Kaburu Matatani kwa Kupanga Kumuua Mandela

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
nelson-mandela-dead-rumours-set-twitter-abuzz.jpg




Mtu aliyepanga njama za kutaka kumuuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amepatikana na hatia.


Mahakama ya Pretoria ilimpata kiongozi wa kundi la -Boeremag linaloamini kuwa mtu mweupe ni bora alipatikana na hatia ya kupanga kummua Mandela mwaka 2002.


Bwana Mike du Toit ndiye aliyepanga milipuko tisa katika eneo la Soweto mjini Johannesburg mwaka 2002.


Kiongozi huyo wa kundi la ki-baguzi ni mtu wa kwanza kupatikana na hatia tangu utawala wa wengi uanze mwaka 1994 Afrika kusini.


Wachanganuzi wanasema kuwa bado kuna hali ya kutopendana katiki ya watu wa rangi tofauti nchini Afrika kusini.
Hata hivyo kundi kama la Boeremag,inayomaanisha Nguvu za Makaburu miongoni mwa Makaburu ,halina ufuasi mkubwa.
Mahakama hiyo ya Pretoria imempata Du Toit, ambaye alikuwa msomi baada ya kusikiliza kesi hiyo kwa miaka tisa GUMZO LA JIJI: Kaburu Matatani kwa Kupanga Kumuua Mandela
 
Back
Top Bottom