Kabwe Vs. Wangwe - kisa cha mafahali wawili?

Mkamap,
hapana ndugu yangu Zitto hakusema hivyo wala hakuangalia kukua kwa uchumi kwa mtazamo huo isipokuwa ni hivi.
Kuna ongezeko la mauzo ya madini yetu nje iwe kwa ounce ama fedha na ndicho kinachotazamwa kwanza na wala tusingepiga kelele zetu ikiwa hakuna ongezeko hilo la mauzo, lakini ni kiasi gani cha fedha sisi Tanzania tunakatiwa baada ya mauzo hayo ndipo hapo ngoma. Na kama unakumbuka rais mwenyewe alisema madini yanachangia mfuko wetu kwa aslimia 1.9 tu, hivyo kutowanufaisha wananchi. Kwa hiyo hata kama ni uchumi wa nchi yetu kukua jambo maana hapa kuangalia ni wapi fedha hizo zinakwenda...jibu lake ni Mafisadi!
Alichosema Zitto ndio ule mfano wa nyanya hapo juu wakati Wangwe anazungumzia banda zima la gengeni ambapo kuna maharage, vitunguu, ndizi, juice na bila kusahau chips vumbi.
Zitto hakuzungumzia maswala ya uchumi wetu kwa ujumla wala pato la taifa na hakuna hata mtu mmoja anayepinga kuwa kuna ongezeko la Watalii nchini isipokuwa fedha nyingi zinalipwa huko huko nchi za nje na haya mashirika ya kigeni.. hapa wanaingia watu tu na ushuru unaolipwa ndani kuchangia mfuko wetu ni mdogo sana.
Kwa hiyo jamani tutofautishe kinachosemwa hapa na sababu kubwa ya hotuba ya Zitto ni kueleza kuwa tunashindwa kupata mafao ya miradi hii inayoendelea kuzalisha vizuri kutokana na mikataba feki na yeye yupo tayari kuhakikisha kuwa janga hili linapata ufumbuzi..
 
Kumbe gazeti la kutaka Serikali iaminiwe ni Uhuru ? Ulitegemea nini ? They are always there to twist for CCM. Hebu tuendeleeni na mada zingine . Zitto simaini kama anataka umaarufu wa kugombea ila he is a very sincere boy .
 
Mkandara
Zitto kasema uchumi ktk madini na utalii una kua VERY WRONG STATEMENT
Kwa maana kuwa kama uchumi unakuwa pia tunapata faida.
Zitto kadanganya jamii ya watanzania.
yeye angesema hivi MAUZO KTK MADINI NA UTALII YAMEONGEZEKA
lakini kuja na suala la uchumi unaongezeka akapotoshe wapotoka,
maana unaweza kuuza sana na mauzo yakaongezeka kwa sababu bidhaa yako unauza bei ya hasara ilihiali uchumi wako unadidimia
 
Hatimaye mpango wa Zitto na Mnyika kumsusia Mbowe CHADEMA umedhihirika. Mwanzoni ilikuwa ikisemwa chini chini kwamba wasaidizi hawa wa karibu wa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho wana mpango wa kuacha chama ili Mbowe akiendeleze mwenyewe na Dr Slaa ambaye mara nyingi hakai ofisini. Ushahidi wa wazi kuhusu mpango huu ni kauli ya Zitto Kabwe kwamba hatagombea tena ubunge ili kwenda kujiendeleza zaidi kielimu na kauli ya John Mnyika ya kwamba naye bado kidogo ataondoka CHADEMA, kama alivyosema mwenyewe akijibu hoja hapa JF, na baadaye kubainika ‘atakwenda kujiendeleza zaidi kielimu’. Lakini wadadisi wa mambo wanaona sababu hii ni danganya toto, sababu halisi ya kuondoka kwao ni kumsusia Mbowe CHADEMA. Wadadisi wa mambo bado wanaendelea kuchunguza kwa nini wameamua kumsusia wakati huu kama ni kutokana na kuamua kutazama zaidi kujenga maisha yao binafsi kibiashara ama wameshafungwa midomo na mafisadi wa CCM. Inasadikiwa kuwa katika uchaguzi mkuu 2005, viongozi waandamizi wa CCM walipopata taarifa kuwa Zitto Kabwe anaongoza Kigoma Kaskazini walitoa baraka atangazwe mshindi wakiamini kwamba wanaweza kumtumia lakini hali imebadilika baada ya sakata la Buzwagi, na sasa wanajutia uamuzi wao. Zitto amekuwa mwiba kwao na sasa wanatafuta kila namna ya kummaliza. Lakini kwa upande wa John Mnyika walipopata taarifa ya ushindi wake jimbo la Ubungo walimuona kama mtu atayewasumbua sana kutokana na umaarufu wa kuwa jimbo la mjini na pia waliona ni mtu mwenye msimamo huru hivyo wakaagiza msimamizi wa uchaguzi asimtangaze ushindi. Mara baada ya uchaguzi kwa habari ambazo zilithibitishwa na Mbowe mwenyewe CCM walijaribu kila njia kumnunua Mnyika bila mafanikio. Hata hivyo, kauli za vijana hawa za hivi karibuni zimedhirihirisha wazi kwamba labda lengo la CCM hasa Jakaya Kikwete kupitia kwa Rostam Aziz la kuwaziba midomo limefanikiwa. Wadadisi wa mambo wanaendelea kufuatilia ushahidi zaidi na pindi watakapopata wataumwaga hadharani. Kuondoka kwa kuwa Zitto na Mnyika kutakuwa pigo kwa CHADEMA kwani Dr Slaa kwa umri wake yuko mbioni kustaafu siasa.
 
CCM will never give up their efforts to vuruga upinzani makini. In upinzani only the strong will survive.
 
Mkamap,
Mjomba naomba somo, Labda mimi ndio sielewi tofauti zilizopo ktk maneno haya:-
1. Uchumi umekua ktk sekta za madini na Utalii
2. Mauzo yameongezeka ktk sekta za madini na Utalii.

Na mwisho ni wapi panaposema kuwa uchumi ukiongezeka pia tunapata faida na wakimaanisha faida gani.
 
Quote: Halisi
Pili, katika uchaguzi, ilibainika wazi kwamba Zitto alikua akimuunga mkono Arfi, ambaye alikua mpinzani wa Wangwe, kwa hiyo kuna kila sababu kwa yeye kutofurahia nyendo za Zitto.


Lakini hili halipaswi kuwa tatizo kwa sababu kwa vyovyote vile isingewezekana kila mtu amuunge mkono Chacha au Arfi. Lakini baada ya uchaguzi huyo aliyeshinda inakuwa basi imetoka na wala yeye mshindaji hapaswi kuanza kutunishia watu msuri. Hayo ya ziara ya mikoani na Jangwani nafikiri unachokonoa na unachokoza jambo ambalo sio muhimu sana.

Kitila nakubaliana na wewe kabisa kwamba suala la uchaguzi huishia baada ya matokeo kutangazwa kama ilivyo kwa Jk, Mwandosya, Salim, Malecela, Sumaye na wengineo. Lakini kumbuka kama ilivyo katika maisha, binadamu wana roho.

Kuhusu masuala mengine ya "yanayochokonolewa", kwa kuwa ni mambo madogo, nakubaliana na wewe kwa asilimia 100, kwamba ni mambo madogo sana kulingana na mambo mazito mengi katika siasa, lakini ni vyema tuwe na angalizo, kwamba hakuna jambo dogo kwa mtu mwenye tabia ya kuweka jambo rohoni (kisasi). Mtu wa aina hiyo ni hatari sana. Kwa kudharau mambo madogo, ambayo hata wahusika hawatayasema kamwe, ndiko kunakotufikisha kusema kwamba, "hivi hawa watu wamekumbwa na nini? au wamenunuliwa? Au ndio wametumwa kutuvuruga?"... Kwa kuangalia kila jambo na kulifanyia uchambuzi sambamba na kufanyia uchambuzi tabia na nyendo za wahusika, kutatusaidia kujua tatizo, ili kama hata hayo mambo madogo hayana maana, basi ndipo sasa tuangalie, hayo yanayosemwa kwamba huenda kuna "mkono wa mtu." Mambo madogo ndiyo yanayosababisha hata mambo makubwa kuharibika na kwa kuwa hayaonekani kwa udogo wake, mambo huharibika kabisa kwa kutojua chanzo cha tatizo.
 
Haya mara usia wa watu ulikuwa - Mnyika akasome aongeze elimu yake, akitaka kwenda ndio haya!.. akibakia Chadema - hana akili timamu, kazi kweli kweli.
 
Mr Mkandara
uchumi kukua maana yake kipato kimeongozeka yani
mfano kama una sh 100 nikanunua viazi na nikaamua kuviuza traansaction yote ikafanyika time matter pia kumlipa mfanyakazi hata kama ni wewe mwenyewe na nikabakiwa na fedha zaidi ya sh100 hapo ndipo unasema uchumi umeongozeka.

lakini ukiuza kwa bei ya faida mfano mauzo kwa mwezi ukawa unapata sh 10 ,basi ukaamua kupunguza bei na kwa mwezi ukauza sh 80 na viazi vyote ukaviuza kwa mda huo na ukapata jumla ya sh 80 hapo ina maana mauzo per mounth yameongozeka lakini umekula hasara kali
.
Na ukiendelea na process hiyo at a given time t u will end na mtaji hasi
Hapo ndipo namgeukia Zitto kapotosha jamii wala haitaji kumtetea
ZITO unapotosha jamii
madini ni sekta inayopata hasara more than ever ni sekta inayolipa hasara kubwa taifa .
 
Mbona hatuwekewe credible sources za hii habari jamani? hii imekaa kidhana zaidi. tuwekewe kauli zao thabiti hapa, bila hivyo mi naona no juhudi zile zile za kujaribu kuwagombanisha viongozi wa CHADEMA

Kwa ufahamu wangu, mwenyekiti wa CHADEMA yupo masomoni HUll, UK na sijasikia ikisemwa kuwa 'amekisusa chama' kwa kwenda kwake masomoni, na in fact wala hajaacha uenyekiti wake! Mbona sijasikia speculations za kuwa mbowe kanunuliwa tayari na mtandao wa CCM kupitia mawakala wake kama inavojaribu kuwa implied na huyo 'mgeni' paparaza muwazi hapo juu?

Hebu kuwa Muwazi in the real sense Paparazi..spinning ya namna hii hapa JF sio mahali pake.
 
alieleta hii mada bado mwanafunzi ndani ya JF au atueleze kuwa kaja kwa Jina Lingine...HUU ni UZUSHI usizishughulishe AKILI ZETU...
 
Mi nadhani katika lugha ya kawaida kabisa, tukiacha technical jargons za nini maana ya 'uchumi' na sales and profit, nadhani alichikuwa anamaanisha Zitto ni kwamba bado sekta bya madini na utalii haimnufaishi mwananchi wa kawaida moja kwa moja ijapokuwa rekodi zainaonyesha sekta hizi kukua katika miaka ya hivi karibuni!
Kuliingizia taifa hasara ndo huko huko kutomnufaisha mwananchi, ambaye ni sehemu ya taia...taifa lisipopata hasara mwanachi ataona hilo kupitia elimu nzuri, barabara, huduma za afya nk
 
Statement kwamba uchumi unakua iko Right no matter what.
Kisicho weza kuwa sahihi asilani ni statement isemayo:
Hali ya uchumi ya Watanzania walio wengi inakua kila mwaka au imekua.
Kukua uchumi ni jambo moja, hali ya uchumi ya mtanzania wa kawaida kukua hilo ni jambo jingine kabisa.

kauri kwamba uchumi unakuwa inasimama juu ya taarifa ya ongezeko la pato la nchi ambalo ni mjinga tu anaweza kubisha.

Ongezeko la pato la nchi kwa ujumla halina maana ya ongezeko la pato la kila Mtanzania. Ni hesabu ionyeshayo hisia kwamba kama wote tungegawana sawa kila mmjoa angepata kiasi fulani. Ni hesabuionyeshayo kipato cha nchi kwa ujumla hata kama anayefaidika na hilo pato yuko nje ya nchi.

Mpaka sasa sijui ni hesabu gani ya uhakika inaweza tumika kujua kipato halisi cha mtu mmoja mmmoja pale Tanzania.

Kuhesabu watu tu ni kazi sasa kujua kipato cha kila mtu si itakuwa ndoto?

Ugomvi mwingine unaanzishwa kwa sababu ya kuto elewa kinachoongelewa,kifupi unahusu uelewa. Wangwe alitakiwa kuomba ufafanuzi juu ya kauri ya Zitto kuhusu kukua uchumi.

Enzi zile mkapa anaingia madarakani kila mtu alikuwa na wimbo mdomoni kwamba Enzi za Mwinyi Pesa ilikuwa nje nje, huku wakilaani kwamba Mkapa kaleta ukapa. Cha ajabu hata wale ambao enzi za Mwinyi walikuwa wakila mlo mmoja kama wako jela nao niliwasikia waki akisi kauri hiyo kwa nguvu.

Ni kweli wakati wa Mwinyi ilikua fungulia mbwa paka nguchilo na panya lakini si kila mtu alineemeka.
Nakumbuka kuna jamaa walikuwa na Local Mtambo wa kutengeneza sabuni za kufulia.
Ile kuruhusu bidhaa kuingia kutoka nje tu hali yao iligeuka kuwa mbaya mpaka wakaishia kuhama hata mji. Watu wengi sana waliathiriwa na uingizaji wa bidhaa toka nje lakini kuna mamilioni ya watanzania walipata nafuu ya hali ya juu lakini si kiasi cha kuwafanya matajiri.

Wageni walo wekeza kila kona kwa baraka zote za chama Tawala SISIEMU ndo wanaoongeza hesabu ya pato la taifa.
Wageni wawekezaji Wakisha zikunja wanazipeleka ughaibuni hapa yanabakia mashimo na maganda tu.

Ili MH Wangwe apinge kauri kwamba Hesabu ya uchumi wa nchi haionyeshi uchumi kukua inabidi aje na tarakimu za miaka 5 mfululizo zenye kuthibitisha kauri yake.
Sivyo, aseme hakubaliani na Hesabu itolewayo na serikali juu ya ongezeko la pato la nchi.
Vinginevyo anaunga mkono kauri ya Zitto ila anaifafanua zaidi ,huku akimkalipia mwenzie bila sababu,kwa kusema ni watu wachache sana ambao kipato chao kinaongezeka Exponentialy.

Kuhusu Mfahari wawili ndani ya Zizi mimi hilo silioni. Kila mmoja ni mbunge kwenye jimbo lake hakuna jambo moja in common ambalo wana differ ila naona mmoja anatoka kwenda kumpinga mwenzie kwa sababu ambazo anazijua yeye. Kwa heshima zao hakuna atakiwaye kuwa msemaji wa mwenzie aua atakiwaye kukubaliana namwenzie kwanza ndipo aseme.

Politics is only for those who fit.
 
alieleta hii mada bado mwanafunzi ndani ya JF au atueleze kuwa kaja kwa Jina Lingine...HUU ni UZUSHI usizishughulishe AKILI ZETU...

Uko sahihi Chuma, hatuwezi kushangilia na kuijadili posti ya mtu ambaye ana posts 3 tu hapa JF, then anakuja na uzushi ambao hauna ushahidi wa kushikika. Huyu bado credibility yake ndogo sana kuweza kushawishi baraza hili.
Just Ignore him!
 
Back
Top Bottom