Kadhia ya kiwanja cha Mbweni Karume ajibu mapigo


Karume: Kanisa halina haki umiliki wa kiwanja


Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Zanzibar; Tarehe: 1st January 2011 @ 23:55

MGOGORO wa kiwanja kati ya Kanisa la Anglikana Zanzibar na Fatma Karume, binti wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, umechukua sura mpya baada ya Rais huyo mstaafu kudai, kwamba kiwanja hicho ni mali halali ya binti yake.

Mbali ya kueleza hayo, amevilalamikia pia vyombo vya habari, ikiwamo Televisheni ya Taifa Zanzibar (TVZ) kwa upotoshaji, huku akiitaka kuomba radhi na kutishia kuyashitaki baadhi ya magazeti.

Karume aliyemaliza miaka 10 ya urais wa Zanzibar Oktoba mwaka huu, alisema hayo jana
wakati wa mkutano na wanahabari uliofanyika nyumbani kwake Mbweni, mjini hapa.

Katika mkutano huo ambao Karume alitumia muda mwingi kuonesha jinsi Kanisa linavyolazimisha kutaka kutambuliwa kuwa wamiliki wa eneo hilo, alisema:

"Zimekuwapo habari za kupotosha, bahati mbaya waandishi wa habari hawajatupa nafasi ya kujibu suala hilo."

Akiwa na binti yake, Fatma, ambaye yuko katika mgogoro wa kiwanja na Kanisa hilo, Karume alisema Kanisa halina haki na kiwanja hicho.

"Nimekuwa nikilihudumia Kanisa, hata lilipokuwa limetelekezwa miaka iliyopita. Kanisa la Anglikana limekuwa jirani yetu tangu mwaka 1968, na mimi binafsi naliheshimu.

Fatma anamiliki kisheria kiwanja hiki na anaheshimu eneo la makaburi lililopo jirani," alisisitiza Karume aliyewashutumu viongozi wa Kanisa hilo kwa kutoheshimu maadili.

Akifafanua zaidi kwa kutoa ushahidi wa kihistoria kuhusu umiliki wa kiwanja hicho tangu mwaka 1932, Karume alisema viongozi wa Kanisa na waumini wake, walifanya kosa kuvamia kiwanja kufanya maombi kabla ya kuharibu baadhi ya vifaa vya ujenzi vilivyokuwa katika eneo hilo Katika mkutano huo na wanahabari, Fatma ambaye ni mwanasheria kitaaluma, alikuwa miongoni mwa waliohudhuria, kama ilivyokuwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar, Ali Mwinyikai na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdallah Mwinyi.

Karume alilazimika kuzungumzia mgogoro huo, baada ya jana baadhi ya vyombo vya habari kuripoti juu ya kundi la waumini wa Kanisa hilo, kuvamia eneo la kiwanja hicho wakidai ni chao na kung'oa vigingi vilivyokuwa vimewekwa katika eneo la ujenzi ili kuonesha hasira zao.

"Tunang'oa na kuharibu vigingi hivi ili kuzuia ujenzi katika kiwanja hiki, kinamilikiwa na Kanisa na tumekuwa tunakimiliki tangu enzi za Wakoloni miaka ya 1920," walisikika wakisema baadhi ya waumini hao mara baada ya kufanya maombi ya dakika 10 yaliyoongozwa na Padri Mathew Mhagama.

Mhagama alipaza sauti akishutumu uvamizi wa kiwanja hicho kinyume cha sheria na uharibifu uliofanywa katika eneo la makaburi wakati wa ujenzi.

"Tumekuwa tukiomba hatimiliki tangu mwaka 1980 kama mbadala wa karatasi tulizokuwa nazo tangu miaka ya 1930," alisisitiza.

Karibu waumini 50 walikusanyika katika Kanisa lao eneo la Mbweni kabla ya kuandamana kwenda eneo hilo la kiwanja lenye ukubwa wa ekari 2.5 ufukweni mwa bahari ya Hindi ambapo walifanya maombi kushutumu kuchukuliwa kwa kiwanja chao ambacho kiko karibu na makazi ya Rais huyo mstaafu
 
MGOGORO wa kiwanja kati ya Kanisa la Anglikana Zanzibar na Fatma Karume, binti wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, umechukua sura mpya baada ya Rais huyo mstaafu kudai, kwamba kiwanja hicho ni mali halali ya binti yake.

Mbali ya kueleza hayo, amevilalamikia pia vyombo vya habari, ikiwamo Televisheni ya Taifa Zanzibar (TVZ) kwa upotoshaji, huku akiitaka kuomba radhi na kutishia kuyashitaki baadhi ya magazeti.

Karume aliyemaliza miaka 10 ya urais wa Zanzibar Oktoba mwaka huu, alisema hayo jana
wakati wa mkutano na wanahabari uliofanyika nyumbani kwake Mbweni, mjini hapa.

Nionavyo huu ni ufisadi mkubwa ambao Karume aliufanya dhidi ya Kanisa kule Mbweni Zanzibar.....................yawaje binti yake amilikishwe kiwanja tajwa wakati wa utawala wa baba yake?

Historia ya kanisa la kianglikani Zanzibar ipo wazi kabisa hatuhitaji Raisi Mstaafu Karume atupotoshe hapo......................Akaea mbali na makaburi ya watu...................visingizio vya kulihudumia kanisa huu ni mwendelezo wa hoija za kifisadi tu ya kuwa tayari nilikwisha kuwanunua hao...............................How despicable for a retired leader to engage himself in such shameful acts...................
 
Hili kanisa si ndio lile lilikuwa na matatizo ya mkuu wake mmoja (mwanamme) kuolewa na mwanamme mwenzie kule Merekani na sokomoko likafika mpaka huku?

Naomba na hawa viongozi wa hili kanisa huko Unguja watazamwe, wasiwe na kale kamchezo kabaya, kwani wanashangaza. Jee, kama wao wamiliki halali kabla ya Fatma kwa nini wasitowe na wao hati zao, si zingeonesha tu kama ni chao au cha Fatma?

Pili, haya makanisa Tanzania nzima, yatazamwe upya kwani yana ardhi kubwa sana kupita kiasi, jee hiyo ardhi yote ni ya nini lwa kanisa?

Baada ya Serikali, kanisa ndio lenye ardhi kubwa Tanzania. Kwa nini?
 
Kwa nini huyo binti anajenga juu ya makaburi? Kweli ameshindwa kujenga sehemu nyingine ilihali lazima ajenge ubavuni kwa babaye!
 
Mimi sipo .............ngoma nzito.....km Kanisa lenyewe linaongozwa na Kasisi Msaidizi wa Kanisa la Angalikan Zanzibar, Mathew Wilfred Mhagama ni lile lisilokuwa na Askofu halafu Jaji mkuu A. Ramadhani Msaafu akamkataa mpya basi kuna mambo huko. Maana Baba km Rais mstaafu ana haki ya kukitetea kiwanja kwani ndiye mwenye mwana mila za kwetu hata mtoto wa kike unaweza kumrithisha kiwanja sembuse nyumba
 

Karume distances his family from land plot row


From SUNDAY NEWS reporter in Zanzibar, 1st January 2011 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 385

RETIRED President Amani Karume has distanced his family from land row with a church, complaining against the media for bias reporting on the matter.

Mr Karume asked the Zanzibar state television (TVZ) to apologize and threatened to take legal action against some newspapers.

''There has been biased reporting. Unfortunately, we were not given the right to reply by journalists,'' Karume said at a press conference he convened on Saturday at his residence in Mbweni area.

The principal Secretary (PS), Ministry of Information, Culture, Tourism, and Sports Mr Ali Mwinyikai, and Urban-West Regional Commissioner Mr Abdallah Mwinyi were present at the conference.

Flanked by his daughter Fatma, who is in the dispute with the Anglican Church over the plot, Karume said that the church had no right over the plot.

''I have been taking care of the church, even at the time when the church was abandoned sometime ago,'' he added.

Unveiling details about the historical ownership of the plot since 1932 to journalists, Karume said that it was wrong for the Church leaders and followers to invade the plot for prayers before destroying some construction materials at the site.

''Anglican Church has been good neighbours since 1968, and I personally respect the church. Fatma legally owns the plot with great respect to the nearby graves,'' Karume emphasized and condemned church leaders for not observing ethics.

A group of members of the Anglican Church last Thursday walked to a plot they claimed to belong to them and pulled out pegs at the building site to express their anger.

''We are pulling out and dismantling these pegs and calling for a stop to any construction on this plot. It belongs to the Church, and we have owned it since colonial days in 1920s,'' said one of the worshipers at the site after a ten-minute prayer led by Father Mathew Mhagama.

Mhagama raised his voice, condemning what he called 'llegal' ownership of the land and partly damaged what was on the grave yard during their presence at the site.

''We have applied for a title deed since 1980s to replace the documents we have since 1930s.''
At least 50 worshipers gathered at their Church at Mbweni area, before marching to the nearly 2.5 acres plot facing the sea.

