafuja


mzalendo.net said:
salamu wazanzibar, kwa kweli mkuki kwa nguruwe kwa binaadamu unauma, hawa watu wa kanisa watapewa eneo lao je sisi tulio tulio chukuliwa maeneo zetu na kanisa je tutarejeshewa?> nauliza wana mzalendo na pia nitahitaji msada wenu kimawazo kuhusu hili, kiufupi ni hivi kanisa la MINARA MIWILI , hii ni sehemu ya wazee wetu yaani babu zangu ilikuwa sehemu yetu kabdla ya kujengwa kanisa hilo wakati wa utawala wa mfalme , wakaja waumini wa kidhungu kwa mfalime wakamuomba kuwa wanataka kujenga skuli ya kusomechea na wakataka wapate eneo la mjini kwa wakati ule oneo ambalo lilikuwa halijajengwa ni hilo hapo minara milwili bahani ardhi ya sarhani suleiman , maarufu arthi ya kina suleiman majisu, mfalme akawaomba wawakonishe ardhi hio kwa mika 100 kwa kisingizio kuwa patajengwa skuli mzee wetu akakubali akatia mkataba nao lakini cha kushangaza wakaanza kujenga kanisa babu yangu akakataa akawaambia mkataba sio kujenga kanisa ni skuli , wakatoliki wakakataa wakamjibu kuwa mfalme anajuwa na katoa ruhusa kwa hivyo wewe nenda kwa mfalme kwa sababu yeye anajua babu yangu baada ya kudhungushwa akazirejesha pesa zote walizotia mkataba nao na watu wa kanisa wakazichukuwa na wakasema utakapokuwa uko tayani tutakupa pesa zako basi wakalichukuwa eneo hilo babu yetu akadhulumiwa mpaka akaondoka duniani na watoto wake na sasa sisi ni virembwe tu na wajuukuu ,na huo mkataba pia sasa muda wake pia umekwisha tangu kujengwa kanisa sasa zaidi ya miaka labda sasa miaka 150 na mkataba ulikuwa ni miaka mia 100 tena sio kujenga kanisa , warka tunao na kopi ya ya mkataba tunayo na baada ya mapinduzi tuliogopa kudai kwa sababuserikali ilikuwa ya maguvu na kiongozi wao yaani nyerere pia mkatoliki , na kisingizio kuwa arhi ni serikali , lakini hivi karibuni haloo yetu aliwafuata watu wakanisa wakakubali kuwa wanajua kuwa hii ni sehemu yetu na kopi ya mkataba wanao wakasema kama munataka pesa zilizo achwa na babu yenu zipo mambo yakeishia hapo je sisi wajukuu vipi tutaweza kudai haki yetu naomba jibu , na serikali ya zanzibar wakifuatilia nani mmiliki wa ardhi hio wanajua kuwa si ya kanisa je sisi tufanye nini je tuendelee na msimamo wa babu yetu kumuachilia m,mungu kwa alivyo danganywa au tnaweza kuwachitaka na muda wa mkataba sasa umeshapita mika kadha je tufanye nini.


mzalendo.net said:
hawa wote ni wageni wacha wayaone ss tutahakikisha sio arizi tu hata makanisa yao tutageuza kuwa vyuo vya quran

Wamemuanza KARUME (mbweni) kisha wanasema wataenda kule kwa Ali Hassan (kwa parisi) kwani amejenga karibu na makaburi ya jimkana,,,hehehehe hata badooooo waneshindwa kuchuku nchi ki katiba sasa wanachukuwa nchi ki ardhi,,,nci ilikuwa chini ya waingereza(wakristo) sasa watanganyika wakristo wanadai ardhi yao waliorithi toka kwa mababu zao waingereza,,,,,,,,,,,,


mzalendo.net said:
Tunatakiwa tupendane Wazanzibari lakini kwa hili naona siwezi kujizuia.Leo Zanzibar Wakristo na Makanisa yamekua mengi kuliko hao wenyeji. Kwa Awamu yake.
Halbadiri ya Mbayana inacheza.Acha Allah (SW) Awatie adabu. Kwani bakora ya Allah ni kali na hua haina haraka. Na Amtizame Komandoo wa Udongo alivokosa macho siku zake hazijafika.
Amani Karume kweli anastahili sifa zakukubali Muafaka wa Amani na Umoja Zanzibar .Lakini asingefanya hivo isipokua anataka aachiwe yale majumba ya Serikali aliojikumbia yeye na familia yake.
Kule Pemba kulikua na Jengo moja pale Bizanje ya Chake Chake. Amelichukua yeye na familia yake . Uwanja wa Kibirinzi haya twende Kumba kumba. Ameunyakua .
hakuna Serikali hata moja iliokua imepora mali na Mashamba ya Wazanzibari kama yake yeye. Ilikua Huruuu kinyanganyiro Zanzibar ilikua ikipapatuliwa kama ndizi changa.
Wallahi Visiwa hivi kama ingekua ni Mtu basi angekua hata ile ngozi hana tena kwakupa-patuliwa ni CCM SMZ na Mabwana zao CCM Tanganyika.
Lakini pia nayeye ana laana kubwa alioianya wakati wa uchagizi wa 2000-2005. Yeye ndie aliekua Akichukua Vipusa wa Kikristo, malaya, wauza gongo, majambzi waliokua wameua huko kwao Nyasa land.
Wanyasa wote walioshinda huko bara aliwabeba kuwaleta Zanzibar. Ili apate kutuliwa kura na CCM abakie Uraisi. Badala yake alishindwa vibaya sana na hasira zake ndio aliagiza JWT lije liwauwe watu Walioandamana kudai haki zao.
.Aliwaulisha Wazanzibari wasiokua na hatiayoyote na wengine Kugaragarishwa na KMKM pale michenzani huku wakiwapiga Magongo vijana hao kama Nyoka.
Leo hii Makanisa yake alioyakaribisha hayo yameanza kulumbana na yeye mwenyewe. Amba Yeye ndie anayeyashughulikia Makanisa na makuburi. kwahivo Hekosa Kibwetere.
Sie yetu macho tu Ishaallah kila Mnafikk atafadhaika na kukashifika hapa hapa Duniani. Amen
Mola Ibariki Zanzibar na Wazanzibari.


mzalendo.net said:
hili kanisa si mali ya makafiri wa tanganyika.
haya makanisa ni mali ya wazungu wakoloni ndio waliyoyaacha hapo sasa hao akia karume na ali hasan na salimin ndio waliowapa watanganyika eti yao.
karume umesema kweli makanisa wazungu waliyawacha yakawa hayana watu hilo ni kweli nyie mukaenda kuleta watanganyika makafiri ili waje wafanye ukafiri na kutia nchi yetu unajisi
sasa munagombana nyie kwa nyie. wewe karume tunaweza kukupa haki kidogo lakini haya mafisi yako yamekugeukia
sasa uwambie kweli kama nyie ndio muliowaleta hapa. na pia hawa muliwaita wazanzibar na sie wazanzibar kutufanya hatuna kwetu
sasa wambie watu wako kweli kama hapa hamna chenu sio makanisa wala ardhi na wazanzibar hatuwataki makafiri hawa uwambie warudi makwao.
nugu wazanzibar ndugu waisla tukaeni macho yanaanza sasa na yatakuwa kweli kuna siku nasie tutavunjia nyumba na misikiti kama hatuamini basi tutaona
makafiri warudi kwao na makanisa yaekwe kumbukumbu za wakoloni watanganyika hawana chao hapa ccm iwarejeshe makafiri wao
 
Fundi Mchundo naona wewe ndiye unaeleta udini na fikra za umaskini bila hata kujua hilo eneo husika ni la nani na nani hapo. Mbona siku zote walinyamaza mpaka yalipowafika wao na hiyo ardhi inaeleweka wenyewe ni akina nani? Ingekuwa wamesimama kwa misingi ya dini yao mbona hawakusema kitu kabla?

Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu eh!

Kwa nini tuandikie mate....? Msikilize Mstaafu Karume mwenyewe:

Mstaafu Karume huku akiwa amekunja uso wake na kutafuna tafuna ulimi wakena kuongeza kwamba.
"Tangu enzi za baba yangu pamoja na mimi nimekuwa na uhusiano mzuri na kanisa hilo…..nimehamia hapa katika mwaka 1968 hakuna mtu yoyote katika eneo hili isipokuwa kanisa" alisema Karume na kuwageukia waandishi wa habari.

