Kabwe Vs. Wangwe - kisa cha mafahali wawili?

Mkamap,
Sasa ikiwa theory yako ya mwanzo imekwenda kama ulivyosema lakini hiyo profit inachukuliwa na mwekezaji (Barrick) ambaye ndiye mwenye mali, hivyo hivyo ktk Utalii unakuta faida inachukuliwa na makampuni ya nje - Je, utapoulizwa hali ya uchumi utasema uchumi haukukua kwa sababu faida hatukuipata sisi!..na utakapo wakilisha takwimu zako ktk taasisi za kimataifa utatumia vigezo gani kuonyesha uchumi haukukua...

Pili, hukunipa neno moja lenye maana ya mauzo kuongezeka ktk uchumi wakati wa hasara... kisha Inakuwaje ikiwa Mauzo yameongezeka na faida itakapitikana badala ya hasara hapo tunatumia neno ama lugha gani. tafadhali naomba darasa..
 
Madela
unayoongea ni sawa kwa mtazamo mwepesi mno
Chukulia Madini ni kama bidhaa ambayo imewekwa ktk maghala kumi tofauti tuseme kila ghala ni mgodi wa machimbo ya madini

sasa basi mwaka wa kwanza ukauza bidhaa kutoka ghala la GEITA na BUNYAKULU kwa bei ya hasara ukapata milioni moja kwa mwaka na ktk nchi ya tz tuseme kuna watu laki moja bila ubishi pato la kila mmoja ni sh 10.

mwaka wa pili ukafungulia maghala mengine 5 hivyo yanayofanya kazi yamefika maghala 7 yani buhemba,buzwag ,biharamulo,mwadui na nyamongo
sasa basi ukauza bidhaa kutoka humo ktk maghala hayo saba kwa bei ya hasara na ukapata sh milioni mbili kwa mwaka na bado ukiwagaiwa wananchi wa tz laki moja unapata kila mmoja pato lake ni sh 20.
Hapo wadanganyika ndipo wanakuja kusapoti pointi mfu eti kwa vile pato limetoka sh 10 hadi 20 kwa mwaka eti limekua .duuuuu

Hey my comrade hapo umepata hasara zaidi hata ya mwaka jana na uchumi umeshuka pia pato lako angalia mwaka jana magala mangapi yalikuwa yanafanya kazi na mwaka huu yanafanya kazi maghala mangapi then tafuta ratio ya pato lako with respect to maghala by considering each yeat.

Nilichokisema toka mwanzo hapo kuwa pato haliongozeki ila yanayoongezeka ni machimbo ambayo kwa sisi tunavyoangalia just availlable amount bila ku consider factors nyingine ndio maana tutabaki gizani na kuua kila shirika tunalokabidhiwa

kwanza mie nazidi kupadwa na hasira tu kwa mawazo kama haya ,sasa hivi katoka hapa jamaa mweupe yani mzungu katoka kuniudhi kwa kuniuliza hivi ninyi watu weusi mnamatatizo gani kichwani ananiambia angalia hii EUROPE kimsingi haina malighafi na bado mda wa kilimo upo limited yani miezi michache tu baridi ikianza na barafu basi kilimo kimekoma akaendelea lakini ninyi afrika Mungu kawajalia madini kilimo mwaka mzima unawezekana kulima,maziwa mito mmepewa, madini ,vivutio vya kila aina mumepewa na kunimaliza zaidi what is wrong with u africans????

Mimi nikajaribu kujitetea japo na simazi kuu kuwa unajua utawala wa kibeberu wa akina kichaka ndio sababu na hii EUROPEAN UN akanimaliza kwa kusema Afrika ni Bara lenye watu wengi kama mngekuwa na akili nzuri Mngekataa kwa pamoja kama bara wala kichaka hata fanya kitu.
Hapo Machozi yakaanza kulegalega sasa nakuja ktk skrini hii watu bado wanashabikia uchumi umekua ebwana machozi yamenitoka

Ndugu zaguni kilichokua ni ongezeko la bidhaa ya madini kutoka tz kwenda kwa wazungu kwa maana machimbo yameongozeka na malighafi imeongezeka na kuchukulika kiurahisi bila matatizo

what i can say is
GOD!!!!!!!
Nothing is impossible under your sun hivyo maombi yangu kwako leo ningeomba hayo madini na mali asili uyapoteze yasipatikane tz mda wa miaka miwili tu harafu baada ya hapo uyarudishe.
 
Mkamap,
Sasa ikiwa theory yako ya mwanzo imekwenda kama ulivyosema lakini hiyo profit inachukuliwa na mwekezaji (Barrick) ambaye ndiye mwenye mali, hivyo hivyo ktk Utalii unakuta faida inachukuliwa na makampuni ya nje - Je, utapoulizwa hali ya uchumi utasema uchumi haukukua kwa sababu faida hatukuipata sisi!..na utakapo wakilisha takwimu zako ktk taasisi za kimataifa utatumia vigezo gani kuonyesha uchumi haukukua...

Pili, hukunipa neno moja lenye maana ya mauzo kuongezeka ktk uchumi wakati wa hasara... kisha Inakuwaje ikiwa Mauzo yameongezeka na faida itakapitikana badala ya hasara hapo tunatumia neno ama lugha gani. tafadhali naomba darasa..

