Kabla ya Kujiita jina hasa kwa kuiga tafadhali jua maana yake: Maana ya jina la DIVA

nyie ndio mlitoa ile DvD inaitwa "WICKED ALBUM" ?
MKAmuongelea mpaka 2pac na aaliya
nnayo home sijui ilikujaje kujaje home
niliipenda...
mkaomgelea na umbrella ya RiRi
 
Watu mnatishana tu! Vipi kuhusu Emmanuel?
Kama Jayz na Beyonce waliamua kujiita kwa tafsiri hiyo, basi hiyo maana na ibakie kwao tu.
 
KABLA UJAJIITA JINA JITAIDI UJUWE MAANA YAKE WASICHANA WENGI SANA WANALIPENDA ILI JINA DIVA UTASIKIA IM THE DIVA... ==DIVA===MUNGU WA KIKE ==SOMA KWA MAKINI SANA ALAFU USIJIITE TENA ILI JINA !!!

Leo ningependa kuongea kuhusu kitu kimoja ambacho ninakiona kikiendelea kuchanua na wakati kinaonekana kuwa kibaya na kisichokuwa na msingi hasa katika maisha ya wanadamu. Ningependa kuwaambia wasichana kitu kimoja, kwa wale waelewa, watanielewa ila kwa wale ambao hawataki kuelewa, hawatonielewa na wala sitotaka kuwalazimisha kunielewa. Kila siku wasichana wamekuwa watu wa kujipa majina mbalimbali kama cute, pretty na majina mengine mengi. Ni vizuri kwa sababu kila mtu anatamani kujipa jina ambalo litakuwa kama alama yake ya kumfanya kujulikana.

Hakuna tatizo kwenye kujipa majina ila yawapasa kuangalia majina yenyewe. Kwa leo nitakwenda kulitafsiri jina liitwalo &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];DIVA' ambalo kila siku wasichana wamekuwa wakilipapatikia sana. DIVA ni jina la Kilatini ambalo lina maana ya MUNGU WA KIKE. Katika kipindi cha nyuma, jina hili halikuwa likijulikana kabisa kwa wasichana wa Kitanzania mpaka pale muimbaji mahili, Beyonce alipoanza kulitaja katika wimbo wake ule wa DIVA. Wasichana wengi wamelichukulia jina hili kuwa jina la kawaida sana ambalo linaweza kutumika kwa msichana yeyote mrembo ingawa si kweli. Huku nikiendelea kutoa ufafanuzi naomba ujiulize swali moja. Wazungu wamekuwa watu wa kuchukua majina mengi tu ya masupastaa na kujipachika wao. Hivi haujawahi kujiuliza hata siku moja sababu zinazowapelekea wasichana wa Kizungu kutojipa jina hilo la DIVA? Wanajua maana halisi ya jina hilo na chimbuko lake na ndio maana hata hawataki kulitumia. Najua wengi watakuwa wanafahamu kwamba Beyonce amekuwa mwanachama mmoja wa dini inayompinga MUngu ya Freemason. Nani ambaye hafahamu hilo?

Kama haufahamu, ngoja nikwambie kitu kimoja ambacho kitakufanya kujua kwamba yeye ni mwanachama halisi wa Freemason. Nitakwenda kukufafanulia hili kwa kupitia video fulani ambayo innaitwa THE WICKED MUSIC INDUSTRY. Ndani ya hii video wamejaribu kutaja alama mbalimbali za Freemason pamoja na kumtaja Bathomet, mungu wa dini hii ambaye amekuwa akiwapa utajiri na umaarufu mkubwa duniani. Jina la mwanamuziki huyu ni BEYONCE GISELLE KNOWLECE ambaye kwa mara ya kwanza alianzia muziki wake kanisani. Alianza kuimba nyimbo za kawaida ambapo kukampatia sana umaarufu alipokuwa katika kundi la Destiny Child. Baada ya kujitoa katika kundi hilo, wimbo wake wa kwanza kabisa kuutoa kama msanii anayejitegemea ulikuwa &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];CRAZY IN LOVE'. Najua video ya wimbo huu utakuwa umeuangalia sana lakini nina uhakika video halisi ya wimbo ule utakuwa haujaelewa kitu chochote kile. Video ile ilitengenezwa kwa kuyazungumzia maisha yake ambayo aliamua kuishi kwa wakati huo.

Itafute video ile na kisha iangalie tena. Kuna scene ambayo inaonyesha kwamba Beyonce yupo ndani ya gari akiangaika na kisha Jay Z akalichoma moto gari lile na yule Beyonce wa ndani ya gari kufa baada ya gari kulipuka. Hapo hapo, Beyonce akaonekana akitokea upande mwingine na kumfuata Jay Z mahali pale na kuanza kucheza nae huku Jay Z akianza kuimba. Nani ameielewa scene ile ilimaanisha nini? Kwa kuangalia tu huwezi kugundua kitu chochote kile ila nitakuelezea hapa ili uweze kuelewa vizuri zaidi. Hapa Beyonce alijaribu kutueleza kwamba Beyonce yule wa zamani alikuwa amekufa garini na sasa alikuwa amekuja Beyonce mwingine. Kuanzia siku hiyo ndio ilikuwa kwa mara ya kwanza Beyonce kujipa jina jingine liitwalo SASHA FIERCE.