They prayed there and condemned the possession of the piece of land next to the retired president Mr Amani Abeid Karume's residence.
 
Mr Karume asked the Zanzibar state television (TVZ) to apologize and threatened to take legal action against some newspapers.

Unapoona Raisi mstaafu yupo tayari kwenda mahakamani kutetea ufisadi aliofanya na binti yake ujue nchi hiyo imekwisha..............
 
Anayejenga ktk makaburini mwekezaji wa kidosi na kanisa limemkodisha kwa 600,000 huyo binti yupo jirani,anaonewa tu.kwani ni vibaya kujenga jirani na baba?zbr ni kama moshi tu mambo ya vihamba.
 
''Anglican Church has been good neighbours since 1968, and I personally respect the church. Fatma legally owns the plot with great respect to the nearby graves,'' Karume emphasized and condemned church leaders for not observing ethics.

Karume mbona hataki kusema ni lini binti yake alianza kumiliki hicho kiwanja...................ni wazi kuwa ilikuwa baada ya 1968...........na huu ni ushahidi wa matumizi mabaya wa madaraka...................
 
Hayo makanisa yasingekuwa yanahitajika yasingejengwa maana hakuna ambaye angekuwa anahudhuria ibada.Kanisa Anglikana lilikuwepo Zanzibar hata kabla ya babu wa babu yako! Hapa wanachodai ni eneo lao ambalo walikuwa nalo miaka nenda rudi. Kinachopigiwa kelele hapa ni dhulma inayofanywa na mwenye nacho. Au unataka kutuambia kuwa kwa sababu ni wakristu basi hawana haki
Amandla.....
Ni ubaradhuli tu unawasumbua ! .................. lakini kazi mnayo ! .................. hapa pangu !!!

 
"Makaburi yale mlioyaona kwa muda wa miaka 20 sasa yanatunzwa na familia yetu… ni mimi binafsi na familia yangu yote ndio tunaoyatizama na baadhi ya wakati hupata nafasi ya kutoa pesa kwa ajili ya kulimiwa majani na kufanyiwa usafi katika eneo lote lile la makaburi yaliopo pale"alisema Karume

"Nimeshangazwa sana na hawa viongozi wa dini ni viongozi wa ajabu sana tena wamepotoka kabisa ..kwa sababu wameshindwa kufuata maadili ..naona wanakosa utu na heshima kwa wakubwa zao" alisema Rais Mstaafu Karume huku akiwa amekunja uso wake na kutafuna tafuna ulimi wakena kuongeza kwamba.

Nimeipenda hiyo yenye red, mzeemzima hangover ya madaraka bado haijamtoka???? African leaders.

Nimesoma sana utetezi lakini sidhani kama kitendo cha baba na au mtu kulimia na kutunza eneo la makaburi kinahalalisha kisheria mtoto na au mjukuu kupewa umiliki wa sehemu husika. Kama hito ndio basis ya binti kupewa kiwanja sidhani kama ilikuwa sahihi.
 
ni kawaida kwa viongozi wetu kujilimbikizia mali sasa wameamua kulidhulumu hadi kanisa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Watuambie kwanza eneo la hotel ya sea cliff masaki dar walilipataje?eia nani aliipitisha?mbona watu wengine hawaruhusiwi kujenga uwazi ule mpaka golden tulip kwa mwinyi?
 
Wakirejeshewa ardhi yao Kanisa basi na sisi ambao wazee wetu wamechukuliwa mashamba yao na wanazo hati halali za umiliki tangu enzi ya ukoloni tupewe.

Mawazo ya kimasikini. Badala ya kusema tuungane pamoja na waanglikana kudai haki yetu tuliyodhulumiwa nyinyi mnasema tukose wote! Matatizo yenu ni kuweka mbele udini kwamba kwa nini wamisheni wapewe haki yao wakati nyie wadini wenzao mnanyimwa. Mnasahau kuwa dhuluma haina dini. Kanisa halikudhulumiwa na serikali bali mtu binafsi. Rais mstahafu mwenyewe amekiri kuwa eneo hilo miaka nenda rudi alikuwapo yeye na waangalikana peke yao. Kama tangu enzi za utawala wa marehemu baba yake eneo hilo lilikubalika kuwa ni la waangalikani itakuwaje leo amkubalie mwanae amege? Au mnataka kutuambia kuwa alijua kuwa kwa sababu ni wamisheni wanaodhulumiwa hakuna atakaye-sympathise nao. Hata wale ambao nao wamedhulumiwa! Kwa mtaji huo, haki itapatikana kweli?

Amandla.......
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom