Kabila Langu ni Lipi

IshaLubuva

JF-Expert Member
Dec 4, 2008
250
11
Katika jamii yetu ya Kiafrika imezoeleka kwamba Mwafrika akizaa na Mzungu/Mwarabu na mtoto akawa nywele na rangi vyenye mwonekano wa Kizungu/Kiarabu basi huyo huitwa Chotara.

Swali langu ni hili, je Mrangi akimuwowa Mchaga mtoto anayezaliwa awe kabila gani? Je huyu naye siyo chotara.

Lakini utamkuta mtu mzazi wake mmoja siyo mwafrika na yeye amefanania kwenye Uafrika lakini anajiita Mwarabu/Mzungu (kuna mmoja Shinyanga watu walikuwa wanamwita "Hakiyamungu mimi Mwarabu" -Ikimaanisha kwamba lazima aape kwa mungu wake ndo mtu ajue kwamba mzazi wake mmoja ni Mwarabu), kwa nini asijiite Mwafrika?
 
uchotara unakuja kwa kuchanganya race, mrangi na mchagga wote ni wabantu mtoto anaweza mwenyewe kuamua kabila gani analipenda la baba au mama. kumbuka hapo zamani watu walibadili kabila kutoka moja kwenda jingine. kwa ufupi inasemekana mtemi millambo wa unyamwezi alikuwa mngoni kiasili. wachagga nao ni mchanganyiko wa makabila mengi mojawapo ni wasambaa
 
chotara ni mtu aliyechanganya race na sio dini wala kabila. dini/kabila mtu anaweza kubadili wakati wowote. nyie vp.
 
Hivi Warangi na/au Wachagga sio Waafrika? I did not know that before! Kwa hakika hii ni 2010!

Uafrika siyo kabila bali ni asili, ila kwenye thread yangu nimeongelea kuhusu matokeo ya mchanganyiko wa watu kimakabila na kiasilia.
 
Kabila lako ni mwanadamu. Usiwe na kabila lingine. Tatizo la Dunia hii ndio hilo,kwamba watu wanagawanyika kwa kufuata kabila,dini,Utaifa. Lazima tuwe na falsafa au dini ,au Chama cha Siasa,ambacho kinawaleta watu pamoja kufanya kazi kwa ushirikiano.
 
.....

Swali langu ni hili, je Mrangi akimuwowa Mchaga mtoto anayezaliwa awe kabila gani? Je huyu naye siyo chotara.

...

Nadhani ulikuwa unamaanisha kuoa.

Mtoto anatakaye zaliwa katika ndoa ya mchaga na mrangi anaweza kuwa chotara pale ambapo mzazi mmoja au wote ni machotara; either mchaga au mrangi alichanganya damu na race nyingine i.e asian, spanish au europian.
 
mie nilikiwaambia watu kama ni mtanzania wanakataa....but i still call myself mtanzania...:)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom