JWTZ waigomea SERIKALI...

Mi nashangaa GT unashobokea porojo...!!!? Jeshini ni mahali penye utaratibu maalumu, na taarifa zote zinatolewa na idara maalumu. JF home of GT sasa hivi inageuka sehemu ya hadithi za vijiweni... Mods kuna haja ya kutafuta utaratibu kuzuia thread zinazopotosha zisizo na chanzo halisi!!!
 
Kama habari hizi ni kweli basi heshima ya JWT imeanza kurejea! Mungu Ibariki JWTZ!
 
safi sana..kazi ya jeshi ni kulinda maslahi ya taifa sio upuuzi wa viongozi au watawala...
big up sana JWTZ kwani kazi yenu kubwa ni kulinda maslahi ya taifa na watu wake sio wanasiasa na sera zao mbovu...
 
Huyo anaugua kwani walishika fedha zake kule Africa ya kusini alizokuwa amekwapua kupittia nafasi yake. Nafikiri hawezi tena kushirikiana na serikali dhaifu.
 
Yale yale ya Mbunge kufumaniwa Singida JF-Kata wanafuata mkumbo kama kawaida yao...hivi hunajua amri akitoa Amiri Jeshi kuna mtu wa kupinga?
 
CCM ni dhalimu sana na kandamizi kimfumo na kimkakati kwa watanzania:-

1) Angalia madai ya mafao ya wazee (sitaki kutaja wale wa iliyokuwa EAC)
2) Angalia danadana za malipo ya walimu
3) Angalia wafanyakazi wa Reli (TRC) na kwa sehemu TAZARA
4) Angalia madaktari na uboreshaji wa huduma za afya kwa ujumla
5) Angalia wanafunzi wa elimu ya juu (ndani na nje)
6) Angalia wakulima wa pamba, kahawa, korosho, mahindi nk jinsi walivyonywa na sasa wako mahtuti
7) Angalia wavuvi ziwa Nyasa, Tanganyika nk
8) Angalia wafugaji na jinsi mpaka sasa wamekuwa wanatangatanga na kuishia kugombana na wakulima kutokana na serikali dhaifu za ccm (sio hii ya Kikwete tu)
9) Nenda kwenye machimbo na migodi utaona zaidi ya kalamu na wino vinavyoweza kuripoti
10) Ongezea na wewe
 
10) Ongezea na wewe[/QUOTE

10) Angalia jinsi viongozi wa CCM walivyoficha mabilioni ya shillingi katika mabenki ya Uswisi kupitia mashirika ya uchimbaji mafuta na madini hapa TZ
 
JWTZ wamesisitiza kuwa hawatapeleka Madaktari katika Hospitali yoyote. Jeshi likasema kuwa anayepaswa kutoa taarifa rasmi juu ya uamuzi wao ni Serikali kwakuwa hilo si suala la kijeshi.
 
Hivi kuna hospitali ya Rufaa ya kijeshi cuz naona rufaa zote ( hata ukitibiwa hospitali za jeshi) uwa zinaenda muhimbili na hospitali nyingine za serikali
 
Bandu bandu humala gogo, huu ndio mwisho wa serikal ya CCM
Katika hali isiyotarajiwa,Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limegoma kutoa Madaktari kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Madaktari wanaogoma katika Hospitali mbalimbali za Rufaa, Teule na nyinginezo.

Viongozi waandamizi wa Jeshi hilo Makao Makuu wameitaka Serikali kutafuta haraka suluhu ya mgomo huo badala ya kukimbilia kwa Jeshi kwa msaada huku tatizo likibaki.

'Tumewaambia waende wakatafute suluhisho' alisema mmoja wa Maafisa Waandamizi wa JWTZ mwenye cheo cha Brigedia Jenerali. 'Hii tabia siyo njema. Tatizo halitakwisha kwakuwa Serikali itakuwa na uhakika wa huduma ingawa si rasmi' aliongeza.

Serikali ifanye nini sasa?
 
Back
Top Bottom