Sasa wewe kweli unajua umiliki wa eneo hilo zaidi ya Karume ambae anasema alipohamia eneo hilo mwaka 1968 hapakukua na mtu isipokuwa "kanisa" peke yake. Hii si mara ya kwanza kanisa hilo kudhulumiwa. Sehemu nyingi walizomiliki kuzunguka Kanisa lao Soko Mhogo walinyang'anywa, hawakupiga kelele maana ni serikali iliyotaifisha. Sasa leo wanadhulumiwa na mtu baki mnataka wanyamaze? Hapa wao hawakusimamia dini, wamesimamia haki ya mmiliki yeyote wa eneo ambae anaporwa na aliyemzidi nguvu. Hata hivyo bila shaka walijua kuwa ndiyo imeishatoka maana watu kama nyinyi badala ya kuangalia haki mtafurahia KANISA kuonewa. Unaposema mkuki kwa nguruwe...tuambie wapi kanisa lilimdhulumu mtu nafasi yake? Ubavu huo wangeutoa wapi katika nchi ambayo asilimia zaidi ya 95 ni waislamu! Mara moja moja acheni udini, angalieni haki. Utakuja kukosa wa kukutetea yatakapokukuta.

Amandla........
 
Jamani kanisa kujengwa zenji ya nini? Kwani zenji kuna wakristo? Si waje huku kwetu bara kuna wakristo kibao ambao wanahitaji makanisa ya kisasa hasa vijijini kwani utakuta kanisa dogo la udongo unaotaka kubomoka kwa uchakavu! Mimi nashangaa kanisa kungangania nchi ya kiislamu wakati nchi yetu ya kikristo tanganyika bado inahitaji makanisa tena zaidi kwa wasio na dini kama vile wamasai, baebeig, na wengine!
 
Hili kanisa si ndio lile lilikuwa na matatizo ya mkuu wake mmoja (mwanamme) kuolewa na mwanamme mwenzie kule Merekani na sokomoko likafika mpaka huku?

Naomba na hawa viongozi wa hili kanisa huko Unguja watazamwe, wasiwe na kale kamchezo kabaya, kwani wanashangaza. Jee, kama wao wamiliki halali kabla ya Fatma kwa nini wasitowe na wao hati zao, si zingeonesha tu kama ni chao au cha Fatma?

Pili, haya makanisa Tanzania nzima, yatazamwe upya kwani yana ardhi kubwa sana kupita kiasi, jee hiyo ardhi yote ni ya nini lwa kanisa?

Baada ya Serikali, kanisa ndio lenye ardhi kubwa Tanzania. Kwa nini?

Kwa mujibu wa imani yetu ya kikristo haishii kwenye mambo ya kiroho tu(kwenda mbinguni) bali pia maendeleo sahihi na halali ya hapa duniani, hivyo tunahitaji ardhi ya halali ya kutosha kwa ajili ya shule/vyuo, hospitali na nyumba za kulelea watu/watoto walio katika mazingira hatarishi/magumu. Maana tunafundishwa kuwa tusipompenda jirani tunayemuona, Mungu wa Mbinguni tutampenda vipi!?
 
mimi najiuliza kwa quality ya discussion hizi ninazoziona hapa kweli watanzania hata washirikishwe namna gani tutaweza kweli kupata katiba mpya inayoangalia mtakabali wa taifa? mbona mmekua cheap kiasi hiki ndugu zangu? mme baki kwenye udogo udogo wa mawazo kwa faida ya matabaka? hivi kweli kabisa kuna watu wanaokubali kwamba ardhi na mali asili zote ni za viongozi wetu ni halali yao wao na watoto wao hata kama watoto hao tayari wameshajiweza? udini umewatawaleni kabisa kuna watu mpaka leo wanaoweza kusema zanzibar haihitaji hiki na kile, je ni kweli bara tunawahitaji wazanzibari? mnataka tufike huko? kweli watu wanaochaguliwa na watu laki 400 wapewe mamlaka juu ya wale milioni 45 kwa sababu tu ya kuwabakiza kwenye mambo kama haya? karume apewe hiyo ardhi na wazanzibari wote wakiwemo kina shein na Hamad na hao wakina karume waachie ardhi ya bara. Nyie great thinkers gani mnaoacha kushangaa na kumuuuliza karume anaingiaje hapo hata baada ya kumaliza kuchukua ardhi yote ya zanzibar wakati wazanzibari wakiwa katika umaskini mkubwa wa kutopea. Angalia hali ya wanachama wa CUF ama CCM wasio viongozi, hata kama wewe si mwanachama je unaona ni sawa kweli?
 
A dispute in which Fatma, daughter of the immediate former Zanzibar President Amani Abeid Karume, is contesting ownership of a piece of land on the main island, Unguja, took a dramatic turn yesterday, when the father visited the site.
Fatma commissioned construction works on the plot recently, but it has transpired that she doesn't have official building permits. The Church, on its part, claims that it is the long-time, rightful owner of the piece of land.
A high-level meeting was held yesterday to resolve the dispute but it didn't yield the anticipated outcome.
Those in attendance included Second Vice President Ambassador Seif Ali Iddi, leaders from Zanzibar Municipal Council, land department and a delegation of five people from the Zanzibar Diocese of Anglican church led by retired bishop John Ramadhani.
Information that leaked from the tripartite meeting stated that officials from Zanzibar urban authorities found themselves in a tough time after they were required to explain whether or not they issued building permits on the disputed plot.
"As far as we are concerned we have not issued any building permit and this matter is strange to us," an official was heard as saying while quoting officials from Zanzibar urban municipality.
Secretary of the Zanzibar Diocese of Anglican Nuhu Salanya confirmed that the meeting was held, in the wake of a police ban on a planned demonstration by Church worshippers to protest against what they described as an invasion of their property. Salanya, however, declined to disclose what was discussed at the meeting.
Recently, Zanzibar's Minister for Lands Ali Juma Shamhuna nullified 20 title deeds of various government officials who owned plots in Mombasa area in Zanzibar urban, including the plot that was owned by CCM Deputy Secretary General Saleh Ramadhan Feruz.

Bado tu mtamtetea? Watakosaje Building Permit kama makaratasi yao yote yamekaa vizuri?

Amandla....
 
Karume ametia aibu Zanzibar

picture-11.jpg

Na Jabir Idrissa - Imechapwa 05 January 2011


Kalamu ya Jabir
NILIPOSIKIA Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi anaapa kwamba serikali mpya haitakubali ufisadi wa ardhi vyovyote vile, nilijua safari ngumu imeanza.

Ni safari ngumu na sina shaka italazimu Balozi Seif mwenyewe, Rais aliyemteua, Dk. Ali Mohamed Shein na waziri anayehusika na usimamizi wa raslimali ya ardhi, Ali Juma Shamhuna, wafunge mikanda.

Bali itakuwa safari ngumu kwa jumla maana ni lazima baraza zima la mawaziri liamue kwani watalaumiwa na wale watakaoguswa na “operesheni futa ufisadi wa ardhi.”

Niliposikia baadaye kuwa baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa kusalimisha hati za kumiliki ardhi kifisadi, nikajua kweli hakuna kisichowezekana.

Kufikia leo, taarifa zisizokanushika zinasema serikali imeshafuta zaidi ya hati 20 za kumiliki viwanja kwenye maeneo ambayo kwa asili yake ni ya wazi – ambazo ilizitoa huko nyuma.

Raslimali ya ardhi imekuwa matatizoni sana katika kipindi cha miaka 20 sasa kote Unguja na Pemba. Kumekuwa na malalamiko mengi ya makundi na watu binafsi kudai wameporwa ardhi.

Lakini katika kipindi cha miaka 10 kilichoishia Oktoba mwaka jana, malalamiko hayo yalizidi. Uporaji ulisikika kila mahali na viongozi wa juu wakitajwa kuhusika.

Tukio la wazi likahusisha vigogo waliovamia shamba la mzee Abdalla Shariff wa Shakani, nje ya mjini Zanzibar. Na licha ya mzee huyo kushinda kesi hadi mahakama ya rufani, hajarudishiwa ardhi aliyoporwa.

Mawaziri, makatibu wakuu na wabunge walihusishwa. Ni wao walifanikiwa kutumia madaraka kushawishi serikali ikatae haki na mpaka leo mwenye haki, Mzee Shariff, akifungwa mdomo.

Mara kadhaa polisi wa kutuliza ghasia walipelekwa kukaza hukumu lakini walirudi bila ya kutekeleza walichotakiwa; na sababu ikawa, “Pale kuna watu wamebeba mawe na bakora wametuzuia.”

Aibu ilioje, polisi kuzuiwa kufanya kazi halali na wanawake na watoto wadogo waliobeba bakora!

Tukio lililotokea wiki iliyopita linathibitisha ukubwa wa tatizo la ufisadi wa ardhi Zanzibar. Kule kuhusisha viongozi wa ngazi za juu wa utawala kumeshtua.

Katikati ya mgogoro wa ardhi ya Kanisa la Anglikana unaohusisha eneo la asili la kanisa hilo kijijini Mbweni Mfuuni, nje ya mji, ni familia ya Mzee Abeid Amani Karume, kiongozi mtukuka aliyeuawa kwa risasi 7 Aprili 1972.

Mkuu wa familia sasa ni Amani Abeid Karume, rais mstaafu wa Zanzibar aliyeongoza kwa miaka kumi serikali ya awamu ya sita – 2000/2010.

Bila ya kutarajia, mstaafu Karume amembeba mwanawe wa kike, Fatma Amani Abeid Karume, akisema anamiliki kihalali kiwanja kilichopo eneo la Kanisa, Mbweni Mfuuni.

Anasema Fatma anazo nyaraka halali. Kupitia picha za televisheni nikashuhudia Karume akiinua nyaraka na kuzionyesha kwa waandishi “mahsusi” walioitwa na familia hiyo ili kupaisha sauti yao.

Sikuwepo. Kwa bahati mbaya pia, waandishi ninaowaamini kikazi hawakuitwa. Sijapata simu ya Fatma, wala ya rais mstaafu Karume.

Ningeuliza, “Bibi Fatma umepata lini hati ya kumiliki kiwanja hapa?” Ningetaka kunukuu kumbukumbu za hati hiyo ikiwemo tarehe iliyotolewa, nani aliidhinisha na ilitolewa kwa maombi gani?

Vyanzo vyangu vinanieleza kumbe Fatma amepata hati mwaka 2009 – mwaka juzi. Hati ilitolewa baada ya shinikizo nyingi na maofisa wa Idara ya Ardhi na Usajili walikimbizana kila mmoja akiogopa kujiingiza. Wanasema ulikuwa “mtego mbaya.”

Ni kama vile siku walipotakiwa kupima eneo la Kibweni, mita chache kutoka nyumba ya mkereketwa mkuu wa CCM, mfanyabiashara Mohamed Raza Dharamsi na pembeni mwa Ikulu ndogo ya Kibweni. Walitakiwa kupima kwa nguvu.

Lakini kiwanja kinachobishaniwa Mbweni ni cha Kanisa la Anglikana, lenye eneo kubwa tangu karne ya 18. Tukumbuke Waanglikana ndio wakristo wa kwanza kuhamia Zanzibar. Walinunua maeneo Unguja na Pemba; hili la Mbweni ni eneo mojawapo.

Kwa sababu za kibinafsi zaidi kuliko haki, hawajapewa hatimiliki licha ya kuhangaikia kwa muda mrefu hasa baada ya kuona hatari ya wajanja kutwaa maeneo yao.

Mpaka leo wanalalamika hawajalipwa fidia kwa serikali kuchukua eneo lao Madungu, Chake Chake, Pemba palipojengwa Posta wala yalipo Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba - Wete.

Hawajatimiziwa ahadi ya wizara inayohusika na raslimali ya ardhi kuwa itatoa hati hizo. Wizara ilishindwa kutoa hati mpaka uporaji umefanyika.

Anaposimama baba hadharani kutetea mwana eti “anamiliki kihalali kiwanja” katika eneo la Kanisa, wakati eneo la mzee Karume – ambalo lenyewe lilitokana na kumegwa eneo la Kanisa – limo ndani ya ukuta uliojengwa kwa fedha nyingi, inasikitisha.

Ukweli ni kwamba kiwanja anachodai Fatma ni chake kipo nje ya ukuta wa eneo kubwa la familia yao. Wala Kanisa halina mgogoro wowote na anayeitwa mwekezaji wa hoteli pembeni na karibu na ufukwe.

Kama Fatma hana nyaraka za kuuziwa kiwanja na Kanisa, aseme amepataje uhalali huo. Isije ikawa alipata katika ule mtindo wa chukua chako mapema ulioshamiri kipindi cha miaka 20 nyuma.

