Kabla hawajatuletea madaktari, je hali ya maisha Iran ikoje?

Don Draper

Senior Member
May 30, 2012
176
87
Nimeambiwa kuwa Iran bado wanaishi kwenye zama za mawe sasa iweje wao leo wanataka kutuletea madaktari?

Hii ni nafasi yetu sote kufanya research kujua huko Iran hali ikoje?
 
iran hospitali zao ni kama za kwetu so wakija hapa wataweza kufanya kazi muhimbili...huwezi mtoa daktari kwenye hospitali za ulaya ukamleta hapa mazingira ya kazi yatawashinda
 
Nimeambiwa kuwa Iran bado wanaishi kwenye zama za mawe sasa iweje wao leo wanataka kutuletea madaktari?

Hii ni nafasi yetu sote kufanya research kujua huko Iran hali ikoje?

Haya mambo ya kuambiwa huwa yanatufanya tudumae kwa kiasi fulani na kukosa kujua mengi sana.Nilianga Press TV ambayo ni ya wairani lakini lugha ya kingereza,na wanacho kipindi chao kinaitwa Iran today.Kwakweli nimepata kujua mengi kuhusu hawa jamaa jinsi walivo hodari kielimu na maendeleo.Mahospitali yao ni ya hali ya juu na ukija ktk usafiri kwa mfano Tehran wanazo treni za Under ground ambazo ni nzuri na safi na za kileo kuliko hata za London.Na ni mahodari wa kutunza historia zao.Kwakifupi sina wasiwasi nao hasa ktk utendaji wa kazi na labda itatusaidia na sisi kuboresha mengi ktk hospitali zetu.

Lakini kwa ushauri tu serikali iliangalie hili suala la mgomo wa madaktari wetu kwani hawa ni wananchi wenzetu na lazima wasikilizwe.Kama watachukua madactari wageni ina maana watanzania watakuwa hawana kazi tena kwasababu ya madai yao na ni ya msingi tu.Na je inamaana madaktari wa kigeni watafanya kazi milele hapa kwetu?Hapana lazima kunakitu ambacho kitaweza kurahisisha matatizo haya.
 
Wako mbali sana wala si wenzio hata kidogo...:hat:
 
Nimeambiwa kuwa Iran bado wanaishi kwenye zama za mawe sasa iweje wao leo wanataka kutuletea madaktari?

Hii ni nafasi yetu sote kufanya research kujua huko Iran hali ikoje?
wewe unaishi dunia ipi? Iran na kwa kifupi nchi za jamii yake si zakujilinganisha nazo kabisa kwani wako mbali nasa katika kila sekta. achana na propaganda za magharibi. open your eyes and mind.
 
Upo dunia gani wewe? eti umeambiwa kumbe hujui kitu....IRAN sio wenzetu ata kidogo fatilia documentary mbalimbali na utaona GREECE AND PERSIAN ndo elimu toka zama na zama imelala....IRAN wanaexport all medicines including medical equipments na mgogoro wao mkubwa ulikua ni shida ya ku import vifaa vya kutibu cancer kwani hii technology ilikua kwa nchi za magaribi km vile huduma za mionzi na ndo mwanzo kutrain watu wao kwenye nuclear issue kwani wagonjwa wa cancer matibabu yake ni miionzi ya nuclear....IRAN ana export vifaa mpaka kwa nchi ULAYA mfano GERMANY ameoda meli kubwa toka IRAN sasa hao utajilinganisha nao na walikua km sisi tu lakini wamewekeza ktk elimu...Tembelea websites zao kwenye ishu za technology na last year ndo ilikua leading nation kwa kuchapisha vijarida vingi vya sayansi...wenzako wanategemea by 2017 warushe asrtonomy ktk sayari, wanaexport ndege,magari,meli,silaha mbalimbali na optical obejct eg binocular,lenses na upuuzi mwingine....Hawa sio waarabu hawa ni wapersia bro
 
ambulance zao ndio hizi:

bus.gif

bus4.gif

ef5.gif
 
Haya mambo ya kuambiwa huwa yanatufanya tudumae kwa kiasi fulani na kukosa kujua mengi sana.Nilianga Press TV ambayo ni ya wairani lakini lugha ya kingereza,na wanacho kipindi chao kinaitwa Iran today.Kwakweli nimepata kujua mengi kuhusu hawa jamaa jinsi walivo hodari kielimu na maendeleo.Mahospitali yao ni ya hali ya juu na ukija ktk usafiri kwa mfano Tehran wanazo treni za Under ground ambazo ni nzuri na safi na za kileo kuliko hata za London.Na ni mahodari wa kutunza historia zao.Kwakifupi sina wasiwasi nao hasa ktk utendaji wa kazi na labda itatusaidia na sisi kuboresha mengi ktk hospitali zetu.

Lakini kwa ushauri tu serikali iliangalie hili suala la mgomo wa madaktari wetu kwani hawa ni wananchi wenzetu na lazima wasikilizwe.Kama watachukua madactari wageni ina maana watanzania watakuwa hawana kazi tena kwasababu ya madai yao na ni ya msingi tu.Na je inamaana madaktari wa kigeni watafanya kazi milele hapa kwetu?Hapana lazima kunakitu ambacho kitaweza kurahisisha matatizo haya.

Press TV ni kama TBC yetu, wanaonesha yale wakubwa wanataka. Ndio Iran wamepiga hatua lakini sio kama ambavyo wengi wanataka tuamini. Wana watu kibao wanaochunga mbuzi kama sisi huku bongo, na meno machafu kuliko ya mnywa wanzuki.
 
Wairan ambao tunaambiwa wanaishi zama za mawe wana hospitali kama hii

20110814025956_1.jpg

20110814025438_3.jpg

20110814025232_6.jpg

20110814025406_4.jpg

20110814025658_2.jpg
 
Viongozi wa ccm wanataka waibe pesa ya wananchi waje waseme waliwalipa madaktari bingwa wakiirani
 
Haya mambo ya kuambiwa huwa yanatufanya tudumae kwa kiasi fulani na kukosa kujua mengi sana.......Kwakifupi sina wasiwasi nao hasa ktk utendaji wa kazi...... na labda itatusaidia na sisi kuboresha mengi ktk hospitali zetu.

.

Nakubaliana na maelezo yako kiasi fulani; lakini hata hao madaktari "tumeambiwa ni madaktari kutoka nje" Je ni jinsi gani mwananchi wa kawaida ataweza kudhibitisha kweli ni madaktari na wala sio kundi la watu tu? Inaweza pia kuwa wanafunzi wanaosomea udaktari wanakuja for exchange program. Ni ukweli usiofichika wananchi wengi hawana imani tena na kile serikali inachosema; inawezekana serikali ikaleta wanafunzi wa medicine ( tena bila cost yeyote) wakatudanganya wame-spend 200 billion on them alafu pesa inaingia mfukoni kwa fisadi.

On a separate note; hii mambo yakuonyesha hospitali za Iran kwenye picha tunaambiwa ndio hospitali zao zilivyo, tunaamini vipi. Je hizo ni hospitali ni za serikali au private? Je hospitali zote ziko hivyo? Je huko Iran kuna matabaka/class? Je hao madaktari wanaokuja ndio 1st class (wanaothaminiwa huko) au ndio yale yale tu? Nafahamu Iran wako way far ahead of us, lakini tunachoonyeshwa kwenye TV/picha kinaweza kuwa sio ukweli halisi, au sicho tutakachokipata. Je ni chombo gani cha serikali kinaaminika kinachoweza kupima ubora wa hawa madaktari?
 
Kuna watu wakiona majengo basi imetosha. Hivi mtu akipiga picha hospitali Private hapa bongo kama Trauma, Aga Khan, na uka-focus kuonesha machine si itaonekana Tanzania mambo swafi?

Kwenye point yako kuhusu ni watu gani wanaletwa, hapa ndipo penye mtahani. wataleja majasusi tupu maana hawa Iran wanataka sana Uranium. Lakini kweli hebu tujiulize, watakaa milele? Wakiondoka tutakuwa na nini? Hii kwangu ni sawa na kuuwa sekta ya afya.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom