Kada wa CCM Mustafa Sabodo amwaga visima kumi Ulanga

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,892
32,308
Wanabodi.

Kada wa CCM, Mustafa Sabodo ametoa msaada wa kujenga visima 10 vyenye thamani ya Sh75 milioni kwenye jimbo la Ulanga Mashariki mkoani Morogoro.

Visima hivyo ambavyo tayari vimeishakamilika vimejengwa katika Kata ya Mwaya vitatu vipo kwenye shule ya msingi Libenanga, Sekondari ya Cilina Kombani na kijiji ch Nkongo.

Kata ya mbuga kisima kipo katika shule ya Mbuga, kata ya Ilonga katika Sekondari ya Ilonga, vingine vipo kata ya Chirombola, kata ya Vigoi. Kijiji cha Ebuyu na Safari.

SOURCE; MWANANCHI MAY 18 2012.
 
Hongera sana Mustafa Sabodo!!!
Tunauthamini mchango wako kwenye jamii yetu!
 
Asijekuwa anachota madini kwa gear ya visima kama bwawa la mindu ,mtz amka akili kumkichwa
 
Sobodo, hongera sana.Pengine itakuja siku tutakuelewa vizuri zaidi unachofikiria au kuitakia Tanzania ni nini.
 
wanabodi.

Kada wa ccm, mustafa sabodo ametoa msaada wa kujenga visima 10 vyenye thamani ya sh75 milioni kwenye jimbo la ulanga mashariki mkoani morogoro.

Visima hivyo ambavyo tayari vimeishakamilika vimejengwa katika kata ya mwaya vitatu vipo kwenye shule ya msingi libenanga, sekondari ya cilina kombani na kijiji ch nkongo.

Kata ya mbuga kisima kipo katika shule ya mbuga, kata ya ilonga katika sekondari ya ilonga, vingine vipo kata ya chirombola, kata ya vigoi. Kijiji cha ebuyu na safari.

Source; mwananchi may 18 2012.

vimesimamiwa na ccm au chadema?
 
Asijekuwa anachota madini kwa gear ya visima kama bwawa la mindu ,mtz amka akili kumkichwa

Mkuu huyu Mzee Sabodo ndio anataka kuwajengea ofisi Chadema sasa kwa maneno yako hayo sijui unamaanisha nini.
 
Mmetafuna kodi za walalahoi sasa mnatekeleza ilani kwa msaada wa Sabodo!
 
Kujenga ofisi ya cdm haina maana tumchekee tu tahadhari iwepo tusije kuwa ngazi ya kupitia
Mkuu huyu Mzee Sabodo ndio anataka kuwajengea ofisi Chadema sasa kwa maneno yako hayo sijui unamaanisha nini.
 
SADOBO anadai alichotoa CDM mpaka sasa ni asilimia 1 tu ya alivyowahi kutoa CCM!!!! mBONA MLIKUWA hamtangazi, kilichowasukuma kufanya hivyo saivi ni nini???

Hongera SABODO mchango wako ni mkubwa sana Tanzania hii!!!
 
Back
Top Bottom