Ndugu yangu Mkandara
kama uchumi umekuwa ina maana ni ile pesa iliyoingia serikalini na kwamba huwa wanachukuwa pato la la serikali na kugawia watu wake na si kuchukua kisichokuwemo yani makapuni ya nje

Mauzo na faida ikapatikana ni uchumi endelevu wenye kumnufaisha mwananchi wa kawaida.
mauzo kuongezeka walakini imepata hasara kwa waswahili kama Zitto ni uchumi kukua usiomnufaisha mwananchi
 
mkamap,
lakini huo mfano uliotoa hapo juu mjomba unaelewa vizuri kuwa sio hali halisi Tanzania. madini yamekuwa yakiongezeka bei zake kila mwaka na hasa dhahabu ndio ime shoot vibaya sana nasi maghaa yameongezeka kiasi kwamba tunaitwa nchi ya tatu Africa.

Hilo neno hasara halipo kabisa ktk madini wala Utalii labda ktk sekta nyinginezo ikiwa ni pamoja na kilimo chetu cha mkono. Tutasemaje kuwa uchumi unaporomoka hali maghala yote yanazidi kuuza zaidi ya mwaka jana. Mbali na hapo ukiuliza mchango wa madini mwaka jana utaambiwa ulikuwa asilimia 1.5 leo hii ni 1.9 je bado tutatumia lugha gani hapa ikiwa pato hili bado ni dogo sana kwa taifa pamoja na kwamba hawa jamaa kina Barrick ndio wanachukua faida yote kufidia gharama zao za uwekezaji.
Sasa wanaposema uchumi kukua ni ongezeko la value of the goods and services produced ina maana ni goods na service zipi ikiwa serikali yetu haishughuliki na hivyo vitu. Hii kweli? ama ni tafsiri ya kijamaa ambapo mali zote ni za serikali... Hapa uncle umenipoteza kabisa ikiwa kinachotazamwa ni pato la serikali.
 
sawa mkubwa
kwani ucle huwa wanajua je? pato la mtanzania ni chini ya dola sijui kwa siku hapo nisahihishe
lakini kwa mtazamo huu mimi naomba nisalimu amri nikubaliane nawe kweli uchumi umekuwa ktk madini toka 1.5% mpaka 1.9%

Lakini ningeomba uwe unatembelea kwenye ofisi za kubadilishia fedha nafikiri kuna kitu utakinoti baada ya kuona jamaa amekazia macho kwenye skrini akiangali jinsi pesa zinavyopanda na kushuka kila sekunde.
Madini kama yanapanda ni kwa kiasi kdogo ila kinachofanyika uncle ni hizo shiling za tz zinaporomoka kwa kasi na ukiona hayo matarakamu ya fedha za bongo unahisi unafedha haswa kumbe upuuzi tupu.
 
Uko sahihi Chuma, hatuwezi kushangilia na kuijadili posti ya mtu ambaye ana posts 3 tu hapa JF

Hapa mkuu napishana na wewe.
Kwani mtu ukianza kuposti unaanza na ngapi? 1,2 na baadae unafika hizo 500.Kitu cha msingi ni kuangalia hoja ambayo imewekwa na si kuangalia ana post ngapi.Mbona tunaaanza kubaguana?

then anakuja na uzushi ambao hauna ushahidi wa kushikika
Apewe nafasi ya kuthibitisha huo uzushi, (kwa kuelekezwa).[Labda kama anafahamika kuwa ni old wine ktk new bottle]

Huyu bado credibility yake ndogo sana kuweza kushawishi baraza hili.
Ana thanks 1 tayari.Kila mtu anautashi wa kuignore au kuandika. Si unajua hata maofisini kuna 'on job training?'

Just Ignore him!

????????????:confused: ........
 
Msitiane vitanzi kama Zitto na Wangwe.

Uchumi unakuwa na faida yaenda kwa wwengine na si Taifa. hilo ndio tatizo. Ni sawa na kusema Mchaga kaongeza uzalishaji wa Kahawa mara tatu katika mwaka, lakini mapato yake hayajaongezeka wala kuwiana na kukua kwake kwa uzalishaji.

Sekta za Madini na Utalii pekee zinatosha kushikilia 35% ya pato la Taifa (minimum) lakini tunachokivuna kutokana na uzembe wetu na ufisadi ni 3-5%!

Dhahabu ni sawa na Mafuta. Leo utaniambia kuwa Angola waendeleze Pamba wakati bei ya Mafuta ni kubwa kuliko Pamba?

Hili ndilo linalotuua Watanzania. Tunajidanganya na Ukulima wa Kijima na kufikiri bei ya Kahawa, Pamba, Korosho, Alizeti na Tumbaku itaongezeka. Kamwe itasuasua na Wazungu watatafuta bidhaa bandia (jute for sisal) ambazo zitafanya Zanzibar ilie kuwa bei ya karafuu inaharamiwa na mabepari.

Ni lini ulisikia kuna substitute ya Dhahabu au Utalii as a commodity?

Kama maneno ya gazeti la Uhuru ni sahihi na si upindishaji habari, basi ni wazi kuwa Zitto alitoa matamko yaliyofanana na Mkwere kuhusiana na uchumi kukua hata kama alihitimisha kuwa faida haiendi kwa Taifa. Alichoanza kutamka ni "Uchumi wa Taifa ni Mzuri na Unakuwa...."

Then ni Haki ya Wangwe na Chadema kuhoji kauli kama hiyo. Baya zaidi ni dhihaka ya Wangwe kuwa acha kudandia nyuma gari la CCM, milango iko wazi! This means that Zitto ni kigeugeu na mguu nje au anajipendekeza kwa Mkwere!
 
Tatizo ninaloona hapa ni kwa viongozi wakuu wa chama kulumbana kwenye vyombo vya habari. Hapo wanapaswa kukiri makosa kama kweli walifanya hivyo, au kukanusha habari kama ni waandishi wamewanukuu vibaya. Hasa reaction ya harakaharaka ya Chacha ya kuanza "kumzodoa" Zitto kwa habari iliyoko kwenye gazeti ambayo hana uhakika kuwa mwenzie kweli kayasema hayo. Alipoulizwa, alishindwa nini kuwajibu kuwa binafsi hajamsikia Zitto akiyasema hayo, au kuwataka wakatafute ufafanuzi kwa huyohuyo aliyeyasema, au kuwataka wawe na subira hadi apate uhakika, au kusema tu hana comment? Hapo ndipo naona udhaifu hasa wa Chacha, kwamba amejidhihirisha ni mtu rahisi "kuokotwa" na waandishi wa habari na kugombanishwa na wenzie.

Mchezo huo waliutumia kusambaratisha ile iliyokuwa NCCR-Mageuzi na walifanikiwa sana. Mwandishi anakwenda kwa Mrema anamwambia Marando kasema wewe ni mlevi wa madaraka, hushauriki. Mrema anamjibu kamwambie yeye ni pandikizi la CCM! Inatoka front page next day. Marando akiona, anaitisha mkutano wa waandishi anaanza kumchamba Mrema. Inatoka kwenye TV, redio, na magazeti. Mrema anaitisha mkutano wake na waandishi, anapinga aliyosema Marando jana yake. Magazeti wanazidi kuuza! Baadae wanaenda kwa Mbatia wanamwambia Mrema anauliza kwa nini unashirikiana na kyasaka? Naye Mbatia hamwulizi Mrema kama kweli kasema hivyo, anawajibu waandishi huyo Mrema hana akili timamu, inatoka tena kwenye magazeti. Wanarudi kwa Mrema, wanamwonesha gazeti "unaona anayosema mwenzio", naye Mrema anawajibu "mbona sisi tunamjua ni shoga siku nyingi hatusemi!" inatoka tena kwenye magazeti. Walifaidi kweli watu wa magazeti kipindi hicho, lakini na chama kikasambaratika, kwisha kabisa.

Hivi wasomi wetu huko Bongo hamuwezi kutuandikia kitabu kuhusu kusambaratika kwa ile NCCR-Mageuzi iliyowika enzi hizo? Lingekuwa somo zuri sana kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo. Tena inaweza ikatengeneza material nzuri sana kwa ajili ya tasnifu (thesis) ya shahada ya uzamivu (PhD) hapo Mlimani. Changamkieni hiyo!
 
Ni rahisi tu, kina Zitto na Mnyika wajibu hii hoja watusawazishie mambo. Jana alikuwepo hapa Zitto, nadhani post ilikuwa haijawekwa. Tuwasubiri watoe majibu.

Ndugu Mnyika na Mheshimiwa Zitto, majibu...!
 
Wangwe, Zitto watishia uhai wa Chadema

*Ndesemburo aonya chama kinaweza kusambaratika


Na Joyce Mmasi


SIKU chache baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoa tamko kuwa hakuna mgogoro ndani ya chama hicho na badala yake kinachofanyika ni mjadala hai, sasa imedhihirika zipo dalili za wazi kuwa huenda chama hicho kigawanyika.


Hali hiyo inadhihirishwa na kauli za viongozi wa juu wa chama hicho, makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Chacha Wangwe na Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe kulumbana hadharani kupitia kwenye vyombo vya habari.


Wachunguzi wa masuala ya kisiasa nchini wanazitafsiri kauli za kushambuliana na kupingana hadharani zinazowahusisha viongozi wawili wa juu ndani ya chama hicho zisipodhibitiwa haraka huenda zikakifikisha chama pabaya na kubakia historia kama vilivyo vyama vya NCCR-Mageuzi na Tanzania Labour Party (TLP).


Mapema wiki hii, Wangwe ambaye pia ni Mbunge wa Chama hicho Jimbo la Tarime alikaririwa na vyombo vya habari akimshutumu Zitto kwa kauli yake ya kueleza kwamba kuwa uchumi wa nchi una kua.


Chacha Wangwe alisema kauli ya Zitto inaonekana kushabihiana na kukubaliana na CCM na akamfananisha na mtu anayedandia gari kwa nyuma kitu alichosema sio msimamo wa kambi ya upinzani wala wa Chadema.


Wangwe anasema katika kauli yake hiyo, Zitto amekuwa na tabia ya kuisifia CCM hali inayotia shaka na kuona pengine mwenzao anataka kupanda gari moja na CCM, ndio maana yeye kwa maoni yake anapinga hadharani na akawataka watanzania pia kujitokeza kusema kama wanaona jambo la kusema.


Hata hivyo, hali hii imeaanza kuwatia wasiwasi baadhi ya wanachama na viongozi wa juu wa chama hicho kwamba ikiachiwa huenda ndio itakuwa tamati ya chama hicho katika ulingo wa kisiasa.


Mmoja wanachama ambao wanatiwa wasiwasi na hali hiyo ndani ya chama hicho, ni mmoja wa waasisi wa chama hicho, Philemon Ndesamburo ambaye alimweleza mwandihishi wa Mwananchi jana kwa njia ya simu kuwa malumbano ya viongozi hao ni dalili mbaya ndani ya chama.
Alisema kiongozi mkubwa ndani ya chama akitoa kauli kwa umma sio sahihi kwa kiongozi mwingine ndani ya chama hicho kuanzisha malumbano hadharani, badala yake tofauti zao zinapaswa kujadiliana ndani ya vikao vya chama.
Ndesamburo ambaye pia ni Mbunge wa Moshi Mjini kwa tiketi ya chama hicho, alisema hali hii ya viongozi wa chama kushambuliana hadharani isipokomeshwa inaweza kuleta mpasuko katika chama hicho.

Alisema hata kama kiongozi mmoja wapo amekosea au kasema kitu ambacho sio halali au ni kinyume na taratibu za chama, ni vyema hoja hizo zikapelekwa kwenye vikao vya chama na sio kuzungumzwa kwenye vyombo vya habari.


?Ni kweli chama chetu ni cha kidemokrasia, lakini tafsiri ya demokrasia sio kushambuliana au kukaribisha malumbano hadharani, bali ni kuzungumza na kukosoana ndani ya vikao vya chama,? alisema Ndesamburo.

Aliwataka viongozi wanaokimbilia kwenye vyombo vya habari kuzingatia kanuni na taratibu za chama za kujadiliana ndani ya vikao halali vya chama kwa kuwa kufanya hivyo ni makosa.


Mwanchama mwingine ambaye hakupenda kutajwa jina lake alisema kuwa malumbano yanoyoendelea kati ya Zitto na Wangwe sio ya kukijenga chama bali ni ya kuwania umaarufu.


Alisema inavyoonekana Wangwe hoja yake nikutaka kummaliza Zitto kutokana na umaarufu ambao amejipatia na kwamba hali hiy ni mbaya na kwa kuwa inaweza kusababisha viogozi hao kupigana ngumi.


Hata hivyo, Mkurugenzi wa vijana wa Chama hicho, John Mnyika alimweleza mwandishi wa Mwananchi jana kwamba hakuna ubaya viongozi kutofautiana hadharani na kwamba hiyo ndio tofauti iliyopo kati ya Chadema na vyama vingine.


Mnyika alisema Chadema ni chama cha kidemokrasia kama jina lake linavyojiainisha na kwamba wanachofanya wanachama au viongozi ni kutumia demokrasia waliyo nayo kukosoa na kuelimisha bila kuzifanya kauli zao kuwa ni msimamo wa chama.


?Chadema ni timu moja yenye nia na malengo yanayofanana, hakuna ugomvi wowote na tofauti za misimamo haziwezi kuvunja chama na badala yake zinakiimarisha chama chetu,? alisema Mnyika.


Mnyika alitoa mfano wa kutokukubaliana kulikozuka wakati Zitto alipochaguliwa kwenye Kamati ya Madini ambapo baadhi ya watu waliamini ndio mwisho wa chama hicho, lakini baada ya vikao vya chama yale mambo yaliisha na hali ikawa shwari kama kwanza.


?Ndio maana nasema, Chadema ni tofauti na vyama vingine, tunafanya siasa ambazo watanzania hawajazizoea, tunapotofautiana kimawazo haimaanishi kuwa kuna ugomvi baina ya mtu na mtu, yale ni mawazo ya watu na kamwe hayawezi kukivunja wala kuleta mpasuko wowote ndani ya chama.


Naye Chacha Wangwe aliiambia mwananchi kuwa anasema anachokiamini na kamwe haaoni kama kuna uhusiano wowote wa kauli zake kuhusishwa na uwezekano wa kuvunjika au kuleta mpasuko ndani ya chama.


?Kutofautiana sio kubomoka kwa chama na mtu mmoja kamwe hawezi kuvunja chama, hivyo nataka ieleweke kuwa hoja ya kuvunjika kwa chama hapa haipo,? alisema na kuongeza: ?Chama chetu kina uhai kiko tofauti kabisa na CCM, sisi tunazungumza hadharani na sio kuficha ficha mambo, ndani ya Chadema tuna uhuru wa kusema na kutoa maoni bila kuingiliwa".


Alitoa wito kwa watanzania wote wawe kama yeye, waseme pale wanapokuwa na hoja, wasifichefiche mambo na akasisitiza kuwa msimamo wake ni kuwa CCM haijafanya lolote na haipaswi kusifiwa na kiongozi kutoka kambi ya upinzani kuwa imeleta maendeleo.


Alisema Zitto amekuwa na tabia ya kuisifia CCM na serikali yake jambo ambalo alisema linawapa mashaka wao kama kambi ya upinzani.
 
Nadhani ukisoma hiyo post ya mtoa hoja hakuna lolote la maana, kwa kweli Zitto wala Mnyika kwa hili hawana la kujibu hapa,,, maana pia mwandishi ameonyesha wazi kwamba hajafanya utafiti wowote amekurupuka tu!
 
hizi ndiyo notes nilizotumia katika warsha masasi, mbeya, dodoma na arusha. Imeripotiwa katika gazeti la uhuru (licha ya kichwa cha habari kuwa spinned, habari yenyewe ilikuwa sahihi kabisa). Baadae mheshimiwa Chacha akatoa maoni yake, ambapo yupo huru kabisa kutoa maoni yake kama Mtanzania. Leo pia nimesoma katika mwananchi kuwa mimi Chacha twaleta mgawanyo ndani ya chama.

Sihitaji kujitetea hapa, hata hivyo mimi sikutoa maoni yangu katika gazeti, ila wakati nawasilisha mada kwa vyovyote vile waandishi walikuwapo.

Mimi kama mtu niliyesomea uchumi, ninajua ukweli kuwa uchumi wetu unakua. Tatizo tulilonalo ni kwamba 'base' ya uchumi wetu ni ndogo hivyo ukuaji haui mpana ie not broadbased growth. Mbaya zaidi, sekta ya Kilimo haikui, ambayo ndiyo inasababisha broadbased growth. Sekta zinakua ni madini na utalii, ambazo mahusiano yake na sekta nyingine ni madogo ie forward and backward linkages. Changamoto tulizonazo ni haya mahusiano.

Nilitoa mfano mmoja pale Arusha: kwamba kama tuna lengo la kuleta watalii milioni moja kwa mwaka nchini, tumejiandaa vipi kuhakikisha kuwa Mkoa wa Singida unazalisha Kuku wengi na Mayai mengi zaidi? Kama kila mtalii atakula mayai 2 breakfast kwa siku na atakaa nchini siku 5 maana yake ni kuwa watu wa singida wazalishe mayai milioni 10 ya kuku wa asili. Kama kila yai ni sh 100, inaa maana umeingiza 1 bilioni katika kuku subsector mkoani Singida. Hii ndio maana ya linkages, na kwa kuwa hakuna linkages tuna import kuku na mayai kutoka Brazil!!!!

Mfano mwingine nikawaambia, kule Geita Gold Mine wafanyakazi wanakula Nyama kutoka Kenya. Kimsingi Ng'ombe hutoka usukumani na kupelekwa Kisumu. Kule wanachinja, wanapack na kuuza Geita. Hivyo Mgodi wa Geita unatengeneza ajira Kisumu Kenya. Tulipoita investors, tulipaswa kuweka mazingira haya kwani sekta za uchumi zinaingiliana ie multiplier effect. Na hapa ndio kazi ya State Intervention kwenye soko. Sisi tukawa makuadi wa soko huria.

Uchumi wetu unakua, drivers of growth ni Mining and quarrying na Trade ie tourism. Twapasa kuweka links za sekta hizi na sekta nyingine na pia kukuza rural growth ili kupunguza umasikini. Hizi ni facts, undisputable facts!


These are my talking notes, nimeshindwa kuattach, network ipo slow

===================================

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MKUKUTA MWAKA 2006/2007

Kabwe, Z.Z, Disemba 2007

• Taarifa ya utekelezaji wa MKUKUTA ni moja ya matokeo ya mfumo wa ufuatiliaji wa MKUKUTA. Lengo la kuzalisha ripoti hii ni kuchangia katika mfumo mzima wa kutoa taarifa kwa mawizara, serikali za mitaa na hata Asasi Zisizo za Kiserikali (AZISE). Taarifa inatoa kwa ufupi mafanikio na changamoto zilizofikiwa katika kufikia malengo ya MKUKUTA.

• MKUKUTA una lengo kubwa la kukuza uchumi na kupunguza umasikini. Hata hivyo wananchi wamekua na maswali mengi sana kuhusiana na takwimu za ukuaji wa uchumi. Kwa mfano, mbona takwimu haziendani na hali halisi za maisha ya wananchi? Mbona kila kukicha hali ya maisha inakuwa ngumu sanjari na mfumuko wa bei?

• Uvumbuzi wa maswali hayo na changamoto za kupambana na umaskini zinaweza kufaulu iwapo kila mdau atauelewa, kisha kushiriki katika utekelezaji wa Mkakati wa Kukuza Uchumi na kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA). Pia taarifa za mwaka za utekelezaji wa MKUKUTA ni muhimu sana katika kuelewa hatua ambazo zimefikiwa.

• MKUKUTA mbali na kuainisha nyenzo na rasilimali za ndani na nje za kupambana na umaskini, umebeba pia malengo ya dira ya taifa 2025 na malengo ya milenia ambayo yanadhamiria ifikapo mwaka 2015 umaskini wa kipato uwe ndoto duniani.

• Katika mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa MKUKUTA taarifa zilizokusanywa zinaonyesha ukuaji wa uchumi unaendelea vizuri, ingawaje mwaka 2006 uchumi ulitetereka kidogo kutokana na tatizo la ukame na kuathiri Sekta za Kilimo, uzalishaji viwandani, umeme na maji.

• Rekodi ya ukuaji wa uchumi hapa nchini toka mwaka 1993 hadi 2000, inaonyesha kulikuwa na ukuaji mdogo wa uchumi toka asilimia 0.4 hadi kufikia asilimia 4.9, lakini kuanzia mwaka 2001, uchumi uliendelea kukua kwa asilimia 5.7 na hadi 2005 ukuaji wake ulifikia asilimia 6.7 na kushuka kidogo kufikia asilimia 6.2 mwaka 2006. Lengo la MKUKUTA ni kufikia ukuaji wa uchumi wa wastani wa asilimia 6-8 mpaka mwaka 2010. Ukame na tatizo la umeme ni moja ya matatizo yaliyopelekea kushuka kwa kasi ya ukuaji wa uchumi mwaka 2006.

• Ukuaji wa kisekta kuanzia mwaka 2000 ukuaji wa kisekta unaonyesha kushuka. Mchango wa kila sekta katika ukuaji wa uchumi unategemea sana ukuaji wa sekta husika. Hata hivyo, kilimo kimeendelea kuwa mchangiaji mkubwa wa uchumi. Sekta ya kilimo ilichangia asilimia 44 ya Pato la Taifa mwaka 2006

• Ukuaji wa sekta ya kilimo ni kwa wastani wa asilimia 4.7 katika kipindi cha mwaka 2000 hadi 2006, kiasi ambacho hakitoshelezi kufikia malengo ya kuondosha umaskini yaliyomo kwenye MKUKUTA. Lengo ni kuwa ifikapo 2010 kuwa na kilimo endelevu kinachokua asilimia 8 - 10. Mwaka 2005 sekta ya kilimo ilikua kwa asilimia 5.1 na mwaka 2006 ilikua kwa asilimia 4.1 na hivyo iliporomoka. Ukame ulikuwa ni sababu kubwa ya kuporomoka kwa ukuaji wa sekta ya kilimo.


• Madini ndiyo sekta inayoibuka kwa kasi, imekua haraka kwa kiwango cha asilimia 15 kati ya mwaka 2000 na 2006. Hata hivyo mchango wake katika uchumi mkuu bado ni mdogo ukuaji wa sekta ya madini bado haujachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza umaskini kwenye maeneo ya uchimbaji. Mwaka 2006 sekta ya madini ilikua kwa asilimia 16.8. Hata hivyo mchango wa sekta hii katika Pato la Taifa ni asilimia 3.8 tu. Lengo ni kufikia mchango wa sekta ya Kilimo katika Pato la Taifa kuwa asilimia 10.

• Sekta ya uzalishaji viwandani nayo imeanza kukua, inakua kwa kiwango cha asilimia 7.5 kuanzia mwaka 2000. Hata hivyo mchango wake kwa pato la taifa bado ni mdogo, unafikia asilimia 8 tu.

• Sekta ya biashara, migahawa na hoteli ambayo inaashiria kushamiri kwa sekta ya utalii, imekuwa kwa kiwango cha asilimia 7.3. Sekta ya Utalii kwa kuwa ina mchango wa moja kwa moja katika pato la taifa, pia inachangia katika sekta nyingine za kiuchumi, lakini bado utalii haujatumika vizuri kukuza pato la taifa na hata kusaidia kuondosha umaskini wa wananchi.

Viashiria vya ukuaji wa uchumi
• MKUKUTA unakusudia kuhakikisha kuwa kuna usimamizi mzuri wa ukuaji wa uchumi endelevu. Kuanzia katikati ya mwaka 1990, kipaumbele kiliwekwa katika ukuaji wa uchumi mdogo na muundo wa usimamizi wa fedha za umma ukizingatia kudhibiti matumizi ya serikali. Hali hiyo imesaidia kupunguza mfumuko wa bei mwaka 2003. Lakini kuanzia mwaka 2004 kumekuwa na ongezeko la mfumuko wa bei ambao unaweza ukaashiria kuwa kuna ongezeko la matumizi ya serikali.

• Mwenendo wa mfumuko wa bei kuanzia mwaka 2000 hadi 2006 ni kama ifuatavyo:

Mwaka Mfumuko wa bei
2000 6.0
2001 5.1
2002 4.3
2003 5.3
2004 4.7
2005 5.0
2006 7.3

• Mwaka 2006 mfumuko wa bei uliongezeka kwa asilimia 7.3. Hali hiyo pia ilionekana katika miezi ya mwanzo ya mwaka huu (2007). Hali hiyo ilisababishwa na ukame uliotokea nchini mwaka 2005/06 ulioathiri uzalishaji wa umeme na hata uzalishaji wa chakula. Kadhalika katika kipindi hicho kulikuwa na ongezeko la mara kwa mara la bei ya mafuta ya petroli.

• Yapo maendeleo yanayoonekana ya kiuchumi ambayo yametokana na kuimarisha kwa mfumo wa utozaji kodi. Makusanyo ya kodi za ndani yameongezeka kutoka asilimia 12.2 mwaka 2000/01 hadi 15.6 mwaka 2006/07. Lengo ni kufikia mapato ya ndani kuwa 25% ya Pato la Taifa.

• Hata hivyo pamoja na kuongezeka kwa makusanyo ya kodi ya mapato lakini matumizi ya fedha za umma nayo pia yameongezeka.Kwa kawaida kuna matumizi ya aina mbili; Kwanza ni yale yanayoongeza Tija na ambayo huimarisha upatikanaji wa huduma za jamii. Hali inaonyesha kuwa kuanzia mwaka 2001 kuna upungufu katika utoaji wa huduma za jamii.

