Kabila la Kiiraqw laweza kupotea kabisa Tanzania


Niliwahi kupita maeneo ya Hanang,Endasak na Haydom kuna totoz nzuri Mungu kawajalia kwa uzuri wa sura.
 
wewe hujui kabisa historia ya Wairaqw. Hawana uhusiano wowote na Iraq na hawawezi kupotea kwenye ramani ya Tz.

Nilipata story ya mzee mmoja pale Dareda,anasema ni kweli wametokea Iraq mnamo karne ya 13. Walipita Ethiopia,Somalia na hadi kuja Tanzania kupitia Kenya (utaweza kuona ndugu zao katika nchi walizopita). Walifika kwa wingi na kuweka makaazi yao katika Mlima Nou (ulimo Msitu wa taifa wa Nou). Kwa vile wao ni wakulima na wafugaji,walipigana sana na jamii za wafugaji kama wabarbaig na wamaasi ili wapate mahala pa kulima.

Ni story niliyopata kwa mzee huyo;kwa sasa naiamini mpaka nitakapofahamu vingine.
 
bora wapotee tu kwanza hawana asili ya tz wana asili ya huko huko iraq

Chifu steveachi, hivi kuna kabila lina asili ya Tanzania?
Chifu hii mipaka ya nchi hapa Afrika tumewekewa na haya mabazazi kutoka Ulaya.
Hapo kale watu walikuwa wanaroam around tu;uwezo wa kupigana vita na wenyewi utaowakuta ndiyo kilikuwa kigezo cha kuweka makazi mahala.

Hivyo kwa mtazamo huo, suala lako linakuwa halina msingi. Kwani makabila mengi kama si yote yaliingia hapa yakitokea sehemu mbalimbali za Afrika na Mashariki ya Mbali.
 
Last edited by a moderator:
gartathaa aten gwaran amortakawan kungaa.....anagwaada daagwaye....amukuug.....
 
Pamoja na sababu hiyo, kabila la ki-Iraqw ni wengi sidhani kama litapotea. Ukianzia Karatu, Daudi, Masieda, Bargish antsi, Arri, Mbulu mjini, Anslay, Gehandu, Gedamar, Titiwi, Kwermusl, Khaday, Kainamu, Nahasey, Tsaayo-raat, Hayloto, Murray, Qwam, Kuta, Siday, Tlawi, Masqaroda, Diyomati, Bashay, Dongobesh, Tumati, Mongahay, Endoji, Bashnet, Gidhim, Maretadu, Gibdiyo, Gidmadoy, Gidarudadaw, Simhha, Haydrer, Semonyandi, Mewadani, Musru, Endagikot, Endaharghadakt, Endamasaki, Endamilay, Endanachan, Endanyawish, Erboshan, Ngw’andakw, Yarotamburda, Qatabella, Qamatananat, Qambush, Datlaa, Dumanangw, Endagew, Muguruchan, Maghang, Haydom mpaka kule Murkuchida ni wao tu. Pia kule Yaeda chini na Mungowamono kwa Wahadzabe wapo wachache.
O la la la haya ni majina ya vijiji au mitaa au nini?
 
aidoma aidori! Habari ni kwamba haiwezekani kupotea hapa nilipo tu tupo kama 3 hivi na ni kusini kabisa mwa Tanzania. Swala la extinction ni out of question faza?
 
Nilipata story ya mzee mmoja pale Dareda,anasema ni kweli wametokea Iraq mnamo karne ya 13. Walipita Ethiopia,Somalia na hadi kuja Tanzania kupitia Kenya (utaweza kuona ndugu zao katika nchi walizopita). Walifika kwa wingi na kuweka makaazi yao katika Mlima Nou (ulimo Msitu wa taifa wa Nou). Kwa vile wao ni wakulima na wafugaji,walipigana sana na jamii za wafugaji kama wabarbaig na wamaasi ili wapate mahala pa kulima.

Ni story niliyopata kwa mzee huyo;kwa sasa naiamini mpaka nitakapofahamu vingine.


Iraqw ni jamii ya wakushi,jamii ya watu wanaopatikana Etiopia, Eritrea, somalia, sehemu ya Chad, Misri Djibouti na kaskazini mwa Kenya na Great rift valey kaskazini mashariki mwa Tanzania. Lugha ya Kush ni tawi la mjumuiko wa lugha mbalimbali unaojulikana kama Afro-asiatic ambayo ni jamii ya lugha zinazotumika katika maeneo ya mashariki ya kati na kaskazini na mashariki mwa Afrika. Afroasiatic imegawanyika katika matawi matano- Kushitic, Egyptian, Berber, Chadic, na Semitic.

Egypian inazungumzwa katika nchi ya Misri na Berber inatumiwa na watu wa Moroco(lugha ya taifa), Algeria na Tunisia na Libya.
Semitic ni subfamily ya afro-asiatic inayotumika katika maeneo ya mashariki ya kati, afrika kaskazini na Horn of Afrika. Matawi yake ni Kiarabu, Amharic, Kiyahudi(Hebrew), Aramaic and Tigrinya.

Amharic inazungumzwa Ethiopia(lugha ya taifa) na Tigrinya inazungumzwa katika nchi ya Eritrea na sehemu ya Ethiopia. Lugha ya kiyahudi yaani Hebrew inatumika Israel na Aramaic ni kiyahudi ya kale iliyotumiwa na yesu na katika vitabu vya agano la kale katika biblia takatifu, pia inatumiwa na watu wachache hadi sasa nchini israel na syria.

Kushites nao wamegawanyika katika Noth Kushites(lugha ya Beja inayotumika Egypt, sudan na Eritrea), Central Kushites(Agaw inayotumika Ethiopia na Eritrea), East Kushites(Oromo, Somali na Afar zinazotumika Djibouti, Eritrea, Ethiopia,Somalia sehemu ya Yemen na kenya) na South Kushites(Iraqw na makabila madogo ya Gorowa, Alawa na Burunge- wanapatikana katika Great Rift Valey of Tanzania).
Iraqw kuwa kushites inadhihirishwa na lugha na mwonekano wao ambao unafanana sana na ule wa watu wa Ethipia na Somalia. Inaaminika kuwa Iraqw walifika katika Nyanda za juu za mashariki mwa Tanzania karne kadhaa baada ya kristo na kwamba ndio jamii ya peke katika Tanzania ambayo ifanya kilimo cha hali ya juu na ujuzi mkubwa katika kilimo cha umwagiliaji na matumizi ya matuta kuzuia mmomonyoko wa udongo ukizingatia wanalima katika kingo za milima na bonde la ufa(Irqwar Da/aw ni mfano).

Vilevile Iraqw inasemekana katika safari yao ya kuja Tazania walifuata bonde la ufa hadi Ngorongoro Crater na walitua katika eneo litwalo sasa ENGARUKA (jina la kimasai ingawa wairaqw wanataja katika simulizi za kale kuwa MAANGWATAY) ambako waliishi hadi wamasai na wabarbaig walivyofika na vita kati yao kusababisha waondoke na kulitelekeza eneo hilo la kihistoria.

Wairaqw ni watu wapole wanaopenda kudumisha mila na kuishi katika mila na desturi complex kama Daawi complexity wakati wa kuoa/kuolewa , meta kwa mtu aliyefiwa na mke/mume, mwanamke kuzaa kabla ya kuolewa-doroway, miscariage na loo, bayni na mengine zaidi. kwa mfano, mwiraq hawezi kuoa masai ingiwa siyo daawi ila mkono wa damu kwa kuwa wamasai waliua sana wairaq hapo zamani. Daawi ni very complex kwani inahusisha ndugu wa ukoo upande wa mama na koo zingine tano za bibi wa mama na bibi wa bibi wa mama...
 
SIzani kama linaweza kupotea haraka! Yapo makabila ambayo uwezekano wa kupotea haraka ni mkubwa kuliko hata wa Iraq.....Afu mbona kama hii habari inarudiwa rudiwa
 
:A S-confused1:
Bado Endagulda, Gwalaytigenik, Gijedamahog, Endaharaqdakt............
:A S-confused1:

Sijui historia ya makabila ya tanzania lakini liko tofauti na makabila mengine. Lilindwe kwa ajili ya kizazi kijacho
 
Ila wadada zao wazuri kama wale wa Singida ila sasa kwa Mgao duu kama Dawasco!
Ni kweli wadada zao ni wazuri, nikiwa JKT, nilikapenda kabinti kamoja ka huko, sio siri, kalinichanginyi!, Kalikuwa kaalimu na kakapangiwa kwao!. Nlikafungia safari, enzi hizo Babati hoteli ya maana ilikuwa moja tuu "Motel Paa Paa"!.

Nkatembezwa kote, mpaka kule juu mlima Katesh unakuta vibinti viziwa nje nje!, kuna watu hawawezi kuamini kuna watu Tanzania wanatembea uchi!. Kule mlimani baridi kali, mimi na jacketi langu lakini bado nasikia baridi, lakini wao na haswa vitoto vyao vinatembea bila nguo kabisa!.

Uhusiano ulipamba moto, nikarudi Dar, baada ya miezi Sita, nikafunga tena enzi hizo Arusha Babati, ni mwendo wa saa 6!, kufika shule alipokuwa anafundisha kule Dareda nikaambiwa kahamishiwa Endasak tarafa ya Bashnet, giza limeingia, hakuna gest wala hoteli!, nikahifadhiwa kwa mwalimu mmoja wa kike aliyekuwa rafiki yake hivyo taarifa zangu alikuwa nazo!.

Katika mazungumzo yetu mwalimu akanishauri, kwa vile mchumba hakunijuluisha kuwa amehama, ni bora kesho yake nigeuze nilalale Babati, keshokutwa yake nirudi Dar, si unajua tena kupenda enzi za ujana!, mimi king'ang'anizi mpaka nimuone!. Usiku ule nililala hapo kwa mwalimu, na kwa Wenzetu Wambulu, ukarimu ni asilimia 100%, nashukuru hata baridi sikuisikia!.

Asubuhi breakfast ya nguvu kwa level ya kijijini, safari ya kumsaka mchumba ikaendelea kwa siku nzima, nilifika hapo shule anapofundisha jioni wameshatoka shule, nikaulizia ulizia nikaelekezwa kwa mwalimu mmoja jirani, nikajieleza nikaambiwa kweli mwalimu huyo yupo ila kwa vile saa hizo ni usiku giza linaingia, nikashauriwa nitafutiwe pa kujihifadhi, mchumba nitamuona asubuhi!.

Mimi king'ang'anizi nikalazimisha lazima nikamuone mchumba!, yule mwalimu akasema nisubiri anitafutie watu wakunipeleka, yeye mwenyewe ndio akatoka, alichelewa sana kurudi, ndipo akaniletea jibu, kuwa mwalimu yule leo alikwenda Babati kufuatilia mshahara wake!, walimu wapya wakiajiriwa, majina yao huchukua hata miezi sita kabla hawajaanza kulipwa mishahara!. Ilibidi nipatiwe hifadhi mahali pengine full mabaridi!, usiku ule ulikuwa kama mwaka!,

Kesho yake saa 12 asubuhi, niligongewa hodi, mwenyeji wangu kufungua, kumbe ni mchumba, nikaitwa nje, kutokana na baridi nya hapo hata sikuhitaji kuoga, nikavaa jeans langu fasta fasta mimi huyo nje!, ile kumuona tuu mchumba nilipigwa na butwaa!, hata kumkumbatia na kumbusu nilishindwa!, mchumba alikuwa amebadilika, amekuwa "meneja!"

Sikuwa na hili wala lile, alinieleza hali halisi, waalimu wapya walipangiwa kazi mahali hapana nyumba, na bila mishahara!, wengi walilazimika kuhifadhiwa kwa waalimu wenzao na kuishi kwa kudura ya Mwenyezi Mungu!. Kwa uzuri wa mwalimu mchumba, baada ya kufika kituo kipya cha kazi, hakupata shida kupata mfadhili wa haja, na yeye alikuwa hana jinsi, ikambidi ajikabidhi jumla!, na matokeo ya "umeneja" ule huo ufadhili!.

Sikuwa na hili wala lile, ni kuanza safari yangu kurudi kulala Babati, kesho yake kkwenda kulala Arusha, keshokutwa yake kurudi Dar. Niliondoka Dar Siku ya Jumapili, nikarudi Jumapili, nimetumia siku 7 kumsaka mchumba wa Kimbulu, nikaambulia patupu!. Nikuwa nimechoka hoi bin taaban, kimwili, kiuchumi na kisaikolojia!.
 
Kabila la Wairaqi maana yake wanatoka katikati ya Tigris na Euphrates. Adma and Eve walikuwa Wairaqi.Nao ndio walioanzisha Western civilization,that is why it was so amusing Waamerika walipokwenda kule na kujaribu kuwapigisha magoti kwa kutumia tomahawk missiles.

Wameshindwa,understandably,Wamarekani ndio imebidi waondoke Iraq kwa aibu,kwa sababu huwezi kuwashinda watu kwa superior technology ambayo wao wenyewe ndio wamekusaidia.

Kwa hiyo Adam and Eve walikuwa Iraq,wanajenga familia,kwa interbreeding,kwa muda mrefu,ili baadae wafanye intermarriage na sorrounding tribes.

Kwa hiyo hao Wairaqi wa Tanzania kama wana mila ambayo inawakataza kufanya in breeding,hiyo ni tradition ambayo imeanza Eden.

Ingekuwa vizuri kama wataalamu wetu wangecheki DNA za hawa watu ili tuweze kujua ukweli juu ya asili ya hao Wairaqi.
 
Kabila la Wairaqi maana yake wanatoka katikati ya Tigris na Euphrates. Adma and Eve walikuwa Wairaqi.
Ingekuwa vizuri kama wataalamu wetu wangecheki DNA za hawa watu ili tuweze kujua ukweli juu ya asili ya hao Wairaqi.
Mkuu Andrew, samahani haiko sahihi, Wairaque wa Tanzania ni jina tuu lakini asili yao sio Ghuba, hawa ni watu wanaitwa "nilotic na semi-nilotic" hawa sio Wabantu, asili yao ni dola ya kale ya Axum na sio Uajemi!.

Ila pia issue sio asili yao, issue ni tishio la extinction!, mnaonaje kwanza mkawajua wako wangapi?.
 
Ni kweli wadada zao ni wazuri, nikiwa JKT, nilikapenda kabinti kamoja ka huko, sio siri, kalinichanginyi!, Kalikuwa kaalimu na kakapangiwa kwao!. Nlikafungia safari, enzi hizo Babati hoteli ya maana ilikuwa moja tuu "Motel Paa Paa"!.

Nkatembezwa kote, mpaka kule juu mlima Katesh unakuta vibinti viziwa nje nje!, kuna watu hawawezi kuamini kuna watu Tanzania wanatembea uchi!. Kule mlimani baridi kali, mimi na jacketi langu lakini bado nasikia baridi, lakini wao na haswa vitoto vyao vinatembea bila nguo kabisa!..
Pole sana Pasco, sipati picha enzi hizo bashnet ilikuwa vipi maana hata sasa ukienda watu wanafunuka mgorori na blanketi kipindi chote cha mwaka(mgorori kwa ndani na blanketi juu) bila kusahahu Kofia staili ya kininja only macho yanaonekana. Viatu ni gum boot na hatua tano mbele huoni mtu kwa ajili ya ukungu.

Kipindi baridi kali ikipita hata Katani zinakauka na katika ule msitu katika ukingo wa bonde la ufa (masabeda Qameyu hadi madunga) digidigi unamkamata kwa mkono kwakuwa hawezi kukimbia. Boys na girls have fine looking faces to the extent that you cant distinguish.
 
Back
Top Bottom