Kabuye (mbunge pekee wa TLP) Kafariki

Nilikuwa napenda kumsikiliza akitoa michango yake Bungeni. Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi.
 
Ama kweli duniani tunapita, Pumzika kwa amani mzee wetu, mchango wako bungeni wenye hisia kali juu ya walala hoi wenzio hatuto usahu
 
Katika siku zake ambazo ni za kuhesabika,(ee bwana utufundishe kuhesabu siku zetu), hakuweza kujilimbikia mali kw aufisadi, hata alipolazimika kuja dar, labda kwenye mkutano wa tlp, hakuweza ku-afford tiketi ya ndege, amekufa kishujaa, kwa kuwa ubunge wake pale dodoma hakuvuna kama akina rostam na wengine

kwa heri kabuye, bwana akubebe mabegani mwake, tazama e bwana kamwe usimwache katika pumziko lake la milele

kwa wengine wanaolamba asali ya taifa, tuiulize tena, kuhusu siku zetu, kwa mzaburi anaandika , jumla ya miaka yetu ni 70 tukiwa na afya njema 80!
 
RIP Kabuye, patriotic. Kamsalimie Nyerere na mtuombee TZ. Wajinga wanatuharibia sana nchi yetu. Kamwambie please.
 
Mzalendo halisi unauliza kama bado mbunge ,huyu babu alishindwa lakini alikuwa amekata rufaa na rufaa yake ilikuwa bado kusikilizwa kwakweli mungu amulaze mahali pema peponi
 
Viongozi hawafi wakiwa madarakani sijasikia raisi kufa kwa ugonjwa wala waziri hapa duniani zaidi sie walala hoi ndio tunaopukutika ,hawa wakifa basi ujue kuna mkono wa mtu.

Poleni wafiwa.
....Kwa Imani yako Hukustahili kutoa hayo maneno....Watakiwa kusema so simple sisi ni wa M/Mungu na kwake Tutarejea.
 
Mwenyezi ailaze roho ya marehemu Phares Kabuye mahala pema peponi. Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
 
nimesikitishwa na kifo chake
Mungu awafariji wafiwa na watanzania ote bila kusahau wananchi wake jimboni.
 
Huu ni msiba mzito kwelikweli. Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema amrehemu marehemu Phares Kashemeza Kabuye. BTN alipofariki Chacha Wangwe Mzee wa Kiraracha Mrema Augstino Lyatonga mzee wa nji hii alidai viongozi wa CHADEMA wamemuua. Je kwenye hili mkono wake? just T.O.L tukizingatia mrema ni mtu wa UT (Uuaji wa Taifa)
 
RIP Mzee Kabuye,

Mtetezi pekee wa WAKULIMA na WAFANYAKAZI bungeni.........

omarilyas
 
Nimemkumbuaka sana huyu Mzee mpaka nikautafuta huu uzi. Pumzika kwa amani mtetezi wa wanyonge Mh. Phares Kashemeza Kabuye
 
Its yet another reminder that we dont live forever and we should always try to be fair to everyone

RIP Kabuye, ulikua unatupa nafuu za moyo hasa kipindi cha hasira kwa wanasiasa, na mafisadi
 
Aisee miaka 5 imepita haraka sana.... kabuye kashemeze nilipenda uchangiani wake na ujenzi wa hoja anapo ongea. ... RIP brother mapambano uliyo yaanza bado yanaendelea sema mrema kageuka popo....
 
nimeona jukumu kuandika kumwombea kheri kwa Mungu kiongozi ambaye hakujilimbikizia mali. Mungu akulinde kiongozi wetu daima tutakukumbuka.
 
Aisee miaka 5 imepita haraka sana.... kabuye kashemeze nilipenda uchangiani wake na ujenzi wa hoja anapo ongea. ... RIP brother mapambano uliyo yaanza bado yanaendelea sema mrema kageuka popo....
Aliwahi kuwaambia wabunge kuwa watu safi Bungeni ni yeye tu na Shein ,wengine wote walitoa rushwa! hakuna aliyembishia hadi leo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom