Kada Mashuhuri wa CCM Newala ajiunga CHADEMA

makada kama hawa wanatakiwa wapewe jukumu maalamu kuendeleza moto wa mabadiliko eneo la kusini hasa baada ya viongozi wakuu wa cdm kuondoka mc4 isife iendelee kuwa hai hadi 2015 ccm itakapozikwa rasmi!!

Well said mkuu.Nadhani viongozi watachukulia kwa uzito ombi lako
 
Kada machachari wa CCM jimbo la Newala Mtwara Adam Lawi Sijaona amekihama chama hicho na kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM.Kada huyo aliyekuwa msaada mkubwa kwa CCM jimboni humo na kipenzi cha wana-Newala amesema CCM sasa imepoteza mwelekeo na kuwataka wakazi wote wa jimbo hilo kumfuata ndani ya CDM.
Kada huyo ni mtoto wa mpigania uhuru wa Tanzania na muasisi wa TANU na CCM.Akihutubia umati mkubwa wa watu kada huyo aliishukuru CDM kwa kupeleka M4C kusini na kusema tangu uchaguzi mwaka juzi si mbunge wala diwani aliyeita wananchi walau hata kushukuru kwa kura walizopata.Kada huyo alikabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CDM Dr Wilbroad Slaa huku umati wa watu ukilipuka kwa shangwe.

Source:Tanzania Daima

Real Liberation is at the door!
 
Adamu aendelee sasa kukijenga chama na 2015 awe mmoja wa wale watakao simama kuomba ubunge pitia jimbo hilo make huyo ni jembe kweli kweli
 
aliapa mkutanoni kwamba newala yote itajivua gamba ndani ya muda mfupi ujao
ukiona watoto wa waasisi wananza kuhama huko magamba jua hali ni mbaya. Sasa mnasubiri nini huko mtwara hameni chama cha magamba kitawadidimiza ni kama panya vile anauma na kupuliza ukiangalia mkono una vidonda tayari. Hivi mnafikiri kuna umaskini zaidi ya huu. Watu wanafanyakazi lakini wanaofaIdika ni ridhione na maswahiba wa baba yake. Anagalia kesho amin usiamini watu wataambulia pilau na kanga za kuchaKAa siku hiyohiyo. Huo ni uzezeta
 
Wameshaona Mwanga sasa mkuu.
 
Teh teh m4c- movement for christians

( NECTA- machinjio ya waislam)
 
Kama sikosei NAPE alinukuliwa akiwafananisha hawa wanaoondoka CCM kwa sasa na oil chafu. Tatizo ni kuwa oil chafu ikiondoka lazima iwekwe oil mpya kwenye injini ili isije ikaungua. Sioni CCM ikifanya juhudi zozote kuingiza oil mpya kwenye injini yao ili kuchukua nafasi ya hii chafu inayomwagika.

matokeo yake injini ni kunoki maana hakuna oil mpya inayowekwa na gari wanataka kuendesha!!!
 
Kila ninapokuatana na habari kama hizi, break ya kwanza ni kuiangalia tena na tena signature yangu...

Mungu lazima atakuwa nasi daima!!
 
Back
Top Bottom