Kabla ya Kupiga Kura Arumeru Soma Gazeti Hili!

KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
864
Mama salma Kikwete amekumbwa na kashifa ya Kupora Ardhi ya Wapiga kura Mkoani Lindi, kwa kutumia madaraka ya Ikulu!!!!!!!!!!

Salma Kikwete
aichafua Ikulu

*Atumia nafasi yake kujimilikisha ardhi mkoani Lindi
*Afanya yale yale ya Anna Mkapa, enzi za Ben Mkapa
*Wenye ardhi walalamika, Mahakama yatoa hukumu


MKE wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mama Salma Kikwete,
ameiingiza Ofisi ya Ikulu katika
kashfa, baada ya kutwaa ardhi yenye ukubwa
wa ekari takriban 250 ndani ya halmashari ya
Mji wa Lindi kwa kutumia kivuli cha Taasisi
yake ya Wanawake na Maendeleo (WAMA),
ANIKA Ukweli linaweza kuthibitisha.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na timu ya
waandishi wa gazeti hili mkoani Lindi na Dar


es Salaam, umebaini kwamba
utwaaji huo wa ardhi aliufanya
kati ya mwaka 2009 na 2010.
Kuibuka kwa kashfa hii kumekuja
baada ya baadhi ya waliokuwa
wamiliki halali wa ardhi hiyo
kufungua shauri katika
Mahakama ya Usuluhishi ya
Migogoro ya Ardhi ya Mjini Lindi,
wakilalamikia kulipwa fidia
kidogo kulingana na ukubwa wa
ardhi na mali zilizomo ndani ya
ardhi yao.
Shauri hilo ambalo lilikuwa
chini ya Hakimu Njiwa J, kama
Mwenyekiti wa Jopo la Baraza la
Ardhi, lilifikia tamati Septemba
7, mwaka jana, kwa baraza hilo
kukubaliana na walalamikaji
ambao katika shauri hilo
waliwakilishwa na Lali Mchokozi,
hamed S. Mahafoudhi na Fatuma
S. Mahafoudhi.
Ardhi ambayo Mama Salma
anadaiwa kujimilikisha,na
ambayo inakadiriwa kuwa na
ukubwa wa ekari 250, ipo katika
eneo la Mabano-Mitwero ndani
ya Halmashauri ya Mji wa Lindi.
Inaelezwa kwamba mke huyo wa
Rais aliitumia Halmashauri hiyo,
chini ya usimamizi wa
Mkurugenzi kutwaa ardhi hiyo
ikiwa ni pamoja na kuwalipa fidia
wamiliki wa mwanzo wa ardhi
hiyo, ingawa karibu wote
walilalamikia fidia hiyo kwamba
ni ndogo.
Kwa mujibu wa hukumu ya
shauri hilo dhidi ya Mama Salma,
walalamikaji hao walifungua
shauri lao katika Mahakama ya
Mkoa wa Lindi, Kitengo cha
Ardhi Desemba 13, 2010, kabla
hukumu hiyo kutolewa
Septemba 7, 2011, kwa
kuwaamuru wahusika wa utwaaji
wa ardhi hiyo kufanya tathimini
upya ya ardhi na mali zilizomo
na kuwalipa fidia stahiki kwa
mujibu wa Sheria ya Ardhi ya
mwaka 1999, kifungu cha 3 (1) (g).
“Napenda kuchukua fursa hii
kukutaarifu kuwa baada ya
kulipwa fidia na taasisi ya WAMA,
unapewa notisi ya siku 90
kuanzia tarehe 15/10/2009 mpaka
tarehe 15/01/2010 uwe umehama
katika eneo husika. Sheria ya
Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999,
Sheria ya Utwaaji Ardhi Na 47 ya
mwaka 1967 na Sheria Na 8 ya
Mipangomiji ya mwaka 2007
zimezingatiwa katika kutekeleza
adhma hii,” inasema sehemu ya
barua ya notisi iliyotumwa kwa
mmoja wa wananchi ambao ardhi
yao imetwaliwa na Mama Salma
Kikwete ya Oktoba 13, 2009 na
kusainiwa na I.H. Chepa kwa
niaba ya Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji wa Lindi.
Mbali na Mchokozi, Hamed
na Fatuma Mahafoudhi, wengine
ambao ardhi yao ilitwaliwa, na
ambao wamelalamikia fidia
ndogo, ingawa hawapingi
kutwaliwa kwa ardhi yao, ni
pamoja na Salima Mohamed
Luka, Lucy Anthony Magulya,
Adamu Matwanje, Morris Musika,
Jane John Alfred, Kaisi Bakari
Kaisi, Abdallah Ismail Sokwe,
Halima Lali Ismail, Hashimu Lali
Ismail, Juma Seleman Madembe,
Mohamed Said Dadi, Habiba
Ally, Halima Mwishante, Alimbe
Ally Abdallah, Mugabo Wekwe,
Yohana Izaka Mnimaika, Jacob
Issa Mpili, Evarist Munyeti
Shileki na Issa Salum Mnala.
Katika madai yake mbele ya
wajumbe wa Baraza la Ardhi,
Mchokozi, pamoja na mambo
mengine, anasema alifunga
safari hadi kwa Mama Salma
Kikwete kulalamikia zoezi zima
uthamini wa ardhi yake, lakini
mke huyo wa Rais akamtuliza
kwa kumwambia asiwe na
wasiwasi atalipwa fidia stahiki,
kabla ya kumpoza na Sh 50,000.
Aidha, anasema eneo lake la
ardhi lilikuwa na ukubwa wa
ekari 10, likiwa na nyumba mbili
za kuishi familia yake pamoja na
mazao kadhaa ikiwamo minazi
20, lakini yalipokuja malipo ya
fidia ya ardhi yake hiyo, alikuta
ametengewa Sh 2,400,000. Hata
hivyo, anasema eneo lake hilo,
kama lingethaminiwa sawa sawa
na mali zake zilizomo angeweza
kupata walau Sh 20,000,000.
Kwa upande wake,
mlalamikaji wa pili katika shauri
hilo, Hemed Salum Mahfoudhi,
aliliambia jopo hilo la wajumbe
wa Baraza la Ardhi kwamba yeye
hakuwa akijua hasa ukubwa wa
shamba lake. Hata hivyo,
anasema hakushirikishwa katika
zoezi zima la kutwaliwa kwa
ardhi yake na wala hakuwa akijua
kama ardhi yake ilishatwaliwa
hadi pale alipitwa kuchukua
fedha za fidia ya eneo lake katika
ofisi ya Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji wa Lindi na
kukuta fidia yenyewe ikiwani Sh
170,000 tu. Kutokana na hali
hiyo, yeye anataka ama alipwe
fidia ya Sh 15,000,000 au ifanyike
tahimini upya ya ardhi na mali
zilizomo kwa mujibu wa sheria ya
ardhi.
Mlalamikaji wa tatu, Fatuma
Salum Mahfoudhi, anasema
wakati fulani mwaka 2009 akiwa
nyumbani kwake alifikiwa na
mgeni aliyejitambulisha kwake
kwa jina la Mussa, na
kumwambia kwamba yeye
alikuwa ni Saveya (Surveyor)
kutoka Halmashauri ya Lindi.
Aliendelea kusema kuwa Mussa
alimwambia alikuwa amefika
hapo kwa lengo la kufanya
tathimini ya eneo lake hilo na
kwamba kazi hiyo alikuwa
ametumwa na mke wa Rais,
Mama Salma Kikwete.
Aidha, Fatuma alilieleza
baraza hilo kwamba ardhi yake
ilikuwa na ukubwa wa ekari tatu
na nusu, lakini pia ikiwa na
nyumba moja yake ya kuishi na
familia yake. Alisema pia
kwamba mbali na nyumba hiyo
kulikuwamo mazao ya miti ya
mikorosho 58, migomba 18 ya
ndizi na kadhalika, lakini fidia
aliyolipwa ni Sh 1,962,000.
Anasema baada ya kulipwa
fidia hiyo, alijikuta akipewa
notisi ya siku 90 kuondoka katika
ardhi yake hiyo, kabla ya
kufunga safari hadi Dar es
Salaam yalipo makao makuu ya
WAMA. Akiwa katika ofisi za
WAMA, anasema alibahatika
kukutana na Mama Salma
Kikwete, ambaye baada ya
kumsikiliza malalamiko yake,
alimjibu kuwa ardhi yao hiyo
yeye haichukui kwa nguvu bali ni
kwa makubaliano yao na
halmashauri yao ambayo hiyo
ndiyo inayoshughulikia malipo
yao ya fidia. Mbali na
Mwenyekiti Njiwa J, wengine
waliounda jopo hilo wametajwa
kwa majina ya Jumaa na Kitenge.
Katika hukumu ya Mahakama
hiyo, Mwenyekiti huyo alisema
haoni mantiki ya walalamikaji
hao kutaka walipwe fidia ya Sh
15,000,000 kila mmoja, lakini pia
Mwenyekiti huyo akasema
anakubaliana na madai ya
walalamikaji hao ya kwamba
fidia hiyo waliyopewa siyo ya
sawa na ya haki, na hivyo
akamwamuru mlalamikiwa,
ambaye ni Halmashauri ya
Manispaa ya Lindi kufanya
tathimini upya ardhi na mali za
walalamikaji hao ili waweze
kulipwa fidia yao stahiki kwa
mujibu wa Sheria ya 1999,
kifungu cha 3 (1) (g).
Sheria na kifungu hicho kwa
mujibu wa hukumu hiyo ambayo
gazeti hili limefanikiwa kupata
nakala yake, inasema pamoja na
mambo mengine, kwamba moja
ya mambo ya msingi kabisa
yanayozingatiwa na sheria ya
asili ya ardhi ni kwa mmiliki wa
ardhi kulipwa malipo ya haki na
kwa wakati.
Juhudi za kumpata Mama
Salma Kikwete au ofisa yeyote
wa WAMA ili kuzungumzia kashfa
hii mpya ambayo wachambuzi
wa mambo wamelielezea kama
mwendelezo matendo wa wake
wa marais kutumia nafasi zao
kujitwalia raslimali za nchi kwa
kutumia vivuli vya taasisi zao,
hazikuzaa matunda hadi
tunakwenda mitamboni juzi
Jumatano.
WAMA, kama ilivyokuwa
EOTF enzi za utawala wa Mzee
Benjamin Mkapa, ni taasisi
binafsi iliyoanzishwa na Mama
Salma Kikwete ikiwa na malengo
ya kuwainua wanawake na
watoto wa kike kimaendeleo.
EOTF nayo ilianzishwa na Anna
Mkapa, wakati Mkapa akiwa
Ikulu, ikiwa na malengo hayo
hayo ya kuwapa fursa za
kiuchumi wanawake nchini.
Hata hivyo, tofauti na
malengo mazuri hayo, Mama
Anna Mkapa, aliitumia taasisi
yake hiyo kununua ardhi katika
maeneo mbalimbali nchini, ikiwa
ni pamoja na kununua majengo
ya yaliyokuwa yakimilikiwa na
Serikali, kwa kutumia kivuli cha
ubinafsishaji uliokuwa
unaratibiwa na Tume ya
Kurekebisha Mashirika ya Umma
(PSPRC) iliyoundwa na utawala
wa Rais Mkapa kwa lengo la
kuharakisha na kusimamia
uuzwaji wa zilizokuwa mali za
umma.
Source :ANIKA UKWELI, IJUMAA, MACHI 30 -APRILI 5, 2012 HABARI 3
 
Ni kawaida yao! wana Chukua Chao Mapema! km kusoma hatujui,jamani hata picha hatuioni?
 
Ni kweli wananchi hao hawakutendewa haki, ila tatizo letu watanzania ni kuvaanisha mambo! Ktk shauri hili sioni nukta ya moja kwa moja inayomgusa mama salma kwa dhati yake yeye kama salma! Kama ni dhulma hapa walioifanya ni halmashauri na sio "salma mke wa rais!!" na sidhani kama hiyo ardhi ni ya "salma" na sio ya "wama!!" tatizo la salma hapo ni nini? Kuunda hiyo taasisi ama kuisimamia? Mali inayonunuliwa na wama inakuwa milki ya mama salma kikwete au ya wanachama wa wama? Mbona salma basi na sio wama???
 
[h=2]Ardhi ni Bomu ambalo litavuruga amani ya Tanzania, Ubinafsi wa watawala utatuponza!!![/h]
Naomba wauze sana ili tuwahi kufika maana mkulima ukimwambia hakuelewi
Ni bora wafanyanye hivyo na hii ni laana kwa vile hawaoni na hawasikii na wanataka kila kitu
Na mwananchi atakapokatazwa au kuawa kwa ajili ya ardhi ndo atajua yanayoongelewa katika jukwaa la siasa za chama chake na je kina msaada gani
Mimi naomba wachukue maeneo yote mazuri wawape wawekezaji kupitia TIC na wafanyanye haraka maana bei ya ardhi ni ndogo sana kwasababu ya umasikini uliokidhiri
Na mfano shamba la miwa Bagamoyo hawana muda mrefu nao watakiona cha mtema kuni
Na kama si mashamba wapewe wachimbe madini na askari wawachape risasi watakaokaribia waya au geti la mgodi na wafanye hivyo katika nchi yote ili wananchi wazoee risasi haraka
Na wawape viwanda vyote ili maskini tuwe wengi na ili tutakapoingia barabarani tuwe wengi
Na dada zetu waruhusiwe kuvaa vyovyote kwani mila zetu ni mbaya na tunaficha miili sana bora tuiweke hadharani na tuweze kununuliwa na wenye hela kwa ajili ya starehe
Na watakaoichoka na milli haiuziki tena na wale tutakuwa nao barabarani kudai haki yetu
Na naomba madarasa ya kutwa yawe mengi kuliko ya bweni ili tuimarishe ukabila na tukose umoja haraka ibaki umoja katika shida na mateso ya watawala
Na wajenge hospitali kwa kuchukua ardhi mapema ili vifo vipungue na wadai tuwe wengi
Na madini nayapitikane nchi yote ili wawahi kututoa na kumpa mwekezaji nasi tuweze kuunganisha nguvu mapema kwa shida zetu na kutolewa katika ardhi ya mababu zetu
Na kila msitu au pori zuri apewe mwekezaji ili alime Jatropha na sisi tukose kuni na madawa ya asili ili tuwe wengi tunaoumia kwa manyanyaso
Na naomba wawekezekezaji wataopewa ardhi waweke fence ya umeme haraka ili watakaokufa kwa kutokujua kuwa umeme unaua ili watakao taka ndugu kwenda kumzika kwanini aligusa na wapigwe bakora za kutosha
Na naomba waekezaji watumie polisi kwa kuwaadhibu wananchi waliokaribu na maeneo yao ili wakione cha moto mapema
Na naomba wawekezaji watumie sumu sana ili madhara yasambae mapema na wawakodishie wabunge ndege na kuwalipa malipo mazuri ili madhara yaendelee
Na naomba wawekezaji wawalipie NEMC nauli na posho ili kuja kukagua na wasiseme chochote
Na naomba kila mwanasiasa apate eneo la madini ili naye awe na mgodi na awalete wawekezaji mwenyewe na waingie ubia na wananchi waambulie kibarua na mikong'onto
Na naomba kila sehemu yenye maji pia apewe mwekezaji ili wananchi wakose maji ili tuwe wengi barabarani
"NASHUKURU KWANI UKOMBOZI UKO KARIBU BAADA YA KUANZA CHA WOTE KUWAPA WAGENI ILI TUKOSE PA KUSHIKA NA ILI TUAMKE KUDAI UHURU UPYA!"​
 
Back
Top Bottom