Kabla sijaenda JF Doctors, ni ugonjwa gani huu?

Mabagala

JF-Expert Member
Nov 27, 2009
1,477
325
Hasa hasa nimeuona Zanzibar, naskia ni ugonjwa upo sana maeneo ya pwani pwani. Ile hali ya kujambishwa, yaani mtu anapita na kupuliza mdomo na kutoa sauti ya ushuzi basi jamaa wa pembeni yake anaumia, ama anaweza akajikunja au akavunja au kuchana vitu mbele yake. wakati niko zanzibar alimanusra huyu jamaa avunje computer yangu. Huku Ukerewe sijaona mtu akitokewa na hiyo hali, ni nini hii kitu jamani? ni samaki wanaokula ama wanakuwaje kuwaje ile sound ya hewa chafu iwaumize?. Na kwanini itokee huko pwani tu? Nisaidieni maana hata kugoogle nimeshindwa kizungu chake nitaanzaje
 
Hahahahaaaa kitu Busha hicho.....sio pwani tu hata bara wapo wenye nayo yan ukipuliza Pyuuuuuuuuuuu anaweza kuanguka chini
 
sijaelewa kabisaaaa, naomba mnifafanulie tafadhali
Mtu mwenye busha yan sehemu za siri za duara zinakuwa Kuuuuubwa kama nazi hadi anatembea kwa shida then ukipuliza kitu km vuvuzela dah anaumia sana na anaweza kuanguka kabisa
 
Mtu mwenye busha yan sehemu za siri za duara zinakuwa Kuuuuubwa kama nazi hadi anatembea kwa shida then ukipuliza kitu km vuvuzela dah anaumia sana na anaweza kuanguka kabisa
Elephantiasis? (lymphoscrotum)
Sasa huo ugonjwa na vuvuzela inakuaje? ukipuliza hivo inamuaffect vipi?
 
mimi pia nataka connection ya vuvuzela na busha! mbona wengine mananiliu yao yanakuwa sio makubwa dizaini ya nazi? anakuwa yupo kawaida tu ila ukipuliza tu umemuumiza! kuna nini hapo? Huku Ukerewe mi sijaona vuvuzela likimuumiza mtu. Je wanawake hawapatwi na hii hali?
 
Elephantiasis ni matende
Hernia ni busha
Mtoa mada, google hernia ujisomee.
King'asti sijui sijaeleza vizuri? ule mlio wa vuvuzela unahusiana vipi na yeye kuumia au kuona raha ya kupitiliza? Je huko umang'ati unaweza ukapuliza tu mtu akawa na hali ya namna hiyo?
 
Elephantiasis? (lymphoscrotum)
Sasa huo ugonjwa na vuvuzela inakuaje? ukipuliza hivo inamuaffect vipi?
Mwali nimependa ulemba huo!!! tena huko tanga naskia ndo kwenyewe, wapo wengi ambao wakiskia tu ile sound tu baasi mtu hoi
 
We ni wale mbun'go Nitonye sio matende kijana....vipi kesi yako na wenye nyumba wako imeisha?Karibu tukae kwangu

mbung'o anaambukiza malale.......mabusha huwa yanasababishwa na aina fulani ya mbu....
 
Elephantiasis? (lymphoscrotum)
Sasa huo ugonjwa na vuvuzela inakuaje? ukipuliza hivo inamuaffect vipi?
Sijapataga connection ila ndo iko hivyo,ila nahisi ni km mtu akikwaruza bati kriiiiiiiii then unaumia meno hope ni km vinaendana ingawa kiutaalamu sijajua kwanini waumie
 
mimi pia nataka connection ya vuvuzela na busha! mbona wengine mananiliu yao yanakuwa sio makubwa dizaini ya nazi? anakuwa yupo kawaida tu ila ukipuliza tu umemuumiza! kuna nini hapo? Huku Ukerewe mi sijaona vuvuzela likimuumiza mtu. Je wanawake hawapatwi na hii hali?

wanawake hawapati....kwa sababu hawana ngogwe.....
hiyo kitu ni maarufu kwa ajili ya ngogwe....

Preta wasitiri kidogo
ngogwe imesaundi kama kokwa

nikichanganya na ile taarabu ya miaka hiyo

mdudu eee mdudu, kaingiaje
mdudu ndani ya kokwa la embe kaingiaje

ha ha ha....Kongosho umenifanya nicheke kama mwehu.....

Similar Discussions

Back
Top Bottom