Kada tofauti zajiunga na USAILI WA JESHI KIMYA KIMYA.

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Sep 2, 2011
4,873
1,216
Usaili uliokuwa umekamilika na leo, na form vi Art ndo wanatangulia monduli kuanza mafunzo na waliobaki watatakiwa kwenda Januari mwakani.

Cha kushangaza usaili ulipokuwa ukikaribia mwisho kuna Madaktar na kada tofauti wapatao 25 waliongezwa kutoka uraiani bila Wanajeshi hao wanaosailiwa bila kujua wametoka wapi,Pia na Wanawake 30 waliongezwa kuungana na wenzao kwenda mafunzo wote hao wametoka URAIANI ambako nafasi hzo hazikutangazwa.
Swali kwa Walinzi wa Ulinzi; Je hao watu 55 mliowaongeza hapo mmewapata wapi?
Wapo vijana wengi wanasubiri Nafasi hizo lakini teali mmesha zijaza kwa mlango wa nyuma...? Jeshi nalo limekuwa la vigogo na watoto wa wakubwa kwa nafasi kubwa?

Source;mmoja wa wasailiwa wa nafasi hizo.

Kiambatanisho.
Kujiunga JWTZ.

Uandikishaji
Askari Mtu yeyote ataandikishwa
kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa sifa zifuatazo: - >Awe raia wa Tanzania
>Awe na Elimu ya kidato cha nne na kuendelea na aweamefaulu..
>Awe hajaoa/hajaolewa >Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25
> Awe na tabia na mwenendo mzuri
>Awe na akili timamu na afya nzuri Masharti ya Utumishi Askari atapewa nambari ya utumishi baada ya kufaulu mafunzo ya awali.
Atalitumikia Jeshi kwa kipindi cha mwanzo cha miaka sita, baada ya hapo atafanya kazi kwa mkataba wa miaka miwili miwili kwa kibali cha Mkuu wa Majeshi.
Maafisa Bodi ya Uteuzi wa Maafisa (Officers Selection Board)
huwafanyia usaili askari
wenye elimu ya kidato cha
sita na kuendelea toka
Vikosini na Shule za askari
wapya (Recruitment Schools). Watakaofaulu masailiano hayo hupewa hadhi ya Afisa
Mwanafunzi (Officer Cadet), na hupelekwa Chuoni (Tanzania Military Academy) kwa mafunzo ya uafisa kwa muda wa mwaka mmoja.
Hichi vijana wengi hukisubiria...
 
Huyo mnyetishaji nadhani ni mgeni ktk majukumu hayo, kwa nafasi hizi za kazi popote pale vigogo vinawapenyeza sana ndugu zao na kama haitoshi hata Askari wenyewe hupiga sana dili kwa kuwapitisha watu na kupewa chochote kitu, bila shaka mnyetishaji alipigwa panga au mtu wake katoswa kaamua kuvujisha LIWALO na LIWE"
 
Umekosea aisee,jamaa hajapgwa panga na januari Anapanda MONDULI KAMA KAWAIDA ILA JUA WATU WAMECHOKA NA MAMBO HAYO.
 
Hakujafanyika usaili ndugu yangu..na ni kweli kuwa majina hayo mengi yamekuwa kimjuano..walichoambiwa ni kuwa wafike kwenye makambi yaliyotengwa ambalo moja liko Dodoma na lingine liko Kigoma..tarehe 15 julai ndio mwisho wa kuripoti kambini..
 
Usaili upi unausemea wewe,huu ni mwezi wa pili sasa umepita tokea usaili wa ndani uanze na umeisha leo kwa waliopita kujiunga na TMA kwa awamu tofauti tofauti,wataanza hao form six Art then wanaobaki pamoja na hao waliöngezwa wataenda Januari
 
Ndugu yangu si tunazungumzia Raia sio askari waliokuwa kazini. Raia walioongezwa hawajafanya usaili na kwa taarifa ni kuwa wanaenda kuanza JKT kwanza.
Source:Mtendaji wa Mkulu pale Mlalakuwa.

Kwanini waingie kupitia usaili wa ndani na si wa nje,na wamewatoa wapi..au ndo utaratibu mpya.
 
Kwa KIGOMA wilayani KASULU ile kambi ya wakimbizi ambayo soon itafungwa ndiyo JKT inakabidhiwa majengo na kila kitu. Rasmi ndy kinakuwa kikosi cha jeshi,unajua hii imetumika KIBONDO ktk kambi ya wakimbizi KANEMBWA walipopewa jkt basi wakimbizi walishindwa kurudi pale maana wangepata kichapo.
 
Back
Top Bottom