Wakubwa na rafiki zao “walichukua, wakaweka waa” kwa kila walichokitaka, siyo utawala tu wakati wa uchaguzi. Nani mwenye ubavu wa kulalamika wakati ule? Yalimkuta kijana wa Kipilipilini Chwaka alipolalamika kuporwa ardhi ya kurithi na kutumiwa kujengea kituo cha petroli cha Gapco, alionyeshwa moto.

Amefunguliwa kesi ya jinai na jamhuri, na mwandishi aliyemsaidia kuchapisha malalamiko yake, Mwinyi Sadallah, akajumuishwa. Eti wachochezi. Hatimaye mpaka leo ukiingia mwaka wa tatu ushahidi tu haujamalizika.

Haya ni matukio yanayokera maana yanadhoofisha utawala bora katika nchi yenye watu wastaarabu.

Sasa hii inayomhusu rais mstaafu Karume ni kashfa nzito. Inaashiria mwanzo wa kufumuka mambo mengi kwa sababu ipo kesi mahakamani inamhusu mjomba wa Fatma, Mansour Yusuf Himid.

Mansour alikuwa waziri kwa miaka kumi ya utawala wa Amani Karume. Sasa ni Waziri wa Kilimo na Maliasili. Ni mmoja wa walioshindwa kesi na Mzee Shariff kule Shakani.

Anatajwa katika kesi nyingine iliyopo Mahakama ya Ardhi akidaiwa kutwaa ardhi visivyo. Uamuzi wa kesi hii ukitolewa, ukweli utajulikana.

Mtoto wa rais mstaafu Karume anatajwa kumiliki kwa hila eneo kubwa la ardhi kijijini Muyuni, Wilaya ya Kusini Unguja, ambako wenyeji wakitumia kwa shughuli za kilimo.

Walilalamika lakini walinyamazishwa kwa mbinu za kidola. Wamenyamaza sawa, lakini hawajaridhika maana wangali wanadai ni haki yao, hawakushirikishwa na wamezuiwa kutumia eneo la asili kwa shughuli zao.

Nahisi itakuwa shida. Mkoa wa Kusini na Kaskazini Unguja kuna malalamiko kwa familia hii kuhusu ardhi. Kuna malalamiko kisiwani Pemba kuhusu hayohayo. Mtandao wa WikiLeaks umeyaona. Mimi si mtabiri, lakini naona mengi yatafumuka.

Gazeti toleo lenye makala hii
0
Average:
 
Sa
Karume mbona hataki kusema ni lini binti yake alianza kumiliki hicho kiwanja...................ni wazi kuwa ilikuwa baada ya 1968...........na huu ni ushahidi wa matumizi mabaya wa madaraka...................

sakata lilifika wapi. .Rutashubanyuma mbona mrejesho hakuna..?
 
Hivi inakuwaje mtu wa nje ya nchi, na wakati mwingine si mkaazi, akamilikishwa ardhi ya Tanzania bara.
Mbona Zanzibar mtu ni vigumu kupata ardhi.
Muungano si kigezo.
 
Kiukweli hili limenichefua sana Waanglikana wasipopatiwa haki yao nitabakia kuwa mtanganyika tuu
 
Kiukweli hili limenichefua sana Waanglikana wasipopatiwa haki yao nitabakia kuwa mtanganyika tuu
Hao waanglikana wanafanya nini? Wametulia tu, Wandishi walioandika sakata hili waliishia wapi?

Wapi Mwinyi Sadalla: ZANZIBAR MPYA - FUNGUO ZA KHERI

Wapi Jabir Idrissa : Karume ametia aibu Zanzibar | Gazeti la MwanaHalisi

Wapi Rushubanyama: Rais Karume aepushwe na mgogoro wa kiwanja

Wapi; Kizibao: Kadhia ya kiwanja cha Mbweni Karume ajibu mapigo


Kadhia ya kiwanja cha Mbweni Karume ajibu mapigo
 
ninqvyojua mimi na kwa kuwa fatma ni mwanaharakati mzuri ktika sheria ss ili aonekane wa hovyo katka jamii hy issues itatiwa stover tuuu moto uwake lakini dada astuke mapema amalizane na hao wauumini ni small case yy km yy baba amweke kando ya hilo.mzee amani
 
Back
Top Bottom