Nikijaribu kukuleta nyuma katika mahojiano yake na gazeti la PEOPLE la nchini Marekani tarehe 18/11/2008, Beyonce alisema hivi "Shasa Fierce alizaliwa katika kipindi ambacho nilifanya video ya CRAZY IN LOVE. Watu wanapokutana nami wanategemea kumuona Beyonce ila inabidi watambue kwamba mtu huyu (Sasha Fierce) ni mtu wa stejini. Ukijaribu kuiangalia video hiyo hiyo ya CRAZY IN LOVE utaona kwamba mtu ambaye alimuua BEYONCE garini alikuwa JAY Z. Nani ambaye hajui kwamba JAY Z ni mwanachama wa dini impingayo Mungu ya Freemason? Kwa maana hiyo JAY Z ndiye aliyemuua BEYONCE kama kwenye video yake inavyoonyesha na SASHA FIERCE kuzaliwa (Jaribu kuiangalia video hiyo kwa mara nyingine tena na uifuatilie). Kwa wale ambao hawakuwa wakifahamu jina ambalo JAY Z amekuwa akipenda kujiita basi ni lazima wajue kwamba jina hilo ni HOOVA. Ukisikiliza nyimbo zake nyingi amekuwa akipenda kujiita jina hili mara kwa mara. Jina hili si la kawaida, hapa anatuonyeshea kwamba amekuwa akijaribu kujifananisha na MUNGU kwani jina jingine la MUNGU ni JEHOVA.

Kwa akili yake kwa sasa anajiona yupo juu huku akiwa na mamlaka ya kufanya lolote lile alitakalo kulifanya na ndio maana amejipa jina hilo ambalo kama hauko makini kamwe hauwezi kuligundua. Kwa kuwa BEYONCE aliona kwamba mtu ambaye alikuwa nae katika mahusiano ya kimaenzi anajiita HOOVA hapo ndipo nae alipoamua kujiita DIVA yaani likiwa na maana ya mungu mwanamke. Kwa maana yao hapo ni kwamba JAY Z ni mungu wa kiume na BEYONCE ni mungu wa kike???.. Nikikurudia wewe ambaye umelichukua jina hilo la DIVA, ulikuwa ukilijua maana halisi ya jina hilo? BEYONCE hakutaka kuficcha na ndio maana akatoa wimbo wa DIVA ambapo alijiita rasmi &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];I AM A DIVA'. Hiyo ndio maana halisi ya jina hilo na ndio maana kila ninapomuona msichana wa Kiafrika anajiita DIVA huwa ninashangaa na kushtuka sana.

Kama wewe unajiona kuwa ni mungu wa kike, basi jina hilo linakufaa sana ila kama unajiona kwamba wewe si mungu wa kike, achana nalo kwani majina mengine kama hayo yanakuwa na nguvu za giza. Hiyo ndio sababu inayowapelekea wasichana wa Ulaya kutotaka kujiita jina la DIVA kwani maana yake inajulikana na kila mtu.

Angalia hii maana ya diva

Diva - Wikipedia
https://en.m.wikipedia.org/wiki/ Diva
A diva (/ˈdiːvə/; Italian: [ˈdiːva]) is a celebrated
female singer; a woman of outstanding talent in the
world of opera, and by extension in theatre, cinema and
popular music. The meaning of diva is closely related to
that of prima donna.
 
Mkuu ni kweli unayoyasema, hiyo documentary niliiona jana, jamaa ameielezea vizuri mno na mifano ya kutosha na moja ya kitu kilichonisisimua ni Pale Michael Jackson alipomwita meneja wa Sony music company enzi hizo kuwa ni devil na jinsi familia ya Michael Jackson ilivyomtoa kafara
Mkuu nitapataje hiyo documentary
 
Nimeshindwa kuelewa au??

Celtic Meaning:

The name Diva is a Celtic baby name. In Celtic the meaning of the name Diva is:Divine one.

Numerology
SoulUrge Number: 1
People with this name have a deep inner desire to use their abilities in leadership, and to have personal independence. They would rather focus on large, important issues, and delegate the details.

Expression Number: 9
People with this name tend to be passionate, compassionate, intuitive, romantic, and to have magnetic personalities. They are usually humanitarian, broadminded and generous, and tend to follow professions where they can serve humanity. Because they are so affectionate and giving, they may be imposed on. They are romantic and easily fall in love, but may be easily hurt and are sometimes quick-tempered.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom