KADA WA CHADEMA ARUSHA AJIUNGA NA CCM: Katibu wa CHAMA AMANI GOLUGWA Hamtambui Kada Huyo

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Posted by Pamela Mollel on October 24, 2012

dscf1991.jpg

Aliyekuwa mwenyekiti mtendaji mkoa wa Arusha kupitia chama cha demokrasia na ma endeleo chadema James Ndarvoi amekiama rasmi chama chake na kujiunga na chama cha mapinduzi(CCM)kwa madai kuwa chama hicho kimegubikwa na chembechembe za ukabila

Hatu hiyo ilikuja hivi karibuni katika kampeni za uchaguzi mdogo zinazoendela katika kata ya daraja mbili Mkoani Arusha ambapo Ndarvoi alitangaza rasmi kujiunga na CCM

Alisema kuwa chama cha demokrasia na maendeleo chadema kinaendeshwa kama taasisi ,huku akidai kuwa chama ni kwaajili ya wanachi na siyo ya mtu kukimiliki au taasisi

"chama cha chadema ni kama taasisi ya watu flani na kinachembechembe za ukabila ndani yake "alisema

Alidai kuwa chama cha CCM kimemtoa mbali huku akisisitiza kuendeleza amani na utulivu ndani ya chama hicho kwa kuwa yeye ni kijana na atashirikiana na wanachi katika kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi

"Wanachama waliopo chadema wahame haraka sana kwasababu wataendelea kutumika katika chama hicho kama daraja la kupitia tu, huku wakiwapendekeza watu wao kugombea nafasi za uongozi "alisema ndarvoi

dscf1465.jpg

Kwa upande wake katibu wa chadema Mkoa wa Arusha Amani Golugwa alikana kumtambua ndarvoi huku akidai kuwa hajawai kuwa mwanachama wao

Golugwa alisema kuwa awali alikuwa amejiunga na CCJ na siyo chadema kama alivyodai kuwa alikuwa mwanachama wao

"Nasema hivi hajawahi kuwa mwanachama wetu na simtambui kama mwanachama wetu, kuna kipindi flani alitaka kujiunga na chadema na siku ya kuchukuwa kadi hakuja kuchukuwa na baadae nilipata taarifa kuwa alijiunga na CCK kipindi hicho"alisema Golugwa

Kwani nini kilimtoa ccm awali kama siyo njaa kali na kukosa msimamo. Huyo hatufai watanzania wazalendo.
 
Kama kweli alikuwa kiongozi wa chadema na ameamua kurudi kwao ni haki yake kikatiba. Hata hivyo, Chadema inapaswa kuwa makini maana siyo kila asemaye Bwana Bwana atauona ufalme wa mbinguni. Anaweza kuwa nyemelezi na pandikizi au ni kweli ameona chadema haimfai. Ni haki yake na jambo la kawaida. Kila la heri rejea kwenu na nenda mwanakwenda.
 
anaona cdm haifai lakini anakwenda wapi kunakofaa ??? CCM!!! chama ambacho m-kiti wake jk anadai kimejaa wala rushwa. chadema mshukuru ametoka sasa na siyo 2015
 
Lazima chadema ifanye hatua za haraka kubadilisha mwenendo wa viongozi wake wa juu hasa mbowe, slaa na zitto kabwe. Hawa wote kila mmoja wao anaongelewa tofauti na raia wa kawaida, Kwa watu makini wasikilize hotuba ya mzee nyimbo aliyoitoa akijiondoa chadema ni maneno mazito sana kuachwa hivi hivi, nachokiona imefika mahali kuna watu ndani ya uongozi wa juu wa chadema washajiona wao ni rais na mbaya zaidi wake zao wamejipa u first lady tayari, hii ni hatari sana.
 
Kama chadema haimfai naye hafai vile vile. Utajuaje kama ameahidiwa cheo hasa ukatibu wa CCM wilayani ambako kumekuwa dampo ya kila garbage?
 
Kabla ya UKOMBOZI wa kweli haiujafika, tutashuhudia mengi kuliko haya.
 
Hivi tangu lini mlisikia Chadema kuna wenyeviti watendaji kama sio uwendawazimu wa huyu Binadamu ni noma, njaa hii mtu anajifanya alikuwa Chadema ili apewe kitu kidogo na Magamba,wajamani kwanza Chadema hakuna Makada Chadema kuna Makamanda,Mwambieni huyo James Ndarvoi atuondolea shombo huku Chadema hakuna mwenyekiti mtendaji.
 
Lazima chadema ifanye hatua za haraka kubadilisha mwenendo wa viongozi wake wa juu hasa mbowe, slaa na zitto kabwe. Hawa wote kila mmoja wao anaongelewa tofauti na raia wa kawaida, Kwa watu makini wasikilize hotuba ya mzee nyimbo aliyoitoa akijiondoa chadema ni maneno mazito sana kuachwa hivi hivi, nachokiona imefika mahali kuna watu ndani ya uongozi wa juu wa chadema washajiona wao ni rais na mbaya zaidi wake zao wamejipa u first lady tayari, hii ni hatari sana.

Kazi kweli kweli,kweli Bongo kuna mizoga kama sio wagonjwa wa akili yaani huyu kajiunga juzi 30/October/2012,Post 13,Rep power 303,Likes received 2,likes given 1 sasa moja kwa moja napata picha huyu ndo kamaliza shle ya kata muda si mrefu.Kajiandae tena mkuu ili uje na issue yenye kueleweka hapo uliandika kwa kiswahili je kama ingekuwa Kiingereza sijui ingekuwaje.
 
Mbona mavazi yake yanaonyesha alikuwa ''gwanda'' au haya ni ya CCK(kama kipo hai) ama alivaa kupiga photo.Huyo Katibu wa CDM mbona anaonyesha kumfahamu sana kwamba hakuchukua kadi, alimtambuaje wakati hakuwa member?????.Hapa za Mbayuwayu changanya na zako.

Kumekuwa na vijitabia vya hovyo vya CDM, mtu akiwa kwao ''jembe'', akitoka hupachikwa majina ya hovyo sana.Inamaana kigezo cha kukubalika CDM ni kuwa Mwanachama milele na usitoke?.Chama kama kinavuna wanachama kutoka vyama vingine eg. CUF,TLP,CCM,ADC ama NCCR kikubali pia kupoteza wanachama wake.

Magamba nao wanakatabia haka ka ''oil chafu'' ila CDM wamezidi.Kama ndoa, watu wanaoana na kuzaa watoto kisha kuachana sembuse vyama.
 
Hapa sasa mambo magumu,
Kila siku tuna changanywa sana wananchi, Utasikia CCM-MAFISADI/WALA RUSHWA......sasa hivi tena mnakuja na kutuambia tena CHADEMA-UKABILA/UDINI...
Sasa sisi tusio wadini, tusio wakabila , tusio wafisadi na tusio penda rushwa mtatuweka wapi..
 
ingia chama cha haki sawa kwa wote chama cha wananchi cuf
 
Huyo hatufai hata kwa mboga na oneinakana ni gamba lilikuja kwa lengo halijafanikiwa kwaheri wazalendo tupo bado.
 
Jamani naomba mnifafanulie. Hivi kila mwanachama wa chama cha siasa ni kada? ...au kada ni nani?
 
Hiyo picha ya Mwenyekiti wa mkoa ya nini hapo, CDM wanaogopa nini hadi wakimbie haraka kukana kuwa hakua kiongozi wao?
 
Hapa sasa mambo magumu,
Kila siku tuna changanywa sana wananchi, Utasikia CCM-MAFISADI/WALA RUSHWA......sasa hivi tena mnakuja na kutuambia tena CHADEMA-UKABILA/UDINI...
Sasa sisi tusio wadini, tusio wakabila , tusio wafisadi na tusio penda rushwa mtatuweka wapi......[/QUOTE]

Tatizo la CDM SLAA na MBOWE na si vinginevyo. Wapishe vijana waliokwisha wapika waendeleze chama.
 
MTEI, MTEI, MTEI , MTEI. Huyu mzee anafikiri chama hiki bado ni chake, kila siku matamko ya ukabila tu na udini. Huyu mzee anakimaliza hiki chama jamani , kwetu sisi tunaoishi huku kaskazini minong'ono ni mingi sana juu ya huyu mzee.
 
Back
Top Bottom