• Ili kufikia malengo ya MKUKUTA kuna haja ya kuwepo kwa uunganishaji mzuri baina ya malengo ya kuuimarisha uchumi mkuu na huduma za jamii sambamba na kupunguza matumizi ya serikali kwa kiasi kikubwa na kuwekeza katika shughuli za kiuchumi.

Uwiano wa kibiashara

• Sekta binafsi inakua vizuri tokea mwaka 2000 hii inatokana na kuwepo kwa mazingira mazuri ya kukopa kutoka katika taasisi za fedha zilizopo nchini na kufanya biashara, kwani mwaka 2006, sekta binafsi imepata asilimia 12.5 ya mikopo.

• Hata hivyo pamoja na kuwa kuna dalili nzuri za matumaini katika upatikanaji wa mikopo, mazingira haya bado hauwanufaishi wengi, wanaofaidi ni wajasiriamali wakubwa wenye mitaji imara na wengi wao wanaoishi mijini.

• Kuna matarajio makubwa ya Tanzania kuvutia wawekezaji wengi wa nje. Lakini ili hilo liwezekane, inabidi jitihada zaidi zichukuliwe kwa serikali kuendelea kuboresha vivutio na miundombinu ili wawekezaji waweze kuzalisha bila gharama kubwa .

Ukosefu wa ajira

• Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2006, inakadiriwa kuna zaidi ya watu milioni 18 wenye nguvu ya kufanya kazi hapa nchini. Ongezeko hili ni kubwa, ikilinganishwa na mwaka 2000/01 ambapo kulikuwa raslimali watu milioni 3.3.

• Hili ni ongezeko la asilimia 4.1 kwa mwaka (watu 800,000 huingia katika soko la ajira kila mwaka).Watu wapatao milioni 16.6 ambao ni asilimia 80.3 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi, wanafanya kazi, ingawa wengi wao wamejiajiri au wanafanya biashara ndogondogo na wengine wanafanya kazi majumbani ambazo hazina mishahara.

• Katika miaka michache iliyopita, uchumi wa Tanzania umeweza kupunguza kwa kiasi kidogo tatizo la ajira mijini MKUKUTA unadhamiria kupunguza Ukosefu wa ajira kutoka asilimia 12.9 mwaka 2000/01 hadi asilimia 6.9 mwaka 2010.

• Tatizo la ukosefu wa ajira haliwezi kushughulikiwa endapo ukuaji wa uchumi hautoshelezi. Ni makosa makubwa kuliona tatizo hilo kama mzigo kwa jamii ni vema msukumo ukawekwa katika ajira na sera za kazi na mikakati ya kuongeza ukuaji wa uchumi.

Mtandao wa barabara
• Kuwa na miundombinu imara kunaashiria kuwa na uchumi imara. Ingawa Uchumi wa Tanzania bado haujaimarika vizuri, tatizo la miundo mbinu limeainishwa katika Taarifa ya utekelezaji wa MKUKUTA.

• Ubora wa mtandao wa barabara kuu na za mikoa umeshuka kutoka asilimia 84 mwaka 2005 mpaka asilimia 78 mwaka 2006. Sababu kubwa iliyosababisha hali hii ni ufinyu wa Bajeti na kuchelewa kwa ahadi za misaada kutoka nje.

Kuboresha Maisha na Ustawi wa Jamii

Elimu
• Lengo kubwa la MKUKUTA ni kuhakikisha kuwa watoto wengi wanajiunga na shule za msingi na sekondari na pia ubora wa elimu unaimarishwa. MKUKUTA umesisitiza sana umuhimu wa watoto wa kike kuingia shuleni.

• Taarifa ya MKUKUTA inaonesha kuwa Tanzania imefanikiwa kuvuka lengo la kuandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza kwa kufikia asilimia 114 mwaka 2006. Lengo lilikuwa asilimia 99 ifikapo mwaka 2010.

• Kwa upande wa elimu ya sekondari MKUKUTA uliweka lengo la kufikia asilimia 50 ya vijana wanaomaliza elimu ya msingi kujiunga na elimu ya sekondari ifikapo mwaka 2010. Lengo hili pia limevukwa kwani mwaka 2006 asilimia 68 ya vijana waliomaliza darasa la saba.

• Changamoto kubwa iliyopo ni ubora wa elimu. Shule nyingi hazina walimu wa kutosha na hata vifaa vya kutosha vya kufundishia.

Afya
• MKUKUTA umeweka malengo kadhaa katika sekta ya Afya. Kwa mfano, lengo la kupunguza vifo vya watoto kutoka vifo 95 mwaka 2002 mpaka vifo 50 mwaka 2010 kati ya watoto 1000 wanaozaliwa. Mwaka 2006 vifo vya watoto vilifikia 68 kati ya watoto 1000 wanaozaliwa.

• Vile vile vifo vya watoto chini ya miaka 5 vililengwa kupunguzwa kutoka vifo 154 mpaka vifo 79 ifikapo mwaka 2010. Mwaka 2006 vifo 133 vya watoto chini ya miaka 5 watoto 1000 vilirekodiwa.

• MKUKUTA pia uliweka lengo la kupunguza kudumaa (stuntedness) asilimia 43.8 mpaka asilimia 20 mwaka 2010. Mwaka 2006 kiwango cha kudumaa kilifikia asilimia 38. Changamoto ni kuongeza lishe kwa watoto ili kuondokana na tatizo hili ambalo kwa kweli ni janga kubwa sana kwa Taifa. Janga lisilozungumzwa kabisa ambalo lina madhara makubwa kwa ustawi wa Taifa. Changamoto nyingine ni kuboresha matibabu ya magonjwa ya watoto.

Utawala na Uwajibikaji
• Utawala bora ni moja ya nguzo muhimu sana katika kuhakikisha ukuaji mpana wa uchumi na uboreshaji wa maisha ya wananchi. Vigezo viwili vinaangaliwa sana, navyo ni jinsia na rushwa.

• Uwakilishi wa wanawake katika vyombo vya maamuzi umeongezeka mpaka kufikia asilimia 30.4 katika Bunge na asilimia 26.8 katika Halmashauri za Wilaya.

• Idadi ya kesi za rushwa ambazo zilizorekodiwa na PCCB zimeongezeka kutoka kesi 1244 mpaka 3121. Inawezekana kesi hizi zimeongezeka kwa sababu mwamko wa wananchi umeongezeka au kiwango cha rushwa kimeongezeka.
 
Ahsante,

Zitto;
Matatizo sio waandishi wa habari tu hata humu ndani JF tunaboronga kishenzi (tunageuza mambo ku-suit our ambitions)... tunashukuru kuwa mkweli siku zote kwa uwezo wako wote uliopewa na Mola wako. Spinning siku zote sio sustainable!!!

Wa kuulizwa vizuri kuhusu madhara ya ku-spin waulizwe CUF.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Baba Zitto

Kama mchumi ukifanya tathmini kuhusu miaka miwili ya serikali ya Kikwete ambaye alichukua nchi kutoka kwa Mkapa uchumi ukikua kwa 6.9% na mfumuko wa bei ukiwa 4.5%, katika mwaka wa kwanza uchumi ukakua kwa takribani 5% na mfumuko wa bei ukaongezeka mpaka 9. Katika mwaka wa pili uchumi ukakua kwa 6.2% na mfumuko wa bei ukashuka kidogo. Je, Kikwete anastahili kujivunia kwamba uchumi umekua kama alivyofanya kwenye mkutano na waandishi wa habari?

Je, Kasi yetu ya kukua kwa uchumi unailinganishaje na nchi nyingine za Afrika? Je, inaridhisha?

Je, kwa rasilimali na fursa tulizonazo- je, unaridhishwa na kiasi chetu cha kukua kwa uchumi kiasi cha kutembea kifua mbele kujigamba kwa uchumi unakuwa?

je, hakuna haja ya kuweka tahadhari kwamba uchumi wetu unakuwa katika kiwango kisichoridhisha na katika mfumo ambao Air Uchumi inapaa huku abiria wakiwa wanashangaa?

Je, ni kwa kiasi gani uchumi wetu unanufaisha sisi wanawake?

Asha
 
Chadema wameguswa pabaya.Ngoja tumsubiri mzee wa kulalamika Mheshimiwa sana Kabwe Zitto zuberi,Ila nakumbuka Zamani kidogo nikiwa naongea na Zitto aliongelea adhma yake ya kuachana na Siasa,ilikuwa mwaka jana.na wakati ule alipopata umaarufu wa kutetea Suala la Buzwagi alisema hataacha kugombea ubunge.Naamini Zitto ni Mwanasiasa Aliyekoma kwa sasa na anaangalia wapi alipo Kada Mpinzani,Mkombozi na Mzee ES.Karibuni Chama Cha Mapinduzi tuung'oe huu Mtandao wa kina RA,
Mapambano ya kifikra katika chama cha mapinduzi ndio yanakuja.stay tuned!
 
Wana JF,

Kuna masuala ambayo huwa yanachanganywa mno na ninaona ni bora nifafanue hapa.

Kwanza, Uchumi unapimwa kwa Pato la Taifa, kimombo GDP. Tukisema uchumi unakua maana yake ni kwamba Pato la Taifa limekua. PT ni jumla ya kipato cha kila mtu, au kila factor of production katika taifa husika. Kwa kuwa ni vigumu sana kukokotoa pato la kila mtu, Tanzania na nchi nyingine nyingi changa, hupima Pato la Taifa kwa kuangalia thamani ya uzalishaji kwa kila sekta. Hivyo uchumi hugawiwa kisekta na rekodi ya uzalishaji kuchukuliwa.

Pato la Taifa sio mapato ya TRA au mapato mengine ambayo serikali hukusanya. Hayo huitwa mapato ya serikali na utendaji wa serikali na uwezo wa serikali kujitegemea pia hupimwa na kiasi cha mapato kama asilimia ya Pato la Taifa. Kiwango cha kimataifa ni asilimia 25. Tanzania tumefikia asilimia 16 hivi ya mapato kama asilimia ya Pato la Taifa.

Hivyo, tunaposema uchumi umekua tuna maana kuwa Pato la Taifa limekua, na hatuna maana kuwa Mapato ya Serikali yamekua. Ingawa Uchumi unapokuwa tax base inaongezeka ie wigo wa kukusanya kodi unaongezeka kutokana na kuongezeka shughuli za uzalishaji katika Taifa.
 
Back
Top Bottom